Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,405
Labda ni wakati wa kuwaleta maadui wengine karibu zaidi; maana kuna wengine wanapiga kelele sana nje ya serikali sasa njia nzuri ni kuwaleta ndani... Fikiria wizara ya madini wakimtoa Ngeleja na kumuingiza mkosoaji wake mkuu; Ngeleja akiwa Mbunge atampa sapoti au na yeye atajitahidi kumsabotage?
Hakuna kitakacho badilika kwani yeyote atakayeteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini, ataendelea kuweka interest za wawekezaji mbele kwanza kabla za wenye rasilimali (watanzania). Kitakachobadilika labda ni uwiano tu wa 80:20, 70:30, n.k. Ngeleja ana mapungufu yake lakini Mbunge yeyoye atakayemrithi ni dhahiri hatoteuliwa based on Merit - kwa mfano the Mwanri's and Magufuli's haitatokea wakateuliwa kushika Wizara kama ya Nishati na Madini. Mbunge atakaye pelekwa pale lazima atateuliwa ili aende kwanza kulinda maslahi ya kisiasa, na pili, kuendelea kulinda maslahi ya wawekezaji, huku pia akiwa na jukumu la kuficha maovu yanayoendelea kule migodini, hasa ukweli kuhusu madhara ya kemikali kwa wananchi wasio na hatia. Kwa wenye rasilimali (watanzania wa maeneo yale), ni bahati mbaya sana kwamba watakachoendelea kuchuma itakuwa ni 'side effects'.
Vinginevyo iwapo atatoka, nadhani Ngeleja hatokuwa na la kufanya zaidi ya ku-adopt into siasa zisizofungamana na upande wowote kwani ni dhahiri kwamba bado 'atajali maisha yake na ya familia yake'.