Chintu uko sahihi kabisa na kumlinganisha SITTA na SLAA ni kumuonea SLAA kwani aliyezuia ile hotuba isijadiliwe ni nani kama siyo SITTA? kwa hiyo yale alisema kutukoga wabongo na Bongo zenye tongotongo (hatuoni)
kuhusu Magufuli; Huyu ndo hovyo kabisa maana yeye ni mkandamizaji mkubwa wa demokrasia na hasa inapofikia kusema lolote kuhusu CHADEMA. Kumbuka maoni yake dhidi ya Mnyika; Dhidi ya Mbunge wa Ukerewe na dhidi ya CHADEMA kwa ujumla. I declare my interest; Mimi ni mwanchama wa CCM lakini unafiki wa Magufuli na viongozi aina yake dhidi ya demokrasia vinanikera sana. Sijafikiria kuhama CCM wala sidhani kama nitafikiria lakini lazima tujue nchi inaliwa na mijitu michache.
Kikwete avunje baraza la Mawaziri; thubutu!!! Kuna kiongozi mmoja wa juu ndani ya CCM aliwahi kusema; Ukitaka Kikwete atoe maamuzi manzito basi ni lazima mumshikilie asipate nafasi ya kutoka hadi aamue vile mnataka na ndiyo maana kuvunja secretariet ya kamati kuu ya CCM ililazimu mikutano ya non-stop hadi saa 6 usiku ndipo akaamua kuvunja na hata aliposhauriwa baada ya kuvunja usimrudishe yeyote kati ya wale wa zamani; alipopewa upenyo tu; Aliwarudisha baadhi yao kama Pindi chana na Chiligati.
Akivunja baraza hili; basi Waziri mkuu atakuwa Lukuvi na huo ndo utakuwa mwisho wa Ujenzi wa Mpanda University; Waziri wa Nishati na madini January Makamba naibu Kafumu Dalai; mambo ya Nje Emanuel Nchimbi naibu Sophia Simba (utani huu); Elimu ya Juu Prof Peter Msolla Naibu...
Hawezi; Nasema hawezi!!!!!!
Nakubaliana nawe mkuu, Ni kweli Sitta ni miongoni mwa watu waliojichanganya sana kipindi cha Kikwete. Mimi simtetei Sitta ila nadhani Sitta angeweza kuwa spika mzuri zaidi kama kungekuwa na Rais jamii ya Dr Slaa. Alijaribu na ana-deserve credit katika hilo, lakini ukiwa mtu makini ni vigumu sana kufanya kazi na Rais asiye na userious kwa lolote, maamuzi mengi mabovu aliyokuwa akifanya Mh Sitta alipokuwa spika alikuwa akiyafanya bila ridhaa ya moyo wake bali shinikizo. Haikuwa kazi rahisi, si unakumbuka kuna kipindi aliomba kuongezewa ulinzi? wenye chama chao wakamtishia kumnyanganya kadi? there were a lot happening behind the scene - Ingawa nakubali alitakiwa abaki jasiri.
Juu ya Magufuli I have mixed feelings, and I think you have a point.