MDAHALO: M4C, Hatima ni Mageuzi au Mapinduzi?

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI

Ingawa huu ni mdahalo, kuna mambo kadhaa muhimu ambayo yanahitaji kuwekwa sawa ili kuepuka upotoshwaji wa hoja. Hivyo nitaomba uvumilivu kidogo. Taifa lipo ndani ya mjadala kali juu ya UMMA WA WATANZANIA NA KIU YA MABADILIKO. Ni dhahiri kwamba mjadala huu umezidi kupanda joto baada ya ujio wa M4C.

Suala la UMMA WA TANZANIA Kuwa na kiu ya mabadiliko halina mjadala tena, badala yake, mjadala sasa ni juu ya AINA ya Mabadiliko ambayo Umma unayahitaji, kuelekea 2015. Kwa mujibu wa wanafalsafa na wanazuoni mbalimbali, Mabadiliko katika taifa hutokea kwa njia kuu mbili ambazo ni: MAGEUZI au MAPINDUZI. Swali linalofuata ni je:

UMMA wa Tanzania Leo Una Kiu ya Mabadiliko ya Aina Gani?

Ni matumaini yangu kwamba Mdahalo huu utatupatia mwanga zaidi juu ya swali hili muhimu. Yafuatayo ni mambo makuu manne yaliyonipa hamasa ya kuja na mdahalo huu:

1. Kwanza, hisia inazidi kujengeka ndani ya jamii kwamba tunavyozidi kuelekea 2015, REACTION YA ‘DOLA' kwa M4C inazidi kuwa Counter – Revolutionary, kama vile tayari vuguvugu la mapinduzi limeanza Tanzania – kwa mfano rejea sakata la Mwangosi, na Mauaji ya Songea, Arusha na Morogoro; Hii imepelekea wananchi wengi kuwa na hisia kwamba kwa mwendo huu, hatima ya M4C inaweza kuwa ni "MAPINDUZI", kutegemeana na jinsi mwitikio wa UMMA kwa M4C, utavyoendelea kujengeka kuelekea 2015.

2. Pili, ni kauli za viongozi kadhaa wa Chadema dhidi ya mfumo wa utawala wa CCM na Serikali yake pamoja na mapungufu na madhaifu mengi yaliyopo yanayopelekea madhara kadhaa kwa watanzania walio wengi. Baadhi ya kauli za viongozi wa Chadema zinazidi kutoa hamasa kwa UMMA kwamba Mabadiliko ya Kweli yatapatikana iwapo CCM sio tu kwamba itaondolewa madarakani lakini pia iwapo CCM itazikwa moja kwa moja kwenye "Political Graveyard ya Tanzania". Kwa mfano, ni kawaida kusikia wananchi wengi wakinena kwamba: Bila ya kuiondoa CCM 2015 na kuizika moja kwa moja, Ukombozi kwa Watanzania itaendelea kuwa ni ndoto. Wananchi wanaojenga hoja kwamba CCM iendelee kuwepo baada ya 2015 pia wapo, lakini wengi ni wanachama wa CCM, sio Wapiga kura huru.

3. Tatu, ni mtazamo wa ‘elites' in Tanzania – hii ni sehemu ya watanzania (wa nje na ndani ya nchi) ambayo ina "enjoy Superior intellectual, Social & Economic Status" kutokana na viwango vyao vya elimu, exposure, access to wealth n.k.; Wengi ya Watanzania wa tabaka hili wana mtazamo wa ‘KIMAPINDUZI' kuliko ‘KIMAGEUZI' – kwa maana ya kwamba, hawaizungumzii CCM kama chama cha upinzani kitarajiwa bali Chama marehemu kitarajiwa. Ikumbukwe kwamba katika taifa lolote maskini kama Tanzania, tabaka hili lina ‘influence' kubwa sana kwenye jamii, hasa ikizingatiwa kwamba sehemu kubwa ya jamii yetu ni predominantly POOR & IGNORANT/maskini na wajinga;

4.
Na Nne, ni UMMA kwa ujumla: Sehemu kubwa ya UMMA inayounga mkono M4C kwa sasa ipo katika State of Confusion, hasa katika kubaini malengo na hatima ya M4C kwa ujumla wake. Wengi wanajiuliza: Juu ya hatima ya M4C; na juu ya mbinu zinazohitajika kuleta mabadiliko, hasa ikizingatiwa kwamba Tanzania imekuwa katika mageuzi ya aina mbalimbali yenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi, tangia mwaka 1986, huku wananchi wengi wakiendelea kulalamika kwamba hawaoni faida ya maana ya mageuzi haya;

Wanafalsafa,Mageuzi na Mapinduzi:

  • ARISTOTLE:
"Poverty is the Parent of Revolution and Crime"

  • ISAIAH BERLIN:
"Injustice, Poverty, Slavery, Ignorance – they may be cured by REFORM or REVOLUTION. But men do not live only by fighting evils. They live by positive goals, individual and collective, a vast variety of them, seldom predictable, at times incompatible".

Viongozi Wetu na Umuhimu wa Mabadiliko Tanzania:


  • MWALIMU NYERERE [in Shivji, Issa: Critical Elements of a New Democratic Consensus in Africa, 2000]:

["To be sure, you few Waswahili, do you really expect to rule Tanzanians through coercion, When there is no hope, and then expect that they will sit quiet in peace? Peace is born of hope, when hope is gone, there will be social upheavals. I'd be surprised if these Tanzanians refuse to Rebel, why? When the majorities don't have any hope you are building a volcano. It is bound to erupt one day. Unless these people are fools (wapumbavu). Many in these countries are fools, to accept being ruled just like that. To be oppressed just like that when they have the force in numbers, they are fools (wapumbavu). So Tanzanians would be fools (wapumbavu), ****** (mazuzu), if they continue to accept to be oppressed by minority in their own country. Why?"].


  • PROFESSOR ANNA TIBAIJUKA [Hansard Julai 12, 2012, akijibu hoja za wabunge].

"…Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nimesimama hapa kuomba trust, lazima tu-build trust. Popote pale nilipopita, nimekuta mahali ambapo kuna trust. Kama hakuna trust; kama sasa hivi we cannot do a permanent election.

Uchaguzi ulishaisha na tunatekeleza Ilani ya CCM. Kwa hiyo, lazima tu-build trust, tuko kwenye nyumba moja. Kama kifo au vurugu; wengine mnasemasema vurugu lakini vurugu tunasema ni ultimate revere. Mbele ya vurugu we are all equal. Ikitokea vurugu hapa kila mtu anabeba
sanduku anakimbia bila kujali ulikuwa opposition au kwenye Serikali kila mtu ni mkimbizi. Kwa hiyo, tusifike hapo na wote hapa ndani ya nyumba hii bila kujali upo chama gani we are all reformers.

Mheshimiwa Naibu Spika, asubuhi katika kuchangia alizungumzia about revolution. Yes, agrarian revolutions, that's what makes revolutions. If you fail agrarian reform a revolution is guaranteed. Yaani ukishindwa kumiliki ardhi, utapata mapinduzi kwa sababu ya ardhi. Katika hili Mheshimiwa Tundu Lissu amesema kama ilivyo. Lakini ukiwa ndani ya nyumba hii ya Bunge wewe si revolutionary, wewe ni reformer. Ndiyo maana tuko Bungeni. Hakuna revolutionary hapa. Sisi ni reformers, tuko hapa tunajaribu kuweka mambo yawe mazuri. Tunachangiana mawazo, tuna-add value."
******

SEHEMU YA PILI: MAANA YA MAGEUZI

Mageuzi ni mabadiliko yenye nia ya kuboresha mfumo uliopo, lengo kuu ikiwa ni kurekebisha mfumo ambao hautendei HAKI Raia, kurekebisha mfumo usiojibu kikamilifu mahitaji ya wananchi (umma), na kuondokana matumizi mabaya ya MADARAKA na RASILIMALI za Umma.

Muhimu:

  • Tofauti na Mapinduzi, Mageuzi YANALENGA KUBORESHA MFUMO ULIOPO, SIO KUONDOA MFUMO ULIOPO.

MAGEUZI NCHINI TANZANIA

Tanzania imekuwa katika mageuzi makuu ya aine NNE, yenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi, BILA YA KUONDOA MFUMO ULIOPO – Soko Huria, Ubepari, pamoja na mahusiano katika uzalishaji na umiliki wa mali ndani ya jamii.

1. MAGEUZI YA KIUCHUMI
Kwanza ni mageuzi ya kiuchumi. Haya yalianza Mwaka 1986 chini ya usimamizi wa Benki ya Dunia na Mfuko wa Kimataifa wa Fedha baada makubaliano baina ya serikali na taasisi hizi kwamba Sera ya Ujamaa na Kujitegemea ilikuwa inaligharimu taifa na wananchi kiuchumi. Mageuzi haya yalilenga na bado yanalenga kurekebisha the "MACRO ECONOMIC FUNDAMENTALS", hasa maeneo katika maeneo yafuatayo:

  • Kukuza pato la Taifa; Kuongeza kasi ya kukua kwa uchumi; Kudhibiti deni la umma/Taifa; Kurekebisha riba katika taasisi za kifedha ili ziendane na nguvu ya soko; Kudhibiti mfumuko wa bei; Kuboresha biashara ya ndani na nje ya nchi; Kuboresha uzalishaji wa Sekta mbalimbali muhimu kwa uchumi wa taifa; Kuboresha mazingira ya Uwekezaji ili kuvutia mitaji toka ndani na kutoka nje ya nchi; & Kuimarisha Akiba ya taifa, n.k.

Muhimu:

  • Chini ya Mageuzi haya ya KIUCHUMI, lengo kuu ni kuboresha hali za maisha ya watanzania kwa imani kwamba kazi hii inaweza kufanikiwa zaidi chini ya mfumo wa UBEPARI & SOKO HURIA, Kuliko Mfumo wa UJAMAA.

2. MAGEUZI YA KISIASA
Pili ni mageuzi ya KISIASA. Mageuzi ya KISIASA yaliingia Tanzania miaka ya mwanzo ya tisini baada ya tume ya Nyalali kumaliza kazi yake ya kutathmini hali ya demokrasia nchini. Katika ripoti yake, Tume ya Nyalali ilikuja na mapendekezo mbalimbali yaliyopelekea kurudishwa tena kwa DEMOKRASIA YA MFUMO WA VYAMA VINGI, huku pia ikipendekeza mambo mengine muhimu yenye kulenga kuboresha Demokrasia Tanzania kama vile Mabadiliko ya Katiba ya nchi (1977) ambayo kwa kiasi kikubwa bado yalikuwa yanaipa CCM hatamu, kuimarisha Utawala wa sheria, Kutenganisha wa mihimili ya dola n.k.

3. MAGEUZI YA SEKTA YA UTUMISHI WA UMMA
Tatu ni mageuzi ya Sekta ya UMMA. Kazi ya Sekta hii ni kuhudumia Jamii. Hapa ndipo uhusiano baina ya Serikali na UMMA upo ‘established'. Kwa kawaida, watumishi wote wa umma huajiriwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za ajira, lakini muhimu zaidi, kwa kuzingatia sifa walizonazo na katika mazingira ya ushindani; Utumishi wa UMMA hau usishi majeshi yetu ya ulinzi na usalama ingawa hata katika majeshi yetu kuna raia wachache wenye ajira kama watumishi wa UMMA. Sekta muhimu katika utumishi wa UMMA ni pamoja na zile za Elimu, Afya, Uhamiaji, Kilimo, Mifugo, Maji, Miundombinu, Ardhi, Benki Kuu, Mamlaka ya Kodi (TRA), n.k.

Lengo kuu la kuleta Mageuzi YA SEKTA YA UTUMISHI WA UMMA ni kuboresha maisha ya wananchi kwa njia kama vile:

  • Kuongeza efficiency (ufanisi) katika utoaji huduma za jamii; Kuongeza effectiveness katika utoaji wa huduma za jamii; Kujenga dhana ya professionalism katika utoaji wa huduma za jamii; Kujenga dhana ya uwajibikaji, n.k.

Ili kufanikiwa katika haya, Mageuzi haya pia hulenga:

  • Kupunguza mianya ya rushwa; Kuboresha usimamizi wa rasilimali watu; Kuboresha mishahara ya watumishi wa umma kama njia ya kuwaongezea motisha kiutendaji; Kujenga mazingira ya transparency (uwazi); Kujenga nidhamu, hasa ya matumizi ya fedha za walipa kodi (fiscal discipline), n.k.

4. MAGEUZI KATIKA USIMAMIZI WA FEDHA ZA UMMA
Na Nne ni mageuzi katika Sekta ya Usimamizi wa Fedha za Umma. Mageuzi haya yanaenda sambamba na yale ya sekta ya utumishi wa UMMA, lakini haya hulenga zaidi:

  • Kuimarisha mfumo wa fedha za umma ili kuzidisha uwazi (transparency), kuimarisha uwajibikaji, kuboresha ‘responsiveness' ya "MATUMIZI YA UMMA" dhidi ya "MAHITAJI YA UMMA"; kuthibiti ufujaji wa fedha za umma; Kuimarisha uwajibikaji; kuboresha mchakato wa maandalizi wa bajeti za serikali; Kuboresha maandalizi ya sera yaendane na mahitaji ya UMMA; Kuboresha Mfumo wa fedha serikalini/Integrated Financial Management Systems; Kuhimiza matumizi ya TEKNOHAMA katika kuboresha maamuzi ya ki-sera na pia katika utoaji wa huduma za jamii (e.g. e-government/e-governance); Kuimarisha mapato ya serikali; Kusimamia na kuthibiti manunuzi ya umma; Kusimamia na kuthibiti deni la umma n.k;

Ina aminiwa kwamba Mageuzi haya yatapelekea mambo makuu matatu: KWANZA, kuimarisha The ‘Macro Economic Fundamentals' tulizokwisha ziona; PILI, Serikali itaweza kutoa huduma bora zaidi za jamii na kwa ufanisi zaidi; na TATU, maisha ya wananchi yataboreshwa, hivyo umaskini kupungua;

SEHEMU YA TATU: DHANA YA MAPINDUZI

Dhana ya mapinduzi inaweza kuangaliwa kwa njia mbalimbali. Nitajaribu kuijadili katika mazingira ambayo yenye uhusiano wa moja kwa moja na mdahalo huu;

MAANA YA MAPINDUZI

Kwa kifupi, Mapinduzi ni mabadiliko makubwa katika mpangilio na uendeshaji wa maisha ndani ya jamii husika. Mara nyingi mapinduzi hupelekea mabadiliko makubwa ya mfumo mzima wa mahusiano ya jamii, kisiasa, kiuchumi, na mara nyingine kiutamaduni. Mapinduzi hutofautiana kwa:

  • Mbinu;
  • Muda/Duration kufanikisha mapinduzi; na
  • Msukumo/hamasa, mfano kiitikadi n.k;

Kuna aina nyingi za mapinduzi, lakini nitajadili zaidi mapinduzi ya kisiasa na mapinduzi ya kijamii:

  1. Mapinduzi ya Kisiasa: Haya yanalenga kuondoa kwa nguvu (nje ya utaratibu wa KIKATIBA) serikali iliyopo madarakani pamoja na mfumo mzima wa dola; Lengo kuu la mapindizu ya kisiasa huwa ni kuondokana na utawala wa kidikteka, utawala usioheshimu Demokrasia na haki za raia, utawala wa kifisadi unaonufaisha wachache na kuumiza walio wengi, n.k. Mara nyingi mapinduzi ya kisiasa uambatana na machafuko na umwagaji mkubwa wa damu;

MUHIMU

  • Mara nyingi, Mapinduzi ya KISIASA hulenga tu kuondoa serikali iliyopo madarakani pamoja na mfumo mzima wa dola LAKINI HAYAGUSI mahusiano yaliyopo ndani ya jamii, hasa katika uzalishaji na umiliki wa mali; Mfano mzuri wa mapinduzi ya namna hii ni yale ya Ufaransa (1789) na mengine mengi, ambapo dola iliyopo madarakani uangushwa lakini mahusiano katika Uzalishaji na Umiliki wa mali hubaki kama yalivyo;

2. Mapinduzi ya Kijamii: Hii ni aina ya pili ya Mapinduzi ambayo huwa na madhara makubwa zaidi katika jamii husika na huwa ya aina mbili kuu:

  • Kwanza – ni Yale ambayo ni BOTTOM – UP - yanaendeshwa zaidi na nguvu ya UMMA (tofauti na yale ambayo ni more 'top – down'). Mfano mzuri ni mapinduzi yaliyotokea Afrika ya Kaskazini hivi karibuni.
  • Pili ni yale ambayo ni TOP – BOTTOM – yanayoongozwa zaidi na certain personalities, na mara nyingi a vanguard party, kama vile Chama cha kikomunisti.

Lengo kuu katika Mapinduzi haya ya Kijamii ni kupangua ‘completely' mfumo uliopo, hasa mahusiano ya uzalishaji na umiliki wa mali, tofauti na mapinduzi ya Kisiasa kama tulivyoona kwamba mara nyingi huacha masuala haya kama yalivyovyo; Mara nyingi, mapinduzi ya Kijamii hubadilisha mfumo mzima wa maisha na mahusiano ya raia kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiutamaduni n.k. Mfano mzuri ni mapinduzi ya Russia ya 1917 na yale ya Cuba mid 20[SUP]th[/SUP] century ambayo yalikuwa Marxist in nature, hence very radical – kwani yalilenga kuondoa mfumo wa kibepari na ku - install mfumo wa kijamii/kikomunisti;

Muhimu:

  • Pamoja na kwamba Mapinduzi ya aina hii hubadilisha mfumo mzima wa kijamii na kiuchumi, hasa mahusiano katika uzalishaji na umiliki wa mali, bado haina maana kwamba walio wengi (kwa mfano WAKULIMA NA WAFANYAKAZI), ndio wanakuwa wamiliki wapya moja kwa moja wa mali na njia kuu za uchumi, badala yake, uthibiti na usimamizi wa uzalishaji na usambazaji mali na mitaji huenda kwa to the new "ELITE", wanaojificha nyuma ya chama cha KIKOMUNISTI au Serikali ya Kijeshi.

Kuna mapinduzi mengine ya aina mbili ambayo hayana uhusiano wa moja kwa moja na mdahalo wetu, pengine indirectly, nayo ni:

  • Mapinduzi yenye Orientation ya KIDINI ambayo hutokea zaidi kwenye jamii ambazo aina fulani ya dini ndio predominant; na
  • Mapinduzi yasiokuwa na uhusiano wa moja kwa moja wa kisiasa au kijamii lakini yenye madhara kwenye jamii husika, pengine kulika mapinduzi mengine tuliyokwisha jadili, kwa mfano mapinduzi ya Kilimo, Mapinduzi ya Viwanda n.k.

Tukijereaa kwenye Mdahalo wetu, focus yetu zaidi ipo kwenye mapinduzi ya Kisiasa na Ya Kijamii, ambapo tumeona kwamba Three Key Themes ndio hujenga dhana ya Mapinduzi:

  • Mobilization of the Mass
  • Movement of the Mass
  • Regime Change

Na pengine ni sahihi kusema kwamba M4C inabeba elements za hizi three themes ingawa haina maana kwamba M4C inalenga Mapinduzi. Vinginevyo mapinduzi huwa yanayohusisha MOVEMENTS na hulenga zaidi kubadili ‘the socio-political institutions' kwa sababu hizi institutions ndio zinazotunga sheria na kusimamia utendaji wa taasisi nyingine zote zinazogusa maisha ya kila siku ya wananchi, kwa mfano Usalama wa raia, ustawi wa maisha ya wananchi n.k. Kuna kila dalili kwamba M4C inalenga hilo, au angalau UMMA unavutiwa na M4C kutokana na hili, ingawa again, haina maana kwamba lengo kuu la M4C ni Mapinduzi.

SEHEMU YA NNE: UFUNGUZI WA MDAHALO

Baada ya kuweka mdahalo huu katika Muktadha Sahihi (Right Context) na Kujaribu kujenga Hadidu Rejea (terms of reference), yafuatayo ni masuala muhimu ya kujadili:

KWANZA, Je: Umma wa Tanzania Una Ufahamu Gani Juu ya Tofauti Hizi Baina ya MAGEUZI NA MAPINDUZI?

PILI, Je: Umma wa Tanzania Una Kiu Ya Mabadiliko Ya Aina Gani Baina ya MAGEUZI NA MAPINDUZI?

TATU, Je: Viongozi wanaoendesha "Mass Movements" wana lengo gani – kuboresha Mageuzi (Reforms) ambazo Serikali ya CCM imekuwa inazitekeleza kwa miaka 26 sasa chini ya usimamizi wa IMF na World Bank au Viongozi wanaoendesha hizi "Mass Movements" wanalenga mbali zaidi ya Mageuzi?

NNE, Je: CCM ina nafasi gani katika kipindi hiki kuelekea 2015 kujenga imani mbele ya UMMA kwamba njia sahihi ya kuelekea kwenye mabadiliko ya kweli kwa wananchi – more economic, social & political justice [kwa pamoja], ni kwa wananchi kuendelea kuiamini serikali ya CCM 2015 na kuwa wavumilivu kwamba CCM itaendeleza MAGEUZI (Reforms) katika sekta za Uchumi, Siasa, Utumishi wa Umma na Usimamizi wa Fedha za Umma, na hatimaye to deliver the promise of: MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?
 
Kwa kifupi sana...wananchi wamechoka, wamechoka na umaskini, wamechoka kunyanyaswa, wamechoka na ubinafsi wa viongozi, ufisadi, kujuana, manyanyaso, kufanywa wajinga.. Sasa wanakua desperate..do not play with despate soul. Any kind of revolution/change that suffice their expectations will be welcomed at this point.
 
Kwa kifupi sana...wananchi wamechoka, wamechoka na umaskini, wamechoka kunyanyaswa, wamechoka na ubinafsi wa viongozi, ufisadi, kujuana, manyanyaso, kufanywa wajinga.. Sasa wanakua desperate..do not play with despate soul. Any kind of revolution/change that suffice their expectations will be welcomed at this point.

Kwa maana hii, UMMA wa watanzania (sehemu kubwa) unaotikia M4C kwa mwamko mkubwa, je ni kwamba:

*Umma huu Hauna ufahamu juu ya Mageuzi yanayoendelea kutekelezwa na serikali ya CCM na kusimamiwa na World Bank na IMF kwa miaka 26 sasa, Mageuzi ambayo yanalenga kuboresha hali zao za maisha? AU

*Wana ufahamu lakini kasi na matunda ya mageuzi haya imeshindwa kukidhi matarajio, matumaini, matakwa na ndoto za watanzania walio wengi, hivyo they are increasingly becoming open to more/other options including Radical ones?
 
Kwa maana hii, UMMA wa watanzania (sehemu kubwa) unaotikia M4C kwa mwamko mkubwa, je ni kwamba:
*Huna ufahamu juu ya Mageuzi yanayoendelea kutekelezwa na serikali ya CCM na kusimamiwa na World Bank na IMF? AU

*Wana ufahamu lakini kasi na matunda ya mageuzi haya imeshindwa kukidhi matarajio, matumaini, matakwa na ndoto za watanzania walio wengi, hivyo they are becoming more open to other options including Radical ones?

* Kwanza sidhani kama kuna mageuzi yoyote yanayoendelea kutekelezwa na CCM [aidha kwa kusimamiwa na taasisi hizo au la] yanayofaidisha UMMA wa Watanzania. ndiyo maana unaona muamko mkubwa kwa M4C.

*Wananchi hawa hawako interested na kujua definition ya MAPINDUZI au MAGEUZI, kama mabadiliko haya yataletwa kwa misingi ya kidini [ kama inavyosadikiwa kwa CUF] au kikanda [kama invyosadikiwa kwa Chadema].

Wanaangalia ni nani anabeba matakwa na matarajio yao. Nilikua namsikiliza Lema leo ameuliza "nani ameona mtoto wa waziri anasoma shule ya kata". Serikali kama hii haibebi matakwa ya wananchi zaidi ya kujinufaisha wao. Hii ni chachu kubwa ya mabadiliko. Mabadiliko haya hayatakua kutoka chini kwenda juu, au vice versa..nafikiri itakua ni mchanganyiko kwa maana kwamba yatatokea juu bila kutaka [unintended consequenses] kwa wakubwa hawa kujipendelea wao na vizazi vyao hivyo basi kulazimisha UMMA kuamka na kuchukua hatua. Ndiyo wanachofanya akina Lema, kuamsha UMMA.
 
Kwanza sidhani kama kuna mageuzi yoyote yanayoendelea kutekelezwa na CCM [aidha kwa kusimamiwa na taasisi hizo au la] yanayofaidisha UMMA wa Watanzania. ndiyo maana unaona muamko mkubwa kwa M4C.

Nakubaliana na wewe juu ya hili, pengine miaka 18 ya Ujamaa ilikuwa bora kwa mtanzania wa kawaida kuliko miaka 26 ya Soko Huria iliyoambatana na mageuzi ya kiuchumi kwa kuanzia mwaka 1986 na kuendelea katika nyanja nyingine kama nilivyojadili.

Wananchi hawa hawako interested na kujua definition ya MAPINDUZI au MAGEUZI, kama mabadiliko haya yataletwa kwa misingi ya kidini [ kama inavyosadikiwa kwa CUF] au kikanda [kama invyosadikiwa kwa Chadema
.

Suala la msingi sio wananchi kuwa na interest juu ya definitions, bali suala ni utambuzi na ufahamu wao juu ya aina gani ya mageuzi wanayohitaji na mbinu gani zitumike kufanikisha mabadiliko wanayohitaji; na tunarudi pale pale kwamba mabadiliko katika jamii hutokana na aidha mageuzi au mapinduzi, sio vinginevyo;

Wanaangalia ni nani anabeba matakwa na matarajio yao. Nilikua namsikiliza Lema leo ameuliza "nani ameona mtoto wa waziri anasoma shule ya kata". Serikali kama hii haibebi matakwa ya wananchi zaidi ya kujinufaisha wao. Hii ni chachu kubwa ya mabadiliko. Mabadiliko haya hayatakua kutoka chini kwenda juu, au vice versa..nafikiri itakua ni mchanganyiko kwa maana kwamba yatatokea juu bila kutaka [unintended consequenses] kwa wakubwa hawa kujipendelea wao na vizazi vyao hivyo basi kulazimisha UMMA kuamka na kuchukua hatua. Ndiyo wanachofanya akina Lema, kuamsha UMMA.

Kuamsha UMMA ufanye mabadiliko kupitia sanduku la Kura 2015 ili Chadema waende kutekeleza Mageuzi yanayoongozwa Serikali ya CCM chini ya World Bank na IMF kwa ufanisi zaidi? Jibu lako hapa litasaidia kutupatia mwanga juu ya:

1.Hatima ya M4C 2015 and perhaps beyond incase CCM itaendelea kuaminiwa na kukamata dola 2015; Vile vile rejea kauli ya Mbowe kwamba CCM ikishinda Uchaguzi 2015, basi atajiuzulu Siasa;

2. Kutoa ishara kwamba pengine Chadema na CCM hawana utofauti kisera bali wana utofauti katika utekelezaji wa sera zile zile zinazoungwa mkono na IMF na World Bank tangia Mwaka 1986 kipindi ambacho Mwalimu Nyerere na Mzee Mtei (ambae alikuwa upande wa WorldBank na IMF), walipishana na Mwalimu juu ya dira ya taifa - KIUCHUMI;
 
M4C ni njia mojawapo ya kutafuta kura ili wapate viti bungeni na Urais.
Haina elements za kimapinduzi na haina policies bayana za kimageuzi.

Na naomba kutofautiana na wewe kidogo, siamini kama umaskini huleta mapinduzi.
 
Nakubaliana na wachangiaji wenzangu. Kitu ambacho hatuelewi watanzania hasa viongozi na wasomi ni kuendelea kufikiri maendeleo yataletwa na hiyo mikakati inayotoka world bank na kwingineko i.e. Mkukuta, tasaf etc.

Haya mataifa yanayotoka eg china, korea, india hata iran kwa asilimia kubwa wamepiga hatua kwa kutumia bongo zao wenyewe ikiwa ni pamoja na kununua au kuiba technology ambayo wanajua itawatoa!

Mapinduzi ninayofikiria mimi ni katika elimu, mtoa mada huenda wewe ni mhadhiri chuo fulani, tunahitaji mfumo utakaofanya watanzania wafikir kwa akili zao namna ya kutoka (to progress) kama wachaga wanavyoanza kwa kuuza karanga barabarani, kaduka, duka, retail, whole sale etc.

Kwa kweli wananchi tumechoka kiasi kwamba hayo mageuzi au mapinduzi yaje tu tuone the other side of the coin. Will be positive with positive thinking (which we lack), negative if we continue the way we think now!
 
M4C ni njia mojawapo ya kutafuta kura ili wapate viti bungeni na Urais.
A Movement for Change lengo lake kuu ni kutafuta viti vya ubunge na Urais? Halafu? Kuendeleza mfumo ule ule wa CCM, hasa utekelezaji wa sera za Mageuzi katika nyanja nilizojadili? Je, UMMA ambao mwenzetu Kwame Nkrumah ameujadili nao una mtazamo na matarajio haya?

Haina elements za kimapinduzi...

Rejea matumizi ya MOVEMENT katika mabadiliko; Vile vile rejea themes kuu zinazounda neno mapinduzi - Mass Mobilization, Mass Movement, na Regime Change; Kusema kwamba M4C ina elements za Mapinduzi ni kutokana na hili; Naomba ieleweke kwamba kusema M4C ina elements za mapinduzi haina maana kwamba Chadema inalenga kuleta mapinduzi; Vinginevyo kama nilivyojadili awali, mwenye maamuzi juu ya mbinu za mageuzi ni UMMA kwani UMMA ndio wenye mamlaka ya mwisho juu ya hatima ya taifa, ndio maana nimeona mjadala huu ni muhimu kwani hatujui mwitikio wa UMMA kwa M4C utakuwa na hatima gani, hasa iwapo CCM itashinda 2015;

na haina policies bayana za kimageuzi....
Which means Chadema under M4C wanatafuta kuingia ikulu literally kwenda kufanya kazi na World Bank na IMF kwa mambo yale yale yanayotekelezwa na serikali ya CCM, ila Chadema wao wataenda kuyafanya kwa ufanisi zaidi?

Na naomba kutofautiana na wewe kidogo, siamini kama umaskini huleta mapinduzi.

Haya sio maneno yangu bali ya Mwanafalsafa 'Aristotle', na alichosema ni kwamba: Umaskini ni Mzazi wa Mapinduzi na Uhalifu, na binafsi nakubaliana nae katika hili; ni muhimu pia tukakubaliana kwamba kauli yako kwamba Umaskini Hauleti Mapinduzi ni tofauti na kauli kwamba Umaskini ni Mzazi wa Mapinduzi;
 
Nakubaliana na wachangiaji wenzangu. Kitu ambacho hatuelewi watanzania hasa viongozi na wasomi ni kuendelea kufikiri maendeleo yataletwa na hiyo mikakati inayotoka world bank na kwingineko i.e. Mkukuta, tasaf etc. Haya mataifa yanayotoka eg china, korea, india hata iran kwa asilimia kubwa wamepiga hatua kwa kutumia bongo zao wenyewe ikiwa ni pamoja na kununua au kuiba technology ambayo wanajua itawatoa! Mapinduzi ninayofikiria mimi ni katika elimu, mtoa mada huenda wewe ni mhadhiri chuo fulani, tunahitaji mfumo utakaofanya watanzania wafikir kwa akili zao namna ya kutoka (to progress) kama wachaga wanavyoanza kwa kuuza karanga barabarani, kaduka, duka, retail, whole sale etc.

Tafsiri yangu kwa hoja yako hapa ipo katika sehemu tatu:

Kwanza, tunahitaji zaidi mapinduzi ya Fikra;
Pili, ni tuendelee na Mageuzi yaliyopo lakini watanzania ndio wawe wamiliki wa mageuzi, sio wahisani;
Tatu, mfumo uliopo - Soko Huria na Ubepari sio tatizo, hivyo viendelee kama vilivyo;

Nisema tu kwamba kama this holds, basi Chadema wana kazi kubwa sana ya ku deliver kwa UMMA iwapo Chadema watafanikiwa kuitoa CCM 2015;

Kwa kweli wananchi tumechoka kiasi kwamba hayo mageuzi au mapinduzi yaje tu tuone the other side of the coin. Will be positive with positive thinking (which we lack), negative if we continue the way we think now!

Mageuzi yapo kwa muda mrefu sasa. Kama umenisoma vizuri, Mageuzi yalianza mwaka 1986 na yanaendelea hadi hivi sasa katika nyanja nilizozijadili; Kitu ambacho hakijawahi kutokea Tanzania bara ni Mapinduzi, tofauti na kwa ndugu zetu wa Visiwani ambao walitwaa nchi yao kutoka kwa Sultani wa Oman kwa njia ya mapinduzi, na muda mfupi baadae kujiunga na Tanganyika, kuunda Tanzania;

Kuhusu mimi kuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu, sijajaliwa kupata nafasi hiyo ingawa ningependelea kulitumikia taifa zaidi kwa njia hiyo;
 
M4C ni njia mojawapo ya kutafuta kura ili wapate viti bungeni na Urais.
Haina elements za kimapinduzi na haina policies bayana za kimageuzi.

Na naomba kutofautiana na wewe kidogo, siamini kama umaskini huleta mapinduzi.

Nakubaliana na wewe 100%
 
A Movement for Change lengo lake kuu ni kutafuta viti vya ubunge na Urais? Halafu? Kuendeleza mfumo ule ule wa CCM, hasa utekelezaji wa sera za Mageuzi katika nyanja nilizojadili? Je, UMMA ambao mwenzetu Kwame Nkrumah ameujadili nao una mtazamo na matarajio haya?



Rejea matumizi ya MOVEMENT katika mabadiliko; Vile vile rejea themes kuu zinazounda neno mapinduzi - Mass Mobilization, Mass Movement, na Regime Change; Kusema kwamba M4C ina elements za Mapinduzi ni kutokana na hili; Naomba ieleweke kwamba kusema M4C ina elements za mapinduzi haina maana kwamba Chadema inalenga kuleta mapinduzi; Vinginevyo kama nilivyojadili awali, mwenye maamuzi juu ya mbinu za mageuzi ni UMMA kwani UMMA ndio wenye mamlaka ya mwisho juu ya hatima ya taifa, ndio maana nimeona mjadala huu ni muhimu kwani hatujui mwitikio wa UMMA kwa M4C utakuwa na hatima gani, hasa iwapo CCM itashinda 2015;


Which means Chadema under M4C wanatafuta kuingia ikulu literally kwenda kufanya kazi na World Bank na IMF kwa mambo yale yale yanayotekelezwa na serikali ya CCM, ila Chadema wao wataenda kuyafanya kwa ufanisi zaidi?



Haya sio maneno yangu bali ya Mwanafalsafa 'Aristotle', na alichosema ni kwamba: Umaskini ni Mzazi wa Mapinduzi na Uhalifu, na binafsi nakubaliana nae katika hili; ni muhimu pia tukakubaliana kwamba kauli yako kwamba Umaskini Hauleti Mapinduzi ni tofauti na kauli kwamba Umaskini ni Mzazi wa Mapinduzi;

OMG!!!! Dr Slaa,Dr Kitila Mkumbo n.k someni madini haya!
 
Mkuu Mchambuzi,

Watanzania ni wavumilivu na wapole sana kiasi cha wakati mwingine tunaona kama tunajinyima wenyewe haki zetu za msingi tunazozifahamu kabisa!

M4C imeleta hamasa sana kwa kuongeza kiu ya mabadiliko lakini bado wananchi hawajui baada ya hayo mabadiliko nini kitafanyika tofauti na sasa! je kwa mfano tutatengeneza mafisadi wapya?

M4C nafikiri usiwe wimbo wa kuitoa CCM madarakani tu bali tuambiwe nini kitafanyika baada ya hayo mabadiliko! Mwanadamu anakawaida ya kupigania kitu kinachompa assurance ya better future akifanikisha,je nini mkakati wa CDM wakishaingia ikulu(wasisubiri ilani ya uchaguzi tu).Mfano tunataka watuhumiwa wote wa ufisadi wakamatwe na kushtakiwa regardless ya cheo alichokuwa nacho,CDM hawako wazi moja kwa moja kwenye hili ingawa ndio wapiga kelele wakuu wa ufisadi.
 
Hapahitajiki kujua aina ya mageuzi au Mapinduzi kwa khali tuliyonayo Watanzania chini ya serikari ya CCM. Tunataka mabadiliko ktk sector zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii kwani hapana penye unafuu. CCM na serikari yake wana mfumo usiozingatia maslahi ya umma, wanawaza familia zao na marafiki zao ktk hayo mageuzi au reform iliyoingelea.

Wewe ni msomi mzuri na umechambua mambo kishule zaidi lakini hizi zote ni ngonjera na hadithi za watawala wetu na mfumo fikilika. Tunataka watu wapya wenye mtizamo mpya utakaotufanya siku moja tuione tena Tanzania aliyoiacha Mjamaa halisi Nyerere.

Ni vigumu kuwaaminisha wataTanzania wa leo kuwa kuna eti Mageuzi ya Kisiasa , kiuchumi na Kijamii yanafanyika wakati kila kukicha ni afadhali ya JANA.

Time will tell CCM ni lazima IFE kwa faida ya Umoja na Amani ya watanzania, kwani bila hivyo pengo lililopo la walionacho na wasionanacho linazidi kupanuaka na hakuna dalili za kuzibwa.
Tanzania ni zaidi ya CCM. Itawezekana tu bila CCM.
 
Mchambuzi unalidwa na kirefu cha CCM, Mapinduzi daima, sijui na wao hawajui mapinduzi ni uhaini? Tendwa mambo gani haya?
 
Haijalishi nikichaa vichaa makahaba washirikina ndio wanao tuongoza kuendelea nasafari ya kuulinda na kuurejesha UTU wa mtanzania iwe ni KWA MAGEUZI YA KISIASA AU MAPINDUZI lakini muhimu kwa watanzania wengi hasa wanao ikubali na kushirikiana CHADEMA nikuing'oa CCM kwanza na kuandika katiba upya itakayo leta SEREKALI YA WATU NDANI YA WATU NANCHI YAO mingineyo yatajipanga baada ya CCM kukabidhi mamlaka kwa UUMA!...Usually

When people are sad they don't do anything they just CRY over their condition but when they gel Angry they bring about a change" (MALCOLM X)
 
UFUNGUZI WA MDAHALO

Baada ya kuweka mdahalo huu katika Muktadha Sahihi (Right Context) na Kujaribu kujenga Hadidu Rejea (terms of reference), yafuatayo ni masuala muhimu ya kujadili:

KWANZA, Je: Umma wa Tanzania Una Ufahamu Gani Juu ya Tofauti Hizi Baina ya MAGEUZI NA MAPINDUZI?

PILI, Je: Umma wa Tanzania Una Kiu Ya Mabadiliko Ya Aina Gani Baina ya MAGEUZI NA MAPINDUZI?

TATU, Je: Viongozi wanaoendesha "Mass Movements" wana lengo gani – kuboresha Mageuzi (Reforms) ambazo Serikali ya CCM imekuwa inazitekeleza kwa miaka 26 sasa chini ya usimamizi wa IMF na World Bank au Viongozi wanaoendesha hizi "Mass Movements" wanalenga mbali zaidi ya Mageuzi?

NNE, Je: CCM ina nafasi gani katika kipindi hiki kuelekea 2015 kujenga imani mbele ya UMMA kwamba njia sahihi ya kuelekea kwenye mabadiliko ya kweli kwa wananchi – more economic, social & political justice [kwa pamoja], ni kwa wananchi kuendelea kuiamini serikali ya CCM 2015 na kuwa wavumilivu kwamba CCM itaendeleza MAGEUZI (Reforms) katika sekta za Uchumi, Siasa, Utumishi wa Umma na Usimamizi wa Fedha za Umma, na hatimaye to deliver the promise of: MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?
Mkuu Mchambuzi,

Hhere you come again! Asante sana kwa hizi, hii ni professional presentation kabisa ambapo ulipaswa ulipwe sii chini ya TZS 500,000 kila unapofanya presentations kama hizi, nadhani kama JF tutaendelea hivi, 2015, JF will have its proper recognition kama true agent wa posive change kwa maendeleo ya taifa.

Mimi nijadili kwa mukhtadha wa conflicting interest baina ya CHANGE inayopiganiwa na Chadema kupitia M4C dhidi ya MAITAINING STATUS QUO ya CCM.Kwa kuanzia naomba kwanza tukubaliane, kuwa "A MAN CAN DO NO MORE THAN WHAT HE CAN"!, yaani binadamu hawezi kufanya chochote zidi ya uwezo wake!. Tangu uhuru mpaka hapa tulipofikia, CCM ndio imetifikisha hapa, na hapa ndio mwisho wa uwezo wa CCM!, nikimaanisha "CCM CAN NOT DO ANYTHING MORE THAT WHAT IT CAN"!, kwa maana hiyo ninamaanisha ili taifa liweze kusonga mbele, CHANGES are innevatible, unless tunaendelea kukubali kupiga mark time hapa tulipo!
KWANZA, Je: Umma wa Tanzania Una Ufahamu Gani Juu ya Tofauti Hizi Baina ya MAGEUZI NA MAPINDUZI?
Umma hauna ufahamu wa kutosha kuhusu mageuzi na mapinduzi, ndio maana nasisitiza sana kuenezwa kwa elimu ya uraia kuhusu mambo ya utawala ili tufike mahali, M4C ijikite kwenye kuwaa inisha Watanzania malengo yake ni kuleta mageuzi na sii mapinduzi, hivyo hakuna haja wala sababu za kugombana na vyombo vya dola. Zile sare za Chadema, zimekaa kimapinduzi zaidi zikiashiria shari kuliko heri!, as days go by, tutawashauri, watumie kitambaa chepesi zaidi kuashiria amani zaidi, kuliko kuendelea na zile khaki nzito kama kombati kuashiria wako vitani!.

PILI, Je: Umma wa Tanzania Una Kiu Ya Mabadiliko Ya Aina Gani Baina ya MAGEUZI NA MAPINDUZI?
Kwa vile nimesema mabadiliko ni innevitable, it goes without saying kuwa Watanzania wanataka mabadiliko, yaani hitaji la mabadiliko sio debatable tena, bali issue ibaki ni mabadiliko gani ya mageuzi na mapinduzi!. Kwa vile hapo juu nimesema Watanzania hawajua wanataka mabadiliko kwa njia gani, ndio maana M4C ikiwaswaga watu kwenye maandamano, turn up ni kubwa, na CCM ikiitisha mikutano yake to maintain its status quo pia turn up yake ni kubwa!. Tutumie elimu ya urai kuwaelimisha Watanzania kuwa hii CCM iliyoshindwa, inaweza ikawekwa pembeni kwa amani na Tanzania ikabaki!.
TATU, Je: Viongozi wanaoendesha "Mass Movements" wana lengo gani – kuboresha Mageuzi (Reforms) ambazo Serikali ya CCM imekuwa inazitekeleza kwa miaka 26 sasa chini ya usimamizi wa IMF na World Bank au Viongozi wanaoendesha hizi "Mass Movements" wanalenga mbali zaidi ya Mageuzi?
Hapa ndipo kwenye mzizi wa fitna na ndipo hapa ambapo huwa natofautiana na Chadema katika politics of confrontations hivyo kuishia kunyoosheana vidole na kuitana majina huyu ni "CCM", "gamba", "mnafiki", "umetumwa" etc, etc. Viongozi wa Chadema wanaongoza M4C, nao hawajui wananchi wanataka nini, hivyo kuendesha M4C kwa lengo la kimapinduzi zaidi "regime change" badala ya kuhubiri reforms "wao wakiingia watafanya nini", wakiamini kwa vile wananchi wana kiu ya mabadiliko, kuhubiri tuu mabadiliko, kunatosha kuwa convince wanainchi wakubali kuibadili CCM come 2015, hata kama Chadema hawajasema wao watafanya nini na kivipi?. Mfano hayo mahubiri ya Elimu bure mpaka chuo kikuu, huduma za afya bure, wanatakiwa kuwatumia wachumi makini, kutoa economic projection ya itawezekana vipi na jinsi ya kutoa huduma za afya na elimu ya mpaka chuo kikuubure kwa taifa la watu milioni 50, with infrastructure cost na oparation cost kwa uchumi wetu uliopo!.

Hivyo kuwathibitishia Watanzania kuwa Tanzania is capable kuyafanya yote hayo na kuwa hii tabia ya serikali ya CCM kuzungusha bakuli lake la Umatonya, ni matokeo tuu ya faile and wrong policies na mismanagement ya resources zilizopo ikiwemo kuzitapanya kwa lavish expenditure, jiserikali kubwa lisilo na tija!, yaani big for nothing!. Marekani ji nchi likubwa ajabu lina mawaziri sita tuu!,(wale sectaries) na wengine wote ni watendaji professionals (under secretaries), ukilinganisha na Tanzania, ni kijinchi kama nyanya tuu, tuna mawaziri 60!, politicians!, unamkuta daktari ndie waziri wa ulinzi, na mjeshi waziri wa habari!. Atotal mess!.


NNE, Je: CCM ina nafasi gani katika kipindi hiki kuelekea 2015 kujenga imani mbele ya UMMA kwamba njia sahihi ya kuelekea kwenye mabadiliko ya kweli kwa wananchi – more economic, social & political justice [kwa pamoja], ni kwa wananchi kuendelea kuiamini serikali ya CCM 2015 na kuwa wavumilivu kwamba CCM itaendeleza MAGEUZI (Reforms) katika sekta za Uchumi, Siasa, Utumishi wa Umma na Usimamizi wa Fedha za Umma, na hatimaye to deliver the promise of: MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?

Hapo ndipo game lote la kuelekea 2015 linapochezwa!. Nilishasema huko nyuma, na nitaendelea kusema na kusema na kusema tena na tena na tena, kuwa CCM imechokwa!. Na Watanzania wamekuwa wakiichagua CCM tena na tena, sio kwa sababu wanaipenda! no!.

Wamekuwa wakiichagua CCM kwa
(1) mazoea tuu,
(2) ignorance na
(3) no credible option hivyo bora "zimwi likujualo"!.

Nikasema kwa vile Chadema wameonyesha nia, na dalili za kuweza kuwapatia mabadiliko wayatakayo, hopes nyingi zimeelekezwa kwa Chadema!, tatizo bado hawajajipanga!. CCM kwa kutambua kuwa imechokwa, na kuna kitisho cha kiukwelii cha uwezekano wa kupigwa chini hiyo 2015!, sasa kina jitahidi by means of hooks and crooks ikiwemo hiyo "safety net" ya bilioni 400, kuwalambisha pipi Wanzania kwa kukidhi matarajio ya muda mfupi na wa muda wakati, huku ikiweka ahadi za kuigeza Tanzania kugeuka "pepo" katika malengo ya muda mrefu ili 2015, Watanzania, waichague tena!. 2015, ni vita ya kugombea "kisu" kati ya CCM na Chadema!. CCM ndio imeshika kwenye mpini, na Chadema imeshika kwenye makali!.

CCM inayo nafasi ya ku proove kwa umma wa Watanzania kuwa bado inao uwezo wa kuleta reforms kwa njia ya change for the better, ikiwa na something in the hand to show kuwa I did, this, I did that, such that if elected again, I can do this and that!. "a bird in the hand, woth two in the bush"!. Yaani kwa CCM "moja shika sii kumi nenda rudi"!. CCM n dio huyo ndege mmoja, anacho cha kuonyesha!, Chadema haina kitu cha kuonyesha isipokuwa ahadi kuwa nikipewa nchi, nitafanya hili na kile!, but with nothing to show, hivyo CCM hapa ndio yenye advantage!.

Chadema nayo kwa upande wake, kupitia M4C, inao mtihani mgumu, wa kuwa convince Watanzania kuwa kwa kipindi cha miaka 50, CCM imeshindwa kuondoa wale maadui wetu watatu wa ujinga, umasikini na maradhi, on top of that, imeongeza maadui wengine wawili, rushwa na ufisadi, hivyo CCM hata ikipewa miaka 100 mingine ya kuendelea kutawala, haitaweza kubadili chochote kwa sababu hapo ilipofika, ndio mwisho wa uwezo wake!. "CCM CAN DO NO MORE THAN WHAT IT CAN"!.

2010 Taanzania ikiwa na population ya watu milioni 40, eligible voters were 25 milions. Waliojindikisha ni 20 milions. Waliopiga kura ni 8 milions, walioichagua CCM ni 6 milions!. Ukisoma website ya CCM, wanajitapa wana wanachama milioni 6!, hivyo CCM ilichaguliwa na wale wana CCM milioni 6 suppose wote walijiandikisha na kupiga kura!. 2015 tutakuwa milioni 50, eligible voters milioni 30!. Nimewashauri Chadema, kuwa M4C iachane kabisa na CCM!, ijikite kuzitafuta zile kura milioni 20 ambazo CCM haiwezi kuzivuna ili tupate mabadiliko kwa njia ya amani kupitia ballot box!.

Kipindi hiki kuelekea 2015, huu ni muda wa kujipanga kisawasawa, huku CCM ikifanya mambo kuonyeshea ina nini na kuna vitu vya kuonekanika, visible vinavyoonekana. Kitendo cha Chadema kubeza kila kitu, as if hakuna zuri hata moja ambalo CCM imefanya, huko ni kujidanganya kwa ku please tuu nafsi zao huku ukweli halisi, ukionekana!. Inatakiwa kwanza wakubali kilichopo, na kuwaeleza Watanzania kuwa wangekuwa wao, wangefanya something better!. Mfano 2015, daraja la Kikwete (Kigamboni) litakuwepo physical na visible!, huwezi kudai daraja lile ni nothing!, bali wanatakiwa from now kusema, wangekuwa ni wao Chadema, daraja lile, wangelijenga pale Feri na lingekuwa ni la kufunua kama London Bridge, hivyo lingekuwa fupi, more economical, karibu, more convenient, na location ni more scenic kwa tourist attractions kuliko kulipeleka kule CCM ilikolipeleka!, hivyo kuzikata tambo za CCM kuwa wametuletea daraja "Kikwete"

Zile singles za "list of Shame", ufisadi, rushwa, etc, by 2015, zitakuwa zimeisha shuka kwenye chart ya top of the pops. 2015 Wanzania wanahitaji hit single za Tukiichagua Chadema, tutapata nini tofauti na hiki tunachopewa na CCM, concentrations isiwe just change and replace CCM with Chadema, bali lets replace CCM with Chadema because CCM imeshindwa kufanya ABCD kwa sababu ya sera zake mbovu (failed policies),ABCD na Chadema wao wakiingia, watafanya ABCD kwa kutumia policies ABCD na resources from ABCD!.

Kwa mliongalia mjadala wa jana US, sisi pia tutatamani kuwapima vagombea wetu kwa utaratibu huu, na tuweke mecchanisim lazima wagombea washiriki debate, sio options bali a compulsory ili kuwapima, tupate kiongozi bora na sio bora kiongozi!.

Thanks.

Pasco.

NB: Kwa msisitizo!, Pasco wa JF sio mwanachama, mfuasi, au mshabiki wa chama chochote cha siasa, bali ni muumini wa kutanguliza mbele maslahi ya taifa ili 2015 tupate ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania.
 
Pasco umemsifia sana mchambuzi na kwa kweli anastahili sifa ulizompa - he really deserve the praise, ila sijaona comments zako kwenye thread ya Aweda ambayo imegusa maslahi ya bosi wako Lowassa. Naomba maoni yako kuhusu mada ya Aweda ya Sumaye kumvaa Lowasa. Nimekusubiri toka jana.
 
Last edited by a moderator:
Mimi si mshabiki wa maneno mengi ila niseme kwa kifupi tu "What ever it will be Watanzania tumechoka tunataka mabadiliko basi" Either hatma itakuwa Mapindizi au Mageuzi cha muhimu ni mabadiliko.

Masuala mengine nini kitafuata ni baada ya CCM kuwa pembeni kwanza.
 
Kwa mtazamo wangu siyo umaskini unaowafanya watanzania waichukie CCM bali utekelezaji wa sera na haki.

watanzania wengi tulitegemea wala rushwa na wahujumu uchumi wakubwa wangepelekwa mahakamani na kuchukuliwa hatua bila kujali nyadhifa zao, lakini leo tumeona yule tuliyempa jukumu la kuwaadabisha wale wa chini yake anawatetea kwa lugha za huyu hajapokea rushwa bali alipewa takrima.

Haiingii akilini hata kwa ambaye hajaenda shule wanasiasa wenye skendo bado wanaendelea kupeta na kupewa nyadhifa za juu.Na hilo ndilo linalokera kuliko yote ndio maana watanzani tuliowengi tunaichukia CCM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom