Mdahalo: Hakuna wakati katika historia ambapo Zanzibar haikuitegemea Bara

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Tangu historia ya kale Visiwa vya Zanzibar zimeishi na kufanikiwa kwa kutegemea bara (eneo la mwambao wa Afrika ya Mashariki) na hata maeneo ya ndani ya Afrika. Kufanikiwa kokote kule kunakotajwa kuhusu Zanzibar kumetokana daima na mahusiano yake ya karibu na bara.

Bila Bara Zanzibar haiwezi kufanikiwa hata leo hii. Lakini zaidi mafanikio yake ya huko nyuma yalitokana sana na Zanzibar kuwa na ukuu wa kutawala maeneo ya bara. Haijawahi kufanikiwa bila kuwa na nguvu ya kiutawala au kisiasa huko bara.

Hili linaonekana hata leo hii katika MUungano wetu ambapo Zanzibar bado wanaonekana kuwa na maamuzi mengi kuhusiana na bara na wanafanikiwa zaidi kwa mgongo wa bara na sasa wapo wanaotaka izidi kufanikiwa kwa kile wanachokiita "kuondolewa kero za Muungano".

Hata Muungano ukivunjika bado Zanzibar itajikuta inaitegemea bara kwa namna nyingi zaidi - kiuchumi, ongezeko lake la watu, kiusalama n.k Hii ni kweli isiyopingika.

Kubali au kataa.
 
Kuna wasanii wengi tu wa Kizanzibari ambao mafanikio yao kwa kiasi kikubwa sana wameyapatia bara.

Bila bara wasingekuwa na hayo mafanikio waliyonayo sasa.
 
Zanzibar hawatakaa wajue umuhimu wa muungano kwao mpaka siku muungano utakapovunjika bse haitakuwa zanzibar tena bali pemba na unguja
wanajiita wazanzibar bse wako ndani ya muungano nje ya muungano hakuna kitu kama zenji
 
Jamani tusijifarague kuwa zanzibar bila bara haiwezekani,,,,,tuwaachen wafanye mambo yao,,,kwani TANZANIA MBONA HAKUNA BAJETI INAYOIANDAA BILA KUTEGEMEA AMERIKA???WHY NOT ZENJ,,,,MIDAHALO MINGINE IWE NA TIJA,,,,SISI KILA SIKU TUNAZUNGUMZIA KUJITEGEMEA,BASI NA WAO TUWAACHE,KAMA SUALA NI HISTORIA BASI NA BARA NAKO KIHISTORIA TUNAITEGEMEA ZANZIBA KIUSALAMA,dunia ya leo kutegemeana kupo kwa kila aina,,,,wewe una hiki yule ana kile,,,yeye anahitaj chako nawe unahitaji chake,,,,,,,,
 
kuna siku Boflo aliweka uzi jukwaa hili, alisema kwa utafiti wake amegundua wazanzibar wanataka kuuvunjilia mbali muungano kwakuwa unawanyonya, upande wa pili wabara hawataki kuuvunja muungano kwasababu wanadai zanzibar itawakumbuka bara muungano ukivunjwa.. pia alihoji vitisho vyote vya nini kwa wazenji?

kwahiyo mwanakijiji hivi vitisho manamtisha nani haswa hata muungano ukivunjika watakaoteseka si ni wazenji sasa nyinyi shida zao zinawahusu nini? fuateni yenu!
 
Last edited by a moderator:
kuna siku Boflo aliweka uzi jukwaa hili, alisema kwa utafiti wake amegundua wazanzibar wanataka kuuvunjilia mbali muungano kwakuwa unawanyonya, upande wa pili wabara hawataki kuuvunja muungano kwasababu wanadai zanzibar itawakumbuka bara muungano ukivunjwa.. pia alihoji vitisho vyote vya nini kwa wazenji?

kwahiyo mwanakijiji hivi vitisho manamtisha nani haswa hata muungano ukivunjika watakaoteseka si ni wazenji sasa nyinyi shida zao zinawahusu nini? fuateni yenu!

exactly....
 
...........Historically can be true but logically, am still sing that good song bro!............LET ZANZIBAR GO!!!!!!!!!........LET ZANZIBAR GO!!!!!!!!!........LET ZANZIBAR GO!!!!!!!!!
 
Tangu historia ya kale Visiwa vya Zanzibar zimeishi na kufanikiwa kwa kutegemea bara (eneo la mwambao wa Afrika ya Mashariki) na hata maeneo ya ndani ya Afrika. Kufanikiwa kokote kule kunakotajwa kuhusu Zanzibar kumetokana daima na mahusiano yake ya karibu na bara. Bila Bara Zanzibar haiwezi kufanikiwa hata leo hii. Lakini zaidi mafanikio yake ya huko nyuma yalitokana sana na Zanzibar kuwa na ukuu wa kutawala maeneo ya bara. Haijawahi kufanikiwa bila kuwa na nguvu ya kiutawala au kisiasa huko bara. Hili linaonekana hata leo hii katika MUungano wetu ambapo Zanzibar bado wanaonekana kuwa na maamuzi mengi kuhusiana na bara na wanafanikiwa zaidi kwa mgongo wa bara na sasa wapo wanaotaka izidi kufanikiwa kwa kile wanachokiita "kuondolewa kero za Muungano".

Hata Muungano ukivunjika bado Zanzibar itajikuta inaitegemea bara kwa namna nyingi zaidi - kiuchumi, ongezeko lake la watu, kiusalama n.k Hii ni kweli isiyopingika.

Kubali au kataa.
Mkuu wangu naona bado unajaribu kuonyesha mapenzi yako ktk sisi kuungana na Zanzibar. Hii dhana ya kwamba Zanzibar bila bara haiwezekani ni sawa kabisa na ile walotumia Warusi ya kwamba pasipo muungano wao nchi nyingine haziwezi kuendelea. Hakuna ukweli wowote ktk maenelzo haya na pengine hufahamu kwamba wakati wa Uhuru wa Zanzibar chini ya Shamte walitaka kuwa karibu zaidi na Kenya kuliko Tanganyika.

Hivyo hivyo sisi pia tuliwategemea Zanzibar zaidi kutokana na kwamba Usalama wetu unategemea sana mahusiano ya Zanzibar, Uchumi wa Bara unaendeshwa pia na Wazanzibar kina Bakhresa na wapemba waliochukua mji wa Kariakoo na Temeke ambazo ni source ya income ya mji wa Dar. Kifupi huwezi kusema mke anamtegemea sana mume fulani au mume anamtegemea sana mke fulani. hata ndoa ikivunjika kila mmoja wao atakuwa na maisha yake na wengine watatokea pengine wabora zaidi - LET ZNZ GO!
 
Mkuu wangu naona bado unajaribu kuonyesha mapenzi yako ktk sisi kuungana na Zanzibar. Hii dhana ya kwamba Zanzibar bila bara haiwezekani ni sawa kabisa na ile walotumia Warusi ya kwamba pasipo muungano wao nchi nyingine haziwezi kuendelea. Hakuna ukweli wowote ktk maenelzo haya na pengine hufahamu kwamba wakati wa Uhuru wa Zanzibar chini ya Shamte walitaka kuwa karibu zaidi na Kenya kuliko Tanganyika.

Hivyo hivyo sisi pia tuliwategema zanzibar zaidi kutokanma na kwamba Usalama wetu unategema sana mahusiano ya Zanzibar, Uchumi wa Bara unaendeshwa pia na Wazanziba kina Bakhresa na wapemba waliochukua mji wa Kariakoo na Temeke ambazo ni sourece ya income ya mji wa Dar. Kifupi huweiz kuema mke anamtegema sana mume fulani au mume anamtegemea sana mke fulani. gata ndoa ikivunjika kila mmoja wao atakuwa na maisha yake na wengine watatokea pengine wabora zaidi - LET ZNZ GO!

nionavyo mimi ndo na wewe umeling'amua hilo,MM yeye anataka kuupalilia kwa kuonyesha kuwa zenji wananufaika na muungano,lakini mimi naweza kusema wakijitenga watapata akili ya KUHANGAIKIA MAISHA YAO
 
...........Historically can be true but logically, am still sing that good song bro!............LET ZANZIBAR GO!!!!!!!!!........LET ZANZIBAR GO!!!!!!!!!........LET ZANZIBAR GO!!!!!!!!!

sure,inawezekana hatujui kiundani tanganyika inapata hasara kiasi gan kwa kuwepo kwa huu muungano,,,,halafu wabara twajifanya tuna huruma ETI wakijitenga watapata shida,,,,hivi huku bara kuna raha GANI????
 
Naungana na wewe MM, mara zote mimi nimekuwa nikisema Zanzibar ni mzigo kwa Tanganyika, hawa jamaa wanachangia kiasi kidogo sana kwenye pato la Taifa, ila cha kushangaza wanataka keki kubwa kuliko ukubwa wa eneo wa nchi yao. Mimi nashauri, ni bora Muungano ufutiliwe mbali, tujue moja.
 
Ndio maana tunasema kama wahenga kuwa "mtoto akililia wembe...."
Please let them go. Pengine wakiona kuna haja na faida watarudi.

Of coz Tumewapa kiburi kwa hofu za kusadikika eti itakua laana nk.......
 
nijuavyo mimi katika karne ya 13 Zanzibar iliwa ni Empire na ikiitwa Zenji Empire, hapajatokea empire nyingine yoyote ndani ya africa yote,,sasa wakati huo hata neno tangnyika hakuna, halikuwepo na wala hathubutu mtu kujinasibu kuwa ilikuwepo tanganyika,, tanganyika katika historia ilizaliwa baada ya Berlin conference ambapo kama mataifa mengine ya afrika yaligaiwa mipaka na wazungu ili yatawaliwe na tanganyika ikaangukia ndani ya mikono ya wajerumaji chini ya Germany East Africa Company pamoja na kenya mnamo mwana 1890,,,,na kwa wakati huo Zanzibar ni dola kubwa kushinda madola yoyote africa na wala africa nzima kwa maana ya bara hakukuwa na nchi isipokuwa Egypt nyengine zote zilikuwa ni kingship or kingdoms ndogo ndogo zilizoongozwa na makabila hata neno tangnyika lilitolewa na wajerumani baada ya kuripoti serikali yao tanga manake hadi dar salama wakati huo ilikuwa sehemu ya Zanzibar na pwani yote hadi kilwa sasa ukisema hakuna muda Zanzibar haikuwahi kutegemea bara itakuwa unachekesha na wala hujui usemalo. tanganyika haiwezi kuifikia Zanzibar hata kwa asilimia 10 kama hufahamu waulize wazee wa zamani wakitangnyika wanajua hivyo,,manake historia ya tanganyika baada ya uhuru nyerere aliipiga marufuku ili watangyika wasijue asili yao wapi na badala yake wakawa wanasomeshwa ya kupigania uhuru nyerere, kinyengetile basi.
 
Back
Top Bottom