Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,999
- Thread starter
- #81
Naam!! kumekuwa na ukimya kwa muda kutoka Zanzibar sasa hivi. Ukimya umetokana na kufanikiwa kwa kampeni hii ya Let Zanzibar Go. Tumewapa uhuru na njia zote za kuweza kutoka kwenye Muungano. Hata wanaosema "Muungano haufai" sasa hivi wanaimba "tunataka Muungano wa Mkataba". Ingawa hiili ni absurd sasa hivi hawazungumzi sana kutaka kuvunja Muungano kwa sababu wanajua kwa uhakika mkubwa watapa haki za kujidai na nchi yao lakini watakuwa wamewahukumu watoto wao kwenye maisha ya umaskini. Na kwa vile tayari wana chembe za mgawanyo wanajua kabisa kuwa Zanzibar nje ya Muungano wa aina yoyote haiwezi kufanikiwa. Kupe hawezi kumsusa ng'ombe!