mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 11,867
- 8,280
Mkuu huo ni uswahili,ukisema wanaopiga mkwara usipost picha zao halafu wewe unapost, sidhani kama kweli wewe ni photo/videographer naona hata kazi zako mnafanya bila mikataba ya kuhusu kitu gani kinatakiwa, kitu ambacho mpiga picha una haki nacho kama photographer ni RAW files hizo hutakiwi kumpa mteja labda kwa makubaliano maalumu,je unajua kwanini hutakiwa kumpa mteja RAW file? bali umpe JPEG file na je unajua kupost picha bila ya mwenyewe mhusika ni kosa na picha za mteja si zako na hata hutakiwi kuweka water mark? fanyeni kazi ki pro brother! msiharibu fani, kila kazi zina miiko yake.Mimi ni mtoa huduma wa Picha na video, mteja ambae hataki atokee mtandaoni wanasema kabisa na Mimi nakuwa Sina tatizo kabisa Wala sitapost picha zao. Kuna kundi la pili wao watakupiga mkwara kabisa kwamba usipowapost "utakoma", hao ndo nawapost kwelikweli!! Na kuna kundi kubwa hawataongelea kabisa lakini wasipojiona wanahisi hawakupendeza. All in all huwa najitahidi kutumia picha chache sana na pia kutowahusisha wazazi Wala waalikwa.
Ni muhimu kuwa na form ya agreement ambayo moja ya vitu wanatakiwa wajibu ni Kama watapenda/hawatapenda picha zitumike.