Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM) apanda Kizimbani

Kama takukuru wataendelea kufanya kazi kwa makini kama walivyafanya kwa mbunge huyo huenda nchi yetu yetu ikapon,kwasababu viongozi walafi wenye tamaa wamezidi sana ndani ya nchi yetu ,imesababisha wananchi kukosa amani kabisa katika nchi yao tukufu,watu hawali wakashiba sababu ya wajinga wachache,mbona tunasikiasikia watoto wa wakubwa wanakamatwa na mihadarati,na wanatoa rushwa mnawaachia,takukuru nawapa pongezi lakini angalieni msije mkawa mnaangusha matawi tu mizizi mnaiacha inaendelea kunyonya maji ndani ya visima vitakatifu vilivyo ndan ya nchi yetu.
:A S cry:tutamwaga machozi mwisho tutashindwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Huyu mbona mtu mdogo sana? kuweza kuwa mfano wa kuigwa kwa wala rushwa wengine?. Tunawataka wale waliosamehewa baada ya kurudisha hela za EPA na wale waliokula deal la Richmond na Dowans. Hao ndiyo haswa wahujumu uchumi ambao warudisha nchi kilometer laki moja nyuma kimaendeleo.

Ukiwatia hatiani hao na kuwapatia kifungo cha maisha bila parole, basi hata nesi ataogopa kuuza dawa zilizo katika kabati la wodini kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi anayofanya kazi.
 
CCM itaielekeza mahakama imtie adabu ili waonekana wanafanya fairplay!
Actually atakuwa SCAPEGOAT!
Na hili ndio kosa la kiufundi wanalolifanya CCM, huu sio muda mwafaka kwao kujisafisha kwa style hii, hii inawapa wananchi ushahidi kwamba kumbe kweli hiki chama kimejaa rushwa na sasa kinajishaua sababu kinaona uchaguzi umekaribia, tatizo ni kwamba wasipowachukulia wala rushwa hatua, DR SLAA anawapigia kelele, kwamba , unaona wanakumbatiana.

Mi naona kama vile mgonjwa huyu hawezi kupona hata ipewe nini CCM inaondoka tuuuu
 
Wana Chadema wapeni TAKUKUKURU pongezi basi angalau, au mnapenda kila siku muwasakame?
 
huyu jamaa natakiwa mvua nyingi na ikiwezekana anyongwe maana watu kama hwa kwenye jamii maskini hawafai tunawapa dhamana ya ktuongoza kinacofuata wanatunyanyasa
 
Wanatafuta sababu ya kupandisha posho watasema mnaona mpaka mbunge anapokea hongo ya 1milioni
 

Huyu nae anajiita "Great Thinker" hapo Uislam umeingiaje, mbona kina maige, Lowasa, Chenge, nawengine hatukuwajadili juu ya ukaji rushwa wao kwa dini zao! shughulisha akili kidogo kuwa greater thinker ni tofauti na great gossiper!
 

Mbunge wa Bahi (CCM), Omary Ahmed Badwel akishuka katika gari wakati alipofikishwa Mahakamani hapo. (Picha zote na Mpiga Picha wa Habari Mseto Blog).


Mbunge wa Bahi (CCM), Omary Ahmed Badwel akielekea katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Mbunge wa Bahi (CCM), Omary Ahmed Badwel akitoka Mahakamani huku akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi baada ya kusomewa shtaka la rushwa ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Jonathan Liana.

Wakili wa Mbunge wa Bahi, Omary Ahmed Badwel, Mpare Mpoki (kushoto) akitoka Mahakamani.

Na Happiness Katabazi
MBUNGE wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Ahmed Badwel (43) leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), kwa makosa ya rushwa ya shilingi Milioni moja toka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Jonathan Liana.
Wakili wa Takukuru,Janeth Machullia na Ben Lincoln walidai mbele ya Hakimu Mkazi Faisal Kahamba kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na makosa mawili ya rushwa. Wakili Machullia alidai kuwa kosa la kwanza ni la rushwa kinyume na kifungu cha 15(1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007, kuwa kati ya Mei 30 na Juni 2 mwaka huu katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam , Badwel akiwa ni Mbunge wa Bahi na Mjumbe Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) na wakati huo akiwa ni ofisa wa serikali kwa maana ya sheria ya Takukuru, alitenda kosa la kushawishi ili apewe rushwa ya jumla ya Shilingi milioni nane toka kwa Sipora Liana ili kiasi hicho cha fedha aweze kuwapelekea wajumbe wenzake wa Kamati hiyo ya Bunge ili waweze kuipitisha ripoti ya fedha ya mwaka 2011/2012 ya Halmashauri hiyo.
Wakili Machullia alidai shitaka la pili ni kwamba kati ya Juni 2 mwaka huu, katika Hoteli ya Peacock,mshitakiwa akiwa na nyadhifa zake zote hizo alipokea rushwa ya Milioni moja kutoka kwa Liana ili aweze kwenda kuwashawishi wajumbe wa Kamati hiyo ili waweze kuipitisha ripoti ya fedha ya Halmashauri ya Mkuranga huku akijua kufanya hivyo ni kosa. Hata hivyo mshitakiwa huyo anayetetewa na wakili wa kujitegemea Mpare Mpoki alikanusha mashitaka yote na wakili wa Machullia alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika.
Kwa upande wake Hakimu Mkazi Kahamba alisema ili mshitakiwa apate dhamana ni lazima awe na wadhamini wawili wa kuaminika ambao kila mmoja atasaini bondi ya shilingi milioni nne na kusalimisha hati zao za kusafiria mahakamani, sharti ambalo lilitimizwa na mshitakiwa huyo na akapata dhamana. Hakimu Kahamba ameahirsha kesi hiyo hadi Juni 18 mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na kupangiwa tarehe ya kuja kumsomea maelezo ya awali mshitakiwa huyo.
 
Back
Top Bottom