Mdahalo Shirikishi: Watanzania Waarab au Wahindi wako wapi kwenye uongozi wa taifa letu?

Mwalimu sihitaji kufanya ligi na wewe, tuendelee na mengine kwani naona kama una nia ya kuharibu mjadala huu, inawezekana hujaupenda.

Tunapopiga kelele kila siku hapa jf wachaga, wachaga, wachaga, wachaga mbona sijawahi kukuona ukisema huo ni ubaguzi?? Mkuu una maslahi na makundi tajwa??

Mwita Gaijini ni muhindi koko wa kkoo ndomana anatetea makundi tajwa!
 
Hapan usipindishe maneno, hakuanzisha kuwazungumzia wahindi na waarabu, soma vizuri post yake: 'watanzania waarab au "watanzania wahindi".

Sasa hao Watanzania Waarab au wahindi" unawa define vipi? rangi? nywele? lugha? nationality mbili?

Hakuna cha kupinda hapo, nilikuwa natoa ufafanuzi wa hoja yako uliyokuwa umeizua kutaka na wengine nao wajadiliwe, nadhani unaona mwenyewe ulichoandika hapo chini.

Unaonesha hukijui unachokiuliza. By waarabu unamaanisha kina nani? Kwa lugha, kwa rangi? maana Uarabu si Utaifa.

Utakuwaje Mtanzania halafu uwe Mwaarabu? huo Uarabu ni nini na Utanzania ni nini? ikiwa unaongelea racial minorities, kwanini tusianze na Wahutu na Watutsi waliopo Tanzania?
 
wao wenyewe wanatubagua, ma binti zao hawataki kuolewa na ngozi nyeusi hasa wa indi ndo usiseme. Utakuta binti atakuta binti yupo tayari kuolewa hila wazazi hawataki kabisa, wannasema eti " watachafua mbegu".

haya mambo mengine ni sifa za mtu tu, wapo kina profesa shivdi UDSM na wengine wengi wapo serekalini. Wakijitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali mimi naamini watachaguliwa, au wanaweza kuteuliwa kutokana na jinsi wanavyo jituma. chakusikitisha zaidi wao wenyewe wanatutenge na kuunda kundi lao la watu wa Asia.
 
Angalia kwanza uwiano wa watanzani weusi na wale weupe mfano warabu na wahindi katika idadi. Je, mwarabu mmoja anaweza kuwakilisha watanzania wangapi? Na muhindi vile vile. Watanzania weusi wako wengi sana. Kwa upande wa U.S.A Huwezi kulinganisha na huku kwani kule watu weusi ni wengi sana kulinganisha na idadi ya warabu na wahindi wa tz.
 
Tena si ndogo!

Said Arfi ni Mtanzania Muarabu?
Salim Ahmeid Salim ni Mtanzania Muarabu?
Mohammed Dewji ni Mtanzania Mhindi?
Said Bakhressa ni Mtanzani Muarabu?
Rostam Aziz ni Mtanzania Mhindi? Mtanzania Muarabu? Mtanzania Muajemi?

Watoto wa hao waliotajwa nao wataendelea kuwa ni Watanzania Waarabu na Watanzania Wahindi? Hadi lini? Na weusi wa rangi zao unahusikaje?
hahahaha kazi ipo hapa
 
Kwa mtazamo wangu watu wenye asili ya uarabu Tanzania wanajihesabu kama WATANZANIA kwanza then waarab second. Kwa upande wa wahindi tuna tatizo kubwa, ni wahindi kwa maana ya foreigners kwanza halafu -wasafiri walioko Tanzania kwa muda second. Ni wahindi wachache mno wanajihesabu kama watanzania. Wengine wote utafikiri wako safarini kuelekea somewhere else.

Ni vigumu sana kwa mtu kuzaliwa i.e France, aishi maisha yake yote France,lakini ashindwe kuongea kifaransa! Wahindi wengi wamezaliwa hapa Tanzania lakini hata kuongea kiswahili imekuwa shida. Wanajitenga, wanaona kama wako hapa kimakosa? Kama mtu haonekani kuwa 'sincere' utampa madaraka kwa nini?

Nadhani siko peke yangu kusema kuwa Wahindi wa sasa (general statement) wamejijengea reputation ya kuhujuma Tanzania. Ni tofauti na wahindi wakati wa Uhuru. Sijui huu mkakati ulianza lini na nani aliulea lakini imani kwa wahindi imekuwa ndogo kwa sababu hawaonekani kabisa kutaka kukaa karibu na watanzania wengine. Nilifikiri miaka 50 baada ya uhuru Uhindi ungehesabika kama kabila, kama ilivyo i.e mpare, mdengereko. Lakini wako kama expats. Na huko tunakoenda mambo yanazidi kuwa mabaya zaidi. Wahindi aina ya Mzee Sabodo ni nadra sana! Very unfortunate.
 
Tungekuwa tunazungumzia Wahindi na Waarabu wala hakuna shida katika hilo, wanajuulikana ni watu gani na wana patikana wapi duniani.

Tunachozungumzia hapa ni Watanzania Wahindi na Watanzania Waarabu.

Hapo ndipo tunaposhindwa kuwajua watu hawa ni nani? Na rangi yao kama si nyeusi ni rangi gani?

* Mwanakijiji yeye kawaita "Waarab" ambalo hata si neno sahihi kwa Kiswahili

Hapo nilitaja wahindi na waarabu moja kwa moja kwa sababu nilikuwa namjibu ribosome katika hoja yake ya wahutu na watutsi.

Kama MMKJJ amekosea kuwaita waarab, inaweza kuwa kweli lakini hiyo haibadilishi content ya kinachozungumzwa hapa.
 
wao wenyewe wanatubagua, ma binti zao hawataki kuolewa na ngozi nyeusi hasa wa indi ndo usiseme. Utakuta binti atakuta binti yupo tayari kuolewa hila wazazi hawataki kabisa, wannasema eti " watachafua mbegu".

haya mambo mengine ni sifa za mtu tu, wapo kina profesa shivdi UDSM na wengine wengi wapo serekalini. Wakijitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali mimi naamini watachaguliwa, au wanaweza kuteuliwa kutokana na jinsi wanavyo jituma. chakusikitisha zaidi wao wenyewe wanatutenge na kuunda kundi lao la watu wa Asia.

Hata wamasai hawataki binti zao waolewe na wabantu (wafupi, wana pua pana) watachafuwa mbegu. Au hujui hilo?
 
Hapo nilitaja wahindi na waarabu moja kwa moja kwa sababu nilikuwa namjibu ribosome katika hoja yake ya wahutu na watutsi.

Kama MMKJJ amekosea kuwaita waarab, inaweza kuwa kweli lakini hiyo haibadilishi content ya kinachozungumzwa hapa.

Watanzania Waarabu, hebu wa define pachanga za nini? halafu hata hilo jina lako linaonesha na wewe una asili ya nje ya Tanzania, sijui tukuiteje? Mtanzania Mtutsi? au Mtanzania Mwaarabu?
 
Hakuna cha kupinda hapo, nilikuwa natoa ufafanuzi wa hoja yako uliyokuwa umeizua kutaka na wengine nao wajadiliwe, nadhani unaona mwenyewe ulichoandika hapo chini.

"Watanzania Waarab" na sika kama ulivyotaka wewe ifahamike kuwa ni Waarabu. Ndio wepi hao?
 
Hata wamasai hawataki binti zao waolewe na wabantu (wafupi, wana pua pana) watachafuwa mbegu. Au hujui hilo?

Robisome siyo kweli, jokes aside, nafahamu watu wengi sana ambao mama ni mmasai lakini baba ni mmbantu.
 
Ubishi mwingine bana
Sasa si ni Mtanzania Mwarabu alafu kuna Mtanzania Mhindi
 
Kwako wewe Mtanzania Mhindi au Mtanzania Muarabu ni yupi?

Kwa wengine hii kukaa tu ukamwita mtu kwa kuongezea suffix mbele ya uraia wake ni sifa moja wapo ya ubaguzi na kuwabagua

Mbona hatukai hata siku moja tukaanza kutaja Watanzania Wachaga wala Watanzania Wasukuma?

a. Yawezekana tumekuwa ni taifa la wabaguzi wa rangi kuliko tunavyoweza kukubali?
b. Ukiondoa taasisi ambazo zinapandisha vyeo kwa merit ya ndani kwa ndani (polisi na jeshi); taasisi nyingine zinapata watendaji wake kwa kuteuliwa; hivi hakuna Mtanzania yeyote ambaye ni minority ambaye anafaa kuwa jaji? Yaani, kati ya wanasheria wote (na wapo wengi tu minority) hakuna anayeweza kupewa ujaji baada ya rekodi yake kuonesha kuwa anafaa?
 
Sasa unataka kunipangia cha kufanya?

Nauliza tena Mtanzania Muarabu na Mtanzania Mhindi ni nani?

Ahsante
Kama hujaelewa mtanzania muarabu na mtanzania mhindi basi nenda chit chat kuna mada za wewe kuchangia......
 
Robisome siyo kweli, jokes aside, nafahamu watu wengi sana ambao mama ni mmasai lakini baba ni mmbantu, mimi mwenyewe mmojawapo.

Na mimi nafahamu wengi sana ambao mama ni muhindi baba ni mbantu. Mmoja wapo ni maarufu sana, kwa jina Kinje Kingunge Ngombale Mwiru. Na pia nawafahamu wengi zaidi ambao ni wa asili za Oman, Yemen lakini mama au baba zao ni wabantu au wamasai au wanyamwezi au wanyalukolo.

Wapo na si odd ni very common Tanzania. Said Arfi? Zakia Meghji? Shamim Khan? Zahra Nuru? Dokta Slaa?
 
Watanzania Waarabu, hebu wa define pachanga za nini? halafu hata hilo jina lako linaonesha na wewe una asili ya nje ya Tanzania, sijui tukuiteje? Mtanzania Mtutsi? au Mtanzania Mwaarabu?

Chagua mwenyewe, kama mimi ni mtanzania muhindi ama mtanzania mtutsi. Kwa namna mnavyojaribu kupiga danadana hapa, sina shaka kwamba wewe una maslahi na makundi tajwa. Jambo la muhimu ni kubadilika na kuweka utanzania mbele kama mnajithamini na kuithamini nchi yenu, lakini mkiendelea kujitenga, msijekumlaumu yeyote mbele ya safari.
 
Na mimi nafahamu wengi sana ambao mama ni muhindi baba ni mbantu. Mmoja wapo ni maarufu sana, kwa jina Kinje Kingunge Ngombale Mwiru. Na pia nawafahamu wengi zaidi ambao ni wa asili za Oman, Yemen lakini mama au baba zao ni wabantu au wamasai au wanyamwezi au wanyalukolo.

Wapo na si odd ni very common Tanzania. Said Arfi? Zakia Meghji? Shamim Khan? Zahra Nuru? Dokta Slaa?
mkuu! mama yake Kinje siyo muhindi! ni chotara wa Kigiriki na Mhaya Mweusi toka Kamachumu huko Kagera.
 
Back
Top Bottom