Mchange awashambulia viongozi wa CHADEMA

Akili timamu wanajua vp japo umri? unaweza kukadiria?
Mkuu JGG, asante. Kuna msemo unaitwa usikatae wito, kataa neno!. Akili timuma huwa inapimwa na contents!. Kwa mfano kwa upande wangu, hii contents ya hii press conference ya leo, inaonyesha kabisa mzungumzaji ni "insane", wenye akili zao timamu hili waliisha lijua ndio maana hadi sasa jamaa yuko huru!.

Thanks.
Pasco
 
  • Thanks
Reactions: JGG
Mkuu Matola, kwanza asante kuzungumzia jinsi waandishi wanavyodharauliwa kiasi hiki!, kazi ya uandishi ni noble profession kama noble professions nyingine zote, ni kazi ya wito na ni kujitolea kama ualimu, udaktari na kazi za kanisa!, waandishi ni watumishi wa watu wakifanya kazi ya kutumikia jamii, ila kwa upande mwingine, katika jukumu lao la kukusanya habari, watu wote wanakuwa ni abiria wao, huwezi kuchagua!, wazima, vichaa, lunatics, etc, wote kwetu ni source.

Ukiisha kusanya, wewe mkusanyaji ndio chujio la kwanza kupima if it makes any sense, ndipo unaandika kuhabarisha jamii!, unamkabidhi mhariri wako nae anaipitia na kuiaproove itoke au isitoke, au kuipunguza, kuichinja na hata kuipotezea!.

Mfano habari hii kwenye magazeti ya kesho, itakuwa ni big news kwenye magazeti ya Uhuru, Mzalendo,itakandiwa sana Tanzania Daima, ila kwenye magazeti kama Citizen na Mwananchi sijui kama inaweza kupita kwa sababu wahariri wataweza kunote insanity ya mtuoa habari, ambayo ameyazungumzia matukio bila coherence wala correlation, na Tanzania ingekuwa ni nchi inayofuata utawala wa sheria "the rule of law", saa hizi jamaa ni zamani, angelikuwa ananye. debe!.

Kwenye noble profession zote kudharaulika ni kawaida sana, hata kwenye fani ya udaktari, Madaktari ndio wanaoheshimika, lakini manesi wale wafunga vidonda etc, wee acha tuu!, kwenye fani ya uandishi, madakitari wetu ndio wahariri, hawa wanaheshikika sana, ila sisi ndio wafunga vidonda wao, kudharaurika ni kawaida!.

Ila nasi tunao msimu wa kuheshimika na kunyenyekewa kama walivyo waalimu kipindi cha mitihani,hivyo nasi mwaka 2015, kuelekea kile kipindi, huwa tunaheshimiwa sana, tunathaminiwa sana, tuna nyenyekewa sana, na kwa wengine wetu, ndio kipindi cha mavuno!.

Thanks.
Pasco.

lipasco huwa liprofessional kwweli.
 
Wewe ndo unaujua ukweli kuliko Mahakama iliyomwachia huru deus Mallya? Uweke hapa huo ukweli

unamaanisha mahakama za bongo au zingine? hivi hujui ni kiasi gani wahalifu wako huru mpaka wananchi wanahukumu wenyewe siku hizi
 
Last edited by a moderator:
Hii kitu inachanganya sana, kila mtu anatoa tuhuma tu haendi kushtaki, hawa wanasema kuna watu wataka kulipua kausafiri kao, hawajaenda mahakamani, mtuhumiwa nae kawatuhumu, wote hakuna alieshtaki kuchafuliwa jina, wengine wana ushahidi wa jinsi pesa zilivyoibwa benki kuu lakini haendi mahakamani, na tuhuma zenyewe zimetolewa mahali ambapo huwezi kumshtaki mahakamani, hata na wale wenye majina ya mafisadi waliowataja pale mwembe yanga nao hawajashitaki wala kushitakiwa. Mi naomba anaejua elimu hii aanzishe uzi wa kutujuza wenzao hii ishu ili twende sawa, tafadhali.

hakuna dola tz. madiwani wa shinyanga hadi leo wapo ndani wanahojiwa juu ya tuhuma walizotoa. nitashangaa kama habiba watamwacha na hapo ndipo nitaona connection kati ya mchange na ccm.
 
mchange anajifunza siasa kwa hiyo anajifunza uongo aibu yake njaa mbaya dawa ya njaa ni kazi kama ajira ni ngumu hapa kwangu nimeanzisha shamba ani pm nitamuelekeza nilipo aje nimpe ajira haya mambo ya aibu anayofanya mwisho wake ni kujitia hatiani bure maake naona kunasiku atasema kwenye kifo cha Wangwe yeye ndo alikuwa anaendesha ili ionekane cdm ndio waliomtuma. Hata huo mkutano na waandishi wa habari kunachama kimegharimikia,
 
Sidhani kama kuna mtu hajui kama Chacha Wangwa aliuawa na viongozi wa chadema.
 
Madai aliyoyatoa Mosses Machange juu ya Viongozi wa ngazi za juu ndani ya Chadema, yachukuliwe kama Usaliti wa kazi walizokuwa wakizifanya ndani ya Chadema? Vyombo vya habari vimeripoti sana taarifa yake ya PRESS COMFERENCE juu ya tuhuma za Mauaji.

Taarifa za mauaji haya ya kutisha, ni zaidi ya SIASA, si vema kuchukuliwa kuwa ni siasa bali ni vema taarifa hii ikafanyiwa UCHUNGUZI na wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya SHERIA kujibu tuhuma. INGEKUWA NI MTU WA KAWAIDA KATOA TAARIFA HIZO, ANGEKUWA MAHALI SASAHIVI. Hii taarifa ni zaidi ya siasa, ina dalili kubwa sana ya ukweli.
Nyakati za mwisho watu hutubu kwa kujutia walioshiriki kuyafanya.
Kina MBOWE, MNYIKA, SLAA,LEMA, LISSU, si mara ya kwanza kuhusishwa na mauaji, WAKAMATWE. Hakuna aliye juu ya Sheria.

Serikali ichukulie jambo hili kuwa la dharura ili kukomesha mitandao ya UGAIDI na MAUAJI humu nchini ambao wanastawi kupitia kivuli cha Siasa. Taarifa iliyotolewa haipaswi kujadiliwa kwenye Thread moja maana ni pana sana, kwa watu wenye ubinadamu walichukulie jambo hili Serious.
Nategemea kuona Wanasheria na Watetezi wa haki za Binadamu humu Nchini kuandaa Makongamano kupitia ITV, STARTV, kama yale ya katiba katika kutetea haki za binadamu.
 
according to Mchange na yeye alikuwa jikoni, alikuwa mpishi,alishiriki kuchochea kuni, Ni kitanda tusichokilalia ila yeye kesha lala anafahamu wanavyouma, Ni Sawa na Shibuda yupo ndani ila bado anatenda na sawa alikotoka-hivi leo Shibuda akiongea yaliyomo CCM kwa sura ya ubaya tutamnanga?, Ni mawazo yangu tu, japo ya Daudi Mwangosi Ni zaidi ya habari
CCM imepoteza pesa bure kumlipa Mchange kwani haya aliyoyasema ni propagada zilezile za miaka yote.
Tulitarajia propaganda mpya zaidi jamani,
 
Kumbe John Mnyika ni muuaji nae kama Mbowe na Slaa? Tunashukuru kwakujua yalio nyuma ya pazia.
 
Last edited by a moderator:
Kipindi kile madiwani wa chadema wale wa shinyanga wanatoa tuhuma kuwa naibu waziri masele na mchange walitaka kuilipua helkopta ya dr slaa ulitoa ushauri kama huu kwa vyombo vya dola?

Nikimnukuu IGP mangu" hizi ni siasa za chadema tu" kwa nini na mie nisiamini kuwa hizi ni siasa za ccm kipitia kuwadi wao mchange?

Huwezi kujua yote aliyoyasema kama ww sio mmoja wao,pili lile swala la mwangosi hata kama kipofu unaweza jua kbs ni nani aliyehusika na yale maauaji,na kama viongozo wa juu wa cdm wanahusika hadi leo tusingekuwa nao uraiani kwani wametafutwa sana kwa kesi mbali mbali na zote za kutunga ndiyo maana wanazishinda,tutumieni akili zetu kwa manufaa ya Taifa letu,kuliko kuwatumia hawa wasaliti kuhamisha mijadala ya kitaifa kihuni kihuni tu
 
Madai aliyoyatoa Mosses Machange juu ya Viongozi wa ngazi za juu ndani ya Chadema, yachukuliwe kama Usaliti wa kazi walizokuwa wakizifanya ndani ya Chadema? Vyombo vya habari vimeripoti sana taarifa yake ya PRESS COMFERENCE juu ya tuhuma za Mauaji.

Taarifa za mauaji haya ya kutisha, ni zaidi ya SIASA, si vema kuchukuliwa kuwa ni siasa bali ni vema taarifa hii ikafanyiwa UCHUNGUZI na wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya SHERIA kujibu tuhuma. INGEKUWA NI MTU WA KAWAIDA KATOA TAARIFA HIZO, ANGEKUWA MAHALI SASAHIVI. Hii taarifa ni zaidi ya siasa, ina dalili kubwa sana ya ukweli.
Nyakati za mwisho watu hutubu kwa kujutia walioshiriki kuyafanya.
Kina MBOWE, MNYIKA, SLAA,LEMA, LISSU, si mara ya kwanza kuhusishwa na mauaji, WAKAMATWE. Hakuna aliye juu ya Sheria.

Serikali ichukulie jambo hili kuwa la dharura ili kukomesha mitandao ya UGAIDI na MAUAJI humu nchini ambao wanastawi kupitia kivuli cha Siasa. Taarifa iliyotolewa haipaswi kujadiliwa kwenye Thread moja maana ni pana sana, kwa watu wenye ubinadamu walichukulie jambo hili Serious.
Nategemea kuona Wanasheria na Watetezi wa haki za Binadamu humu Nchini kuandaa Makongamano kupitia ITV, STARTV, kama yale ya katiba katika kutetea haki za binadamu.

madai ya Mchange sio mapya yamesemwa saaana, polisi wamepuuza basada ya kuona ni siasa tu. Sasa wewe unataka polisi wapoteze muda kwa madai ya upuuzi.

Mtu wa kwanza wa kukamatwa ni Mchange mwenyewe. Ukiona polisi hawafanyi hilo wewe tulia tu, hiyo ni tabia ya msaliti yeyote aliyechanganyikiwa.
 
Kipindi kile madiwani wa chadema wale wa shinyanga wanatoa tuhuma kuwa naibu waziri masele na mchange walitaka kuilipua helkopta ya dr slaa ulitoa ushauri kama huu kwa vyombo vya dola?

Nikimnukuu IGP mangu" hizi ni siasa za chadema tu" kwa nini na mie nisiamini kuwa hizi ni siasa za ccm kipitia kuwadi wao mchange?

Huwezi kujua yote aliyoyasema kama ww sio mmoja wao,pili lile swala la mwangosi hata kama kipofu unaweza jua kbs ni nani aliyehusika na yale maauaji,na kama viongozo wa juu wa cdm wanahusika hadi leo tusingekuwa nao uraiani kwani wametafutwa sana kwa kesi mbali mbali na zote za kutunga ndiyo maana wanazishinda,tutumieni akili zetu kwa manufaa ya Taifa letu,kuliko kuwatumia hawa wasaliti kuhamisha mijadala ya kitaifa kihuni kihuni tu

ur too general mkuu, usitetee watu kwa maneno ya kukaririshwa, hapa yametajwa mauaji mbalimbali wewe na mimi hatuna uwezo wa kuchunguza ila kuna wataalam na vyombo. Suala la kusema ni taarifa ya kuahirisha mijadala ya katiba, nalo nachelea kusema ni upotoshaji maana askari na majgdaji wa kuchunguza tuhuma hizi hawapo BMK na pia hao kina Lissu si wamegomea bunge? Wapelekwe jela.
 
Madai aliyoyatoa Mosses Machange juu ya Viongozi wa ngazi za juu ndani ya Chadema, yachukuliwe kama Usaliti wa kazi walizokuwa wakizifanya ndani ya Chadema? Vyombo vya habari vimeripoti sana taarifa yake ya PRESS COMFERENCE juu ya tuhuma za Mauaji.

Taarifa za mauaji haya ya kutisha, ni zaidi ya SIASA, si vema kuchukuliwa kuwa ni siasa bali ni vema taarifa hii ikafanyiwa UCHUNGUZI na wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya SHERIA kujibu tuhuma. INGEKUWA NI MTU WA KAWAIDA KATOA TAARIFA HIZO, ANGEKUWA MAHALI SASAHIVI. Hii taarifa ni zaidi ya siasa, ina dalili kubwa sana ya ukweli.
Nyakati za mwisho watu hutubu kwa kujutia walioshiriki kuyafanya.
Kina MBOWE, MNYIKA, SLAA,LEMA, LISSU, si mara ya kwanza kuhusishwa na mauaji, WAKAMATWE. Hakuna aliye juu ya Sheria.

Serikali ichukulie jambo hili kuwa la dharura ili kukomesha mitandao ya UGAIDI na MAUAJI humu nchini ambao wanastawi kupitia kivuli cha Siasa. Taarifa iliyotolewa haipaswi kujadiliwa kwenye Thread moja maana ni pana sana, kwa watu wenye ubinadamu walichukulie jambo hili Serious.
Nategemea kuona Wanasheria na Watetezi wa haki za Binadamu humu Nchini kuandaa Makongamano kupitia ITV, STARTV, kama yale ya katiba katika kutetea haki za binadamu.

Habib Mchange ameongea maneno mazito ila alipoingiza swala la mwangosi tu hapo ndio alipoharibu na kuona tamthilia yake yote ya uongo.
 
Back
Top Bottom