Mbunge Shally Raymond: Kupata Ndoo ya Maji Same ni Elfu 4 Hadi Elfu 5

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943

Mbunge Shally Raymond: Kupata Ndoo ya Maji Same ni Elfu 4 Hadi Elfu 5

Mbunge Shally Raymond amelieleza Bunge kuwa bei ya maji hivi sasa kwa jimbo la Same Mashariki mkoani Kilimanjaro ni kati ya shilingi elfu 4 na shilingi elfu 5 kwa ndoo huku akisema adha ya maji katika jimbo hilo inawakumba zaidi Wanawake.

Kufuatia hali hiyo ameitaka Seikali kumpa majibu ni lini Serikali itakamilisha mradi wa maji wa Mwanga, Same na Mombo ili kuwasaidia Wananchi kuondokana na adha hiyo.

Akijibu swali hilo Naibu waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 86 na ni matarajio ya Serikali hadi kufika mwezi Juni mwaka huu uwe umekamilika.

_MG_1686wqasde.JPG
 
Back
Top Bottom