"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu za Kufanya Miujiza ya Uponyaji kwa Imani. Kila Mtu Anazo!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,608
Wanabodi,

Huu ni muendelezo makala zangu kuhusu "works of powers", nguvu za kutenda miujiza, "psychic powers!", leo nitajikita zaidi katika nguvu za uponaji "faith healing!". Nitakuwa na maeneo yafuatayo.
Utangulizi:
Naomba kuweka UTANGULIZI huu kuwa imani ya kweli has got nothing to do na dini yoyote!. Wakristo na Waislamu ni watoto wa baba mmoja Nabii Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mwanaye wa kwanza Ismail aliyemzaa na mjakazi wa Kimisri Hagir, na Wakristo ni uzao wa mwanaye wa pili Isaka aliyezaliwa na mkewe Sarah.

Uzao wa Ismail ndipo akazaliwa Mtume Mohamed (SAW) na uzao wa Isaka ndio akazaliwa Yesu aitwae Kristo Kiislamu ni Issa bin Maryam.
  1. Faith Healing ni nini?
  2. Faith Healing Inafanyikaje?
  3. My Own Testimonial (ushuhuda wangu)
  4. Nguvu za Uponyaji zinatoka wapi?
  5. Je Wahubiri wa Uponyaji ni Lazima wawe Wakristu?
Nakuhakikishia, ni Hakika Asilimia 100% kwa 100% Uwezo huo unao, ila kwa vile hujitambui, hautumii!. Jitambue, utumie!
  1. Somo la Kwanza, Faith Healing ni Nini?!.Kwa wale ambao ni wageni, nawashauri kabla hujaanza na uzi huu, wapitie kwanza hapa, Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanazo bila wao Kujijua! Na tuanze kwa kukumbushana tuu kidogo the basics!
  2. Sisi binadamu tumeumbwa na Mungu kwa mfano wake. Ule uhai aliotupulizia, una nguvu za KiMungu ndani yetu. Haijalishi wewe ni wa dini gani, ni wa imani gani, au hata wasio amini, wote tumeumbwa na Mungu, hivyo uwezo wa KiMungu uko ndani yetu, ni kwa kuutumia uwezo huu, ndipo muujiza hufanyika!.
  3. Faith Healing, ni uponyaji kwa kutumia imani!. Ambapo ule uponyaji huitwa muujiza. Historia ya kupona kwa miujiza ilianza zamani na sehemu kubwa ilijikita katika dini!, huko mimi siendi. Lengo la uzi huu ni kukujulisha wewe kuwa miujiza yoyote inayotokea, inawezekana kwa uwezo iliomo ndani yako wewe mtendewa muujiza na sio mtenda!
  4. Hii Faith Healing ni kitendo cha mtu mwenye ugojwa fulani, kupona kwa njia ya imani tuu bila kutumia dawa yoyote, hivyo kipona kimiujiza, na uponyaji huu sometimes unahusisha hadi kufufua wafu, au kuzuia kifo, vipofu wanaona, viziwi wanasikia, bubu wanaongea, vilema wanaponyeka, viwete wanatembea, wagumba wanapata watoto, maradhi yoyote yanaponyeka.
  5. Miujiza hii imegawanyika katika makundi makuu matatu, ya kwanza ni ile miujiza inayofanywa na Mungu mwenyewe, muujiza mkuu ukiwa ni uumbaji! wa ulimwengu na kumuumba Adam. Miujiza inayofanywa na Mungu mwenyewe mingine ina sababu na mingine haina sababu, mfano muujiza wa kuiamuru bahari ya Sham kufunguka, ilikuwa na sababu ili Wana wa Israel wapite, lakini muujiza wa Bikiri Maria kupokea mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, haukuwa na sababu kwanini Maria, kulikuwa na mabikira wengi tuu!. Hii miujiza ya Mungu mwenyewe huitwa miujiza mikuu!. Miujiza iliofanywa na Yesu, nayo inaingia kwenye kundi hili la miujiza mikuu kufuatia imani kwa wanaomuamini Yesu ni Mwana wa Mungu, hivyo ni Mungu!
  6. Kisha kuna miujiza inayofanywa na sisi binadamu kupitia uwezo wa KiMungu ulio ndani yetu. Hii inajumuisha miujiza iliyofanywa na manabii, miujiza iliyofanywa na binadamu kwa uwezo wa Mungu ilio ndani yetu na mambo mazuri, na mema yote yanayofanyika duniani, ni kazi nzuri ya roho wa Mungu aliye ndani yetu.
  7. Pamoja na uwepo wa Mungu ndani yetu, mwovu shetani pia naye yupo duniani, na anazo nguvu kama za Mungu kutenda karibu kila kitu ambacho Mungu anatenda isipokuwa Mungu ana nguvu zaidi ya shetani!. jambo moja tuu!, upande wa uumbaji!. Yaani God is the creator and giver of life na ni ndani ya hii life ndimo zilimo nguvu za Mungu ndani yetu. Tofauti pekee kati ya Mungu na shetani, ni "life" shetani hawezi kuumba ila ndie muagamizi wa life. Maovu yote yanafanyika humu duniani ikiwemo miujiza ya uovu, ni kazi ya shetani. Zile sifa kuu tatu za Mungu, Omnipotence, hana mwisho, na shetani pia hana mwisho, tofauti ni Mungu ni wa milele na makao yake ya milele ni peponi, mbinguni au ahera kwenye furaha ya milele, na shetani makao yake ya milele ni motoni, kwenye ziwa la moto, akiungua na kuteseka milele!. Mungu ni Omnipresence, yaani yuko kila mahali, kitendo tuu cha mwanaadamu kupuliziwa pumzi ya uhai yenye Uuungu ndani yake, kunapelekea ndani ya kila binadamu kuna Mungu ndani yetu!, shetani naye alitupwa duniani, yeye na jeshi lake, nao pia wako kila mahali! ila ni nje ya miili yetu!. Mungu ni Omniscience, ana uwezo wa kujua kila kitu kabla hakijatokea, there is nothing new under the sun, hivyo lolote litakalotokea, lilikuwa litokee, ila shetani naye ana uwezo wa kuijua mipango yote ya Mungu na kujitahidi kuiangamiza!.Hivyo faith healing ni uwezo wa kufanya miujiza ya uponyaji kwa kutibu kwa kutumia nguvu za Uungu zilizo ndani yetu, au kwa waliomkaribisha shetani ndani yao, basi ni uwezo wa uponyaji au kutibu kwa kutumia nguvu za shetani zilizo ndani yao!, waganga, wanga, wachawi, wapiga ramli, wasoma nyota etc.
Somo la 2. Faith Healing unafanyikaje na inatibu vipi?
  1. The most powerful thing kwenye mwili wa binaadami ni "will powers", "where there is a will, there is a way!. Hii "Will power" ni nguvu ya Mungu iliyo ndani yetu yenye uwezo wa kufanya kila kitu, ikiwemo miujiza!. Ili hii "will powers iweze kutenda miujiza, it has to be invoked!
  2. Prescription ya faith healing, ni imani kuamini, na inafanyika kwa aina nyingi na kwa namna nyingi. Aina maarufu ni ile ya kuombewa na wahubiri/wachungaji/mitume/manabii/masheikh/viongozi wa dini/walokole/wanajimu/waganga wa kienyeji/watoa tiba mbadala etc, etc, dawa pekee kwenye tiba hii ni imani! Kitendo cha kuamini ndicho kina invoke zile doors za forces of will to act upon a specific desease and cure it!
  3. Kinachofanyika ni kwanza kutengeneza imani ya kuamini unachotakiwa kuamini. Kwa wale wa imani ya Kikiristu kwanza ni kuamini kwa dhati kuwa Yesu anakoa, Yesu anaponya, hivyo anayekuhubiria kwa kulitaja jina la Yesu, "Katika Jina la Yesu Zishindwe!", "Katika Jina la Bwana", etc, etc. Kitendo cha kuamini kuwa Yesu anaponya, kunafungua milango ya "powers of will" zilizo ndani yako ndizo zinazokuponya!. Kinachoponya ni nguvu ya Uungu iliyoko ndani yako, lile jina la Yesu, limetumika kama ufunguo tuu wa kufungulia hizo potentials zilizoko ndani yako!
  4. Wale wahubiri wa miujiza, wanachofanya ni kuutumia uwezo wao wa kuconvince ili kuifungua imani yako, ili ifungue hazina ya nguvu za uponyaji zilizoko ndani yako ndizo zinazotenda miujiza na sio yule mhubiri wala hilo jina!. Mhubiri ni make believe tuu na Jina la Yesu ndio ufunguo wa imani yako ili kufungua nguvu zilizo ndani yako kukuponya baada ya kuamini kwa dhati umeponywa!
  5. Wako watu kibao wanatibu kwa faith healing bila kulitaja jina lolote na watu wanapona!, kinachotakiwa ni kuamini tuu!, ndiko kunakofungua milango ya "powers" na haijalishi unaamini nini, iwe Mungu, Allah, Budha, Mti, jiwe, milima, kichuguu, hirizi, mganga or whoever, whataver as long as unaamini utapona, unapona!
  6. Namna ambayo hizo powers of will zinavyofanya kazi, ni un explainable scientifically, biologically, or medically, ila kinachoonekana ni matokeo tuu, viziwi wanasikia, vipofu wanaona, na viwete wanatembea na vilema wanaponyeka! ndio maana inaitwa miracles, miujiza na jina rasmi la kibinaadamu inaitwa ni kazi ya Mungu, au miujiza ya Mungu, na kwa vile nguvu zinazotumika ni nguvu za Mungu zilizo ndani yetu, hivyo ni haki kuita hii ni kazi ya Mungu.
  7. Wengi hukumbilia kwa wahubiri kuomba kuponywa wakati tayari wameathirika!. Kwa kujua kuwa hizo nguvu za uponyaji ziko ndani yetu, unaweza usisubiri hadi kuugua ndipo uinvoke will power ikutibu, ikiisha jitambua tuu, its you, and no one else, then unaweza kuivoke hiyo will powers ikazuia usipate ugojwa, yaani prevention is better than cure!
  8. Hivyo kwa kuanzia anza kwa kujiandaa kuamini ili hiyo imani yako ifungue milango ya nguvu za Mungu za kufanya uponyaji zilizo ndani yako sio tuu zikuponye, bali pia kuzitumia as shield kuzuia magonjwa yoyote yasikufikie wewe na familia yako!
Somo la 3: Ushuhuda Wangu (My Own Testimonials)

  • Nikiwa primary, nilisumbuliwa sana na malaria, dawa zilikuwa choloquine, baadaya kupona nilikuwa nawashwa sana!, nikawa napewa na phenogan, lakini wapi, ukijumlisha nilikuwa kibonge na vipele vya jasho, ilikuwa baada ta kupona napata mateso makubwa zaidi kuliko hata nilivyokuwa naumwa!. Nikaanza kudevelop uoga wa dawa za malaria, hivyo nikiumwa, bora nisiseme, nijikaze hadi nikizidiwa saana ndipo niseme!.
  • Tangu nilipoingia sekondari uoga huu wa dawa,ukazidi, nikawa nikisikia dalili ya kuumwa kwa mbali, napiga moyo konde, kisha dalili zinapotea. Tangu baada ya kumaliza sekondari, nilikaa 10 years bila kuugua malaria!. Mwaka 2000, nikapata trip ya Canada nikatakiwa kuomba migrant visa, inatolewa Nairobi, ila pia shurti upime ngoma kwenye accredited hospital ilioorodheshwa, hivyo nikaenda Agha Khan hatua ya kwanza ni kupima full blood picture!, jamaa alinipima tuu, akaja ana shangaa, how could this man survive vidudu vingi ajabu vya malaria sijui ni plus plus ngapi!.
  • Jamaa wa maabara akaniita na kuniambia nina malaria nyingi ya ajabu kiasi kwamba anashanga ni vipi niko hai?!. Kwa kiwango hicho, I was supposed to have been dead long ago!. Sikumuhadithia, nikamweleza hapa nimekuja kupima ngoma ndio mpango mzima!, jamaa akasema kwa kiwango cha malaria kilichopo, natakiwa kwanza nirudi kwa daktari, ndipo nikaridi kwa daktari na vipimo, Dr pia akashangaa!. Akasema first thing natakiwa kuwa addmited haraka sana!, nikamgomea kuwa siumwi, sikubali kuwa addmited nahitaji tuu kipimo cha HIV!.
  • Ndipo yule dr akanieleza kuwa huwezi kupimwa HIV kwa sababu damu yangu ina kiwango kikubwa mno cha vimelea wa malaria beyond human survival, hivyo white blood cells hazionekani kabisa!, kipimo cha ngoma enzi hizo kumbe kilikuwa kinapima tuu kiasi cha kinga iliyopo, wakikuta imeshuka, ndipo wanajua ni HIV+ve, akanieleza nina very chronic malaria, hivyo kipimo kitaonyesha ni positive hivyo ili nipime, ngoma lazima kwanza niitibu hiyo malaria!. Akanieleza hata wagonjwa wa TB wakiscreen inaonekana ni ngoma, ukiitibu ukapona ndipo inapimwa ngoma!.
  • Hiyo daktari nikamweleza ukweli kuwa huwa naugua malaria lakini kutokana na kuogopa dawa, sithubutu kuitibu, it's 10 years now!. Akashangaa na kusema hakuna hii kitu ya mtu kutougua malaria tropical Africa. Akanihimiza kukubali admission, pesa ikawa ni issue!, ndipo akaniambia kama tatizo langu lilikuwa chloroquine sasa kuna metakelfin na fansidar hivyo element ya kuwashwa hakuna!, lakini kutokana na kiwango kikubwa cha malaria kwenye damu yangu, ana recomend drip ya quinine ili kuipinguza kidogo kodogo!. Sina pesa za kulazwa Agha Khan, kwanza nimekwenda tuu hospitali hiyo kwa sababu ni mark hospital kwa migrant visa ya Canada.
  • Hivyo nikasisitiza nipewe tuu vidonge. nikapewa metal kelfin kunywa winne siku ya kwanza, kisha vinne tena siku ya pili na viwili siku ya tatu, siku ya nne nirudi kucheki!. Siku hiyo nikanywa usiku, na maji mengi kwa maelekezo ya daktari!, mwili ulikuwa unawaka moto, sikulala usiku kucha ni kukoroma tuu kwa kugumia maumivu, kesho yake sikuweza kuamka, mwili wote umevimba, chakula hakipiti, maji hayapiti, siwezi kuamka, kiukweli nikajua sasa ndio safari!.
  • By that time wife keshahamia US, na mimi naenda kuhamia Canada kwenye issue nyingine kama prospective husband wa a Tanzanian lady mwenye Canadian citizenship!. Hivyo nikaomba msaada home kwa wazee, nikafuatwa nikapelekwa Tumaini Hospital nikalazwa, wakachukua vipimo upya wakakuta kuvimba ni reaction ya sulfa, hivyo wakabadili dawa nitundikiwe drip ya quinine kuishusha hiyo malaria wakati huo mwili unajoto kali ajabu!.
  • Drip ya kwanza imekwisha uvimbe umepungua lakini malaria bado ipo na homa bado juu, drip ya pili ikaisha hali ile ile, drop ya tatu naingia siku ya pili, hali ile ile, nikaona madaktari wanapisha, kama panic fulani, homa gani hii haishuki, Dr, Mkuu wa Pale Dr. Yongolo akasema ikifika siku ya tatu haijashuka, nitahamishiwa muhimbili!. Pia akamleta Dr Mmoja binti mrembo toka Muhimbili akiita Dr. Masha Makata, Msukuma ni Msukuma tuu, hata mgonjwa vipi, binti mrembo mweupe!, mbona nilipata nafuu ghafla, nikakaa kitandani!.
  • Kiukweli Masha alikuwa very friendly, akajaribisha dawa nyingine nyingine, homa ikashuka, vidudu vya malaria sasa havipo, lakini bado naumwa!. Nikaomba Masha aje baada ya ndugu kuondoka, ndipo nikaconfess kwake kuwa hii inawezekana kuwa ni ngoma!, nakamuomba akanipime kisiri siri ili nijue cha kufanya na sio kuunguza tuu fedha hospitalini. Akasema mgonjwa mwenye hali kama yangu, haruhusiwi kupima ngoma, ila kila mgonjwa anaelazwa kwa lolote, pia anapimwa ngoma, hivyo na wao walikuwa wanasubiri 7 days ndipo nipimwe!, nikaziona ni mbali, nikamsihi anisaidie, akanigomea kuwa yeye kama daktari hawezi, ila kunisaidia ataniitia mtu wa maabara niongee nae!.
  • Jamaa wa maabara akaja siku ya nne, akatoa damu, na kwenda kuipimia Muhumbili majibu atampa Masha. Siku hizo ukipima leo majibu kesho. Asubuhi ya suku ya 5, Dr. Masha kaja asubuhi, smiling na mimi nazidi kupata nafuu, huku roho inadunda. Niliisha panga nini cha kufanya iwapo nitakuwa positive maana nimeisha shuhudia shughuli ya kuwahudumia terminal ill HIV victims ndani ya familia, by then vidonge vya kupunguza makali vinatoka Nairobi au South na ku drain the family at the end of the day bado mtu ni safari!. Niliisha jiandaa kisaikolojia kuzuia kutesa watu!. Ndipo Masha akaniambia niko negative!. Amini usiamini nilipona pale pale nikataka kusimama drip ikanizuia!.
  • Mwaka huo wa 2000, ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kutibiwa malaria ndani ya miaka 10!, na ndio mara yangu ya mwisho kutibiwa malaria mpaka hii leo 14 years on, no more malaria!. Hata nikijisikia kuumwa, nikipimwa na kukutwa nayo, never again nitathubutu kuitibu!.
Somo la 4: Jee Nguvu Hizi za Uponyaji zinatoka wapi?.
  1. Msingi wa Nguvu za uponyaji ni Mungu, kwa jina lolote lile. Siku Mungu alipotuumba, alituumba kwa mfano ambapo mwili wetu una sehemu kuu mbili, mwili na roho. Mwili ni hii body inashikika, inaonekana, ina uzito, ina tabia zote za maada/matter. Sehemu ya pili roho, ni pale alipotuumba kwa ,mfano wake na kutupulizia pumzi ya uzima, life, life force, spirit, spiritual body, astra body, roho, uhai. Kinachofanyika ndani yangu kuzuia malaria ni kufuatia ule uoga wangu kuogopa kuteseka na dawa za malaria, ninapo jisikia dalili tuu za awali kabisa, kwa mwili kuwa hypasensitive to touch, nikijigusa tuu vinyelea vya mkono, you feel something, then nasema kwa imani, it can't be malaria!. Hii inaitwa "denial the negativivity", kwa kujitamkia tuu maneno hayo kimoyo moyo, hiyo malaria stops there and then!.
  2. Hizo powers zipo ndani yetu zimehifadhiwa, namna ya kuzifungua ni kwa imani tuu!. Ukiamini, Milango ya powers inafunguka, "powers from within" zinaufanya mwili kuwa stronger na vile vidudu vya malaria harmless ila vipo!. Kadri siku zinavyokwenda vijidudu vinazidi ku pile, ila ni harmless. In ten years time vikawa vingi sana but harmless, nilipopimwa mpimaji anashtuka, daktari anashtuka, mimi niko ok.
  3. Kitendo cha kukubali kunywa ile dose, ni "accepting defeat" hivyo nika break ile barrier ya strength ya powers from within, hivyo ile kinga ya nguvu zangu ikatoweka, wale wadudu waliokuwa dormat wakarudi kuwa active, nisingewahiwa hospitali, pale ndio ingekuwa safari!. Once ukishajiaminisha kitu fulani kibaya kwako ni never, then don't and never accept defeat!. Ukiisha weka nia, never go back, ng'ang'ana hapo hapo hata kama hujaona matokeo spontaneously, never give up, Mungu ana namna zake za kujibu, halazimishwi!.
  4. Tangu ile 2000 mpaka leo, 2014, sijawahi kuugua tena malaria, lakini sasa sio mimi tuu bali na nyumba yangu yote, nimeishield, hatuugui malaria sisi wote tunaishi humo!. Nina watoto 7!, watano wakubwa na wawili wadogo. Wale wakubwa wote watano hawaishi home, wawili wakubwa wako chuo, mmoja yuko A level boarding na wawili wako O-level boarding, home niko na wale wadogo wawili tulio nao home malaria ni no tangu wamezaliwa na hakuna trips zozote za hospital zaidi ya cliniki. Wale wa boarding, sometimes wanapata malaria wakiwa shule/vyuo ila wakirudi home, no more malaria!.
  5. Baada ya kufanikiwa kwenye malaria, nikaamua kusema no kwa baadhi ya magojwa mengine!. Hata katika pita pita zangu, ukikutana na "njia" ambayo sio, machale yanakucheza hivyo sipiti "njia" hiyo!. Na baada ya kutopita, hautapita muda mrefu sana utasikia ya kusikia kuhusu ile "njia" uliotaka kupita!.
  6. Kwa vile hizi works of powers hazina uthibitisho wowote, scientifically, biologically, anatomically or medically to prove how they work, then siwezi kusema conclusive kwamba hizi kwangu ni powers za kuzuia malaria, inawezekana its just a game of chance kwamba mbu wote wanaoingia nyumbani kwangu au kokote nilipo ni wale mbu wasio na malaria!.
  7. Pia licha ya kuwa na hiyo kinga dhidi ya malaria, au machale ya kuziepuka "njia" fulani fulani katika "pita pita" yangu, sasa basi ndio tusilale na neti, si tuna kinga?, au kule katika ile "pita pita" ndio nijipitie tuu peku peku ati kwa sababu nina kinga!. No way!.
  8. Hata wale wanaotibiwa maradhi kwa imani, haina maana akiumwa ndio asiende hospitali ati kwa sababu tuu anamtegemea Mungu!, au alikuwa na ukimwi, kifua kikuu, cancer, akatibiwa kwa imani, akapona, basi hospitali ndio basi!, no!. Faith healing is not a substitute to medical treatment, but rather a complementary!.
  9. Namalizia kwa msisitizo, kuponywa kwa miujiza, nguvu za uponyaji zinatoka kwako wewe mgojwa mwenyewe na sio hiyo anayekuombea!. Wachungaji wengi au waganga, hujifanya wao ndio wenye hizo nguvu za kuponya!, No way, wao wanakupatia tuu ufunguo wa kuzifungulia hizo nguvu zilizo ndani yako ndizo zinazoponya. Hata kile kikombe cha Babu, what you drink is nothing!, imani kuwa kikombe kinaponya ndio imewafungulia njia wenye imani, nguvu zao zilifunguka zikawaponya, na wale wenye imani haba, it was a waste, wastage of time and resources!.
  10. Ukiwa na very strong faith kuwa sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, hivyo tunazo nguvu za Mungu ndani yetu, chochote utakachopanga kwa imani, kitafanikiwa!, sky is the limit!.
Anza sasa kuzifungua hizo nguvu zako na kuanza kuzitumia kufanya mambo madogo madogo.
Somo la 5: Je Wenye kuweza Kuponya wa Miujiza lazima wawe Wakristo?!.
  1. Baada ya kwanza kukubaliana kuwa Muumbaji wa Vitu vyote ni Mmoja, God!, The Creator!, haijalishi mtu una imani gani, au hata kama huna imani, maadam uliumbwa na Mungu na Mungu ndiye aliyeziweka hizi nguvu kwa viumbe wake, hivyo mbele ya Mungu, binadamu wote ni sawa, na wote wanazo hizi nguvu, na wote wanaweza kuzitumia na wamekuwa wakizitumia!.
  2. Kufuatia msimamo huu, watu wote wana uwezo wa kuponya na sii lazima wawe ni Wakristu ila kasi ya uponyaji kwa kutumia imani, imekuwa more popular na Wakristu kwa sababu wanaamini mwenye hizi nguvu za uponyaji ni kupitia kwa Jina la Yesu Pekee!. Ukweli ni kuwa, nguvu za uponyaji, ziko ndani yetu!, Ili uweze kuzitumia ni lazima kwanza uzifungulia milango "open the gates" hizi nguvu zilizofungiwa ndani yako, ndipo ziweze kufanya uponyaji, kitendo cha kuamini "Ni Katika Jina la Yesu!", hiyo ni catalyst tuu ya kuzifungulia milango!. Watu wengine wowote, wenye imani nyingine yoyote, pia wanaweza kuyafanya haya yote alimradi wazifungulie milango hizi nguvu kwa imani yoyote!.
  3. Wakristu wanaamini kawa muujiza wa kwanza wa uponyaji ulifanywa na Yesu, alipomfufua Lazaro, na kaendelea kuponya wagonjwa kwa vipofu kuona, viziwi kusikia, na wenye ulemavu mbalimbali kutakaswa, hivyo powers hizi za uponyaji zimehusishwa na Jina La Yesu, ndani ya Ukristo kama kulivyo na madhehebu mengi tofauti na yote yakimwamini Yesu, vivyo hivyo imani hii ya uponaji inatofautiana sana kati ya dhehebu na dhehebu, ambao Kanisa Katoliki liko makini sana na tiba hizi za imani, wakati makanisa ya wokovu, wakizikumbatia powers hizi kama fimbo ya kukamatia waumini na wafuasi.
  4. Kanisa Katoliki linaamini Mungu hufanya uponyaji pale tuu anapoamua kupitia nguvu alizowapa Makasisi wake ndani ya sala, hivyo hakuna utaratibu wa kuwapeleka wagonjwa au wenye matatizo makanisani kuombewa, kwa sababu maisha yetu sii ya dunia hii, kinachotakiwa kufanyika kwa mgonjwa mahututi, ni kumpatia sakrament ya Upako Mtakatifu ili kumuondolea dhambi zake zote hapa duniani ili akifa aingie mbinguni au peponi moja kwa moja!. Na Baada ya kuzuka kwa wimbi kubwa la uponyaji, Askofu Milingo wa Zambia alitumia powers za asili kuponya makanisani, aliitwa na kupewa kifungo huko Vatican, na kwa hapa kwetu Tanzania, Padri Nkera nae alitimuliwa na kikundi chake cha Wanamaombi kikapigwa marufuku, lakini kufuatia wimbi kubwa la kupoteza waumini wanaokimbilia makanisa ya Wokovu, hatimaye Kanisa Katoliki limelegeza masharti kwa kuwaruhusu watu wanaoitwa Wana Karismatiki kuendesha maombi ya uponyaji bali sio ndani ya nyumba za ibada!.
  5. Kwa vile tumetawaliwa zaidi na dini kuu mbili Ukristo na Uislamu, na hizi sio dini zetu za asili, nguvu za uponyaji wa miujiza zilikuwepo tangu zamani, enzi za mababu zetu, na wazungu na Waarabu walipokuja kutuletea dini zao, walitukuta na uwezo mkubwa, ila wakatuhadaa kuwa hao miungu wa asili tunaowaabudu, sio Mungu wa kweli, bali Mungu wa kweli ni Mungu wao God na Allah, hivyo wengi wetu kujikuta tumezaliwa kwenye hizi mbili kuu bila choice na wote huishia kujikita katika imani ya dini uliyozaliwa nayo tuu, lakini ukweli wa nguvu za uponyaji zaidi ya kwenye Ukristu, pia kwenye Uislamu upo, kwenye Hindu upo, kwenye Budhiism upo kila mahali na hata wengi waganga wa kienyeji, wale ambao ni waganga wa ukweli, ukiachana na hawa wa longo longo, nao wanazitumia nguvu hizi hizi za uponyaji zilizomo ndani yetu, ile kupiga manyanga ndio catalysti yenyewe ya kuzufungulia nguvu hizi za uponyaji zilizo ndani yako, ndizo zinazokuponya bila wewe kujijua huku ukiamini ni huyo Mganga!.
  6. Nguvu hizi za uponyaji, zinasemekana kuweza kuponya magonjwa yoyote yaliyoshindikanika mahospitalini ikiwemo AIDS, cancer, ugumba, vipofu kuona, vilema kutembea, viziwi kusikia, etc etc ila mimi kama mhanga wa ajali, nimefuatilia kwa karibu baadhi ya hawa wahubiri wanaojifanya wana uwezo wa uponyaji, sijaweza kufanikiwa kuuthibitisha uwezo huo!, nyingi na hivi mnavyoviona kwenye TV kama ni uponyaji, asilimia kubwa ni viini macho tuu, ila pia uponyaji wa ukweli upo kwa sababu unatokea ndani ya yule mgonjwa mwenyewe, ambaye anaponywa kwa imani yake huku mhubiri akichukua credts.
  7. Wengi wa hawa wahubiri wa makanisa ya Wokovu, wameishajua powers za uponyaji ziko ndani ya kila mtu, hiyo wanaihifadhi kama siri yao ila wanaitumia imani yako kukuponya and in return kuvuta fungu kwa hoja ya kufanya kazi ya Bwana, na mengi ya magonjwa yanayoombewa ni yale yasiyoonekana!, mapepo, magonjwa na ndani etc, sijapata kushuhudia popote hapa Tanzania kipofu anaona, kiziwi anasikia, kilema miguu inanyooka anatembea!, wengi wa hao mnaowaona kwenye TV ni stage acting to make believe!, ndio maana utaishia kuwaonea pale majukwaani tuu!, hakuna any follow-up ya uthibitisho wa ndugu, jamaa au majirani kuthibitisha huyu alikwa kilema sasa anatembea zaidi zile shuhuda za madhabahuni!,
  8. Kwa vile nguvu hizi za uponyaji ni za kutoka kwa Mungu, process nzima ya uponyaji bado haina scietific proof ya ni nini haswa kinatokea, mtu amekuwa diognaized with aids then anaombewa, anarudi kupimwa, aids haipo tena!, kufuatia kukosekana kwa uthibitisho wa kidaktari ugonjwa huo umeponaje!, nasisitiza mtu ukiwa unaumwa chochote serious, pamoja na posibilitiy ya kujitibia kwa imani, nenda hospitalini ukapate ushauri wa kitabibu na sio kuzitegemea nguvu hizo pekee!. Kuna wengi walioitegemea imani pekee, wakaishia kupata maafa ya kufiwa, kufiliwa na kuwapoteza wapendwa wao, kwa magonjwa ya kawaida tuu ambayo mahositalini wangetibiwa na kupona!.
  9. Pamoja na kuwepo kwa uwezo huu wa uponyaji miongoni mwetu, pia sometimes utapeli wa iaina fulani pia upo!, utakuta wahubiri wetu hawa hawa, wanapofanya zaira za mahubiri nje ya vituo vyao vya kawaida, ndiko wanakofanya miujiza mikubwa ya ajabu!. Tumewashuhudia wahubiri wetu wakipokelewa na kukaribishwa Ikulu za watu wengi huko huko wakifanya uponyaji wa ajabu ambao hapa nyumbani hawaufanyi!, hizi ni make belive tuu na mwisho wa siku kitu muhimu kwao ni ile number ya M=Pesa/Airtel Money/Tigo Pesa au Z-Pesa ndio mpango mzima!.
  10. Na mwisho kama nilivyoeleza kwenye mada zangu zilizotangulia, Mungu yupo ni mwenye nguvu na ndiye aliyetupatia huu uwezo ndani yetu!, ila pia shetani naye yupo!, na yeye pia ana uwezo!. Yesu alipoondoka alituasa kuwa "Watakuja watu, watafanya miujiza ya uponyaji na kutoa mapepo kwa jina langu lakini sio wangu!", hivyo wale wenye imani haba, wanaweza kujikuta wanapotezwa maboya na hawa wahubiri wa miujiza wakidhani uwezo wao unatoka kwa Mungu, kumbe unatoka kwa shetani, na nguvu wanazotumia ni nguvu za giza!. Hivyo kuna uponyaji unafanyika kwa nguvu za Mungu na mwingine ni kwa nguvu za giza!.Jee utajuaje kama hizi ni nguvu za Mungu au ni nguvu za giza?!. The ony way kutambua ni kwa ku "listen from yourself!", " only the voice from wthin ndio inaweza kukuonyesha kweli!.
Nasisitiza hizi mada ni kwa watu ambao ni open minded!, Nawaomba sana wale wahafidhina na ma conservatives wa imani za dini zao, shikilieni mafundisho ya dini zenu, na wenye nia ya kuanzisha malumbano ya dini, tukutanie Jukwaa la Dini, tuwekane sawa!

Natanguliza Shukrani.

Paskali
 
Wanabodi,nina jambo linanitatiza sana hadi hivi leo ni miaka mingi imepita.Tulikuwa na mgonjwa katika familia yetu alipata mapepo.Mwanzo tulijua ni magonjwa ya kawaida maana alikuwa na homa kali tukampeleka hospitali lakini wapi.Tukaamua kumpeleka kwenye maombi na ndiko huko hayo madude yalilipuka na kuongea.

They were more than one and very,very powerful.Hakuna msaada tuliopata huko kwenye maombi.Haya madude yalidai kuwa wao ni "walinzi" na wamekuja kumlinda "kiti" wao dhidi ya "pepo wachafu" waliotumwa toka chanzo fulani kumuua.Kila aliyejaribu kuyakemea haya madude alipata habari yake!yalizungumza uchafu wake pale pale na mwishowe "watumishi" wengi wakatoka nduki,tukakosa msaada.

Nakumbuka kuna mtumishi mmoja aliposhindwa kazi alianza kuizungumza vibaya(kuteta) familia yetu huko nje,cha ajabu sisi hakuna aliyejua lakini haya madude yalijua na kusimulia anayosema yule mtumishi na yakaamuru atalala kitandani wiki mbili na kweli jamaa aliugua vibaya hawezi kuamka kitandani na baada ya wiki mbili walikuja pale nyumbani mama yake,baba yake,bibi,babu..yaani nusu ya ukoo kumuombea msamaha,yale madude yakatamka "tumemsamehe" wale ndugu waliporudi kwao wakakuta jamaa mzima,wakamleta pale analia na kuomba msamaha.Yale madude yakamwambia kwa kuwa ameomba msamaha "toka moyoni" mtoto wake wa kwanza(ambaye wakati huo alikuwa form iv) atafaulu masomo yake na kufanikiwa sana maisha kwa sharti la kuwa "mcha Mungu".

Wadau nawaambia ukweli yule dogo alipiga div one point 9 na aliendelea vema na masomo yake baadae nikasikia yuko Canada manake tulikuwa majirani na huyo mhubiri baadae tukahama.Hakuna mtumishi aliyekanyaga home wala kutaka kusikia habari ya mgonjwa wetu.

Baada ya kuona hivyo,pale karibu palikuwa na sheikh mmoja jirani yetu(marehemu hivi sasa).Alipoona tabu tunayopata,alikuja na kuomba kuzungumza na yale madude.Akawa anaongea nayo kwa upole akitii kila walichotaka huku akiwaomba waseme shida yao na kwa nini hawamwachi mtoto wetu.Ndio huyu sheikh ambaye yalimwambia the whole story,kwamba kuna mapepo yalitumwa kumuua kiti wao,wao kama "walinzi wa bloodline" yetu wakaja kuintefere kumuokoa na watafanya hivyo kwa yeyote kati yetu.

Wakatoa masharti ya kuondoka kwamba "kiti" wao (mgonjwa) awe mcha Mungu wa kweli,aachane na pombe,uzinzi na kila asichotaka Mungu.Yeye binafsi awe na imani na si kutegemea wahubiri na watu wengine,na wakatuasa tusimpeleke kwa waganga kwani hakuna mganga atakayemweza,zaidi ya yeye mwenyewe kuwa mcha Mungu basi.Yule sheikh akatuambia yote hayo na kutuasa tusihangaike zaidi ya kufuata masharti.Sisi ni familia ya kikristo lakini hakuna mtu yale madude yaliongea nae kwa amani isipokuwa yule muislam sheikh kwa kuwa aliyasikiliza na kuyatii kulingana na imani yake ilivyomruhusu hivyo alitusaidia kiasi manake sie hatukuelewana nayo,we were negative kama mjuavyo imani ya ukristo na hivi viumbe ni negative kabisa.

Yakaja mambo ya familia,"tumpeleke nyumbani jamani" basi watu hawakufuata ushauri wa sheikh,tukampeleka kwa waganga nyumbani huko.Ndani ya wiki tatu kila mganga wa kienyeji wa wilaya ile alikataa kutupokea baada ya kusikia yaliyowakuta wenzake.Jamaa kupitia nguvu ya yale madude alikuwa akiharibu nguvu za waganga na kuwadistabilize "kikazi" kabisa.Mbaya zaidi jamaa hakutaka harufu ya pombe.Vilabu vyote vya pombe vilifungwa na ilikuwa kawaida kumuona anaamka usiku na kwenda kuwatwanga watu waliofanya uovu(uzinzi n.k) karibu na mazingira tuliyokuwepo na kila aliyepigwa kofi alianza kuumwa hadi baada ya siku kadhaa mbele walijaa watu pale tulipofikia wanakuja "kusamehewa" wapone na ikawa hivyo.Mji wote ukawa kimya kutokana na haya madude.

Baada ya kuona kila kitu kimeshindikana,ikabidi ukoo mzima uje na kuweka kikao na kuyaomba haya madude kumwachia kijana wao.Yakatoa masharti yale yale ila kwa ukali kwamba kiti wao asipokuwa na mwenendo mzuri kiimani yatawakuta makubwa wote.Yakasema familia nzima tunatakiwa kuwa hivyo.Tukayaambia tutafanya.Yale madude yakaondoka yenyewe bila shinikizo la maombi wala uganga,for the first time jamaa akafumbua macho na kurudiwa na fahamu zake baada ya miezi 9!tukamweleza yote,cha ajabu akasema alikuwa akisikia na kuona kila kinachoendelea pamoja na kwamba muda wa miezi yote hiyo hakuwahi kufumbua macho(lakini alitembea bila kujikwaa wala kukosea).

Tukarudi mjini,jamaa akatoka kwenye mainstream religion na kujiunga na dhehebu fulani la wakristo "siasa kali", akabatizwa, akaendelea na masomo elimu ya juu,hadi leo it's almost 20 years ni engeneer mkubwa huko ulaya,ametulia na family yake,ila ndio mlokole ile mbaya.

Najiuliza na ndio nakuuliza Pasco na wanabodi wengine,hii ni aina gani ya majini yanayomuelekeza mtu kwa Mungu?yanayomuelekeza mtu wema?yanayofanya uponyaji dhidi ya majini wengine?idadi ya wahubiri na waganga wa kienyeji walioyashindwa haya madude ni kubwa mno,what kind of powers is this?

Hivi kweli haya ni majini au kuna aina nyingine ya viumbe Mungu anavitumia kulinda watu ila vyote tunaita mapepo na kuwa negative navyo?nimefupisha ila nina mengi.
 
Huu uponyaji tunapigia mstari wapi? Vipofu kuona? Viwete kutembea? Bubu Kusema? Viziwi kusikia?
VVU kufa damuni?

Ni ni kuponya magonjwa ya kisaikolojia zaidi?
 
Makitu kama hii huwa naprefer zaidi kumeza hivyo wanabodi nawasihi muendelee kunitafunia!
Na kadri navyomeza hii makitu kuna demonstrations flani zinadevelop from within!
 
Najiuliza na ndio nakuuliza Pasco na wanabodi wengine,hii ni aina gani ya majini yanayomuelekeza mtu kwa Mungu?yanayomuelekeza mtu wema?yanayofanya uponyaji dhidi ya majini wengine?idadi ya wahubiri na waganga wa kienyeji walioyashindwa haya madude ni kubwa mno,what kind of powers is this?hivi kweli haya ni majini au kuna aina nyingine ya viumbe Mungu anavitumia kulinda watu ila vyote tunaita mapepo na kuwa negative navyo?nimefupisha ila nina mengi.

Mkuu Kerubi, kwanza asante kwa simulizi hii!, nimeguswa sana na simulizi yako, na bahati nzuri I can tell a true story from just a story!, hii yako ni true story kabisa.

  1. Mungu alituumba kwa udongo kwa mfano wake, huu mwili ndio udongo, na katupulizia pumzi ya uzima, ambayo ndio roho, spirit. Hapa duniani tunapoishi ni ulimwengu wa mwili, yaani "physical world", na besides kuna ulimwengu wa roho, "spiritual world", hivyo binadamu anapokufa, kinachokufa ni mwili tuu, roho haifi, inaendelea kuishi kwenye ulimwengu wa roho.
  2. Kwenye huu ulimwengu wa mwili, kuna watu wanatumia powers za Mungu zilizo ndani yetu kufanya mema na kupata mafanikio makubwa, hawa ni kama wahubiri wa miujiza, waganga wa ukweli, na watu wengine waliofanikiwa kwa njia halali na kusaidia wengine. Vivyo hivyo kuna watu wanatumia nguvu za giza kufanya maangamizi, au kupata mafanikio kwa kumtumika shetani, kwa kujua, au bila kujua!, hawa ndio wanga, wachawi, wanajimu, waganga wa maangamizi etc.
  3. Baada ya kufa na roho kuhamia kwenye ulimwengu wa roho, wale walioishi kwa wema na kumtumikia Mungu, roho zao zinaendelea kuishi as good spirits, kama mizimu ya mababu, na wale walio mtumikia shetani, roho zao zinaendelea kuishi as bad spirits, hawa ndio mashetani, majini, mapepo wachafu etc.
  4. Hayo unayoyaita madudu, ni spirits za mababu zenu ambao wako kama guardian angels. Hawa pepo wanaweza kumuingilia binadamu yoyote wakati wowote but for a reason. Hiyo mizimu huwa ipo tuu ukifanya mambo kinyume cha matakwa ya mila yenu, au kama kuna jambo baya limetumwa na evil spirits kuleta maangamizi kwenu, hao spirits wana intervene na kumuingilia mtu ili ku prevent asidhurike. Kile kitendo cha mizimu kumuingilia mtu na ku take control of his/her body, ndicho kinaitwa mtu kupandisha mashetani, au kukumbwa na mapepo!. ambapo kuna mapepo wema na mapepo wabaya!.
  5. Inavyoonyesha ni kweli kuna watu waliwaloga kwa kuwatumia mapepo wachafu, kuwatupia majini ili kuwaangamiza, mizimu ya mababu zenu ikaingilia kuzuia. Kwa vile miili yetu in a mwili na roho, hiyo roho ndio hizo hizo spirits, ukizitumia vizuri ndio hao watenda miujiza, na ukizitumia vibaya ndio hao wachawi wa maangamizi.
  6. Kuna binadamu wengine wanatumia nguvu za giza, kuwaangamiza wenzao, kwa kuwaloga, kuwatupia majini, mapepo wachafu ili wadhurike. Mizumu ya mababu wa mdhurika ikiingilia kati ndipo kunatokea mpambano kati ya good spirits, mizimu na evil spirits, ndipo utasikia mtu ana mapepo mengi, au mtu anakwenda kuombewa, mapepo yanafurushwa, but within no time yanarudi, au mengine, hata uyafurushe vipi, hayatoki, haya ndio mizimu, na kwenye mtu aliyechaguliwa kuwa makao yao, humuita "kiti"
  7. Wengi wanaofanya "kiti" huwa na nguvu za ajabu!, wengi huishia kuwa waganga wa kienyeji, wengine ndio hawa wahubiri watenda miujiza!, wengine ndio hawa watu wenye mafanikio makubwa sana ya ajabu na husaidia watu kwa kutenda mema!. Kila wanalolitenda linafanikiwa. Ikitokea mtu ukamtibua huyu mtu ambaye ni "kiti" akikasirika, yatakukuta ya kukuta!. Ndio maana wale ambao wako very powerful, wakishajijua wakitibuka ni maafa, unawaku wako very carefull na hasira zao!. Nilisikia alikuwepo yule Shehe mmoja maarufu wa Bagamoyo Mlingotini, alikuwa hata akinyooshea tuu kidole mti, hukauka hapo hapo!. Mwalimu Nyerere alikwenda kuombewa dua kwa shehe huyo, akampa sharti la kufunga bila kula kwa siku nzima. Ile kufika saa 10 jioni, Mwalimu akawa uaumwa sana kichwa!, akamwambia Shehe yule kichwa kinaniuma sana, siwezi kuendelea na dua, shehe akamwambia tulia tuu, dua ilipomalizika, walifuturu pamoja, ndipo Shehe akamuuliza vipi kichwa bado kinaendelea kuuma?!, akasema kimetulia!.
  8. Kwa kawaida watu wenye ulinzi huu wa mizimu, wakikutana na mambo ambayo siyo, kwanza kichwa huanza kugonga kwa nguvu kabla hayajapanda, na mara zote yakipanda hutoa conditions, kama kuna mtu mbaya inambidi atoke, atatoa conditions kutokunywa pombe. etc. Niliwahi kupata demu mwenye hayo makitu, bila mimi kujua, siku anaingia kwenye gari yangu, nimetoka kupata ile kitu (white pepar) na nyingine nimefunga take away napeleka home!. Binti kupata ngafla kichwa kikamgonga akashuka mbio, akaniita nishuke, akaniuliza nimebeba nini kwenye gari, kwa vile sikujua kitu, nikasema sijabeba chochote!. ndipo akanijulisha yeye anayo hayo makitu, yametaka kumpanda kwa sababu hayaitaki kabisa ile kitu!. Masharti yalizidi, mara usinywe pombe, ukichepuka anatuja!, nilishindwa nikaachia!.
  9. Good spirits wanatumia nguvu za Mungu na wanatenda au kuamrisha kutenda yaliyo mema. Bad spirits wanatumia nguvu za giza na kutenda maovu. The dividing line between good spirits and bad spirits is very thin, ndio maana kila wakati katika maandishi yangu nasisitiza mtu kupata ufahamu wa kuijua kweli1, kuna wengi wanamtumikia shetani kwa kutojua, wakidhani ndie Mungu kwa sababu shetani naye kupitia hizo evil spirits, pia ana nguvu za kutenda miujiza!.
  10. Information is power, be informed familia yenu imebarikiwa kuwa na mtu wa hivyo, mtu akiwalogo uchawi wake unamrudia au wanaotaka kuwachezea kwa nguvu za giza, wanawapitia mbali. Mkiweza kumconvince huyo ndugu yenu, kuwa mhubiri, atatenda miujiza mikubwa.
Pasco.
 
Nitatumia muda wakuwa kwenye foleni kesho kuisoma hii kitu, nimawazo yangu mtu hawezi kuandika uzi mrefu uliopangwa vema kama huu bila kuwa na tija kwa jamii.
Mkuu Pleo, hii kitu kwa fonts nilizotumia ni kama page mbili tuu za Bible, na huwa nazipandisha siku za Jumapili moja moja ninapopata nafasi.

Ila pia naelewa maisha ya kisasa ni more materialistic than realistic, watu wanajikita zaidi katika material world, ya "vitu", nitapata nini, hawana tena timu na vitu vya "intangible life values", hivyo uzi huu utakuwa na tija kwa wachache sana ambao ni "realistic".

Pasco
 
Pasco umesema hizo will power za kuponya ukiziamini, unaweza hata kuzuia maradhi yasikufike na sio tu kuponya ugonjwa ulionao! Si ndio?
Jee mimi nikiamini siwezi kupata ukimwi, then najiachia peku peku kwa vimwana, ni vipi siwezi kuupata huo ukimwi? Na ni nikiupata ni vipi hivo vidudu vya ukimwi vitashindwa kufanya kazi yake?
...
Naomba jibu plz!
 
Pasco umesema hizo will power za kuponya ukiziamini, unaweza hata kuzuia maradhi yasikufike na sio tu kuponya ugonjwa ulionao! Si ndio?
Jee mimi nikiamini siwezi kupata ukimwi, then najiachia peku peku kwa vimwana, ni vipi siwezi kuupata huo ukimwi? Na ni nikiupata ni vipi hivo vidudu vya ukimwi vitashindwa kufanya kazi yake?
...
Naomba jibu plz!
Mkuu Mashaxizo, yesi ukiamini huwezi kupata ukimwi, huupati, ila hizi nguvu ili zifanye kazi, unatakiwa kutenda yalio mema tuu, kuzitumia kutendea uovu, utaadhibiwa!, mimi baada ya kujitambua kuwa nikimtaka mwanamke yoyote, kwa kudhamiria, then lazima nimpate, awe ni demu wa mtu, mke wa mtu haijalishi, hivyo kwenye ujana, niliutumia vibaya, ilipofika muda wa payback, the price is too high!.

Mungu alisema piga hodi, utafunguliwa, tafuta utapata, this means ukiomba chocho utapewa, ila usi fanye abuse of powers!.

Mfano ukiamini mwizi hawezi kuingia nyumbani kwako, ni kweli mwizi hawezi kuingia, lakini usilale mlango wazi, simply tuu eti kwa sababu you have the powers kuwazuia wezi!. Vivyo hivyo, una powers za kuzuia ukimwi, usirande peke peku kwa makusudi simply because you have the powers, hiyo ni abuse, hivyo bakora utazipata!.

Hata hawa wanaotumia faith healing kuponya au kuzua magonjwa, ugonjwa ukikushika very seriously nendo hospitali, jana kuna mtu na mkewe wamefungwa jela kule Marekani kwa kosa la kuua bila kukusudia ambapo mtoto wao wa miezi 8 alipata ugonjwa wa pneumonia, wakampeleka kanisa la wokovu kuombewa badala ya hospitali, mtoto kafariki, wazazi ni jela miaka 8, kwa kukua bila kukusudia!.

Pasco.
 
Kuberi afunikaye Majini ni kama binadamu tu! Sote tupo duniani kwa ajili ya kumuabudu Mungu! Kiukweli kabisa Majini wananguvu na uwezo zaidi yetu!
Vile vile majini wako wema na wabaya!
...
Wema hawana madhara kwa binadamu, wanamuabudu Mungu, na kufanya kila jambo jema! Wale viumbe wanatabia ya kupenda wanadamu, so, jini mwema akimpenda mwanadamu, humlinda binadamu huyo na maovu either ya kutendewa or anayotenda huyo mwanadamu! Jini hatokosa masharti akimpenda mwanadamu, masharti hayo ukienda kinyume ndio hapooo utakapoona mzuka wa jini!
...
Sasa basi jini mwema kama huyo, hauwezi kumtoa kwa maombi ya bible or Qurani, coz yeye mwenyewe ni mjuzi wa hivo vitu na ANAAMINI anachokifanya sio kibaya! So ukitaka kumfurusha huyu utafute jini aliemzidi nguvu tu! Tena kuna hatari hata usifanikiwe coz anaweza kukublock katikati ya process!
...
Majini mabaya ndio wanadhuru watu bila sababu, wanafanyisha watu vitendo viovu ie sodoma na uovu mwengine!
Majini hawa nawafananisha na majambazi, wizi, walaunga, wavuta bangi, malaya na wengineo!
...
Majini hawa ukiwapiga kisomo cha dini Quran/Bible ni lazima wadhurike na kukimbia mbio nyingi sana, kwa sababu wanajijua wao ni waovu.
...
Sjui nimeeleweka hapa.
 
Last edited by a moderator:
Duh!nimechoka kabisa.umekwenda deep sana mkuu ila hapo kwenye suala la spirit za wafu kuendelea kuishi kama mizimu ni pagumu kweli kwangu kumeza maana mafundisho ya biblia ni contrary na hii belief kabisa unless sijaifahamu tafsiri sahihi ya biblia on this matter.I only consider your answer because so far you are the only person to give me such a logical answer to my question but now another question comes in my mind,does it mean kwamba kuna kasoro kwenye mafundisho ya mainstream religions kuhusu hii dhana ya spirits?naumiza kichwa kwa vile nataka kujua status ya zile spirits zisizo za kawaida zilizompanda ndugu yangu.Unajua kitendo cha mtu mmoja kuamrisha mwingine kuumwa na akaumwa kweli si kawaida,kwa sababu kila mtu ana ulinzi wa Mungu,yaani hapo ndio palinichanganya,how powerful were these spirits?na wametaka mtu awe mcha Mungu,amekuwa hivyo,wameondoka hadi leo hawajarudi,so they were serious about that na si kutuhadaa!sasa jini gani huyu anaamrisha ibada kwa Mungu na utu wema?so far hili ni jibu pekee logical nililopata kwa swali langu in 20 years,ngoja nikalifanyie research mkuu kwenye kipengele hicho cha wafu kugeuka mizimu,halafu ntarudi.Ahsante sana mkuu for a very,very logical and detailed answer.
 
Makitu kama hii huwa naprefer zaidi kumeza hivyo wanabodi nawasihi muendelee kunitafunia!
Na kadri navyomeza hii makitu kuna demonstrations flani zinadevelop from within!

Ok! Itakua vizuri nawe tukikuuliza.
Tuanzie hapa:
Kwa mtazamo wako na hizo power zako with in, Jee ukiamini tu, kila kitu kinakwenda sawa or kuna some sort of limitation? (i mean jee ni vitu/mipango/matarajio yote huenda sawa kwa kuamini tu bila ya kuwa exception or mikakati mengine apart from belief?)
 
sio bure naona unaendelea kusisitiza kuwa YESU haponyi au ndo mambo ya NWO ,umetumwa kuja kuiangamiza jamii yetu
Mkuu Kamanda, sijasema popote Yesu haponyi nimesema Yesu alifanya miujiza ya uponyaji na hadi kumfufua Lazaro!.

Ninachozungumzia humu ni zile nguvu za uponyaji zinatoka wapi?!. Wengi wanaponywa kwa kutumia neno tuu "Katika Jina Yesu, Uponywe!", au mapepo yatoke!. Jee kinachoponya ni nini?!, ni hilo jina linaingia ndani yako na kukuponya?!, yaani wengi wanadhani ni jina ndilo linaloponya!, No!. Wengine wanadhani ukiisha lija "Kwa Jina la Yesu" hizo nguvu za uponyaji, zinatoka kwa yule muhubiri wa uponyaji, na Yesu analeta nguvu, na kukuingia wewe na kukuponya, na ndio maana ukiisha ponywa unaambia sema "Asante Yesu!".

Ninachofundisha mimi humu ni kuwa hizo nguvu, hazitoki kwa Mhubiri, wala haziletwi na Yesu!, hizo nguvu zimo ndani yetu, ziliwekwa na Mungu mwenyewe ile siku ulipotuumba kwa mfano wake!. Kinachofanywa na Jina la Yesu, ni kuzifungulia tuu hizo nguvu zilizoko ndani yako na kufanya muujiza wa uponaji, Jina la Yesu ni catalyst tuu, nguvu ziko ndani yetu, na namna ya kuzitumia ni kuamini tuu!, ndio maana hata Yesu mwenyewe, wale aliyewaponya, aliwaambia kilichowaponya ni "imani yao!".

Haya sio mambo ya NWO, hii nimkweli tuu ambayo sio wengi wanaifahamu na kuitumia!, nimekuambia sijakwenda hospital more than 20 years nikiumwa chochote ukiondoa ile ajali niliyoipata!, where does hiyo NWO comes in?!.

Kweli hii ninayoifundisha humu, ndio kweli hii hii iliyofundishwa na Yesu mwenyewe, tofauti yangu ni kuwa broader zaidi kuwa ukiamini kuwa you have the powers, hizi nguvu zitafunguliwa na kufanya uponyaji regardless wewe ni wa imani gani!.
Its about opening the gates of powers from within you!.
Pasco.
 
Back
Top Bottom