MDAHALO: M4C, Hatima ni Mageuzi au Mapinduzi?

Wanajamvi hebu tutoe tathimini zetu kuhusu vuguvugu la mabadiliko la chadema (M4C) kama limechangia kuleta afya kwa chama ama limeididimiza chadema. Tuzingatie matokeo ya udiwani kata 29 ambayo kampeni na nguvu kubwa ziliwekwa kuhakikisha cdm inajitanua zaidi. Karibuni kwa michango mature yenye lengo la kuboresha mapungufu.
 
kimahesabu tulishinda chaguzi hizo ingawa hatukushinda kwa kiwango tulichokitalajia wengi...na hii ni changamoto kuhusu M4C kapitie mahojianao ya Zitto utapata maelzo zaidi..
 
Chadema wanapozungumzia (M4C) wana maanisha nini? M4C inasimama badala ya movement for Change ina maana kubwa.

Mabadiliko kama mabadiliko yana maana na dhana kubwa mno ambayo inahitaji umakini kujadili kwa kina.

Dhana ya M4C ya chadema sijaielewa kabisa. Ndio maana mimi naiita ”movement for power” na hii M4C ni kivuli tu cha kufikia malengo yao ambayo kwa uhakika sio yenye malengo ya kuleta mabadiliko katika nchi yetu.

Msuguano uliopo sasa hivi kati ya CCM na Chadema ni msuguano wa kugombea madaraka na hauna chochote cha kufanya kwa mabadiliko ya umma. Ni uchu ule ule wa madaraka unawaongoza viongozi wengi wa Afrika hadi kuleta machafuko katika nchi zao. Sioni tumaini lolote kwa watu wa Taifa hili litakaloletwa na watu wa vyama hivyo hata kidogo.

Tunahitaji uongozi na mwelekeo, hatujui tunapoelekea kama Taifa. Tunahitaji uongozi. Taifa hili halitopata mabadiliko yeyote pasipo uongozi. Tunahitaji kuondoka kutoka hapa tulipo. Hatuwezi kuondoka hapa tulipo pasipo Order. Na order huletwa na kiongozi madhubuti. Anayejua nini nachotaka kufanya na wapi anataka kulipeleka Taifa. Kiongozi atakayeleta umoja wa Taifa na kuonyesha dira na mwongozo. kiongozi atakayeaminika kwa wanachi kwa maneno na matendo. Atakayeonyesha mfano kwa vizazi vijavyo. Kwamba hii ni njia ambayo kama Taifa tunapaswa kupita, kwasasa mapito yetu kama Taifa hayajulikani. Kwasasa siioni baadae yetu itakuwaje hakuna tumaini la baadae na haijulikani Taifa hili litakuwaje, hakuna tumaini.

Tumaini la vizazi vyetu liko gizani kutokana na kukosa uongozi. Sisi kama taifa tunapaswa kukusanya nguvu na kukua. Lengo la Taifa lolote ni utawala na uongozi wa dunia hatujawa Taifa ili tuwe wa mwisho au tutawaliwe daima. Ni lazima tukue kama Taifa na tuonyeshe uwezo wetu na hili litafanikiwa kama tukiwa wenye nia moja.

Tunahitaji kiongozi atakayeleta tumaini na mwelekeo katika Taifa letu, tumaini ambalo limeondoka miongoni mwa mamilioni ya watu wa Taifa hili. Umoja wetu ndio msingi wa kukua na kuendelea kwa Taifa hili. Hatuwezi kukua kama kila mtu atajiangalia mwenyewe na kuacha yale ambayo yametuunganisha kama Taifa. Tutaendelea haraka zaidi na kwa kasi kama tutakuwa wamoja na kila mmoja wetu kama atajitolea kwa moyo wake wote kulijenga Taifa hili na kulipenda. Kitu ambacho kimetuunganisha sisi ni Taifa letu na ni lazima tulijenge na tuwe na mapenzi nalo.

Hatuwezi kuendelea kama tutakandamizana wenyewe kwa wenyewe tabaka moja likijiona bora zaidi ya jingine. Tutaendelea kama tutaheshimiana kama watu wa Taifa moja na wenye nia na dhamira moja ya kulijenga Taifa hili hadi kufikia kilele chake cha maendeleo na ukuaji.

Taifa limekosa uongozi ni Taifa la watu walalamikaji hakuna anayeonyesha uongozi kwa kile kinachopaswa kufanywa kama Taifa. Watu wetu lazima wajue Taifa lao linaelekea wapi na ni nini wanaamini kama TAIFA.

Taifa letu liko katika mgawanyiko mkubwa na kutoridhika kwa watu wake juu ya mwelekeo na baadae ya Taifa. Tunahitaji tumaini hili linyanyuke. Tumaini hili ambalo wazee wetu waliopigania uhuru katika Afrika waliokuwa nalo, kuiona Afrika ikijitegemea na kuwa huru. Hili ni tumaini ambalo lazima liwepo mioyoni mwetu wote na ni lazima lifanikishwe kwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa.

Hatutaweza pasipokuwa na uongozi wenye maono, pasipo uongozi imara Afrika itaendelea kudumaa na kuwa tegemezi Daima. Lakini Afrika na Tanzania inahitaji kukua. Hii ni changamoto ambayo tunayo na inahitaji jitihada zisizofifia ili kuikamilisha ndoto yetu ya kuwa huru na watu wanaojitegemea. Sidhani pasipo umoja tunaweza kufaniisha hili. Tunahitaji viongozi wasio wabinafsi ili Afrika na Tanzania ikue. Tunahitaji viongozi wasio tetereka katika dhamira zao kuifanya Tanzania na Afrika kuwa huru na zenye kujitegemea. Hii ni vita na ni lazima ipiganwe.

Tunachangamoto katika taasisi zetu ambazo ndizo mashine katika maendeleo yetu kama Taifa. Kuna kutoridhika na kukosa uzalendo miongoni mwa wasomi wa Taifa hili. Matatizo katika mifumo yetu ya elimu na Afya. Ambayo imepelekea migogoro ya mara kwa mara baina ya serikali na watumishi hawa wa umma.

Ni dhahiri lazima tufahamu kwamba sisi sote lazima tuwe na dhamira moja ya kulijenga Taifa hili na hatutaweza kulijenga Taifa hili pasipo juhudi za pamoja na kujitolea kwa upande wa serikali na kwa upande wa watumishi wa UMMA. Serikali inawajibika kuwapelekea nyenzo na kila msaada ambao utasaidia watumishi wa umma kufanikisha kazi yao ya kutumikia umma. Lakini watumishi wa umma wanawajibika kufanya kazi kwa bidii na kwa nidhamu kutumikia watu wa Taifa lao na kuwa na mapenzi kwa Taifa lao. Hatutaweza kulisukuma gurudumu la Taifa hili pasipo jitijada za pamoja na dhamira ya pamoja.

Lazima tutengeneze serikali ya watu ambayo raia na viongozi wao watakuwa pamoja katika jitihada zao za ujenzi wa Taifa lao, kwa manufaa yao na sio kikundi kidogo cha watu au chama. Hili ni TAIFA ambalo nalihitaji ambalo kila mtu anachangia katika maendeleo ya Taifa lake kwa moyo mmoja na kujitolea, kila mtu akitambuliwa kutokana na mchango wake na kuheshimiwa. hili ndilo Taifa ninalohitaji.

Taifa ambalo litamwezesha mtu kukua na kukuza kipaji chake. Taifa la watu huru na wanaofuata na kuheshimu sheria zilizo tungwa kwa misingi ya Haki. Haya ndio mabadiliko ninayoyahitaji na hii ndio ”M4C INAYOHITAJIKA KUWEPO” Kubadili mitazamo ya watu kutoka katika ubinafsi kuja katika utaifa ili tujenge Taifa hili kwa moyo mmoja na kujitolea. Hatutaweza kubadili taifa hili kama hatutakuwa wamoja. Badiliko ya kweli ni kubadili fikra na mitazamo ya watu kuhusu Taifa lao, na watakapo fikiria chanya kuhusu Taifa lao hapo ndipo mabadiliko yatakapo tokea. Ya kwamba tuna uwezo wa kukua na tunauwezo wa kuendelea na kuwa kama Taifa lolote kubwa haya ndio matumaini yangu.

Watu wa Taifa hili wanahitaji kukua, wanahitaji kuona Taifa lao likinyanyuka na kuendelea, wanahitaji kuona Taifa lao likiwa Imara wamechoshwa na udhaifu. We will only achieve this if we have strong leadership. We can move as the Nation, we can be strong and independent. We have that potential.

Tuna mapambano mawili kuwaondoa viongozi mafisadi wote nchini mwetu lakini tunawajibu wa kulijenga na kuliendeleza Taifa hili kwa moyo wetu wote bila kubakiza kitu. Mapambano yetu sio kuondoa ufisadi tu bali kujenga nchi. Kujenga jamii zetu na kuleta ustaarabu. Kuleta umoja wa kitaifa na Wajibu. Tunaweza kuondoa chama kimoja tukikiingiza chama kingine cha kifisadi na nchi yetu ikaendelea kuwa palepale. Kinachojalisha ni mawazo mapya yatakayokuja na kubadilisha dira na mwelekeo wa Taifa hili kama upepo wa kisulisuli. Kuleta uzalendo na uwajibikaji katika Taifa.

Mabadiliko ya kweli katika Taifa hili yatakuja kutoka katika mabadiliko ya Fikra na Chama. Kwakuwa chama kinaweza kuwa Reformed kwa kubadili mitazamo yake na mwelekeo wake kinapoona kinakosea, wanapobadilika wanaweza kubadili dira na mwelekeo wa nchi.

Chadema na movement for Change ni propaganda tu. Wanaweza kuingia madarakani lakini maisha ya watu yakaendelea kuwa duni na yasiyo na matumaini. Sioni tofauti kati Ya CCM na CHADEMA katika mawazo yao na jinsi wanavyoendesha siasa zao. Hawawezi kulikomboa Taifa hili wala kuleta matumaini kwa waliokata tamaa. M4C is the movement for power. We are going to replace one tyranny with the Other. Uhuru wa kweli na maendeleo bado ni mgumu kwa aina za siasa ninazoziona.

The only true revolution is by changing the way people are thinking, by implementing new ideology and new values. We can not develop by the same thinking and the same values, we must change how we think. Watu wetu lazima waelewe hili tunalijenga Taifa letu kwa mawazo yetu, ubora wa mawazo yetu ndio ubora wa Taifa letu. Tunahitaji kiongozi atakayeleta mawazo mapya, mwenye akili na maono.

Lengo la kiongozi yeyote yule makini ni kuleta watu pamoja ili kujenga Taifa lao kwa manufaa yao kwa pamoja. Binadamu amepata maendeleo makubwa pale tu walipoanza kuishi pamoja na kuundwa serikali zao kwa manufaa yao. Hatujaunda serikali kusudi itawale na kunyima haki raia. Siasa ni chombo pekee chenye uwezo wa kukusanya watu kwa kushawishi juu ya faida ya pamoja tutakayoipata kama tutafanya jambo fulani kwa faida ya sasa na ya baadae ya taifa. Ni Siasa iliyokusanya watu na kuwa mataifa. Watu walishawishika kuunda mataifa kwasababu ya faida ya pamoja itakayopatikana kutokana na mtu kuishi katika Taifa. Siasa ikiwa chanzo cha vurugu na mgawanyiko katika Taifa hupoteza maana yake. Viongozi wenye uchu ambao hawafikiria chochote zaidi ya faida ya kipindi kifupi na sio baadae yetu na baadae ya vizazi vyetu.

Tuna kitu kimoja cha kufanya na kilichotuunganisha. Ni Taifa hili. Ni Tanzania. Naweza kukuita ndugu yangu kwakuwa tunaishi Taifa moja. Taifa hili likizama wote tunazama. Baadae ya Taifa hili inatutegemea sisi hakuna atakayejenga baadae yetu zaidi yetu. Kitu pekee ninachotaka kukiona ni kuliona Taifa hili likinyanyuka na likichukua nafasi yake katika Dunia. Hili ni tumaini ambalo kila mmoja wetu lazima awe nalo na kila mtu atakaye kabidhiwa mamlaka ya uraisi lazima awe nalo, kuwanyanyua watu wetu kutoka hapa tulipo. Sio ubinafsi na wala sio maslahi ya Chama bali dhamira yetu ya kulifanya Taifa hili liwe kubwa iliyozama ndani ya mioyo yetu. Ni lazima tuamini hivi ama sivyo hatutafanikiwa. Ni lazima tuamini tunauwezo wa kuwa Taifa kubwa kama Mataifa mengine na tutie jitihada kwa kufanikisha hilo.

Tumekuwa Taifa kutoka katoka katika makabila, koo na familia. Tumeunda kitu kimoja. Nguvu yetu itategemea sana umoja wetu pasipo kuangalia tofauti zetu za kikabila wala kidini ila dhamira yetu ya pamoja ya kujenga Taifa imara kwa vizazi vingi Vijavyo.

Mabadiliko ya kweli yatakayo likomboa Taifa hili ni mabadiliko ya fikra na mitazamo ya Watu. Tukifanikiwa kubadilisha mitazamo ya watu. Tutafanikiwa kubadilisha tabia na mabadiliko ya kimatendo tutarudi katika Taifa letu na kulitumikia kwa pamoja kwa maslahi ya wote.

Ni lazima tuangalie upya dhamira zetu kwa Taifa hili. Na tuwe wa kweli wa nafsi. Tujenge undugu wa watu wa Taifa moja. Tufikiri na kuamua mambo kutokana na fikra sahihi. Taifa hili litajengwa na busara na maono yetu.

Swali langu kwa ”Chadema movement for Change” what change the wan’t to bring in our country? Kuibadilisha CCM na kuwaweka wao madarakani? Watanzania wanahitaji zaidi ya hilo. Wanahitaji heshima na maendeleo ya Taifa lao. Wanatakiwa kutushawishi ni aina ya Taifa gani wanataka kulijenga. Tunu gani wanataka kuziweka kwenye Taifa letu na mwelekeo wao ni upi kama Chadema ni nini wanaamini? Wataleta matumaini gani kwa Tanzania? Tumeona katika Afrika vyama vingi vilikuja kama wakombozi wa wananchi lakini viliishia kuwa vyama visivyo kuwa na dira na vya kifisadi.Kwasababu waliongozwa na uchu ul ule sawasawa na wa watu walioko madarakani. Watanzania awahitaji ku replace tyranny with another Tyranny wanahitaji uhuru na maendeleo.

kitu Tanzania inachohitaji ni programmu itayobadili mitazamo na fikra za watu wetu juu ya nchi yetu. Kuingiza mioyoni mwa watu roho ya kulitumikia Taifa na uzalendo kwakuwa bila vitu hivi viwili Taifa haliwezi kusonga mbele. Bila umoja kamwe hatutaweza kusonga mbele. Lakini TAIFA hili linahitaji kukua na kusonga mbele katika umoja wetu. Naamini kabisa kama tukiwa wamoja na tukiwa determined kuliondoa Taifa hapa lilipo tunaweza.

Najua watu wa Tanzania wako katika Great distress na wamepoteza matumaini. Wengi wao wanajihisi sio sehemu ya Taifa hili. Tuna tatzio ni sawa na Chama kilichopo cha CCM ambacho kwa hakika hakina uhalali wa kuendelea kuwepo kutokana na ufisadi na kushindwa kuliongoza Taifa hili. Lakini pia vyama vyetu vya kisiasa vingi haviko imara kuleta mabadiliko ambayo tunahitaji ya kifikra, Wame focus mno katika kuitoa CCM madarakani bila kutayarisha programmu mbadala kwaajili ya kuleta mabadiliko kwa watu wa Taifa hili.

Chama chochote kitakacholeta mabadiliko katika Taifa hili ni kile ambacho kina maadili ndani yake. viongozi wake wana discipline na wanaheshimiana. Chenye ideology inayoeleweka na inayosambazwa kwa wananchi ili waijue na wajue chama chao kikiingia madarakani kitawafanyia nini. Kisicho okota okota ovyo viongozi wa kugombea katika majimbo bali kuwatayarisha katika maadili na discipline ya hali ya juu. Chenye Viongozi wanaoheshimu familia na majirani. Chenye watu wanaopenda jamii na kujitolea kujenga jamii.

Maendeleo ya kweli kwa jamii yeyote ile ni transformation ya roho, akili, mwili na mali, bila ya vitu vyote hivyo kukamilika binadamu hajakamilika kimaendeleo. Kwahiyo maendeleo ya binadamu sio ya mali tu lakini ya vile anavyofikiri, roho yake na ubora wa afya yake. Katika Taifa hli tunahitaji Order na bila order tunatambua taifa lolote halitoweza kuendelea. Na order hii itakuwepo tu kwa kuwa na viongozi wanaoheshimiwa na jamii. Utii huu wa jamii kwa kiongozi wao utakuja tu viongozi pale watakapojiheshimu na kuwa wa kweli na kuangalia mienendo yao ya kimaadili. Tunahitaji kiongozi atakayesema na watu kumsikiliza na kuhimiza utii wa sheria.

Tunawalea watoto wetu bila kufahamu haki zao na wajibu wao kwa Taifa kama Raia.

kila raia ana haki na wajibu kwa Taifa lake. Wajibu huu lazima uwe ndani kabisa ya kila mmoja wetu. Kwasababu sisi sote kama Taifa tumeungana kwa sababu ya lengo fulani, kuna sehemu tunahitaji kufika kwa pamoja, ni lazima tuwe na dira. Dira hii itapatikana kwa viongozi wenye maono. Kwahiyo kuwa wamoja ni muhimu. Hatuwezi kugawanyika kama Taifa tukafikiri tutafika popote hakuna. Those who are sincere in their hearts and speaks truth will bring direction to this Nation. Hatutaweza kuleta dira katika Taifa hili kwa propaganda na uongo. Sisi ni watu wamoja na muelekeo wetu ni mmoja. Hatutaweza kuleta ukombozi wa Taifa hili kwa style hii tunayoenda nayo.

Kwahiyo nina wasiwasi na Vuguvugu hili ambalo vijana wengi wanaliamini litabadili maisha yao. Ukweli ni kwamba vijana wa Taifa hili kwanza ni lazima wabadili tabia zao na kuwa watu wa kufikiri zaidi na watu wa kulipenda Taifa hili kiukweli. Wawe raia wanaowajibika kwa Taifa lao na wenye maadili. Kwasababu wao pekee ndio wenye uwezo wa kubadili mwelekeo wa Taifa hili kama wana fikra sahihi na kama ni wamoja na wazalendo. Kuna tatizo la kimaadili miongoni mwa vijana hili i lazima tulisema na baadae ya Taifa lolote inategemea sana vijana wao wamewaandaaje. Hii ni kazi ya wazazi katika familia na shule. Kwahiyo ni lazima tuangalie upya uundaji wa kijana wa Taifa katika fikra sahihi ili tupate raia bora.

Tunaweza kubadili CCM na kuwaweka CHADEMA ili kubadili chama tu. Lakini bila programmu sahihi na watu sahihi ili kubadili fikra za watu wa Taifa hili , Taifa letu litaendelea kubaki palepale bila kupiga hatua yeyote kubwa. Kwasababu bila Order katika jamii Taifa lolote halitoweza kupiga hatua. Na order hii inaenda deep mpaka ngazi ya familia. Ni jinsi gani tunaendesha familia zetu katika misingi ya adabu? Je tuna akina baba wawajibikaji wanaoweza kutawala familia zao katika misingi bora? Taifa huundwa katika ngazi ya familia. Ubora wa Taifa lolote hutegemea ubora wa familia. Lakini familia haiishi peke yake kuna majirani na mahusiano yakiwa mazuri katika ngazi hiyo ni hatua moja kubwa ya kuwa na mahusiano mazuri ya kitu kilichokikubwa zaidi ambacho ni Taifa. Bila mahusiano haya kama Taifa hatutapiga hatua. Kwahiyo Taifa letu linahitaji Social reformation, political reformation na economic reformation. Lakini kitu muhimu zaidi ni mahusiano yetu kama Taifa na kama mtu mmoja mmoja. Tukifikia hatua hii tutakuwa tayari kumpigania mtanzania mwenzetu hata mmoja atakapopata matatizo katika mataifa mengine. Ni lazima tupendane kama Taifa na kama mtu mmojammoja.

Mwisho Taifa hili linahitaji busara. Ni kiongozi mwenye busara na maono tu, atakayeweza kuliongoza taifa hili na kulitoa hapa lilipo. Atakayeunganisha vipande vilivyopo ili vifanye kazi kwa ufanisi na kutoa mazao. Tuna watu wa fani tofauti na vipaji tofauti lakini hatujafanikiwa kwasababu tumekosa kiongozi atayeunganisha vipande hivyo ili viweze kufanya kazi kwa ufanisi. We are not a well productive society kwasababu tumekosa a Leader. Ambaye kila mtu ata m admire na kumsikiliza because of ''intellegent, wisdom and Virtue''

we are time poor who do you think can read this lengthy rubbish, try to be brief and to the point.
 
hii nchi nin kSIKINI KWA SABABU WALIOPEWA MADARAKA YAANI POWER WANAYATUMIA KWA MASLAHI YAO WENYEWE HIVYO KULETA MABADILIKO NI LAZIMA UCHUKUE MADARAKA.
 
Chadema w
anapozungumzia (M4C) wana maanisha nini? M4C inasimama badala ya movement for Change ina maana kubwa.

Uuuh....There is a word SUMMARY...Why ignore it?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom