Mbunge Selasini apata ajali mbaya! Akimbizwa hospitali, watatu wafa papo hapo akiwamo mamake

Aisee hapa akatowe sadaka kwani Mkono wa Mungu ndo umemwokoa wala si utaalamu wa kuendesha
 
Nimefungua haraka haraka nikajua kapata ajali nyingine kumbe mleta uzi kaleta picha lakini kichwa cha habari ni tofauti. Bora ungeandika hivi. "Picha ya gari la mh Selasini alilo pata nalo ajali" ingekuwa poa.
 
Mungu aipe faraja familia ya mh. Selasini kwa pigo ililopata

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Amakweli watu wengine wanajua kulaumu bila sababu. Habari zinasema "Alikuwa akitokea Arusha kumtoa baba yake hospitalini" Sasa sijui kama hiyo Ipad anagekuwa nayo ingemezesha kumtoa Babake hospitali bila yeye kwenda?.


Ahsante sana mkuu, jibu sahihi kwa watu wavivu kusoma! Yeye anachojua kukandamiza button tu.
 
Labda kwa masahihisho kidogo ni kuwa Mh Selasini alikuwa anatokea Arusha kwenye Mazishi ya shemeji yake ambaye ni Padri Floridi Mahoo. Kwenye gari la Mbunge walikuwamo watu sita.
1.Mama mzazi wa Mh Mbunge - Amefariki
2. Mama mzazi wa Padre walioenda kumzika - amefariki
3.Shangazi wa mama wa padri - amefariki
4.Shemeji wa marehemu Padri-amefariki
5.Mke wa Mh Mbunge -ameumia yupo KCMC
6.Mh Mbunge - ameumia.
Wana JF tuwaombee wanafamilia hizi waweze kuipokea misiba hii.

Mkuu katika hao waliofariki yupo mama mkwe wake mh. yaani mama mzazi wa mke wake. Hili ni pigo kubwa sana. Selasini analalamika kiuno kinamuuma pamoja na kifua huku bega lake likiwa limeshuka. Ila hali yake si mbaya. Mke wake ameumia shingo na madaktari wanasema pingili moja imeachia ila yuko stable anaongea vizuri tu na ana kumbukumbu safi kabisa. Hajajua kama wenzake waliokuwa kwenye gari kama wamefariki bado wamemficha kwani akijua hali inaweza kuwa mbaya. Amefungwa vyuma kichwani kusaidia shingo kurudi pahala pake.

Tuzidishe tu maombi yetu kwao katika wakati huu mgumu. Manake wamepotelewa na wazazi wao wote. Ikumbukwe pia kwamba baba mzazi wa Joseph Selasini naye yupo KCMC alikolazwa kwa muda sasa baada ua kupat stroke. Ina maana baba, mtoto na mkwe wote wapo hospitalini wakati huko kuna misiba.
 
hivi majuzi tulishuhudia ajali ambayo ilitokea eneo la boma ng'ombe ambayo ilimuhusisha mbunge wa rombo joseph selasini ambapo watu watatu walifariki hapo hapo na baadae mwingine kufariki baadae akiwa hospitalini

Wananchi wengi wa rombo wanaamini kwamba ajali hiyo ilikua ni mtego wa kishirikina ambapo kwa maelezo ya awali ya mbunge ni kwamba tairi ya kulia ilipasuka alafu ikatokea boda boda kwa mbele ambayo inadaiwa kuchangia pia ajali hiyo na baada ya ajali hiyo boda boda hiyo haikuonekana

Kutokana na hali hiyo imepelekea wananchi wengi wa rombo kuihusisha ajali hiyo na imani za kishirikina kwa kudai kuwa kuna watu wengi wana mipango ya kumuondoa mbunge wao mpendwa ambapo hii ni ajali ya pili kwa mbunge huyu

Maoni yangu kama mwananchi wa united republic of rombo ni kwamba daima sisi wananchi wa rombo tutaendelea kumpa support mbunge wetu kwenye shida na raha na wote wamtakiao mabaya watashindwa kwani kwa sasa wananchi wa rombo tumeungana pamoja.....

Hali ilivyo nyumbani kwa mbunge joseph selasini ni kwamba baba yake mzazi mzee Romani selasini ambaye ni diwani wa kata ya makiidi kupitia tiketi ya magamba yupo hospitalini ukiwa ni mwezi tangu alazwe kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kisukari hadi sasa hivi hamna mtu anayejua kuhusu kaka yao mkubwa masumbuko lamwai

....ni maoni na wayasemao warombo inawezekana isiwe kweli lakini lisemwalo lipo nawasilisha
 
mimi naamini ni ajali kama zilivyo ajali nyingine na hakuna mkono wa mtu,cha muhimu tumuombee apone haraka na arudi kwenye majukumu yake.
 
WanaJ,
Tumekuwa tukihabarishana habari za siasa na jamii pia. Lakini kwa CDM ni msiba mkubwa sana kwani Mhe. Selasini anaweza akakosa vikao vya bunge lijalo kutokana na majeraha aliyonayo na pia msiba wa watu 4 ambao ni ndugu wa damu. Someni nukuu hii muweze kuona ni kwa jinsi gani jamaa yetu alivyo na maumivu ya viungo na mawazo pia. Tumwombee Mungu ampe nguvu mapema awahi bunge la bajeti.

"Hivi ndivyo ilivyokuwa jana kwenye mazishi ya mpendwa wetu Fr. Florid Mahoo. Na kama vile haitoshi, baada ya mazishi safari ya watu kurejea makwao ilianza na ndipo gari la Mh. Joseph Selasini Mbunge wa Rombo lilipopata ajali maeneo ya Bomang’ombe na kusababisha vifo vya wamama wane: mama yake Fr. Mahoo, mama yake Mh.Selasini (watoi/watoo), mke wa kakae Fr. Mahoo na shangazie. Mh.Selasini na mkewe wamelazwa KCMC akiwa ameteguka bega na mkewe dislocation ya shingo. Mh. Selasini amemwoa dadake Fr.Mahoo. Ni msiba mzito mno ukizingatia kuwa babake Fr. Mahoo alifariki mwezi wa tatu mwaka huu".
 
WanaJ,
Tumekuwa tukihabarishana habari za siasa na jamii pia. Lakini kwa CDM ni msiba mkubwa sana kwani Mhe. Selasini anaweza akakosa vikao vya bunge lijalo kutokana na majeraha aliyonayo na pia msiba wa watu 4 ambao ni ndugu wa damu. Someni nukuu hii muweze kuona ni kwa jinsi gani jamaa yetu alivyo na maumivu ya viungo na mawazo pia. Tumwombee Mungu ampe nguvu mapema awahi bunge la bajeti.

"Hivi ndivyo ilivyokuwa jana kwenye mazishi ya mpendwa wetu Fr. Florid Mahoo. Na kama vile haitoshi, baada ya mazishi safari ya watu kurejea makwao ilianza na ndipo gari la Mh. Joseph Selasini Mbunge wa Rombo lilipopata ajali maeneo ya Bomang'ombe na kusababisha vifo vya wamama wane: mama yake Fr. Mahoo, mama yake Mh.Selasini (watoi/watoo), mke wa kakae Fr. Mahoo na shangazie. Mh.Selasini na mkewe wamelazwa KCMC akiwa ameteguka bega na mkewe dislocation ya shingo. Mh. Selasini amemwoa dadake Fr.Mahoo. Ni msiba mzito mno ukizingatia kuwa babake Fr. Mahoo alifariki mwezi wa tatu mwaka huu".

Duh apewe pole. Huyo Mama yake Fr. Mahoo ni Mama yake Mzazi Mke wa Mh. ina maana mh. amepoteza mama na mama mkwe. Pia ikumbukwe kwamba Baba Mzazi wa Mh. Selasini naye yupo KCMC alikolazwa kwa muda sasa. Walikuwa wakitoka msibani kupitia kumuona mzee pale KCMC bahati mbaya wakafika KCMC wakiwa majeruhi.
 
hii news nimesikia toka kwa mtui wa karibu na wao....ni kuwa baba yake father alikuwa mganga na nasikia jamaa alipokufa wakachoma vitu vyake kibao...na b4 alisema asipelekwe hosp na wao wakampeleka akawaambia watakoma.....so kuna jini pembe litawamaliza ukoo mzima
 
Back
Top Bottom