Mchange awashambulia viongozi wa CHADEMA

Mungu wangu MTU huyu bado hajakamatwa polisi mko wapi vyombo vya usalama MTU huyu muhimu sana kwenu
 
Mkuu Chakaza, kwanza asante!. Habari ni bure!, bahasha za khaki ni by the way tuu!, ziwepo, zisiwepo, bado habari kama ni habari itasimama tuu!. Lengo la bahasha ni logistics

Ila pia kwa habari hii, kwa jinsi nilivyoisoma!, narudia tuu ile kumbu kumbu yangu kuwa, kuwa ...sio mtu lazima mpaka aokote makopo!.

Thanks.

Pasco.
Nimekupata mkuu, kula like yangu.
 
Masikini Mchange amekuwa ki.chaa. Dah! Hakuna hata connection ya facts anabwabwaja tu. Ulikuwa wapi siku zote usiitwe polisi kwa ushahidi?? Anyway kwa kuwa umekuwa chi.zi basi
 
Yaani we ndo umejua leo? Huyo ni muuaji anayejulikana siku nyingi. Amekua akitumika kwa sababu hajitambui na hawezi kuwa na maisha nje ya siasa.

Wewe hujawahi kushangaa mtu aliyefeli chuo kikuu cha Dar es Salaam kurundikiwa madaraka kibao wakati hana elimu? Sababu kubwa ni kuwa huwa anaweza kutumika kirahisi kuua watu.

Vipi kuhusu waziri wako Lukuvi ana shahada au stashahada ya nini hadi kupewa uwaziri?
 

Huyo bwana Red yaani kama kuna mtu kabugi siasa ni huyu dogo fisadi, ana hekalu kamjengea mwanamke wake aliyemzalisha maeneo ya Kimara Matosa ntaupiga picha Muda ntautupia humu

We hoja wala hauna,Sema ni mshabiki mzuri sana
 
Mi nakuambia kuwa Saccoss ya CHAGGADEMA inatakiwa uwe umejitoa ufahamu haswaaaa


Sent from my iPad Air using JamiiForums
 
magazeti yataandika "Mchange awavua nguo CHADEMA" jingine "Mbowe, Lissu, Slaa waumbuliwa na Mchange"
 
Hivi ni kwa nioi waandishi wa habari wanadharauliwa kiasi hki? Hao waandishi wanaowasikiliza vichaa kama hawa huwa wanauliza na maswali magumu pia?

Cc: Pasco
 
Last edited by a moderator:
Duh! Mimi nimeishia hapa, maana hili jaamaa nalikana na ndio maana watu walisema hakika kama Picha zisingekuwepo leo hii tungeamnishwa kuwa CHADEMA ndio wamefanya maujai yale.

"Wakati Dunia Nzima Leo inaamini kwamba polisi wa F.F.U walihusika kumuua David Mwangosi tarehe 2.9.2012 pale Nyororo Iringa,MBOWE, LISSU, MNYIKA na SLAA wanaujua ukweli, wanajua ni namna gani mchezo huu ulipangwa, namna gani mpiga picha aliandaliwa, namna gani taarifa za awali zilisambazwa na namna gani mlipuaji alifika eneo latukio na kutekeleza kazi yake maalum na baadae kuondoka kwa utaalamu wa hali ya juu, wanafahamu fika. Na kwenye hili pia mpaka sasa polisi wanahangaika kujinasua, lakini bado wamekwama. "

huyu jamaa anatuona sisi ni wapuuzi kama yeye mkuu.
 
HABIBU MCHANGE AKANA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA ULIPUAJI WA HELKOPTA ILIYOWABEBA MNYIKA NA SLAA.

Leo mchana katika mkutano wake na waandishi wa habari,Mchange amewashambulia waziwazi viongozi wakuu wa chama cha demokrasia na maendeleo na kuwatuhumu kuhiska na mauaji ya aliyekua mbunge wa CHADEMA Tarime,marehemu Chacha Wangwe,kisha kumkana mtu aliyehusika na mauaji hayo Deus Mallya,wakati alikuwa mjumbe katika kamati iliyokuwa chini ya John Mnyika,na rafiki wa Mnyika lakini Mnyika kumkana hajawai hata kumuona.

Kisha kawataja Lissu,Mbowe na Slaa kuajiri vijana na kuwalipa kuwatesa vijana wanaoonyesha kuiunga mkono CCM katika kampeni mbalimbali za chama,hasa kwa kumwagia watu tindikali.

Pia amesema Lissu ni mbinafsi na fisadi aliyedhurumu fedha za miradi ya mazingira,na kujenga nyumba ya ghorofa Tegeta,Mbowe anahujumu mamilioni ya CHADEMA,na Slaa akihujumu fedha za chama kulipia mkopo wa NSSF.
===================================


We ulikuwa na nafasi gani ndani ya CHADEMA? ikiwa mtu km wewe ulikuwa kiongozi basi nadhani kuna ukweli mahali fulani kuwa chadema ina tatizo la mifumo ya upatikanaji wa uongozi na wapo wengi ndani ya chama wa aina yako. Lissu some of us look forward to your contributions for the party to be properly institutionalised to avoid these kinds of nonsense
 
Waandishi wa habari kuwaita wakusikie mpaka ukidhi vigezo gani jamani, msaada.... Pasco

Mwenyewe huwa najiuliza the same question, yaani utoko km huu hao waandishi walifanya nini? Au ndo ile kijana wa kikwete riz1anasema ni makanjanja?
 
Last edited by a moderator:
Hivi ni kwa nioi waandishi wa habari wanadharauliwa kiasi hki? Hao waandishi wanaowasikiliza vichaa kama hawa huwa wanauliza na maswali magumu pia?

Cc: Pasco
Mkuu Matola, kwanza asante kuzungumzia jinsi waandishi wanavyodharauliwa kiasi hiki!, kazi ya uandishi ni noble profession kama noble professions nyingine zote, ni kazi ya wito na ni kujitolea kama ualimu, udaktari na kazi za kanisa!, waandishi ni watumishi wa watu wakifanya kazi ya kutumikia jamii, ila kwa upande mwingine, katika jukumu lao la kukusanya habari, watu wote wanakuwa ni abiria wao, huwezi kuchagua!, wazima, vichaa, lunatics, etc, wote kwetu ni source.

Ukiisha kusanya, wewe mkusanyaji ndio chujio la kwanza kupima if it makes any sense, ndipo unaandika kuhabarisha jamii!, unamkabidhi mhariri wako nae anaipitia na kuiaproove itoke au isitoke, au kuipunguza, kuichinja na hata kuipotezea!.

Mfano habari hii kwenye magazeti ya kesho, itakuwa ni big news kwenye magazeti ya Uhuru, Mzalendo,itakandiwa sana Tanzania Daima, ila kwenye magazeti kama Citizen na Mwananchi sijui kama inaweza kupita kwa sababu wahariri wataweza kunote insanity ya mtuoa habari, ambayo ameyazungumzia matukio bila coherence wala correlation, na Tanzania ingekuwa ni nchi inayofuata utawala wa sheria "the rule of law", saa hizi jamaa ni zamani, angelikuwa ananye. debe!.

Kwenye noble profession zote kudharaulika ni kawaida sana, hata kwenye fani ya udaktari, Madaktari ndio wanaoheshimika, lakini manesi wale wafunga vidonda etc, wee acha tuu!, kwenye fani ya uandishi, madakitari wetu ndio wahariri, hawa wanaheshikika sana, ila sisi ndio wafunga vidonda wao, kudharaurika ni kawaida!.

Ila nasi tunao msimu wa kuheshimika na kunyenyekewa kama walivyo waalimu kipindi cha mitihani,hivyo nasi mwaka 2015, kuelekea kile kipindi, huwa tunaheshimiwa sana, tunathaminiwa sana, tuna nyenyekewa sana, na kwa wengine wetu, ndio kipindi cha mavuno!.

Thanks.
Pasco.
 
Nkuu Chikutentema, kwanja, achante!. Sifa ya kuita Press Conference ni

1. Uwe na umri wa miaka 18
2. Uwe na akili timamu

Thats all.

Thanks.

Pasco

Akili timamu wanajua vp japo umri? unaweza kukadiria?
 
Wewe ni kibaraka na mchumia tumbo

Mwanzoni sikuamini km kweli kuna binadamu wanalipwa kwa hii kazi ya social media comments, wewe lazima unalipwa au unanufaika na mfumo ulipo wa kifisadi, ila lazima tutawatoa ikulu kwa njia yoyote, wengine tuko tayari kupigania kizazi hiki na watoto wetu, jiandae
 
Back
Top Bottom