Mapengo 17
R I P
- Mar 28, 2014
- 1,232
- 609
Nimekuwa nikisikia tetesi kuwa Mchungaji Faustine Munishi alifukuzwa Tanzania na akakimbilia nchini Kenya na nilikuwa natamani sana kujua sababu iliyofikisha hapo ni nini?
Wakuu leo kwa bahati nzuri wakati naangalia tv nimemuona Mchungaji Munishi na Juliani wakihojiwa live katika chanel ya KBC1 iliyoko Kenya, na kwa bahati nzuri swali la mwisho aliloulizwa na mtangazaji ni kuhusu mahusiano yake na Nchi ya Tanzania yakoje?
Munishi akajibu kuwa mahusiano yake na Tanzania kwa upande wa kisiasa hayako vizuri, na mgogoro huo ulianza punde tu aliporecord wimbo unaosema CCM imezeeka.
Kwa hiyo viongozi wa CCM ambao ndio watawala ndio hayuko nao vizuri, jambo linalomsababisha hata akija huku Tanzania asipewe heshima na sanaa yake isipewe kipaumbele, lakini akabainisha kuwa yeye na watanzania wako na mahusiano mazuri wala hawana tofauti yeyote.
Aliendelea kusema kuwa uwepo wake wa Kenya haina maana kuwa yeye ni mkimbizi na wala hataki kuchukua uraia wa nchi yeyote maana yeye ni Mtanzania na anaipenda Tanzania.
Mchungaji Munishi au maarufu kwa jina la wimbo wake wa Malebo akaendelea kusema kuwa pamoja na kuwa na migogoro na wanasiasa lakini yeye hapo alipo hana kadi ya chama chochote na wala sio mwanasiasa, ila tu serikali ya CCM kwasababu inatawaliwa na mabepali ingawa wanaigiza kama wanatawala kwa mfumo wa ujamaa ndio wanaomletea zengwe hilo, ila anaamini siku moja wataondoka madarakani na yeye atarudi nyumbani kwao Tanzania na kuishi vizuri tena kwa amani.
Baada ya Mchungaji Munishi kuongea maneno hayo yote nikajiuliza maswali haya, "Viongozi wa CCM wamepata wapi madaraka ya kumfukuza mtu nchini kwake? Kwanini serikali hii inaendeshwa kibabe wakati Tanzania ni nchi ya kidemocrasia? Kuna dhambi gani kwa mchungaji au kwa raia kutoa mawazo yake ya kuikosoa serikali au chama tawala?
Huyu ndiye Mchungaji Munishi aliyekimbilia Kenya baada ya kufukuzwa Tanzania