Mdahalo: Hakuna wakati katika historia ambapo Zanzibar haikuitegemea Bara

Naam!! kumekuwa na ukimya kwa muda kutoka Zanzibar sasa hivi. Ukimya umetokana na kufanikiwa kwa kampeni hii ya Let Zanzibar Go. Tumewapa uhuru na njia zote za kuweza kutoka kwenye Muungano. Hata wanaosema "Muungano haufai" sasa hivi wanaimba "tunataka Muungano wa Mkataba". Ingawa hiili ni absurd sasa hivi hawazungumzi sana kutaka kuvunja Muungano kwa sababu wanajua kwa uhakika mkubwa watapa haki za kujidai na nchi yao lakini watakuwa wamewahukumu watoto wao kwenye maisha ya umaskini. Na kwa vile tayari wana chembe za mgawanyo wanajua kabisa kuwa Zanzibar nje ya Muungano wa aina yoyote haiwezi kufanikiwa. Kupe hawezi kumsusa ng'ombe!
 
Nguruvi3
Nilifikiri tumefikia hatua ya kuacha kuongelea Zanzibar na sasa tunaanza na muziki wa Tanganyika.

Kwa nini Zanzibar imegoma kuvunja muungano?
Jibu umeliweka hapo.

Sasa tujiulize, Kwa nini Tanganyika haichukui hatua ya kuvunja muungano?

Au kwa nini Tanganyika haifukuzi Zanzibar tegemezi kutoka katika muungano?

Mimi nitaeka suala la nyengeza hapa... Kwanini Tanganyika (Tanesco) haiwakatii umeme Zanzibar?
 
Nonda, inabidi uangalie jambo hili kwa uwiano. Tanganyika inamuona ZNZ kama mshiriki wa muungano na kutazama mazingira yaliyopo kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa.

Kiuchumi siku zote Tanganyika imeangalia ZNZ kwa udogo wake na pengine kujiuliza watu milioni 1.5 ni sawa na wakazi wa Ilala, hivyo ni rahisi wao kuchanganyika na Tanganyika bila kuiathiri Tanganyika ingawaje kinyume chake kina ukweli.
Utakapokaa meza moja na ZNZ na kuwaambi wachangie bajeti sawa ya nchi au ya muungano ni kukosa fikra.

Tanganyika inaona ni rahisi ku-accomodate ZNZ katika soko la biashara na ajira tofauti na itakavyoiangalia Kenya au uganda. Ni hakika si ZNZ tu hata nchi kama Burundi na Rwanda zinaangaliwa kwa jicho hilo.

Mathalani, kisisa, inajulikana kuna Warundi na Wanyarwanda wengi sana wanaishi bila bughudha ili mradi tu wanazingatia taratibu za nchi. Wote kama WZNZ ni wafaidika wa Tanganyika bila kuathiri Tanganyika kwasababu ya ukubwa na population. Lakini pia Tanganyika inafahamu vema ZNZ kisiasa.

Kiutamaduni ZNZ ina bahati sana kwasababu ipo karibu sana na Tanganyika kuliko nchi nyingine. Hata Uarabuni MZN hathamiwi kama anapokuwa Tanganyika. Aghalabu utasikia nenda kwa mpenda au Yakhe na wamejaa kila kona ya nchi hii. Pamoja na mambo mengine ya kijamii mwingiliano wa lugha na dini vimesadia sana.

Kwa mantiki hiyo Mzanzibar anaoenekana kama ndugu zaidi Tanganyika kuliko raia wa nchi nyingine ya ukanda huu.
Tatizo limeanza kujitokeza huko nyuma pale ZNZ walipoona wao ni bora zaidi kuliko Tanganyika na wana upper. Unakumbumbuka walianza na kuweka vikwazo vya Passport. Hapo Tanganyika ikaona undugu ni wa mashaka na kuwaambia WZNZ waje kwa passport. Hilo tu lilikuwa ujumbe tosha na wzn walinywea. mpaka leo

ZNZ imekua inalalamika hata pasipo na mashiko cha kushangaza hakuna maendeleo yanayotokana na wao kujiona bora zaidi au kuendeleza chuki na ubaguzi sifa za awali za wale wanotajwa na vitabu vitakatifu kuwa kama unafiki.

Kelele za sisi si koloni, wimbo wa taifa, bendera, chama cha mpira, CHANEZA, tunaibiwa kodi TRA, tunataka hela zaidi tusomeshe watoto wetu, hatulipi umeme n.k. Kibaya zaidi kuanza kuwachoma moto Watanganyika na kuweka sheria za kuwabana wao na si raia wa nchi nyingine, zimewaamsha Watanganyika wengi waliokuwa hawajali sana uwepo wa ZNZ.

Tanganyika haiwezi kuwafukuza wznz kwa kuona hawa ni ndugu zetu kwa mambo mengi, wanatutegemea, tumewakaribisha na tunawagharamia kama wao wanaona kuna walakini hewala warejee kwao.
Ndiyo wanasema znz ikitaka chochote ruksa hata leo wakiondoka katika muungano radhiaya marwidhaiyatan.

Maana ya haya ni kuwa kama umeamua kubeba mizigo nani atakukataza.
Ukarimu wa Tanganyika ni kwasababu hakuna cha kupoteza na ZNZ wanaodhani wanapoteza basi waamue.

Pia ina maana kuwa hakuna sababu ya kumchoma mznz moto wala kumuita malaya, jambazi n.k kama wanavyofanya wznz kwa kujua udhaifu wa ZNZ hasa katika ustaarabu.

Njia ya kuwafukuza wznz ni ya kisayansi tu ambayo ni kuweka masharti muhimu katika mambo yanayowagusa.
Kwa bahati nzuri Wznz wanaingia katika mtego huo. Ukiomba Tanganyika maana yake umefunga milango.
Tanganyika itawaangaliwa Watanganyika kama ZNZ inavyowaangalia watu wake.

Ukitaka mkataba Tanganyika itauliza unaweka nini mezani? mkataba wa nini. Kama hakuna mkataba, serikali 3 ua mbili maana yake ZNZ kwaherini. Kunasababu ya kumfukuza mtu hapo?

In other words, stay if you want, go if you decide.ZNZ wanaweza kuondoka any time na ni haki yao.
Je, umeona jinsi walivyobadilika ghafla. Abiria wanaomba nahodha abadili uelekeo. Serikali 3, mkataba, Uswiss, EU, Muungano wa New York na Cuba n.k.

Ni nani anayeng'angania muungano, yule anayedai serikali 3, mkataba wa Hawaii na Ghana au yule anayesema hey, please make up your mind otherwise pack and go!

Kwa muktadha huo Tanganyika haina sababu ya kuwafukuza Wznz. Inabana kidogo tu watasalimu amri kama walivyosalim wakati wa Passport, kama wanavyosalim sasa kwa kudai serikali 3 au mkataba wa Haiti na Congo.

Hakuna sababu wa kutoa povu, ni kukaza uzi kidogo tu. Seif keshatambua ugumu, Ali Salehe anajua, Ahmed Rajab la haulaa!! huyu ndiye amejisalimisha kabisa anasema tujadili aina ya muungano, kiburi na uchochezi wa kuvunja kwisha.

Sasa kunasababu ya kumfukuza mtu anyesema chonde chonde! Wakitaka waondoke, wakikubali wawe na nidhamu na kusema kwa kutumia mdomo na kichwa. Wadai wanachostahili na wakatae wasichostahili.

Ndoto za mchana hizo...
 
Ndoto za mchana hizo...
Ndoto ni zipi Mkubwa Takashi!
Hoja zipo hapo jibu hoja, kusema ndoto haitoshi, onyesha wapi ndoto za lunch zilipo.

Narudia, anayetapa tapa ni mznz kwa sasa. Umesikia Mtanganyika akiomba serikali 3 au mkataba wa Vanuata na Yemeni.
Mwanasheria mkuu wa Unguja kagoma, Maalim Kagoma, Seif ndiyo kabisa! yeye amekana hata sera za chama chake anataka EU sasa. Ahmed Rajab hana la kusema bali mkataba, Ally Salehe Kimyaa! Mansour serikali 3. Jusa serikali 3.
Nani amebaki?

Wznz wameulizwa serikali 3 ziweje hawana jibu ila kibwagizo tu, tatu mkataba!
Kwanini hamtaki kuvunja dau!

In short, sasa ZNZ kimyaa! option iliyobaki ni mkataba, nao tunauliza wa nini? Maana huu uliopo ni mkataba.
Mnataka mkataba wa kitu gani msichokisema? Ninyi ni koloni na mnadai uhuru pack and go simple!

LET ZNZ GO!
 
tupe yarehe hasa lini katika historia Zanzibar iliwahi kutegemea tanganyika?

Hesabu ni wazenj wa ngapi wapo bara na wabara wangapi wapo zenji hapo ndio utakapojua kuwa nani anamtegemea mwenzake, ukimaliza kuhesabu rudi tena nikupatie utegemezi mwingine u wapi?

 
Naam!! kumekuwa na ukimya kwa muda kutoka Zanzibar sasa hivi. Ukimya umetokana na kufanikiwa kwa kampeni hii ya Let Zanzibar Go. Tumewapa uhuru na njia zote za kuweza kutoka kwenye Muungano. Hata wanaosema "Muungano haufai" sasa hivi wanaimba "tunataka Muungano wa Mkataba". Ingawa hiili ni absurd sasa hivi hawazungumzi sana kutaka kuvunja Muungano kwa sababu wanajua kwa uhakika mkubwa watapa haki za kujidai na nchi yao lakini watakuwa wamewahukumu watoto wao kwenye maisha ya umaskini. Na kwa vile tayari wana chembe za mgawanyo wanajua kabisa kuwa Zanzibar nje ya Muungano wa aina yoyote haiwezi kufanikiwa. Kupe hawezi kumsusa ng'ombe!

Kwanza munge jaribu kuzuwia zile bahasha zenye hela zinazo sambazwa mitaani ... 5,000 tsh ndani ya bahasha kuna maoni yameshaandikwa tayari "mimi napenda Muungano uliopo uendelee kama uliyo, Serikali mbili, ya Jamuhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi"... Sasa kwa taarifa yenu, zile hela watu wanakula , na maaoni yao yatakua kinyume na matakwa yenu.

Tume inasubiriwa ianze kuchukua maoni Mjini Magharib hapo ile "trailer" aliyoonyeshwa SITTA, movie yake ndio itaanza. Simba wa UAMSHO wananoa makali yao.
 
Ndoto ni zipi Mkubwa Takashi!
Hoja zipo hapo jibu hoja, kusema ndoto haitoshi, onyesha wapi ndoto za lunch zilipo.

Narudia, anayetapa tapa ni mznz kwa sasa. Umesikia Mtanganyika akiomba serikali 3 au mkataba wa Vanuata na Yemeni.
Mwanasheria mkuu wa Unguja kagoma, Maalim Kagoma, Seif ndiyo kabisa! yeye amekana hata sera za chama chake anataka EU sasa. Ahmed Rajab hana la kusema bali mkataba, Ally Salehe Kimyaa! Mansour serikali 3. Jusa serikali 3.
Nani amebaki?

Wznz wameulizwa serikali 3 ziweje hawana jibu ila kibwagizo tu, tatu mkataba!
Kwanini hamtaki kuvunja dau!

In short, sasa ZNZ kimyaa! option iliyobaki ni mkataba, nao tunauliza wa nini? Maana huu uliopo ni mkataba.
Mnataka mkataba wa kitu gani msichokisema? Ninyi ni koloni na mnadai uhuru pack and go simple!

LET ZNZ GO!

Kimya kina mshindo....LET ZNZ GO!
 
Kwanza munge jaribu kuzuwia zile bahasha zenye hela zinazo sambazwa mitaani ... 5,000 tsh ndani ya bahasha kuna maoni yameshaandikwa tayari "mimi napenda Muungano uliopo uendelee kama uliyo, Serikali mbili, ya Jamuhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi"... Sasa kwa taarifa yenu, zile hela watu wanakula , na maaoni yao yatakua kinyume na matakwa yenu.

Tume inasubiriwa ianze kuchukua maoni Mjini Magharib hapo ile "trailer" aliyoonyeshwa SITTA, movie yake ndio itaanza. Simba wa UAMSHO wananoa makali yao.
Tunawatakia kheri simba wa UAMSHO na tunawaunga mkono kwa kila hali. Kinachonitatiza ni kuwa Simba wa vita Maalimu Seif Sharif Hamad, Ahmed Rajab, Ali Salehe, Ahmed Rajab, Mansour, Mwanasheria mkuu, Ismaili Jusa wote wamesalim amri, sasa hawa wa UAMSHO wataweza?

Tume ikifika mjini magharibi ambako ni ZNZ zaidi kuliko kwingine watu wasiume maneno, ni kusema Vunja muungano! period.

Nitakushangaa Takashi nikisikia simba wa uamsho wakijiuma uma. Nitashangaa nikisikia tunataka mkataba, au muungano kama ule wa Botswana na Senegal, au Ujerumani na Comoro!
Simba wa Uamsho wakijing'ata tu tutawaomba WZNZ wakae katika majamvi watulie tuli.
 
Shida moja ya Wazanzibar ni watu wabishi . Kama hamtaki Muungano mbona ni kitu rahisi ? Fungasha mizigo yenu wote na muondoke bara mtaona kama kuna mtu atawafuata huko visiwani
 
Mkuu Nonda,
Hatimaye kile anachosema mwanakijiji sasa kipo wazi, ima serikali moja au Let znz go.
Nadhani Nonda ni mpiga debe mkuu wa serikali 3. Huko nyuma wewe na Takashi mlishambulia hoja yangu ya uwepo wa Tanganyika ni maumivu kwa Zanzibar.

Napenda kuwajulisha kuwa wale mnaodhani wanawaonngoza, kumbe wanawadanya na hawajui wasemalo.
Kwa mwaka wa tatu mjadala wetu kuhusu ZNZ ukiwa na washiriki kama Jasusi,JokaKuu na Mkandara kwa uchache tumekuwa tunasema ZNZ na Wznz wanadanganywa, na tumeonekana wachochezi mawakala n.k.

Someni gazeti la Rai mwema toleo la wiki hii na hapa nanukuu kidogo tu kutoka kwa Ahmed Rajabu

''Wakati huohuo sidhani kama hapa tulipofika Wazanzibari wataridhika kuwa na muundo wa Muungano wa Serikali tatu ikiwa muundo huo utapendekezwa kuwa ndio uwe muundo mbadala wa kulifunika kombe na kuunusuru Muungano''

Ahmed Rajab amewakimbia wote kwa hoja yake ile ile aliyokuwa anaipigia debe miaka miwili. Bwana Rajab ambaye ni mkomoro anayeishi Nairobi na Uingereza amekuwa akiwapumbuza wznz kuhusu serikali 3 akishirikiana na Seif Hamad.
Wote kwa pamoja sasa wanakimbilia mkataba na wala hawana wazo la kuvunja muungano tena. Wamesalim amri baada ya kusikia Let znz go na kuwaacha akina Nonda na Takashi wakiwa na hoja za serikali 3.

Ahmed na Seif wamesoma maoni ya Watanganyika waliosema hakuna faida na Znz twaende zao.
Tumesema na binafsi nimeandika katika uzi huu na kule duru za siasa ya kuwa kitendo cha znz kuitaka Tanganyika irudi ni kujichimbia kaburi.

Tanganyika itakuwa na utaratibu wake na wala haitaweka nafasi ya wznz kutumia mianya ya muungano kunufaika. Tanganyika itasema ZNZ ni mzazi mwenzangu, tukae na tuongee tunamlea vipi mtoto muungano.
Kila nchi na hadhi yake. Seif na Ahmed ambao wantusoma wamebaini kuwa huko wanakowapeleka wznz ni kaburini na azma yao ya utegemezi haitakuwepo.

Sasa wamekimbilia mkataba. Tutawafuata huko huko na kuwauliza mkataba wa nini.
Znz ina bendera wimbo wa taifa,Rais bunge na sasa wanataka kiti UN. Swali wanataka mkataba wa kitu gani wasichokisema?

Hapo pia Ahmed Rajab anawaingiza mkenge maana kila mznz anaimba mkataba! mkataba! mkataba.
Muulize wa nini hakuna anayejibu au ajuaye una husu nini.
Tatizo la wznz ni kufuata mkumbo na jazba ndio maana Ahmed na Maalim Seif wanachezea akili zao kama kindergaten!

Sasa nielezeni enyi wana wa nchi ya ahadi;
Seif Sharif Hamad na Ahmed Rajab wamekana serikali 3. Ninyi mna hoja gani tofauti baada ya wakubwa kusalim amri.
Je mada hii isemayeo ZNZ ni tegemezi itake isitake ni uongo?

Ahmed na kundi lake la wana wa usultani linakana mchana kweupe! Hii ni aibu na dhalili kwa vichwa vya kizanzibar, kwamba watu milioni 1.2 wamemkabidhi Ahmed akili zao. Leo anasema serikali 3 wznz wote wanaimba, kesho anasema mkataba wznz wote wanajiunga na kwaya, keshokutwa atasema serikali 5 kama kawaida wznz hawana tafakuri wataimba tu utake usitake

Nasema kawakana vizuri sana na Kasalimu amri! mwenye hoja aje hapa Tusemezane, lakini kwanza ajue kuwa Ahmed amesalim amri na hataki tena serikali 3.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom