Mdahalo Shirikishi: Watanzania Waarab au Wahindi wako wapi kwenye uongozi wa taifa letu?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,996
I have written about this topic before and I feel like I need to revisit it. It seems that our country is becoming more and more homogenous when it comes to racial make up of the top echelon of our country's leadership. ALL high positions of the country are being held by the racial majority - blacks. I'm more concerned about the Union Government:

Have a Look ( I don't mind kusahihishwa kama sitakuwa sahihi katika observation yangu):

Ikulu: Rais, Makamu - wote weusi
Waziri Mkuu - Mweusi
Mawaziri wote - weusi
Manaibu Wote - weusi

Mahakama
- Majaji wote wa Mahakama ya rufani (nadhani wapo watatu ambao wamechangia damu -sasa sijui tunatumia kipimo cha damu kidogo ya mwarabu we ni mwarabu au cha Wamarekani damu kidogo ya mweusi we ni mweusi!)!
- Majaji wote wa Mahakama Kuu ni weusi (sina uhakika waliochangia)
- Mahakimu sijui (lakini predominantly ni weusi bado - nakumbuka aliwahi kuwepo hakimu mmoja Mhindi sijui kama yupo)

Bungeni
Spika na Naibu Spika - weusi
Wenyeviti wote wa Kamati za KUdumu (ziko 17) - weusi

Jeshi la Polisi
IGP - Mweusi
Makamisha 4 wa juu - weusi
Makamanda wote wa Mikoa (nadhani ukiondoa mmoja - sikumbuki) ni weusi
(zamani walikuwepo polisi wa kigoa na singasinga)

Jeshi la Wananchi
Uongozi wake wote ni weusi!
Of course baada ya uhuru walikuwepo wazungu wachache waliobakia na wengine kupigana vita ya Kagera.

Naweza kwenda mbele na mbele; Hili linaniacha na maswali fulani ya kuchokoza:

a. Yawezekana tumekuwa ni taifa la wabaguzi wa rangi kuliko tunavyoweza kukubali?
b. Ukiondoa taasisi ambazo zinapandisha vyeo kwa merit ya ndani kwa ndani (polisi na jeshi); taasisi nyingine zinapata watendaji wake kwa kuteuliwa; hivi hakuna Mtanzania yeyote ambaye ni minority ambaye anafaa kuwa jaji? Yaani, kati ya wanasheria wote (na wapo wengi tu minority) hakuna anayeweza kupewa ujaji baada ya rekodi yake kuonesha kuwa anafaa?
c. Je serikali yawezekana haina mpango wowote wa kujaribu kurecruit minorities kwenye serikali yetu? Sijawahi kuona polisi au jeshi wakijaribu kuvutia watu wa minority - kwanini wakati baada ya uhuru tulikuwepo na vijana walioingia kwenye taasisi hizo na wakapanda vyeo taratibu? Ni kweli wahindi hawawezi kazi za polisi au jeshi (huko India nani anazifanya au Pakistani)?
d. Ni kwanini racially minority hawaonekani kwenye uongozi wa juu wa taifa letu kwenye maeneo YOTE? IS THERE ARE SYSTEMATIC DISCRIMINATION GOING ON?

Ikumbukwe kuwa Tanzania ilipozaliwa ilizaliwa ikiwa na tofauti moja kubwa - rangi haikutakiwa kuwa kigezo cha mtu yeyote kupewa au kunyimwa kazi katika Tanzania kama yeye ni Mtanzania. Tulikataa kabisa ubaguzi wa rangi na Nyerere alionesha hilo kwenye Jamhuri ya Kwanza na hata baada ya Muungano. What went wrong?

What is going On? Should we care? au watu weusi wamejiaminisha kuwa wao ndio "Watanzania zaidi" ndio "wazawa" hivyo "wanastahili zaidi"? Au wapo watu wanaamini kuwa "wahindi na waarabu" walishatutawala n.k n.k n.k hivyo hawastahili? Inawezekana kuna watu ambao akichaguliwa Waziri au kiongozi wa juu mahali fulani watawakuwa kama yule aliyelia baada ya Richa Adhia kuvaa taji la Miss Tanzania?

Je kuna umuhimu wowote wa Tanzania kuhakikisha kuwa hakuna systematic discrimination au kuwaacha minority pembeni? Fikiria US kwa mfano weusi wanamake up about 12-13 percent ya population lakini leo wanaye hadi Rais mweusi! Au Wamarekani wako mbali sana katika haya mambo ya rangi?
 
hao waarabu hata wakizaliwa nchini na wakaishi na kukulia huko tanzania huwa wanajifanya sio wazawa.....hata wanavyoishi wanaisha kama sio wazawa...wazazi wao ndio wanaoshiriki kuihujumu nchi na wanasaidiana na na viongozi wa nch kula mali za watanzania kwa njia haramu wao(waarabu na wahindi) wakiwa wamejificha chini ya mwamvuli wa ''wafanya biashara'' ...kushika nafasi serikali kuko wazi lakin hawapendi ...zamani mwalimu aliwatumia hasa wahindi kwenye serikali lakini kwa wakati huu wengi wao wamejikita katika ''wizi''
 
am not sure kama kuwajaza watu weupe ili mradi tuonekane nasisi tunajali watu wa asili nyingine ni solution.

whats matter here is qualification and experience? mfano mdogo

kila mtanzania (nasisitiza mtanzania either kwa kuzaliwa au kuomba uraia) anahaki ya kuteuliwa kuwa mgombea wa URAIS but hakuna hata mmoja (either mhindi, mwarabu etc) aliyejitokeza kuchukua fomu katika vyama vya siasa, sasa sie tufanye nini?? tukawabebe kariakoo tuwalazimishe wajaze form ili wawe marais???

mbona watu wengi wenye asili ya kiarabu, (kina rostam) wapo bungeni ? (au hilo nalo hujaliona??), mi nadhani hatuna haja ya kufanya jambo kuonekana tunajali watu wa aina nyingine, NO!! cha msingi ni qualifications za mtu na uwezo wake wakufanya kazi. Hebu niambie ni watu wangapi wenye asili ya kiarabu au kichina au kihindi wapo maofisini?? (obvious ni wachache sana), na sababu kubwa ni kwamba wengi wao uwezo wao sio mkubwa sana, (wengi wamekuja fanya biashara tuu huku)

Wengi ya watu weupe (asili za magharibi) ambao wanauraia wa Tanzania ni waarabu, wahindi sasa wengi ya watu hawa wamekaa kibiashara biashara tuuu.

Kwa hiyo sidhani kama kuna ulazima sana eti kwasababu wamarekani wamepata Rais mweusi na sisi tu-force kupata viongozi wajuu wenye ngozi nyeupe..

bora waaarbu kiasi flani,tunaishi nao uswahilini na tunashirikiana nao kwenye shuguli mbalimbali,wahindi ni wabaguzi sana,unakuta mhindi kazaliwa agha khan lakini kiswahili hajui vizuri.,hawana uzalendo wengi wao,pesa zao zinawekwa kwenye benki za nje(india,canda,uk)
uzalendo wao kwa nchi ya india kwanza halafu bongo inafatia
 
Mifumo yetu na fikra za watawala ndani ya tanzania inasababisha minority wengi kubakuliwa katika taasisi fulani na hii pia imeenda mbali sana hadi kwa. Citizen wa kawaida kuwaona wahindi na waarabu kama kundi la mafisadi na wahujumu uchumi wakati siyo kweli
 
Kabla ya kutoa michango tungependa kufahamishwa yafuatayo:-

1. Watanzania Waarabu na Wahindi ndio Watanzania gani? Wana sifa gani?

2. Inaonyesha kuwa tathmini yako iliangalia rangi, mweusi Vs ???...Mtu asiyehesabika kuwa mweusi ni mwenye sifa ipi? Rangi yake kuanzia hue gani ndio anakuwa sio mweusi tena?
 
Nadhani hao minority ndio wanapaswa kuonyesha utayari wao katika kushiriki nafasi za uongozi wa juu ndani ya nchi yetu, na katika kuonyesha utayari wa kutaka kushiriki uongozi wa nchi yetu lazima waonyeshe kweli kwamba wao ni watanzania kwanza kabla ya uhindi wao ama uarabu wao.
Ikiwa wataendelea kujiona kwamba wao ni wahindi kwanza, ama waarabu kwanza, sidhani kwamba kutakuwa na ulazima wa kuwajumuisha katika nafasi za juu za uongozi wa nchi, achilia mbali nafasi nyenginezo za utumishi wa umma.

Chukulia mfano, kama hawajitokezi kuomba kujiunga na majeshi yetu JWTZ, Police, Magereza, Zimamoto sidhani kama kuna mtu wa kulaumiwa katika hilo zaidi ya wao wenyewe. Kwamba haitawezekana ateuliwe kuwa CDF, ama IGP ama kamishna wa magereza au Zimamoto ilihali hakuna yeyote toka kundi la minority aliyeajiriwa ndani ya majeshi hayo.

Hawa wenzetu wamejikita zaidi kwenye biashara, sasahivi ndio wameanza kuchangamkia kwa wingi sana siasa kwakuwa kwa kupitia huko wanapata unafuu wa kufanya dili zao kiurahisi kwakuwa wako ndani ya chama tawala.
Na kama nilivyotaja hapo awali kwao utanzania ni utaifa wa pili, sasa kama ni ubaguzi basi wao wenyewe ndio wanaojibagua.
 
Kabla ya kutoa michango tungependa kufahamishwa yafuatayo:-

1. Watanzania Waarabu na Wahindi ndio Watanzania gani? Wana sifa gani?

2. Inaonyesha kuwa tathmini yako iliangalia rangi, mweusi Vs ???...Mtu asiyehesabika kuwa mweusi ni mwenye sifa ipi? Rangi yake kuanzia hue gani ndio anakuwa sio mweusi tena?

Nilichokiandika wala siyo kitu kigumu kihivyo...
 
Nadhani hao minority ndio wanapaswa kuonyesha utayari wao katika kushiriki nafasi za uongozi wa juu ndani ya nchi yetu, na katika kuonyesha utayari wa kutaka kushiriki uongozi wa nchi yetu lazima waonyeshe kweli kwamba wao ni watanzania kwanza kabla ya uhindi wao ama uarabu wao.
Ikiwa wataendelea kujiona kwamba wao ni wahindi kwanza, ama waarabu kwanza, sidhani kwamba kutakuwa na ulazima wa kuwajumuisha katika nafasi za juu za uongozi wa nchi, achilia mbali nafasi nyenginezo za utumishi wa umma.

Kwako wewe Mtanzania Mhindi au Mtanzania Muarabu ni yupi?

Kwa wengine hii kukaa tu ukamwita mtu kwa kuongezea suffix mbele ya uraia wake ni sifa moja wapo ya ubaguzi na kuwabagua

Mbona hatukai hata siku moja tukaanza kutaja Watanzania Wachaga wala Watanzania Wasukuma?
 
kuna topic ilikuwa hapa jana ikilaumu waarabu wa iringa kwa kuwakandamiza watanzania wenzetu ,labda tujue waarabu na wahindi hawapo hapa kwa kushiriki na kutatua matatizo yetu,ndio maana wengi wao wana uraia wa nchi mbili,mkianza kutoana damu hawapo!!wanachotaka ni hela zetu na raslimali kama walivyoiba meno ya tembo miaka ya nyuma wakati baba zetu wamelala
 
Nilichokiandika wala siyo kitu kigumu kihivyo...

Ni kigumu hivyo.

Kama unataka tukae tujadili kundi la watu fulani, basi ni lazima tuanze kwa kuwajua hao watu tunaowajadili wana sifa gani.

Kama hatujui sifa zao tutajadili vipi? Tutajuaje kama kweli hawapo kwenye nafasi za uongozi au wapo wakati hatujui sifa zao?
 
Ndio maana nimesema kuwa nilichosema na kuandika hapo siyo kigumu hivyo; soma tu wenzio utaona wameelewa and you will catch up. Sijaandika kitu kigumu sana kuweza kufikirika... "racially minority" unaweza kuigoogle... itakusaidia kukupa picha nazungumzia nini.
 
Hujaandika kitu kigumu kuwa hakifikiri, ulichoandika ni kitu kisicho na mashiko.

Utaanzaje kujadili kundi la watu bila ya kujua definition yao wala scope yako ikoje?

Sina cha kujifunza kutoka kwa hao walichangia maana umuulize mmoja wao hana jibu la Mtanzania Muarabu wala Mtanzania Mhindi ni nani kama ulivyokosa wewe

Salim Ahmeid Salim ni Mtanzania Muarabu?
 
Katika mazingira hayo unaiacha mada tu na kuendelea na mada nyingine ambazo umezielewa; nalo si gumu kulifanya.
 
Kwako wewe Mtanzania Mhindi au Mtanzania Muarabu ni yupi?

Kwa wengine hii kukaa tu ukamwita mtu kwa kuongezea suffix mbele ya uraia wake ni sifa moja wapo ya ubaguzi na kuwabagua

Mbona hatukai hata siku moja tukaanza kutaja Watanzania Wachaga wala Watanzania Wasukuma?

Sidhani kama hili ni gumu kiasi hicho kulielewa, unless uniambie unatafuta ligi isiyokuwa na sababu zozote za msingi.

Mtanzania Mchaga, Mkurya, Msukuma ama Mzaramo ni Mtanzania tofauti kabisa na Mtanzania Mhindi ama Mtanzania Muarabu. Hiyo suffix hiyo unayoisema ina maana kubwa sana, sio kwa nia ya kuwabagua lakini huo ndio ukweli wenyewe.

Na kama hatutaki kuukubali huu ukweli kwamba tuna watanzania wenzetu ambao tunawaita wahindi ama waarabu kwa sababu zilizo wazi kabisa, basi hilo ni jaribio la dhahiri la kuukana ukweli na kutokuwa tayari kuukabili na kurekebisha pale tunapoona pana mapungufu.
 
Mimi nafikiri hao ni raia waadilifu wanaofuata ushauri wa viongozi wetu. "Watanzania kujikite zaidi kwenye kujiajiri tusitegemee serikali kwa kila kitu, Vijana ni VIONGOZI WA KESHO, tuachane na siasa kwa sasa.
 
Na kama hatutaki kuukubali huu ukweli kwamba tuna watanzania wenzetu ambao tunawaita wahindi ama waarabu kwa sababu zilizo wazi kabisa, basi hilo ni jaribio la dhahiri la kuukana ukweli na kutokuwa tayari kuukabili na kurekebisha pale tunapoona pana mapungufu.

Mnawaita Wahindi ama Waarabu kwa sababu zilizowazi kabisa. Sawa.

Kuna ugumu gani wa kuainisha sababu hizo?
 
Back
Top Bottom