Kwa maoni yangu M4C inapaswa kuja na Package ya mageuzi ya kiujumla kwa watanzania kutokana na kwamba mapokeo yake na wananchi yamekuwa makubwa kupita kiasi, Kwa utafiti wangu mdogo nimeona walinzi wa M4C ni wananchi kwa uwingi na ujumla wao, nimeona wengi wamekuwa watetezi wakuu wa Chadema na hawapendi waguswe kwa namna yeyote kwa namna nyingine kama chama wameweza kushawishi jamii iweze kuwaonea huruma na kuwaamini katika yale wanayooamini kama dira ya mageuzi.
Kwa sasa unaweza ukasoma saikolojia ya wananchi ukaona kwamba wanachotaka ni kwamba CCM isiwepo madarakani na ukiuliza sababu wengi watakwambia wamechoka hawataki hata kusikia, ni hii hali unaweza kuithibitisha kwa jinsi wananchi wanavyokataa kupokea maneno, hotuba au maelezo, taarifa kutoka kwa watu wanaoonekana wako upande wa CCM, yaani wananchi hawaamini tena mfumo wa aina yeyote wa kiuongozi wa CCM iwe kiutawala au kiserikali au kichama unaweza kuyathibitisha haya ka njia mbalimbali ukisikiliza mawazo ya wananchi kwa mfano wanaposhiriki kwenye vipindi vya redio,televisioni,midahalo,makongamano unaona kabisa roho na nafsi zao zimegeuka na hawana tena mapenzi na CCM.
Sasa basi nikija kwenye mjadala kama M4C inaelekeza Mageuzi au Mapinduzi mimi kwa nafsi yangu naona ni mageuzi kwa sababu wametumia njia ya ushawishi,uwepo,na ukaribu na wananchi kutia hamasa kwenye vichwa vya wananchi na kuwaaaminisha wananchi kwamba CCM imefikia kikomo cha uwezo wa utawala,lakini ni lile la kufanya mambo kwa kushirikisha wananchi na kuwapa imani kwamba mwananchi yuko juu ya watawala,hili limepelekea kuongeza nguvu ya wananchi kujiamini na kujua kwamba wanaweza kudai haki zao.
Sasa ni juu ya CCM kupambana na kuweza kuweka misingi imara ya chama chao,kuondoa makundi ikitokea hata ikishindwa isije ikawa kama vyama vingine vya ukombo bali kibaki kujipanga na kurudi madarakani tena .