Mdahalo: Hakuna wakati katika historia ambapo Zanzibar haikuitegemea Bara

Jamani apa naongelea suala la security hawa jamaa wenyewe kwa wenyewe wana bifu sasa wakibaki alone si patafuka moshi

usiwaze hivo,kuwaza hivo ni kuonesha kua hakuna njia mbadala ya maisha tena,,,,,,ina maana bara wanawapenda sana wazenji kiasi kwamba hawataki kuwaona wakiuana???mbona january 2001 mkapa ndo alihusika kuwaua wazenji????wale tukijitenga nao wataish tu jamani,,,,kWATANGANYIKA SISI YUSIJIFANYE TUNAWAHURUMIA SANA WAZENJI,NI UNAFIKI HUO
 
Dhana hii ya Zanzibar kuitegemea Bara na kwamba bila bara Znzibar haiwezi sidhani kama ni sahihi.

Zanzibar inaweza ikawa inaitegemea sana bara kwa sasa kwasababu tu ya aina ya muungano uliopo lakini wakiwa nje ya muungano wataitegemea bara kwa maana ya kibiashara na pengine makazi kama ilivyo swazland na kwa south africa nk

Nchi kutegemea nchi nyingine kwa shughuli za kiuchumi ndio utandawazi wenyewe

umenena mdau,,,,,maana wale jamaa hawajapewa fursa,,,kama ndio vyuo vikuu vimeanza juzi tu hapa,,,hata Masters hawajaanza kutoa,,,,,Pia sisi watanganyika tunataka kujipa ukubwa kuwa zenji bila bara haiend,,,,,huu ndo uzush,sisi wenyewe hata vyandarua tunapewa na BUSH,hapa kiti muhim ni kuubadili muundo wa muungano au kuwaacha na maisha yao tu,,,,,WATASONGA WALE,SUDAN KUSINI ITAENDELEA HUKU ZENJI IKIWA INASHANGAA
 
hivi muungano ukivunjika hawa akina mwinyis, jumbes, bakhresas, amours, Karumes na other zanzibari political and economic elites waliolowea na wanaoishi Tanganyika tutawafanya nini?

Kabla ya kuwafikiria hao elites , uliowataja . Una wazo gani kwa hawa wachina, wasomali, wacongo,waburundi, wakenya ,wamalawi n,k. Ua ni waznz pekee ,kuwepo kwao hapo Tanganyika kunahitaji lazima kuwepo na Muungano?
 
Mwanakiji na wenzako, naomba nikusahihisheni.

"SISI SI WABARA, SISI NI WATANGANYIKA, TUNA VISIWA VYETU HUKU TANGANYIKA"

Acheni kurudia makosa yale yale kila siku.

Mtanganyika anayeishi kwenye visiwa vya Tanganyika ndio anayewezakuniita mimi M-bara.

Somo limeeeleweka.
 
hivi ni faida gani ambazo anazipata mtanganyika wa kawaida kwenye huu muungano.?
 
Liwalo na liwe muungano uvunjwe tuu then tuone nani anamuitaji mwenzake the most
 
Kabla ya kuwafikiria hao elites , uliowataja . Una wazo gani kwa hawa wachina, wasomali, wacongo,waburundi, wakenya ,wamalawi n,k. Ua ni waznz pekee ,kuwepo kwao hapo Tanganyika kunahitaji lazima kuwepo na Muungano?

Haya ni mawazo potofu...toka lini Tanganyika imeungana rasmi kisiasa au kiuchumi na china,drc,somalia au kenya? hawa hadi sasa wanaomba uraia, au work permit etc waznz wako hapa kama wananchi kwa miaka karibia 50...i didnt have to ans this but i thought unahitaji elimu ndogo ili uelewe tofauti
 
Mkandara,
..Ikiwa watagundua mafuta au gesi basi hawatatutegemea. vinginevyo nakuhakikishia watatafuta kila namna waendelee kuwa pamoja na Tanganyika.

..kuhusu utalii, mapato ya Tanganyika ktk sekta ya utalii ni around shilingi trilion 1.4, wakati Zanzibar wanaingiza around bilion 163.

..kukumbusha tu, katika bajeti hii ya juzi ofisi ya makamu wa raisi imetengewa kitita cha shilingi bilion 32 mahsusi kwa ajili ya Zanzibar. kabla ya hapo ZNZ waligoma kulipa sh bilion 40+ ambalo lilikuwa deni la tanesco.
Joka Kuu, kutegemeana ni jambo la kawaida na ZNZ itakuwa znz hata nje ya muungano.
Ukweli unabaki pale pale kuwa mpaka wa ZNZ ni Tanganyika na kupitia Tanganyika ZNZ inapakana na nchi 8 za Afrika mashariki. Hili linafanya ZNZ iwe na urahisi wa kufanya mambo yao.

Pili, utegemezi wa ZNZ kwa Tanganyika ni kama ule wa kuwa na bajeti ya ulinzi na uslama wasiolipia hata senti tano, bajeti ya elimu ya juu wasiolipia hata senti tano, achilia mbali umeme na mishahara.
Makamu wa Rais kapewa bilioni 32 kuziba pengo la bajeti.

Utegemezi wa ZNZ ni kutokana na ukweli kuwa hakuna nchi yoyote duniani iliyochukua WZN wengi kuliko Tanganyika.
Uwepo wa soko la ajira na biashara unapunguza msongamano mkubwa sana ZNZ.

Utegemezi wa ZNZ ni kuwa kisiwa hicho hakina ardhi ya kutosha kwahiyo baada ya muda maisha yatategemea nani mwenye pesa na siyo utu.

Uhashidi wa utegemezi wa ZNZ kwa Tanganyika unapatikana katika ukweli kuwa, wao wanadai nchi yao lakini WAMEGOMA NA WAMESHINDWA kuvunja muungano. Kelele zote za kuvunja muungano baada ya kupokelewa na Watanganyika sasa wamekaa kimya. Mtaani tunasema wameufyata.

Leo Maalimu Seif ameendelea na hadithi zake za kutapa tapa akisema watu watoe maoni kuhusu aina ya muungano.
Napenda muelewa hakusema kuvunja muungano kama wakati anaufakamia urais, amesema AINA YA MUUNGANO.
Maana yake anajua adha itakayomkabili mznz nje ya muungano akiwa na dola huru.

Maalimu Seif ameshauri uwepo muungano kama wa serikali 3 au mkataba au ule wa Ulaya.
Baada ya hoja za serikali 3 kushindwa kuetetewa na Wznz kwa hofu ya kuweka wazi utegemezi wao ikiwa ni pamoja na hoja ya mkataba sasa wanfikiria kama ule wa Ulaya.

Muungano wa Ulaya anaouongelea mfilisika wa siasa Malaimu Sefi ni kuwa tuwe na nchi mbili tofauti lakini turuhusu free movement of capital and labour. Hii ni ishashara nzuri kuwa ZNZ inategemea na itatemea Tanganyika hata kama ipo peke yake. Hatuwezi kuwa na 'EU' ya Tanganyika na ZNZ huu ni ushauri wa kupuuzwa sana.
Tunatakiwa tuwe na free movement of people, capital and labour tukiwa ndani ya EAC kama nchi tofauti.

ZNZ kwa kujua utegemezi wake ni Tanganyika ndiyo maana inakuja na suluhu za kuchekesha sana.
Mkataba hawauelezi uwe wa nini, tunajua wanataka uwe wa kusaidia shida zao
Serikali 3 hatujui ziwe za nini, tunajua wanataka zisadie shida zao
Muungano wa Uswiss hatujui ukoje, tunajua ni kutapa tapa
Muungano wa EU, tunajua ni kutapa tapa kwanini tusiwe na EU model ndani ya EAC, eti tuwe na ya Tanganyika na ZNZ?

Kwanini wamegoma kuvunja muungano? Jibu ni kuwa utegemezi utafikia mwisho, znz itakuwepo tu kama ilivyo Haiti au Comoro ambazo ni huru na zina dola.

Kitendo chao cha kushindwa na kugoma kuvunja muungano ni ushahidi wa kutaka Utegemezi na hapo namjibu Mwanakijiji kuwa 'Nakubali' utegemezi ni lazima na muhimu kwao watake wasitake.
 
JokaKuu

Iliwekwa thread juu ya Jussa Kumtukana/kumdhalilisha Sitta.Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...tta-nyerere-na-wa-tz-bara-18.html#post3071438

Hii ripoti inayotajwa na Jussa, Prof. Teddy ameigusia katika kufikia hitimisho la utafiti wake/wao?

Mimi napata tabu kuamini kuwa Zanzibar wanaweza kugoma tu kutochangia au kulipa kile walichokubaliana na Tanganyika kifanyike. Lazima kuna kitu kimejificha au kinafichwa hapa.

Lakini leo nikubali hitimisho la Prof. Teddy kuwa Zanzibar ndiyo tegemezi au inayonufaika na Muungano/ inapata faida.
Sasa tuone upande mwengine wa hoja, Tanganyika inaibeba Zanzibar(inaipa faida Zanzibar) na kwa hivyo, Tanganyika inajiingiza hasara/ inapata hasara na inaendelea kufanya hivyo.

Kuna hoja ya kuwa Zanzibar wanang'ang'ania muungano. Kama hitimisho la Prof. Teddy ni sahihi basi inaingia akilini kuwa Zanzibar yenye kupata faida(inayofaidika) kung'ang'ania muungano.
Je kwa Tanganyika ambayo inapata hasara kwa nini mbali na umaskini uliopo(inakopa, misaada na ufadhili) inaendelea kuipa Zanzibar faida huku yenyewe inapata hasara, na tuseme,hainga'ng'anii muungano?

Kitu ambacho mimi sikifahamu, au hakiingii akilini ni kwa nini Tanganyika iingie hasara na iendelee kubeba kiroba cha misumari? Je huu si ndio hasa ungefaa kuitwa ung'ang'anizi wa muungano?

Lakini, Hasara yote hii ambayo Tanganyika inapata katika Muungano badala ya kudai kuvunja muungano, inafanya kila mbinu kuleta serikali moja. Pia wanatokea watu wenye mawazo kuwa tudai serikali moja. Je hili ndio suluhisho la kutoingia hasara? Au kukiwa na serikali moja ndio faida itapatikana(Manufaa ya muungano yatapatikana)? Kwa vipi?

Na mfumo huo wa serikali moja utakuwa ni mfumo wa aina ipi ya Muungano?

Mimi nasimama kuwaomba wabunge wa Tanganyika wapeleke Mswada binafsi wa kutaka Zanzibar ifukuzwe katika Muungano. Au wabunge wote wa upande wa Tanganyika (bara) wanabariki mazingaombwe ya muungano unaoutia Tanganyika hasara? Uzalendo uko wapi?

kimsingi mkuu ukiuangalia muungano kwenye angle yako utapasuka kichwa kwa maswali na mawazo.Huu muungano ni wa kisiasa na siasa mara nyingi hazina mantiki. Kwa hiyo Nyerere et el waliamua tu juu juu kufanya hiki kitu bila ya kuangalia athari za kiuchumi na mantiki yake kiuongozi.

Huwa naona aibu nikijaribu kumuelezea mgeni toka nje ya nchi haswa hawa jirani zetu wa maziwa makuu namna huu muungano ulivyo/unavyofanya kazi. Mara nyingi uwa haiingii akilini kwa mtu makini yeyote kuhusu huu muungano na jinsi unavyojaribu kuuelezea ndivyo unavyoonekana irrational
 
Haya ni mawazo potofu...toka lini Tanganyika imeungana rasmi kisiasa au kiuchumi na china,drc,somalia au kenya? hawa hadi sasa wanaomba uraia, au work permit etc waznz wako hapa kama wananchi kwa miaka karibia 50...i didnt have to ans this but i thought unahitaji elimu ndogo ili uelewe tofauti

Kumbe jibu analijua lakini huachi kuuliza masuala ya kipumbavu...Kuwepo kwa waznz Tanganyika hakuhitaji Muungano.Sawa na kuwepo kwa waTngka Zanzibar vile vile hakuhitaji Muumgano, sheria za uhamiaji zipo.
 
Joka Kuu, kutegemeana ni jambo la kawaida na ZNZ itakuwa znz hata nje ya muungano.
Ukweli unabaki pale pale kuwa mpaka wa ZNZ ni Tanganyika na kupitia Tanganyika ZNZ inapakana na nchi 8 za Afrika mashariki. Hili linafanya ZNZ iwe na urahisi wa kufanya mambo yao.

Pili, utegemezi wa ZNZ kwa Tanganyika ni kama ule wa kuwa na bajeti ya ulinzi na uslama wasiolipia hata senti tano, bajeti ya elimu ya juu wasiolipia hata senti tano, achilia mbali umeme na mishahara.
Makamu wa Rais kapewa bilioni 32 kuziba pengo la bajeti.

Utegemezi wa ZNZ ni kutokana na ukweli kuwa hakuna nchi yoyote duniani iliyochukua WZN wengi kuliko Tanganyika.
Uwepo wa soko la ajira na biashara unapunguza msongamano mkubwa sana ZNZ.

Utegemezi wa ZNZ ni kuwa kisiwa hicho hakina ardhi ya kutosha kwahiyo baada ya muda maisha yatategemea nani mwenye pesa na siyo utu.

Uhashidi wa utegemezi wa ZNZ kwa Tanganyika unapatikana katika ukweli kuwa, wao wanadai nchi yao lakini WAMEGOMA NA WAMESHINDWA kuvunja muungano. Kelele zote za kuvunja muungano baada ya kupokelewa na Watanganyika sasa wamekaa kimya. Mtaani tunasema wameufyata.

Leo Maalimu Seif ameendelea na hadithi zake za kutapa tapa akisema watu watoe maoni kuhusu aina ya muungano.
Napenda muelewa hakusema kuvunja muungano kama wakati anaufakamia urais, amesema AINA YA MUUNGANO.
Maana yake anajua adha itakayomkabili mznz nje ya muungano akiwa na dola huru.

Maalimu Seif ameshauri uwepo muungano kama wa serikali 3 au mkataba au ule wa Ulaya.
Baada ya hoja za serikali 3 kushindwa kuetetewa na Wznz kwa hofu ya kuweka wazi utegemezi wao ikiwa ni pamoja na hoja ya mkataba sasa wanfikiria kama ule wa Ulaya.

Muungano wa Ulaya anaouongelea mfilisika wa siasa Malaimu Sefi ni kuwa tuwe na nchi mbili tofauti lakini turuhusu free movement of capital and labour. Hii ni ishashara nzuri kuwa ZNZ inategemea na itatemea Tanganyika hata kama ipo peke yake. Hatuwezi kuwa na 'EU' ya Tanganyika na ZNZ huu ni ushauri wa kupuuzwa sana.
Tunatakiwa tuwe na free movement of people, capital and labour tukiwa ndani ya EAC kama nchi tofauti.

ZNZ kwa kujua utegemezi wake ni Tanganyika ndiyo maana inakuja na suluhu za kuchekesha sana.
Mkataba hawauelezi uwe wa nini, tunajua wanataka uwe wa kusaidia shida zao
Serikali 3 hatujui ziwe za nini, tunajua wanataka zisadie shida zao
Muungano wa Uswiss hatujui ukoje, tunajua ni kutapa tapa
Muungano wa EU, tunajua ni kutapa tapa kwanini tusiwe na EU model ndani ya EAC, eti tuwe na ya Tanganyika na ZNZ?

Kwanini wamegoma kuvunja muungano? Jibu ni kuwa utegemezi utafikia mwisho, znz itakuwepo tu kama ilivyo Haiti au Comoro ambazo ni huru na zina dola.

Kitendo chao cha kushindwa na kugoma kuvunja muungano ni ushahidi wa kutaka Utegemezi na hapo namjibu Mwanakijiji kuwa 'Nakubali' utegemezi ni lazima na muhimu kwao watake wasitake.

Bw, Nguruvi3

Nyerere ndio alikuja Zanzibar kuomba Muungano. Hakuna mznz anaelilia Muungano ,hiyo dhana yako potofu kuwa wznz wanalilia Muungano jaribu kuifuta kichwani vinginevyo inakuzeesha vibaya.

Wanao lazimisha Muungano ni Vingunge wenzio wa Bara, kwa maana ya sio watu wa pwani. Wameanza kugawa hela Zanzibar, kila kwenye bahasha kuna 5,000 tsh na maoni yamesha andikwa tayari ya kutaka Muungano uendelee kama ulivyo. Muungano mkiwa tayari mtauvunja nyinyi kwasababu ndio mnashikilia mpini. Lakini sisi tutaendelea kuwasakama na kuwanyima usingizi mpaka mtaachia wenyewe.

Harakati bado hazijapamba moto ,ndio kwanza mazoezi tu.... LET ZNZ GO!
 
Kumbe jibu analijua lakini huachi kuuliza masuala ya kipumbavu...Kuwepo kwa waznz Tanganyika hakuhitaji Muungano.Sawa na kuwepo kwa waTngka Zanzibar vile vile hakuhitaji Muumgano, sheria za uhamiaji zipo.

wewe ndiyo mpumbavu kwa kuchukulia vitu juu juu...kwa nini russia na ukraine wana matatizo kuhusu uhamiaji, kwa nini sudan na south sudan wana matatizo hayo hayo...nchi zikiwa moja kwa muda mrefu na baadae kuvunjika lazima raia wa pande zote mbili waangaliwe kwa macho zaidi na kuwekewa vizingiti kuliko wahamiaji au raia wa mataifa ya nje...kumbuka muungano hautavunjika kwa mapenzi ya karibu ya watawala...na hapa kuna shida katika pande zote za wananchi wanaoishi katika pande nyingine...wenyewe hawatakua sawa na wahamiaji wengine at least kwa muda fulani ambao nafikiri utakua ni mrefu tu kutokana na urefu wa muungano wenyewe...Mkapa alivyosema watz ni wavivu kufikiria hakukosea na wewe ni mmoja wao ukijumlisha na avatar yako ya kijinga unaonekana huko chini sana kwa umakini na upambanuzi wa mawazo na uwezo wa kuelewa kuanza mdahalo chanya na mimi....
 
Zanzibar haiwezi kusimama bila ya bara? Nafikiri tunahitaji kutoka nje ya box ili tuweze kufikiria kwa kina zaidi au kuna umuhimu wa kufanya utafiti kidogo kuhusu nyingine au visiwa vilivyo katika mazingira sawa na Zanzibar.

Just a food for thoughts.
1) Je bara imeweza kusimama yenyewe baadaya ya miaka 50 ya Uhuru?
2) Ni asilimia ngapi ya budget ya budget yetu inategemea wahisani, na je inajitosheleza au kwa kuwa tumesharidhika na kufunga mkanda kila leo?
3) Je Tanganyika ni bora zaidi kwa vigezo vipi kwa maisha ya mtu wa kawaida? Tusizungumze mali asili ambazo mimi na wewe ni kama hazitunufaishi ipasavyo
 
Zatara,

..umetoa hoja nzuri kwamba Tanganyika ni omba-omba kwasababu bajeti yetu inategemea wahisani.

..lakini ZNZ ni omba-omba zaidi na zaidi kwasababu bajeti yenu inategemea omba-omba mwingine ambaye ni Tanganyika.

..yaani ikifikia mahali mtu[ZNZ] anamuomba au "kumpiga shindano" ombaomba kama Matonya[Tanganyika], basi ujue mtu huyo[ZNZ] ana hali mbaya kwelikweli.
 
wewe ndiyo mpumbavu kwa kuchukulia vitu juu juu...kwa nini russia na ukraine wana matatizo kuhusu uhamiaji, kwa nini sudan na south sudan wana matatizo hayo hayo...nchi zikiwa moja kwa muda mrefu na baadae kuvunjika lazima raia wa pande zote mbili waangaliwe kwa macho zaidi na kuwekewa vizingiti kuliko wahamiaji au raia wa mataifa ya nje...kumbuka muungano hautavunjika kwa mapenzi ya karibu ya watawala...na hapa kuna shida katika pande zote za wananchi wanaoishi katika pande nyingine...wenyewe hawatakua sawa na wahamiaji wengine at least kwa muda fulani ambao nafikiri utakua ni mrefu tu kutokana na urefu wa muungano wenyewe...Mkapa alivyosema watz ni wavivu kufikiria hakukosea na wewe ni mmoja wao ukijumlisha na avatar yako ya kijinga unaonekana huko chini sana kwa umakini na upambanuzi wa mawazo na uwezo wa kuelewa kuanza mdahalo chanya na mimi....

Wewe na huyo Mkapa Unae muamini nyote kundi moja, miaka kumi ya utawala wake nini kikubwa kawafanyia watz? Laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake, Kwa mauwaji aliyowafanyia waznz. Asisahau siku CCM ikiondoka madarakini basi na yeye safari ya mahakama za kimataifa anayo...

Muulize waziri wako wa Afya ananijua mimi nani... MSIBABAISHE WATU HAPA NA HIZO PRE-INSTALLED MIND SET ZENU...
 
Zatara,

..umetoa hoja nzuri kwamba Tanganyika ni omba-omba kwasababu bajeti yetu inategemea wahisani.

..lakini ZNZ ni omba-omba zaidi na zaidi kwasababu bajeti yenu inategemea omba-omba mwingine ambaye ni Tanganyika.

..yaani ikifikia mahali mtu[ZNZ] anamuomba au "kumpiga shindano" ombaomba kama Matonya[Tanganyika], basi ujue mtu huyo[ZNZ] ana hali mbaya kwelikweli.

@Jokakuu,
Mi naamini kuna nchi /Visiwa ambazo ni maskini na ambavyo havina resources za kutosha kama zanzibar. Ila Zanzibar inaweza kusimama vizuri peke yake kama itakuwa na viongozi bora (Ambalo nina mashaka sana). Pia Mainland inaweza kusimama vyema iwapo itakuwa na uongozi bora, siamini sana katika swala la muungano.

Please, we don't have to let pressure make us panic when we get stranded. Kuna tatizo somewhere... na linajulikana. Hii swala la Wabara wanachukua kazi zetu warudi kwao.... Mara waunguja warudi kwao ili turithi maduka... Mimi binafsi naona tunahitaji kuona nje ya hapo
 
..ni kweli matatizo ya wa-Tanganyika pamoja na ya wa-ZNZ kwa kiasi kikubwa yanasababishwa na UONGOZI MBOVU.

..tatizo la wenzetu wa-ZNZ ni kwamba badala ya kuwashughulikia viongozi wao, wameamua kuelekeza hasira na chuki kwa wa-Tanganyika.

..tafuta video za Uamsho utakuta wa-ZNZ wanalalamika kwamba wa-Tanganyika wamepelekea popobawa,malaya,ukimwi,pombe, pamoja na uchafu mwingine mwingi. soma maandiko yao ktk www.mzalendo.net uone jinsi wanavyochochea chuki dhidi ya wa-Tanganyika.
 
Joka Kuu,
Kwanini wamegoma kuvunja muungano? Jibu ni kuwa utegemezi utafikia mwisho, znz itakuwepo tu kama ilivyo Haiti au Comoro ambazo ni huru na zina dola.

Kitendo chao cha kushindwa na kugoma kuvunja muungano ni ushahidi wa kutaka Utegemezi na hapo namjibu Mwanakijiji kuwa 'Nakubali' utegemezi ni lazima na muhimu kwao watake wasitake.

Nguruvi3
Nilifikiri tumefikia hatua ya kuacha kuongelea Zanzibar na sasa tunaanza na muziki wa Tanganyika.

Kwa nini Zanzibar imegoma kuvunja muungano?
Jibu umeliweka hapo.

Sasa tujiulize, Kwa nini Tanganyika haichukui hatua ya kuvunja muungano?

Au kwa nini Tanganyika haifukuzi Zanzibar tegemezi kutoka katika muungano?
 
Nonda, inabidi uangalie jambo hili kwa uwiano. Tanganyika inamuona ZNZ kama mshiriki wa muungano na kutazama mazingira yaliyopo kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa.

Kiuchumi siku zote Tanganyika imeangalia ZNZ kwa udogo wake na pengine kujiuliza watu milioni 1.5 ni sawa na wakazi wa Ilala, hivyo ni rahisi wao kuchanganyika na Tanganyika bila kuiathiri Tanganyika ingawaje kinyume chake kina ukweli.
Utakapokaa meza moja na ZNZ na kuwaambi wachangie bajeti sawa ya nchi au ya muungano ni kukosa fikra.

Tanganyika inaona ni rahisi ku-accomodate ZNZ katika soko la biashara na ajira tofauti na itakavyoiangalia Kenya au uganda. Ni hakika si ZNZ tu hata nchi kama Burundi na Rwanda zinaangaliwa kwa jicho hilo.

Mathalani, kisisa, inajulikana kuna Warundi na Wanyarwanda wengi sana wanaishi bila bughudha ili mradi tu wanazingatia taratibu za nchi. Wote kama WZNZ ni wafaidika wa Tanganyika bila kuathiri Tanganyika kwasababu ya ukubwa na population. Lakini pia Tanganyika inafahamu vema ZNZ kisiasa.

Kiutamaduni ZNZ ina bahati sana kwasababu ipo karibu sana na Tanganyika kuliko nchi nyingine. Hata Uarabuni MZN hathamiwi kama anapokuwa Tanganyika. Aghalabu utasikia nenda kwa mpenda au Yakhe na wamejaa kila kona ya nchi hii. Pamoja na mambo mengine ya kijamii mwingiliano wa lugha na dini vimesadia sana.

Kwa mantiki hiyo Mzanzibar anaoenekana kama ndugu zaidi Tanganyika kuliko raia wa nchi nyingine ya ukanda huu.
Tatizo limeanza kujitokeza huko nyuma pale ZNZ walipoona wao ni bora zaidi kuliko Tanganyika na wana upper. Unakumbumbuka walianza na kuweka vikwazo vya Passport. Hapo Tanganyika ikaona undugu ni wa mashaka na kuwaambia WZNZ waje kwa passport. Hilo tu lilikuwa ujumbe tosha na wzn walinywea. mpaka leo

ZNZ imekua inalalamika hata pasipo na mashiko cha kushangaza hakuna maendeleo yanayotokana na wao kujiona bora zaidi au kuendeleza chuki na ubaguzi sifa za awali za wale wanotajwa na vitabu vitakatifu kuwa kama unafiki.

Kelele za sisi si koloni, wimbo wa taifa, bendera, chama cha mpira, CHANEZA, tunaibiwa kodi TRA, tunataka hela zaidi tusomeshe watoto wetu, hatulipi umeme n.k. Kibaya zaidi kuanza kuwachoma moto Watanganyika na kuweka sheria za kuwabana wao na si raia wa nchi nyingine, zimewaamsha Watanganyika wengi waliokuwa hawajali sana uwepo wa ZNZ.

Tanganyika haiwezi kuwafukuza wznz kwa kuona hawa ni ndugu zetu kwa mambo mengi, wanatutegemea, tumewakaribisha na tunawagharamia kama wao wanaona kuna walakini hewala warejee kwao.
Ndiyo wanasema znz ikitaka chochote ruksa hata leo wakiondoka katika muungano radhiaya marwidhaiyatan.

Maana ya haya ni kuwa kama umeamua kubeba mizigo nani atakukataza.
Ukarimu wa Tanganyika ni kwasababu hakuna cha kupoteza na ZNZ wanaodhani wanapoteza basi waamue.

Pia ina maana kuwa hakuna sababu ya kumchoma mznz moto wala kumuita malaya, jambazi n.k kama wanavyofanya wznz kwa kujua udhaifu wa ZNZ hasa katika ustaarabu.

Njia ya kuwafukuza wznz ni ya kisayansi tu ambayo ni kuweka masharti muhimu katika mambo yanayowagusa.
Kwa bahati nzuri Wznz wanaingia katika mtego huo. Ukiomba Tanganyika maana yake umefunga milango.
Tanganyika itawaangaliwa Watanganyika kama ZNZ inavyowaangalia watu wake.

Ukitaka mkataba Tanganyika itauliza unaweka nini mezani? mkataba wa nini. Kama hakuna mkataba, serikali 3 ua mbili maana yake ZNZ kwaherini. Kunasababu ya kumfukuza mtu hapo?

In other words, stay if you want, go if you decide.ZNZ wanaweza kuondoka any time na ni haki yao.
Je, umeona jinsi walivyobadilika ghafla. Abiria wanaomba nahodha abadili uelekeo. Serikali 3, mkataba, Uswiss, EU, Muungano wa New York na Cuba n.k.

Ni nani anayeng'angania muungano, yule anayedai serikali 3, mkataba wa Hawaii na Ghana au yule anayesema hey, please make up your mind otherwise pack and go!

Kwa muktadha huo Tanganyika haina sababu ya kuwafukuza Wznz. Inabana kidogo tu watasalimu amri kama walivyosalim wakati wa Passport, kama wanavyosalim sasa kwa kudai serikali 3 au mkataba wa Haiti na Congo.

Hakuna sababu wa kutoa povu, ni kukaza uzi kidogo tu. Seif keshatambua ugumu, Ali Salehe anajua, Ahmed Rajab la haulaa!! huyu ndiye amejisalimisha kabisa anasema tujadili aina ya muungano, kiburi na uchochezi wa kuvunja kwisha.

Sasa kunasababu ya kumfukuza mtu anyesema chonde chonde! Wakitaka waondoke, wakikubali wawe na nidhamu na kusema kwa kutumia mdomo na kichwa. Wadai wanachostahili na wakatae wasichostahili.
 
Back
Top Bottom