Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM) apanda Kizimbani

Bado Kidogo 2015

JF-Expert Member
May 24, 2012
207
78
Mbunge wa CCM apanda kizimbani

Mbunge wa jimbo la Bahi kupitia chama cha (CCM), Omary Ahmed Badwel amefikishwa katika Mahakama ya Kisutu akikabiliwa na mashtaka mawili ya kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi milioni moja.

Source EATV
 
Na hii nadhani automatically inamdisqualify kuendelea kuwa mbunge, in case akiwa proved beyond reasonable doubt kuwa aliomba kikweli!
 
Na hii nadhani automatically inamdisqualify kuendelea kuwa mbunge, in case akiwa proved beyond reasonable doubt kuwa aliomba kikweli!

Kabisa lakini kesi inaweza kuchukua hata miaka miwili hadi kwisha, hukumu inatoka muda wa kuchagua viongozi kwa mujibu wa katiba umepita hivyo kusubiri uchaguzi wa 2015.
 
Kumbe ccm kuna watoa rushwa? au huyu mbunge kagoma kutoa mchango wa j2. maana lowasa anatesa tu
 
huyu mwarabu njaa kweli.
cdm shusheni kikosi kazi pale kabla magamba hayajabana.lile jimbo liko wazi tokea uchaguzi mkuu walivyomchakachua jamaa yangu wa pale cct.
 
sala zetu zimeanza kusikilizwa

Hakuna kitu hapa ze komedi at its best. CCM wakiona ratings zao hazipandi kwa kesi hii wataifutilia mbali au haitasikika kabisa kama vile zile za Kina Mramba, Mgonja, Jeetu Patel zilivyotoweka katika sura ya maigizo ya kimahamaka.

Hii kesi itakufa kama zilivyokufa zilisopita, ingekuwa aliyekamatwa ni mbunge wa CDM au chama chochote ambacho ni tishio kwa CCM, kesi hii ingekuwa ni wimbo wa kubembelezea mwana mpaka 2015. Maana ingeandikwa kwa mwezi mara 30 na kwa mwaka mara 365.
 
Kama takukuru wataendelea kufanya kazi kwa makini kama walivyafanya kwa mbunge huyo huenda nchi yetu yetu ikapon,kwasababu viongozi walafi wenye tamaa wamezidi sana ndani ya nchi yetu ,imesababisha wananchi kukosa amani kabisa katika nchi yao tukufu,watu hawali wakashiba sababu ya wajinga wachache,mbona tunasikiasikia watoto wa wakubwa wanakamatwa na mihadarati,na wanatoa rushwa mnawaachia,takukuru nawapa pongezi lakini angalieni msije mkawa mnaangusha matawi tu mizizi mnaiacha inaendelea kunyonya maji ndani ya visima vitakatifu vilivyo ndan ya nchi yetu.
:A S cry:tutamwaga machozi mwisho tutashindwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


 
Back
Top Bottom