Mbwembe za Ma-Doctor

Rushwa zenyewe elfu mbili, elfu tano!

Eti mgonjwa au ndugu wa mgonjwa anaambiwa: "Hela/ Pesa ya Daktari a.k.a CCD (Chakula Cha Daktari)"

Mbona tunaaibishwa!

Kama wanaokataa rushwa wapo ni wachache na wale wanaokataa inategemea ni rushwa gani na ni rushwa kwa ajili ya nini (japo zote ni rushwa tu), lkn hii ya kusema elfu mbili, tano ya kumpatia Daktari, mjue mnaliwa na wafagiaji - wafanya usafi mawodini, kwenye ma-corridor n.k

Mkuu umenikumbusha wakati nafanya MMED OBGY Muhimbili wakatuhumu idara kuongoza kwa CCD, duh! Iliniuma sana nkiwaza 24hrs call, unapiga ceasarian section 15, hujatoka theatre hiyo ccd saa ngapi, mara nikambamba porter anadai ccd kwa mgonjwa, kumbe na other residents idarani walikuwa wanamjua jamaa kwa kudai ccd. Ni kweli wachukua ccd wengi ni wafagizi. Anakuja na file nsaidie kumwona huyu ndugu yangu, huku keshamtel huyo jamaa huyu doc bila elfu 20 hakuoni, ye ndo anazitia ndani zote.....

Alikua anahojiwa ofisini, lakini kwanini alikua amekitundika shingoni? kwani hakuna sehemu ya kukitunzia?
Kwani angekiweka basi mezani asingekua dr?

Duh, unanichekesha sana!
Ngoja nikwambie ukweli wangu.
Mimi mwenyewe huwa nakaa nako shingoni na wakti mwingine huwa sikumbuki kama nimekaweka shingoni.
Huyo Doctor unayemzungumzia (Chief wangu na MO i/c wa hospital niliyofanyia intern) sidhani kama alikachukua akakaweka shingoni baada ya kumwona mwandishi wa habari ameingia ndani; atakuwa alikuwa na mgonjwa baadaye akakiweka shingoni sehemu ambayo ni rahisi kukichukua na baadaye akapata wageni!.

Jamaa kakomaa!!!
Eti hakuna kifaa kingine cha ku-represent u-Doctor?
Au hakuna mahali pengine pa kukiweka ofisini?
Kama ni cha muhimu katika first aid, kwenye FIRST AID KIT kimo?

Mimi ni mjeshi wa kujitegemea (Private soldier - siyo "Private" ya mjeshi asiye hata na mbavu begani!).Huwa sichekeshwi ovyo ovyo, lkn leo nimecheka!

Kwani tatizo liko wapi haswa!?Anaebeba ni yeye na sio wewe sasa kwanini kinakusumbua?!

Walimu nao utataka wasiwe wanatembea na kalamu unless wanasahihisha?!
Polisi wasitembee na bastola/bunduki/virungu unless kuna tatizo sehemu?!
Wanajeshi nao wasiwe na vitendea kazi vyao mpaka wawe vitani?!
Mchungaji asiwe na biblia mpaka pale anapohubiri?!
Sheikh asiwe na Quran mpaka pale anapofundisha?!

Mi hata wangetembea navyo mpaka mitaani bado nisingeona tatizo maana wao ndo wenye matumizi navyo kwahiyo wanajua wapi na wapi viwepo karibu na wapi visiwepo!

Jana kwenye kipindi TBC, kuna dr alikua anahojiwa huku akiwa nacho.

Swali la kujiuliza kwanini kwa wakati ule? Kama swala ni atambulike kuwa yeye ni dr kasomea miaka 6, mbona jina lilikua lina-display kwa kuanza na "Dr"?

HATA GUSTINO LYATONGA MREMA, YULE KADA MAARUFU WA sisiem NA MBUNGE WA JIMBO LANGU NI doktoR!!!

Peripheral pulses not felt

Cold extremities

Pupils dilated

No pupillary response to light

First and second (S1S2) heart sounds not heard(kazi ya stethoscope)

Person certified to be dead!

Asante Doctor!

hizi sio mbwembwe sema huelewi kazi ya hicho kifaa, kwani umewakuta baa nacho? Hospital ndio ofc ya dr sasa aitundike wapi?

stethoscope ni muhimu sana....! madactari wote twafaa tuwe nacho mfano mtu aki collapse popote iwe barabarani, nyumbani hospitali. katika zile "ABC" ( AIR , BREATHING & CIRCULATION ) ... hiki kifaa kinatumika kuangalia na kuhakikisha hiyo mifumo inafanya kazi fresh....

Stethoscope ni muhimu sana! tena kuna brands zake .. baadhi ni bei mbaya mfano brand kama " littman stethoscope" , bei yake mbaya sana.. na dactari akiwa nayo anajisikia ikiwa shngoni au kwenye koti...!

Similar Discussions

Back
Top Bottom