Ismail Jussa Ladhu akiongea katika mdahalo uliorusha na Star Tv amesema CCM ni kilichochoka hakifai tena kupewa nafasi ya kuongoza nchi kwa hata sasa wanainchi wanajionea chama hicho kuwa ombwe la uongozi.
Akiongea kwa kujiamini amesema chama hicho hakijui mpaka leo kinasimamia itikadi gani ujamaa au ubepari.
Akielezea chama cha CHADEMA amesema kuwa ni hatari kuwa na viongozi ambao hawatembei katika maneno yao ambapo alisema CDM wamesimama kupinga posho lakini wabunge wake wanachukua posho mf. shibuda, pia katibu mkuu Wilbrod Slaa alikuwa anapinga posho na mishahara ya wabunge kuwa mikubwa lakini leo ndio amewashinikiza cdm wamlipe mshahara wa mbunge.
Kwa kweli ameongea kwa ufasaha mkubwa na amewataka viongozi wenzake kuacha malumbano na matokeo yake tujenge nchi ili tuwaletee wanainchi maendeleo.
kusema kuwa ccm haifai kuongoza nchi jusa alikuwa na maana gani wakati naye pia ni kati ya hiyo serikali ambayo haifai kwahiyo hapa anadhiirisha hajui anachoongea kwani ameshajisahau kuwa naye ni sehemu ya serikali.
kuhusu swala la chadema kupinga posho lilikuwa ni swala la principal kukataa posho na waliweza kufikisha ujumbe wao na watanzania wote akiwemo maalim seif aliyewaunga mkono CDM tulisikia na kwa idadi yao ya wabunge hakuna cha ziada ambacho wangeweza kukifanya. wanaweza kususia posho lakini hiyo sio dawa kama ki sera bado posho itaendelea kutolewa cha msingi ni kubadilisha kabisa mfumo wa kulipana posho na siyo kususia kwani kususa tu hakubadilishi sheria.
kuhusu swala slaa sioni kama hoja ni mshahara kwani mzee anastahili kila senti anayolipwa na yeye ni mtu mmoja hana uwezo wa kuilazimisha kamati kuu imlipe pesa anayotaka yeye. slaa anastahili kila senti kwa maana bila yeye sidhani chama hiki kingefika hapo kilipo na wanachama wao
hasa ndio walipaswa kupiga kelele lakini kama wao wanaunga mkono mshahara huo wewe ni nani kutoka chama kingine kuja kuoji issue za CDM.