MDAHALO: Kikwete akivunja baraza la mawaziri atathibitisha udhaifu wake

..tatizo ni kwamba ameboronga kwa kiasi kikubwa and there is no time to correct the situation.

..labda aombe kuongezewa miaka mingine 5 ndiyo ataweza ku-accomplish kitu chochote za maana.
 
Je, unafikiri sasa hivi akivunja baraza la mawaziri au kufanyia kufanyia mabadiliko makubwa atajionesha kuwa ni kiongozi makini?

kwa kuwa atavunja baraza kwa shinikizo la wabunge na wananchi bado hataonesha kuwa kiongozi makini kwa sababu kama angalikuja yeye na hiyo idea tungemuona kuwa makini.
ila kwa ukweli hata pasingetokea hili by nature hayuko makini na hatakuwa.
 
acha alivunje, asipolivunja maana yake anafurahishwa na uozo unaendelea, na ndio itakuwa anaizika ccm:bathbaby:
akivunja atakuwa amekubali kuwa ni dhaifu asipovunja atauonesha udhaifu wake kuwa ni dhahiri.
 
Hana la kumshushia heshima kwa kuvunja baraza kwani hajawahi kulivunja baraza tangu ameingia madarakani ila alipata bahati mbaya kwa waziri mkuu wake wa kwanza kujiuzuru na kupelekea baraza lake la mawaziri kuvunjika.
 
raisi wa kwanza mzuri katika zama hizi ni yule atakayetuwekea mfumo mzuri. hata raisi awe mzuri kiasi gani mfumo wetu ni mbovu. ila kikwete anayo nafasi ya kuwa raisi wa historia kwa kutuwekea mfumo kupitia katiba mpya. akivunja atamuweka nani? ambaye anauhakika atafanya kazi vizuri.
tuko na tatizo la kimfumo, leo hii mwanasiasa anapewa wizara akianza kujifunza tu mda umeisha, kuna matatizo ya kiutendaji leo raisi anakupa wizara uongoze ina shirika yeye anateua mkurugenzi anateua mwenyekiti wa bodi sasa huyu akivurunda kama waziri umfukuze au ukamshitaki? je alipewa kwa uwezo wake wa kuliongoza au ni sababu nyingine. sasa tume ya katiba ndio itutatulie matatizo haya
mawazili wawe wataalamu sio mtu anachakuliwa sababu ni mbunge na kubalansi kutoka kila mkoa,
shirika lililo ndani ya wizara waziri ateue bodi na bodi iendeshe mchakato wa kumpata mkurugenzi
shirika kuna uozo bodi timua mkurugenzi tafuta mwingine, mmeshinwa wazili anawatimua, ameshinwa yeye ni raisi kumuwajibisha na mwingine akija anatafuta bodi yake na wao wanatafuta mkurugenzi

nafasi ya waziri mkuu tuondoe tumpe majukumu ya planning na kusimamia mipango hiyo kwa kila wizara mfano raisi akija na maisha bora kwa kila mtanzania waziri mkuu anatafsiri into action na kusimamia na huyu awe ni mtu mwenye ujuzi huo na mawaziri wawe na ujuzi katika sekta zao na uongozi

mfumo wetu ulivyo ni bahati nasibu na wazuri kwa kusimamia system haziwataki mtu kama mrema tusingekuwa tunamdhihaki
weka system itupeleke mbele sio watu maana ni ngumu kuwabaini
 
Kumekuwepo na tetesiza uwezekano wa kuvunjwa kwa baraza ka mawaziri wakati wowote kuanzia sasa. Na wapo watu ambao wametoa wito kwa rais kufanya hivyo. Je hoja ya mdahalo huu ni ya kweli au siyo kweli na kwa nini?

Hivi kwani mtu akiwakataa wezi na kuwawajibisha ni udhaifu? Pls badili heading yako kwanza ikae kizalendo
 
Aweza kuvunja baraza bila ya yeye akabakia mbora?

Itawezekana tu pale atakapovunja pia baraza la washauri wake, hawa ingawa hawaonekani kwetu lakini tunawaona kupitia ktk sura ya maamuzi yake...na hasa mfitini mkuu, ndumila kuwili, Nyoka wa mdimu Rweyemamu
 
Mawazo mgando!!! Namshauri ****** asiyafanyia kazi. You have stupid ideas as you look.
 
binafsi sidhani kama wabunge/mawaziri wengi wanatetea maslahi ya umma per se. Wabunge wengi wa ccm pamoja na baadhi ya mawaziri ambao we perceive them kama wachapa kazi na wenye msimamo wanafanya hivyo ili kujijenga kisiasa kikanda au kitaifa; kwa wengi pia ni njia ya kujikinga na dhoruba la chadema huko majimboni mwao as we head towards 2015. Sitashangaa kuona wabunge wengi wa sasa ccm kuhamia chadema katika kipindi cha mwisho mwisho kuelekea 2015. Hivyo mkuu kimbunga, sina ushahido tosha wa kuwaamini mwanri na magufuli kwa asilimia 100, wote hao nawaweka katika makundi hayo juu.

mimi naona muda umefika kwa sisi watanzania kusema 'no'kwa hawa wezi.
Kama serikali inalinda wezi pia tuseme sasa basi maana hakuna mtu atkaye toka nje ya tanzania kututete kama sio sisi wenyewe.

Kwa kuwa rais wetu naye anaka kimya kanakwamba mawazi wake wameonewa katika hili

kazi ni moja tu tuandamane mapema kabla hawaja malizia raslimali zetu.
 
..Udhaifu mkubwa utakuwa ni kushindwa kuvunja baraza,
kwa jinsi gani ni mdhoofu kuwawajibisha wakosefu!
 
JK kesha onyesha Udhaifu toka siku ya kwanza alotangaza nyumba za serikali hazitarudishwa..Toka siku ile watu wengi walianza kuondoa HOPE waliyoiweka kwake baada ya kujinadi sana ktk uchaguzi wa mwaka 2005, mimi nikiwa mmojawapo na lilipotokea sakata la EPA, Richmond, Buzwagi na TRA kupewa wahindi nilijua fika hatuna rais isipokuwa mwanasesere ktk vitabu vya Juma na Roza na Damasi.

Lakini pamoja na udhaifu wake, yeye ni reflection yetu sisi sema tu tumeshindwa kujitazama ktk kioo kwa kuhofia kujiona tulivyo na sura kama goti la mguu kihulka (wanafiki).. Kwa sababu tumeshindwa pia kufanya maamuzi magumu kutokana na sababu kama zake..Maana yeye ni mwajiriwa wetu na tunapomtaka yeye kama mwajiri wa serikali afanye maamuzi magumu akashindwa halafu nasi waajiri wake pia tukasuasua ina maana sisi wote ni jamii ile ile.
 
Back
Top Bottom