MCs, Wapiga Picha, Make-up artists n.k na matumizi ya Picha zetu

Mimi ni mtoa huduma wa Picha na video, mteja ambae hataki atokee mtandaoni wanasema kabisa na Mimi nakuwa Sina tatizo kabisa Wala sitapost picha zao. Kuna kundi la pili wao watakupiga mkwara kabisa kwamba usipowapost "utakoma", hao ndo nawapost kwelikweli!! Na kuna kundi kubwa hawataongelea kabisa lakini wasipojiona wanahisi hawakupendeza. All in all huwa najitahidi kutumia picha chache sana na pia kutowahusisha wazazi Wala waalikwa.

Ni muhimu kuwa na form ya agreement ambayo moja ya vitu wanatakiwa wajibu ni Kama watapenda/hawatapenda picha zitumike.
Mkuu huo ni uswahili,ukisema wanaopiga mkwara usipost picha zao halafu wewe unapost, sidhani kama kweli wewe ni photo/videographer naona hata kazi zako mnafanya bila mikataba ya kuhusu kitu gani kinatakiwa, kitu ambacho mpiga picha una haki nacho kama photographer ni RAW files hizo hutakiwi kumpa mteja labda kwa makubaliano maalumu,je unajua kwanini hutakiwa kumpa mteja RAW file? bali umpe JPEG file na je unajua kupost picha bila ya mwenyewe mhusika ni kosa na picha za mteja si zako na hata hutakiwi kuweka water mark? fanyeni kazi ki pro brother! msiharibu fani, kila kazi zina miiko yake.
 
Mimi pia ni Mc na mada yako ina hoja nzuri sana, nakufafanulia hivi...... kinachotakiwa kufanyika ni huyo Mc, photographer au mtu wa mavazi aongee na wewe akuombe kuwa ataitumia picha yako kwenye kurasa zake za kijamii kama sehemu ya kutangaza biashara yake, na wewe utataka kuiona hiyo picha/video ili kujiridhisha kwamba haitakuwa yenye kudhalilisha utu wako.

Una haki ya kukataa asiitumie picha yako bila hata kumpa sababu, na akitumia kiburi akaamua kuitumia picha yako bila idhini yako unaweza kumshitaki.......kuna rafiki yangu mmoja Mc aliwahi kuingia kwenye matatizo kwa ajili ya suala kama hilo
Umesema ukweli Mc
 
Soma uelewe bro sio unapayuka tu!! Nimesema wanaopiga mkwara kwamba USIPOWAPOST, meaning wanataka kupostiwa ndo nawapost! Na nilianza kusema wale wanaotaka wasipostiwe pia sina shida Wala situmii picha zao!! Soma uelewe maana naona umeandika vitu sijasema
 
nenda mahakamani mkuu kashitaki upige hela..

mimi wananiuzi wale wanaotupiga picha club na kuzirusha kwenye magroup yao...huku nikutoheshimu privacy za watu...
 
Mkuu nadhani unakumbuka kuna picha iliwekwa mitandaoni ya mchezaji wa Simba ambayo wako pamoja na mke wake,picha ile haikustahili kuwekwa mitandaoni kwani ilionyesha mke wake ni mtu mzima kuliko mume lakini kumbe ulikuwa ni upotoshaji tu ama wa makusudi au kwa kutokujua,ile picha ilileta taharuki na usumbufu kwa wandnoa hao,laiti kama kungekuwa na makubaliano fulani ili picha isngewekwa mitandaoni, hadi sasa sielewi lengo la aliyeiweka ile picha mtandaoni, tatizo pia hawa wenye visimu wanakuwa na vihere here sana wakipiga tu hao wamerusha ,hilo ni kosa ndio maana kwenye harusi au matukio mengine kunakuwa na tangazo kabisa kuwa hairuhusiwi kupiga picha iwe kwa simu au kifaa kingine kwa mtu ambaye hahusiki wengine huenda mbali zaidi hadi kutoruhusu kuingia na simu ukumbini, hizi simu zimeharibu sana maisha wengine hupiga hadi selfie kwenye majeneza wakiaga marehemu!
Hiyo sikuona mkuu, na watu wanavyojua kuchambua watu sasa. Pole kwao
 
Hii ni serious case, nitaiongelea kwa kina baadae.

Seriously? Bila consent ya mhusika? Hivi mwenzi wake kama anaujua mpapa wake itakuwa songombingo?
Hapana wengi hawajaolewa ,asilimia kubwa wanaomba wapostiwe ni maslay queen, kwenye hizo page ili nao wapate wateja wapya(wa gain new followers)kutoka pages mpya tofauti na A/c zao
 
Aristotee anawasuka, anawawekea mziki wakate viuno halafu anawaposti.
Nyingine niliona ya watoa huduma ya waxing, Yani mtu ananyolewa downstairs huku anarekodiwa...can you imagine mpapa unapostiwa insta dunia nzima inauona.
Bila shaka hii ni marekani kwa mafyatu
 
Ni wewe huyu huyu kabla hujanipa kazi ulisema nikutumie Ig handle yangu ili uone kazi zangu

sasa bila hao wenzako kukubali kupostiwa hizi kazi zangu ungeziona vipi?
 
Wakuu, Habari za muda huu?

Leo nakuja kwenu na hii mada ama sijui niite tabia ama vipi. Yaani kumekuwa ni kawaida sasa ya makundi haya: Wapiga picha, watu wa make up, ma-MC, mafundi nguo etc. Yaani wao wanakupa huduma na unalipia na bado wataku-post kwenye Mitandao ya Kijamii (Social Media) kila sehemu.

Kama alikuwa mpiga picha basi utajikuta kila mahali, au kama alikuwa MC wako basi naye atapost picha za sherehe nzima kwa jinsi alivyopiga picha yeye au kuchukua video. Inafika wageni waalikwa mnajikuta huko mitandaoni. Kama alikushonea nguo vivyo hivyo, kama alikupaka makeup naye ni yale yale.

Na kuna wale umenunua nguo, kiatu etc basi kwa kuwa anakujua, siku ukivaa tu hicho kitu labda ukapost bila hata kuwatag. Watakuja hapo “asante kwa kutuchagua” “asante kuturuhusu tukuhudumie” au watachukua picha wakapost kwao na maneno kibao. Je, kama mwenyewe nilikuwa sitaki watu wajue nimenunua kwenu?

Ni nadra kukutana na wanaokuuliza/muuliza mwenye tukio lake kabla hawajapost.

Kwa kweli hii tabia inakera sana, bora hata pangekuwa na makubalino au punguzo la bei katika huduma zao. Mkubaliane kabisa kwamba atatumia picha zako kutafutia wateja hivyo mkubaliane bei kabisa. Sio nakulipa kila kitu halafu mara paaa! picha zimejaa mtandaoni au ukiamka siku inayofuata unakuta familia nzima mpo mtandaoni.

HOJA YANGU:
Jamani hii ni sawa?

Ulinzi wa data upo wapi? Hivi watu wanajua kwamba wana haki juu ya picha/taarifa zao? Hivi wenye matukio wanajua kwamba wanaweza kataa kupostiwa, wanajua ni haki yao kuruhusu au kukataa? Na hao wanaoposti wanajua ni kosa bila ridhaa ya mhusika?

Nini maoni yako?
mi nishawahi kumuwakia mtu, nilitengeneza saa ya mtu kama zawadi na ni surprise si nikakuta kaipost kwenye mitandao yake bila makubaliano!! sema tu hjuwa na hela nilimsamehe kidogo nimdai fidia!!
 
Mimi pia ni Mc na mada yako ina hoja nzuri sana, nakufafanulia hivi...... kinachotakiwa kufanyika ni huyo Mc, photographer au mtu wa mavazi aongee na wewe akuombe kuwa ataitumia picha yako kwenye kurasa zake za kijamii kama sehemu ya kutangaza biashara yake, na wewe utataka kuiona hiyo picha/video ili kujiridhisha kwamba haitakuwa yenye kudhalilisha utu wako.

Una haki ya kukataa asiitumie picha yako bila hata kumpa sababu, na akitumia kiburi akaamua kuitumia picha yako bila idhini yako unaweza kumshitaki.......kuna rafiki yangu mmoja Mc aliwahi kuingia kwenye matatizo kwa ajili ya suala kama hilo
n si kuomba kwa mdomo, ni kuoma kwa maandishi sababu unaweza kuweka na mtu akakubadilikia na akikupeleka mahkamani anakufilisi, watz tunachukulia vitu rahisirahisi sana, mtu upo zako kwrnye sherehe ya mtu huna hili wala lile mara unajikuta kwnye page yq mc watu wanakutafuta mara nimekuona mra hivi na vilee.....,
 
Mkuu nadhani unakumbuka kuna picha iliwekwa mitandaoni ya mchezaji wa Simba ambayo wako pamoja na mke wake,picha ile haikustahili kuwekwa mitandaoni kwani ilionyesha mke wake ni mtu mzima kuliko mume lakini kumbe ulikuwa ni upotoshaji tu ama wa makusudi au kwa kutokujua,ile picha ilileta taharuki na usumbufu kwa wandnoa hao,laiti kama kungekuwa na makubaliano fulani ili picha isngewekwa mitandaoni, hadi sasa sielewi lengo la aliyeiweka ile picha mtandaoni, tatizo pia hawa wenye visimu wanakuwa na vihere here sana wakipiga tu hao wamerusha ,hilo ni kosa ndio maana kwenye harusi au matukio mengine kunakuwa na tangazo kabisa kuwa hairuhusiwi kupiga picha iwe kwa simu au kifaa kingine kwa mtu ambaye hahusiki wengine huenda mbali zaidi hadi kutoruhusu kuingia na simu ukumbini, hizi simu zimeharibu sana maisha wengine hupiga hadi selfie kwenye majeneza wakiaga marehemu!
Jeneza
 
Back
Top Bottom