Mdahalo wa Mwl.Nyerere foundation kuhusu Katiba Mpya katika ukumbi wa Ubungo Plaza

swagazetu

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
4,251
1,467
Kwa mujibu wa ITV leo 4/8/2014 Mwalimu Nyerere Foundation wataendesha mdahalo kabambe kuhusu Katiba mpya pale Ubungo Plaza kesho Jumatatu tarehe 4/8/2014 kuanzia saa 9 alasiri wasemaji na waliokuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mzee mwenyewe Joseph Sinde Warioba, Dr.Salim Ahmed Salim, Bwana Mdogo Humphrey Polepole na Mzee Joseph Butiku.

Mdahalo utaonyeshwa moja kwa moja kwenye ITV, pia utasikika kupitia Radio one na Capital Radio.

Leo tutarajie ufafanuzi toka kwa Mh.Warioba juu ya waraka wa mapendekezo mapya aliyoyapeleka kwa serikali akibadilisha baadhi ya mapendekezo ya Tume. Itakuwa ni jambo la maana mh.Warioba akilisemea hilo ili jamii na umma uweze kuona uhalisia na ukweli wa kauli ya mh.Lukuvi aliyoisema jana pale Nkrumah Hall chuo kikuu cha dsm.

Warioba itabidi atueleze tujue maoni yake yanahusu nini? Je, ni ya kwake binafsi au ya Tume? kama ni ya kwake binafsi je! tumwelewe kwamba tume yake imepika mambo kama wajumbe wengi wa bunge la katiba toka CCM walivyodai? Na iwapo maoni/mapendekezo hayo mapya ni ya Tume,, ni ya Tume ipi maana tume yake ilishavunjwa?

Watanzania tuwasihi Tanesco wasikate umeme ili watanzania wengi wasikie ufafanuzi kwa hoja zilizopindishwa na wapindishaji. Na pia watoe ufafanuzi kwa baadhi ya hoja ngumu na tata.

Aidha, tutarajie wajumbe wa iliokuwa Tume ya Katiba kuonesha mwanga wa namna ya kutoka hapa ambapo BMK limenasa.
===========================================

Updates

=>Warioba anasema waliteuliwa wajumbe toka makundi tofuati wenye misimamo na itikadi tofuat kidin, kisiasa na kiuchumi lakn tofaut hzo walieka kando na kuangalia maslah ya taifa!
Anawaomba makundi yote yanayopaswa kuwa BMK washauriane kuondoa maslahi binafsi na kujal maoni ya wananchi ktk maeneo yote muhimu.

=>Jaji warioba anasema hakuna mawaziri wa muungano wanaotembelea Zanzibar kwa ajili ya mambo ya Muungano.
Mambo yote ya muungano ni ya bara.

=>Anasema Nchi mbili zimeunganika lakini moja haina Sovereignty, Tanganyika iko huru kufanya mambo yake ya maendeleo lakini Zanzibar mpaka iombe ridhaa ya Bara.

=>Anakana Maneno aliyoyasema Lukuvi, anasema Rasimu ya kwanza ilikuwa na sura mbili ambazo zinazungumzia maliasili/ Ardhi.
Tulipomaliza kazi yetu, tulikabidhi serikali rasimu.
Anasema hiyo barua aliyowaandikia Serikali ataitoa kwa waandishi wa habari, ili mambo yawe wazi.

=>Muda wa maswali na maoni umeanza.
  • UKAWA watafute mwenyekiti mwenza aongoze bunge la katiba na Sitta-Mchangiaji
  • Machali anauliza swali kuhusu serikali viongozi wake kuto kuheshimu maoni ya wananchi anaomba kupata busara kwa Wazee kama Warioba na Butiku wananchi wachukue hatua gani
  • Ni lini mtu anatoa maoni kama kiongozi wa nchi au mtu binafsi, Je maoni ya Kikwete hayakuharibu mchakato wa Katiba?
  • Tume ilijengaje imani hadi ikakamilisha kazi ya kutoa rasimu na kwanini BMK imeshindwa. Nini kifanyike

Mama Hellen Bisimba, amesema je wananchi wako tayari kuendelea kuona pesa yao iendelee kutumika vibaya ndani ya bunge la katiba?
Maria Sarungi, anasema wanasiasa wamejikita katika uchaguzi wa 2015. so muafaka itakuwa ngumu

JIBU
=>Walishauriana wakati mwingi na raisi, Raisi alitoa maoni kwanza kama mtanzania mwenye haki pili kama raisi, anaheshimu maoni yake pale alipoyatolea.
Raisi ni mwanachama wa chama cha mapinduzi, yapo maoni yaliyoelekea huko

=>Walijiandaa kujua ni nini kifanyike, itafika mahali BMK watakua pamoja, wamepunguza sana madaraka ya raisi pia atengane na bunge. Hatakua sehemu ya bunge na mawaziri wake hawatakua bungeni. Watafute lugha inayojenga na maslahi yao yawe Taifa

=>Machali na Ukawa waambiwa waende wakakae, hii ni busara ya hali ya juu kutoka kwa Warioba, Kifupi warioba ana wasihi Ukawa warudi bungeni.

=>Joseph Butiku Anaongelea mambo muhimu yaliyojitokeza katika mchakato:
Anasema wajumbe wengi kwenye Tume walikuwa na umri mkubwa, anasema watu wanasema wao ni wazee wakufa.
Anasema watu wasikilize maneno ya wazee, anauliza mchakato sio wa vyama ni wa wananchi.
Anasema mchakato sio wa vyama ni wananchi.

=>Vitabu vingine wameweka kwenye Tovuti lakini Tovuti imefungwa, Anauliza nani kafunga Tovuti....?

=>Madhumuni ya mchakato huu umeelezwa ndani ya sheria.

Awadhi Said kutoka Zanzibar ndiye anayeongea sasa.
=>Ni wakati wa uwazi, muungano utoe fursa na haki sawa. Serikali ya muungano ina majukumu mawili, mambo ya muungano na Tanzania Bara ukijumlisha na serikali ya ZNZ tayari tuna serikali tatu hivyo hoja ya gharama sio. Kilichopendekezwa ni serikali mbili zilizo chini ya serikali ya muungano zitanganishwe.
=>Tanzania bara itabeba gharama nyingi kuliko ya visiwani sio hoja kwa sababu gharama zinatokana na mahitaji. Anatolea mfano mahitaji ya polisi Zanzibar na Tanganyika, Polisi mmoja alinde watu 400 na mali zao, tanzania bara 120,000 polisi, na kwa tanzania visiwani watahitaji polisi 2700

Mama Mwantumu ndiye anaeongea sasa

=>Mama Mwanatumu ameanza kuongea yeye alikuwa n mjumbe wa tume na pia mstaafu kutoka Serikalini. anaongelea takwimu, anasema wananchi waliongelea madaraka ya Rais yapunguzwe.
=>Anakanusha kuwa sio kweli kwamba wao wanajificha kwenye kivuli cha wananchi

[JFMP3]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=175278&d=1407229135[/JFMP3]
[JFMP3]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=175277&d=1407228820[/JFMP3]
 
Attachments

  • Hotuba ya Palamagamba kabudi .mp3
    8.9 MB · Views: 598
  • hotuba ya warioba.mp3
    9.9 MB · Views: 730
Nafikiri hatuna viongozi wenye utashi, weledi, uwezo na patriotism ya kuweza kutupitia Katiba mpya yenye dhana ya kujenga a good society ndani ya Chama tawala na ndani ya upinzani.

Tukubali tumechemsha na tusitishe zoezi Hadi tujipange upya! Tutapoteza pesa bure.

Si walioko madarakani, si wapinzani na si wananchi wanaweza kusema kwa nini tunataka Katiba mpya, na kwa nini lazima iwe sasa.

Siasa za kubezana, mchakato ulio na mapungufu makubwa na ubinafsi kamwe havitatupa Katiba mpya itakayoleta ustawi wa taifa Letu tukufu.

Ujasiri unahitajika kwa upande wa Uongozi kukubali hili zoezi halina tija kwa wakati Huu. Kuzomeana hakutatupa matokeo tuliotarajia. We lost the game!! Sad.

Videos

Last edited by a moderator:
Nafikiri hatuna viongozi wenye utashi, weledi, uwezo na patriotism ya kuweza kutupitia Katiba mpya yenye dhana ya kujenga a good society ndani ya Chama tawala na ndani ya upinzani.

Tukubali tumechemsha na tusitishe zoezi Hadi tujipange upya! Tutapoteza pesa bure.

Si walioko madarakani, si wapinzani na si wananchi wanaweza kusema kwa nini tunataka Katiba mpya, na kwa nini lazima iwe sasa.

Siasa za kubezana, mchakato ulio na mapungufu makubwa na ubinafsi kamwe havitatupa Katiba mpya itakayoleta ustawi wa taifa Letu tukufu.

Ujasiri unahitajika kwa upande wa Uongozi kukubali hili zoezi halina tija kwa wakati Huu. Kuzomeana hakutatupa matokeo tuliotarajia. We lost the game!! Sad

its so sad serikali ya CCM imefikia hatua ya kukodisha watu wa kuzomea wale wote wanaojenga hoja zenye maslahi ya taifa kwenye jambo la muhimu kama hili ambalo sio la leo wala kesho tu bali ni kwa ajili ya vizazi kwa vizazi.
 
Tujiandae kisaikolojia. maana umeme unaweza kuzimwa nchi nzima. kama watawala waliweza kufunga tovuti ya tume ihi je watashindwa nini kuminya mdahalo wa leo? maana kuanzia saa 7 mchana tume itakua inatoa helimu ya rasimu ya katiba na saa 9 mchana wataenda hewani. sasa unategemea nini kile kikundi cha walafi wa madaraka wa ccm watakubali? kuumbuka???
 
Mchamba mavi huwa hachambi mara moja na hata akichamba katu haachi kunuka...

Ubaya au uzuri wa CCM na serikali yake sasa ndio wajionesha kwa uzuri kabisa
 
Nafikiri hatuna viongozi wenye utashi, weledi, uwezo na patriotism ya kuweza kutupitia Katiba mpya yenye dhana ya kujenga a good society ndani ya Chama tawala na ndani ya upinzani.

Tukubali tumechemsha na tusitishe zoezi Hadi tujipange upya! Tutapoteza pesa bure.

Si walioko madarakani, si wapinzani na si wananchi wanaweza kusema kwa nini tunataka Katiba mpya, na kwa nini lazima iwe sasa.

Siasa za kubezana, mchakato ulio na mapungufu makubwa na ubinafsi kamwe havitatupa Katiba mpya itakayoleta ustawi wa taifa Letu tukufu.

Ujasiri unahitajika kwa upande wa Uongozi kukubali hili zoezi halina tija kwa wakati Huu. Kuzomeana hakutatupa matokeo tuliotarajia. We lost the game!! Sad

Katiba ya wananchi haitungwi na wanasiasa.. Kosa kubwa lilikuwa ni kukubali wabunge kuwa ndo wajumbe wa bunge la katiba.. Kama kweli wanataka katiba ya wananchi basi ufanyike uchaguzi wa kuwachagua wajumbe wa bunge maalumu la katiba.. Kigezo kimoja kikubwa cha kugombea ni mgombea kutokuwa mwanasiasa au kufungamana na chama chochote.. Hiyo ndo njia pekee ambayo itasaidia kupatikana kwa katiba ya wananchi..
 
Kwa mujibu wa ITV leo 4/8/2014 mh.jaji Mstaafu Warioba, Salmu A. Salmu,Butiku na takribani iliyokuwa Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Watz juu ya katiba mpya itakuwa pale Peal Hotel kuanzia saa 7 na itakuwa live hewani kuanzia saa 9 hadi saa 12 kupitia ITV, Radio One na Capital Radio.

Washiriki ni wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Warioba na wasomi wanasheria kadhaa, akiwamo,Kalamaganda Kabudi.

Leo tutarajie ufafanuzi toka kwa Mh.Warioba juu ya waraka wa mapendekezo mapya aliyoyapeleka kwa serikali akibadilisha baadhi ya mapendekezo ya Tume. Itakuwa ni jambo la maana mh.Warioba akilisemea hilo ili jamii na umma uweze kuona uhalisia na ukweli wa kauli ya mh.Lukuvi aliyoisema jana pale Nkrumah Hall chuo kikuu cha dsm.

Warioba itabidi atueleze tujue maoni yake yanahusu nini? Je, ni ya kwake binafsi au ya Tume? kama ni ya kwake binafsi je! tumwelewe kwamba tume yake imepika mambo kama wajumbe wengi wa bunge la katiba toka CCM walivyodai? Na iwapo maoni/mapendekezo hayo mapya ni ya Tume,, ni ya Tume ipi maana tume yake ilishavunjwa?

Watanzania tuwasihi Tanesco wasikate umeme ili watanzania wengi wasikie ufafanuzi kwa hoja zilizopindishwa na wapindishaji. Na pia watoe ufafanuzi kwa baadhi ya hoja ngumu na tata.

Aidha, tutarajie wajumbe wa iliokuwa Tume ya Katiba kuonesha mwanga wa namna ya kutoka hapa ambapo BMK limenasa.
 
Naombeni sana sana Tanesco mzime umeme japo kwa leo tu......je kuna link yoyote tunaweza kusikiliza kwa sisi ambao tutakua bado kwa mkoloni??
 
Tanesco wameshapata taarifa wameambiwa wakate umeme kuanzia sa7 mpaka sa12
 
Mhe. Jaji warioba na timu yake kama wataamua kutumia busara zao zote basi inawezekana UKAWA wakarejea "Ulingoni".
 
Hapa ndio ukweli utajulikana Maana ccm wanataka kufanya kua Ukawa niwabaya kutokurudi Bungeni Ngoja Tume itasema yale Mapendekezo niyawananchi na wala si ya tume
 
Kwa mujibu wa ITV leo 4/8/2014 mh.jaji Mstaafu Warioba, Salmu A. Salmu,Butiku na takribani iliyokuwa Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Watz juu ya katiba mpya itakuwa pale Peal Hotel kuanzia saa 7 na itakuwa live hewani kuanzia saa 9 hadi saa 12 kupitia ITV, Radio One na Capital Radio.

Washiriki ni wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Warioba na wasomi wanasheria kadhaa, akiwamo,Kalamaganda Kabudi.

Leo tutarajie ufafanuzi toka kwa Mh.Warioba juu ya waraka wa mapendekezo mapya aliyoyapeleka kwa serikali akibadilisha baadhi ya mapendekezo ya Tume. Itakuwa ni jambo la maana mh.Warioba akilisemea hilo ili jamii na umma uweze kuona uhalisia na ukweli wa kauli ya mh.Lukuvi aliyoisema jana pale Nkrumah Hall chuo kikuu cha dsm.

Warioba itabidi atueleze tujue maoni yake yanahusu nini? Je, ni ya kwake binafsi au ya Tume? kama ni ya kwake binafsi je! tumwelewe kwamba tume yake imepika mambo kama wajumbe wengi wa bunge la katiba toka CCM walivyodai? Na iwapo maoni/mapendekezo hayo mapya ni ya Tume,, ni ya Tume ipi maana tume yake ilishavunjwa?

Watanzania tuwasihi Tanesco wasikate umeme ili watanzania wengi wasikie ufafanuzi kwa hoja zilizopindishwa na wapindishaji. Na pia watoe ufafanuzi kwa baadhi ya hoja ngumu na tata.

Aidha, tutarajie wajumbe wa iliokuwa Tume ya Katiba kuonesha mwanga wa namna ya kutoka hapa ambapo BMK limenasa.
Hawezi akafanya kosa la kupeleka mapendekezo baaday tume kuvunjwa.
Anachoweza na kuingia katika ku clarify baadhi ya mambo ili kunusuru mchakato lakini akiwa kama Raia.
Naamini ndiyo maana amewaleta na wenzie,most of the time hatujamuona Salum Ahmed Salum akifafanua haya mambo.
Kuna jitihada kubwa za kuficha aibu iliyotokea!!!
 
Huyu Mzee Warioba anatafuta sababu za kufa haraka kwa pressure. Alishaambiea apumzike, kiherehere cha nini?
 
Ndoto za Mwalimu Nyerere na swaiba wake Nkwame Nkruma ilikuwa ni kuileta AFRICA moja yenye sauti kubwa sana duniani cha ajabu ni kuona tumesahau na sasa ni kupeana vyeo ni upuuzi na inakera sana kila kukicha waafrika wanatengana ndoto ni kupeana ulaji na ukwasi wa utajiri. Serikali moja inatosha kuelekea THE UNITED STATES OF AFRICA.
 
Kwa sasa tunataka way foward,waambieni wananchi nini cha kufanya baada ya miCCM kufanya uhuni,mambo ya kusema wamechakachua vile na hivi kila mtu anajua.kama ni maandamano,kama ni kuvamia bunge kesho tukavamie tupige kufuri hakuna kima kuingia pale
 
Bunge la katiba limejaa wanasiasa, tena wanasiasa wenye upinzani toka zamani. Kundi la 201 wajumbe 161 ni wana CCM, bado humohumo kuna wanasiasa kutoka vyama vingine mfano mtatiro nk, msitegemee katiba mpya hapo
 
Huyu Mzee Warioba anatafuta sababu za kufa haraka kwa pressure. Alishaambiea apumzike, kiherehere cha nini?

Ndg wala usiwe na presha. Ujio wao inaweza kuwa ni aibu kwa UKAWA kwan huo ni mkakati mahususi wa kuwarudisha ukawa bungeni ili tukawanyonye mbavu huko huko.
Kwa maana hiyo warioba na wenzi watakua wanauma kidogo ccm na kupuliza ukawa.
 
Back
Top Bottom