Mbunge Jonas Van Zeeland Aipambania Mvomero Kupata Maji Safi na Salama kwa Wananchi Wake

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943

MBUNGE VAN ZEELAND AIPAMBANIA MVOMERO KUPATA MAJI SAFI NA SALAMA KWA WANANCHI WAKE

"Je, lini Serikali itakamilisha mradi wa kusambaza maji katika tarafa ya Tuliani?" - Mhe. Jonas Van Zeeland, Mbunge wa Jimbo la Mvomero

"Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa kusambaza maji katika Tarafa ya Tuliani toka mwezi Disemba 2022 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 3.905. Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa tenki la kuhifadhi maji Kijiji cha Rwamba lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita 150,000; Ujenzi wa madakio matatu ya Maji katika Vijiji vya Ubili, Mlaguzi na Rwamba; Ujenzi wa mtambo wa kutibu maji (Treatment Plant); Ujenzi wa vituo 15 vya kuchotea maji pamoja na uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa bomba umbali wa kilomita 70" - Mhe. Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Maji

"Utekelezaji wa mradi umefikia wastani wa asilimia 45 ambapo kwa mujibu wa Mkataba unatarajiwa kukamilika mwisho mwa mwezi Machi 2024. Kukamilika kwa mradi huo unatarajia kunufaisha wananchi wapatao 40,786 waishio kwenye mji wa Tuliani pamoja na Vijiji 9 vya Kigugu, Mlaguzi, Mbogo, Lukenge, Mlumbilo, Rwamba, Ubili Kwelikwegi na Mafuta" - Mhe. Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Maji

"Kwa kuwa Kata ya Mzia ni miongoni mwa Kata ambazo zina changamoto sana ya Maji na tarehe 30 Machi, 2023 mlisaini mkataba na Mkandarasi kwaajili ya kusambaza maji Vijiji vya Ewura, Bwage, Kibatula na Mzia lakini mpaka sasa ni zaidi ya miezi 10 na kazi haijaanza kwasababu Mkandarasi hajalipwa mlichokubaliana (Advance Payment)" - Mhe. Jonas Van Zeeland, Mbunge wa Jimbo la Mvomero

"Ni lini mtamlipa ili kazi iweze kuanza? Tuna miradi kichefuchefu katika wilaya ya Mvomero. Waziri upo tayari kuongozana na mimi baada ya Bunge kwenda kuikagua hii miradi?" - Mhe. Jonas Van Zeeland, Mbunge wa Jimbo la Mvomero

maxresdefaultxcvbgtyh.jpg
 
View attachment 2902557
Hizo ndio kazi ya mbunge na Bado hajamaliza!
 
Back
Top Bottom