Mdahalo Shirikishi: Watanzania Waarab au Wahindi wako wapi kwenye uongozi wa taifa letu?

Mimi huwa nakereka hata ninapowaona kina rostitamu na wahindi wengineo wakiwa wabunge....potelea mbali niite mbaguzi ama la lakini kama uliwahi kwenda India au huko uarabuni ama kwa kupitia vyombo vya habari ukaona treatment ya mtu mweusi kutoka Afrika wala usingeshangaa..
 
Ndio maana nimesema kuwa nilichosema na kuandika hapo siyo kigumu hivyo; soma tu wenzio utaona wameelewa and you will catch up. Sijaandika kitu kigumu sana kuweza kufikirika... "racially minority" unaweza kuigoogle... itakusaidia kukupa picha nazungumzia nini.

Unaonesha hukijui unachokiuliza. By waarabu unamaanisha kina nani? Kwa lugha, kwa rangi? maana Uarabu si Utaifa.

Utakuwaje Mtanzania halafu uwe Mwaarabu? huo Uarabu ni nini na Utanzania ni nini? ikiwa unaongelea racial minorities, kwanini tusianze na Wahutu na Watutsi waliopo Tanzania?
 
Nimejiuliza maswali mengi sana kutokana na hoja iliyopo mezani,hawa wahindi na waarabu katika ubinafsishaji ndio wengi wao waliuziwa mashirika na viwanda mbalimbali ambavyo vingine vimekufa na vingine vimebadilishwa matumizi yake.pia hoja ya pili ni kuwa hawa jamaa tupo nao tu ila wanauraia zaidi ya nchi moja,ndio maana wahindi wengi wanaishi kwenye nyumba za NHC.

Pia jamani mlishawahi kujiuliza kuhusu waarabu ambao walishawahi kututawala enzi ya ukoloni,watu wetu wengi walisafirishwa katika soko la utumwa kupekwa nchi mbalimbali na wengine uarabuni,sehemu za ulaya na bara la amerika weusi ni wengi,je hawa watu weusi waliopelekwa nchi za kiarabu waliishia wapi?jiulizeni jamani!!

pia katika maeneo mengi ambayo wapo ndugu zetu waarabu uchumi huwa unadumaa sana mfano maeneo ya Tanga,wengi ya wenye hela ni waarabu ila ni wakandamizi kwenye ajira,kwa maana ya kuwa wanawalipa wafanyakazi wao mshahara kidogo,pia hawatoi fursa za kimaendeleo tanga haibadiliki miaka nenda miaka rudi.

Pia wahindi ajira zao ni za uonevu,maslahi kiduchu,mishahara ya upendeleo kwa maana mnaweza kuwa unafanya kazi position moja na mhindi mishahara ikawa tofauti.
 
Mnawaita Wahindi ama Waarabu kwa sababu zilizowazi kabisa. Sawa.

Kuna ugumu gani wa kuainisha sababu hizo?

Mwalimu sihitaji kufanya ligi na wewe, tuendelee na mengine kwani naona kama una nia ya kuharibu mjadala huu, inawezekana hujaupenda.

Tunapopiga kelele kila siku hapa jf wachaga, wachaga, wachaga, wachaga mbona sijawahi kukuona ukisema huo ni ubaguzi?? Mkuu una maslahi na makundi tajwa??
 
Mimi huwa nakereka hata ninapowaona kina rostitamu na wahindi wengineo wakiwa wabunge....potelea mbali niite mbaguzi ama la lakini kama uliwahi kwenda India au huko uarabuni ama kwa kupitia vyombo vya habari ukaona treatment ya mtu mweusi kutoka Afrika wala usingeshangaa..

Tupe mfano hai mmoja tu na chombo cha habari kipi na tukio lipi lilimhusu mtu mweusi huko "India" au "uarabuni". Halfu hiyo Uarabuni ndio wapi? maana hata Igunga kua Uarabuni, hata Bujumbura kuna Uarabuni.

Kuwa muwazi kidogo na uende shule ukasome tena kuuelewa Uarabu ni nini na Uhindi ni nini na Utanzania ni nini.

Inaonesha wewe na mleta mada hamjui somo la Uraia.
 
Mwalimu sihitaji kufanya ligi na wewe, tuendelee na mengine kwani naona kama una nia ya kuharibu mjadala huu, inawezekana hujaupenda.

Tunapopiga kelele kila siku hapa jf wachaga, wachaga, wachaga, wachaga mbona sijawahi kukuona ukisema huo ni ubaguzi?? Mkuu una maslahi na makundi tajwa??

Wachaga wanajulikana ni wachaga, waarabu ndio kina nani? wanatokea wapi? kumbuka kusema mwaarabu ni kama kusema mswahili, sasa wewe mwita sio mswahili?
 
MADA IMETULIA!
Mwanakijiji: Tatizo la Nchi hii siyo Rangi, Tatizo ni FIKRA mgando kwa majority, Bado watu wengi Bongo ni Bendera fuata upepo.Bado tuwavivu Wakufikiri!! Bado Viongozi wengi wanateuliwa au kuchaguliwa si kwa Uwezo wao wa kazi na uzalendo unaoweza leta tija katika nchi hii bali ni ujamaa/urafiki/undugu/ uhusiano usio rasmi/ utiifu woga/ukabila/udini n.k kweli tunao wahindi au warabu au wasomali wenye uwezo mkubwa wa kiutendaji lakini mfumo wetu utendaji umejaa UBINAFSI na WOGA.

Kuna mabo mengi ya msingi Viongozi wanayapotezea kwa mfano hivi kwanini tunadharau WALIMU hapa Tanzania, mwalimu ndio FANI inayolipwa mishahara DUNI kuliko watumishi wengine wote tunaposema mishahara maana yake ni packege anayopata mtumishi as a take Home, siyo ujanja ujanja wa wanasiasa, Walimu wanapokua nje ya Vituo vya kazi km vile kusahihisha MITIHANI ati hawalipwi Pdm km watumishi wengine wanalipwa posho as per karatasi watakazo sahihihsha hii ni Aibu kubwa na ni Ushenzi!!!

Lakini pia angalia walimu wa shule za msingi wanaokuwa na watoto wanaohitaji kujifunza wao walimu wamefaulu kwa VIGEZO vipi kuwa walimu, div.iv point 28 aibu ktk vyuo vyetu vya leo hii ELIMU NI BIASHARA hakuna mwanafunzi anaye FAIL. Kweli hivi ndivyo wanafanya wenzetu east africa?tutaweza kushinadana ktk SOKO la ajira??

Je waliopewa dhamana hawalioni hili? kama siyo ujinga!!! mwisho mi nasuport wenye mamalaka waangalie wenye uwezo wa kiutendaji, maadili na uongozi atherwise nchi itakuwa ianaongozwa kwa makundi,makundi ya ajabu ajabau ambayo yatajenga siasa za Hovyo humu nchini.
 
Unaonesha hukijui unachokiuliza. By waarabu unamaanisha kina nani? Kwa lugha, kwa rangi? maana Uarabu si Utaifa.

Utakuwaje Mtanzania halafu uwe Mwaarabu? huo Uarabu ni nini na Utanzania ni nini? ikiwa unaongelea racial minorities, kwanini tusianze na Wahutu na Watutsi waliopo Tanzania?

Yeye amechagua kuwazungumzia wahindi na waarabu, wewe unaweza kuanzisha mjadala wa wahutu na watutsi, wala hakuna shida katika hilo.
 
Our case is very unique...naona wengi wameamua kuwa wafanya biashara zaidi kuliko kwenda kwenye utumishi wa umma. Sijui madhara yake in the long run but as we move along inawezekana tukawaangalia kama vile ni "strangers".
 
Mwalimu sihitaji kufanya ligi na wewe, tuendelee na mengine kwani naona kama una nia ya kuharibu mjadala huu, inawezekana hujaupenda.

Kigugumizi cha nini sasa? Sababu zipo wazi, si mzitaje? Mnashangaza sana kusema hiki kitu kinajuulikana na kipo wazi lakini mkashindwa kutoa maelezo. Nini tatizo?

Hamuoni kuwa bila ya kuweka scope ya Mtanzania Muarabu na Mtanzania Mhindi ni nani, tunaweza kujikuta tunajadili vitu tofauti katika mada moja?

Manake kwa mwengine Salim Ahmeid Salim ni Mtanzania Muarabu wakati kwa mwengine sio.

Tunapopiga kelele kila siku hapa jf wachaga, wachaga, wachaga, wachaga mbona sijawahi kukuona ukisema huo ni ubaguzi?? Mkuu una maslahi na makundi tajwa??

Ndio yale yale ya kupangiana cha kuchangia hapa JF. Sikeshi JF kuwa kila mada itakayowekwa nitaiona na kuijadili. Sina kumbukumbu ya kuona mada ya kuwachambua Wachaga jukwaa hili la siasa, kama ipo unaweza kusaidia kumbukumbu yangu

Ahsante
 
Yeye amechagua kuwazungumzia wahindi na waarabu, wewe unaweza kuanzisha mjadala wa wahutu na watutsi, wala hakuna shida katika hilo.

Tungekuwa tunazungumzia Wahindi na Waarabu wala hakuna shida katika hilo, wanajuulikana ni watu gani na wana patikana wapi duniani.

Tunachozungumzia hapa ni Watanzania Wahindi na Watanzania Waarabu.

Hapo ndipo tunaposhindwa kuwajua watu hawa ni nani? Na rangi yao kama si nyeusi ni rangi gani?

* Mwanakijiji yeye kawaita "Waarab" ambalo hata si neno sahihi kwa Kiswahili
 
Slaa ni Mu Iraq na hakuna ubishi katika hilo tena wa asili na asili na asili. Mbona yupo kwenye siasa?

Mwaarabu Mtanzania ni yupi?

Said Arfi wa chadema ana asili ya Oman au Yemen mama yake Mnyamwezi? au Mmanyema au Msukuma, sasa huyu anakuwa Mtanzania au? tum define vipi?

Mtazania Mwarabu, kwa rangi? utaifa? lugha? unajuwa mnanichanganya mnapoleta mada ambazo ni za kibaguzi baguzi.

Moja ya "minority races" ya Tanzania ni mbirikimo, na mtu mzima (mwenye umri zaidi ya miaka 18) yeyote ambae ni chini ya futi tano ni mbirikimo, Mzee Mwanakijiji, umefika futi tano?

Talking about race is racism. You are simply a racist.
 
Yeye amechagua kuwazungumzia wahindi na waarabu, wewe unaweza kuanzisha mjadala wa wahutu na watutsi, wala hakuna shida katika hilo.

Hapan usipindishe maneno, hakuanzisha kuwazungumzia wahindi na waarabu, soma vizuri post yake: 'watanzania waarab au "watanzania wahindi".

Sasa hao Watanzania Waarab au wahindi" unawa define vipi? rangi? nywele? lugha? nationality mbili?
 
Tungekuwa tunazungumzia Wahindi na Waarabu wala hakuna shida katika hilo, wanajuulikana ni watu gani na wana patikana wapi duniani.

Tunachozungumzia hapa ni Watanzania Wahindi na Watanzania Waarabu.

Hapo ndipo tunaposhindwa kuwajua watu hawa ni nani? Na rangi yao kama si nyeusi ni rangi gani?

* Mwanakijiji yeye kawaita "Waarab" ambalo hata si neno sahihi kwa Kiswahili
Ndo kazi ya kiuwalimu hii, mpaka wakueleze nini wanazungumzia hapa wakishindwa basi thread closed
 
Mwalimu sihitaji kufanya ligi na wewe, tuendelee na mengine kwani naona kama una nia ya kuharibu mjadala huu, inawezekana hujaupenda.

Tunapopiga kelele kila siku hapa jf wachaga, wachaga, wachaga, wachaga mbona sijawahi kukuona ukisema huo ni ubaguzi?? Mkuu una maslahi na makundi tajwa??
Mkuu mjibu tu mwalimu aridhike...............
 
duuu kazi kweli kweli!!!!!!!!!

Tena si ndogo!

Said Arfi ni Mtanzania Muarabu?
Salim Ahmeid Salim ni Mtanzania Muarabu?
Mohammed Dewji ni Mtanzania Mhindi?
Said Bakhressa ni Mtanzani Muarabu?
Rostam Aziz ni Mtanzania Mhindi? Mtanzania Muarabu? Mtanzania Muajemi?

Watoto wa hao waliotajwa nao wataendelea kuwa ni Watanzania Waarabu na Watanzania Wahindi? Hadi lini? Na weusi wa rangi zao unahusikaje?
 
Back
Top Bottom