Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini abaini gari lake kufunguliwa nati za tairi mbili za nyuma

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
selasini.jpg



MBUNGE wa Chadema katika jimbo la Rombo, Joseph Selasini, naye ameanza kuonja “machungu ya utawala wa Rais John Magufuli.”

Taarifa zinasema, jana Selasini aligundua gari yake kufunguliwa nati zote za tairi zake mbili za nyuma.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo Jumapili mjini Dodoma, Selasini amethibitisha kunyofolewa nati kwenye tairi zake zote mbili.

Alisema, “ni kweli tairi zangu zimefunguliwa nati. Hili limenitokea juzi pale Africa Dream hapa Dodoma.”

Selasini amewatahadharisha wabunge wenzake kuwa makini kwa kuangalia na kuyachunguza magari yao kabla ya kuwasha na kuanza safari.

Anasema, “juzi gari yangu ilifunguliwa. Mhe Anna Gidery na Mama Roze Kamili waliniona nilipoondoka pale African Dream tairi ikicheza sana kiasi cha kutaka kutoka wakafikiri ni bearing. Walinipigia sana sikuweza kushika simu kwa kuwa huwa sipokei simu nikiwa naendesha.”

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja huku mjadala juu ya upotevu wa Sh. 1.5 trilioni ukiwa umepamba moto.

Selasini ni miongoni mwa wabunge wa upinzani nchini wanaosisitiza kufanyika kwa uchunguzi thabiti na kuitaka serikali kutolea majibu madai ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG).

Amesema, “jana sikulitumia gari hilo kwa kuwa nilikuwa katika ziara ya kamati na nilikutana na Anna akaniambia walichukuwa wameona ili niwahi garage.

“Leo nimegundua stud(nati) zote za tairi zilikuwa zimefunguliwa kiasi cha kuzizungusha kwa mkono. Hii ni hatari na inathibitisha kuwa tunatafutwa kwa njia nyingi.”
 
Chadema punguzeni makelele kila siku achen uoga hata Kama unafuatiliwa na ndg zako tu mnaisakama serikali wekeni ulinzi Wa kutosha sasa gari lmefunguliwa nati huna ulinzi nyumbani wekeni mageti bhana....
Waache kulalamika wakati wanao uwezo wa kuweka ulinzi binafsi hata kufunga 3D camera ndani na nje kwenye Magari na nyumba zao,waache kuishi kizamani, wabaya wachonganishi wa serikali wanaweza tumia mwanya huo.
 
Huu ni upumbavu Wa hali yajuu yaan mtu hata akigongwa na nzi tayar anaanza kusakamwa na utawala Wa raisi magufuli.

Mtu kapaki gali sehem za hovyo wahuni walitaka kuchomoka na tairi anakimbilia kuulaumu utawala Wa magufuli..

Kweli mtu ukikosa hoja unakuwa unatapatapa sana. Naona upinzani ni mwendo Wa kutafuta huruma tu
 
Waache kulalamika wakati wanao uwezo wa kuweka ulinzi binafsi hata kufunga 3D camera ndani na nje kwenye Magari na nyumba zao,waache kuishi kizamani, wabaya wachonganishi wa serikali wanaweza tumia mwanya huo.
Kweli kabsa mm spendi hzo kelele zao
 
Labda ni WEZI wa tairi za gari. hawakufanikiwa kuziiba. Ukawawahi
Kwani kila jambo jamani ni NJAMA za watu fulani?

Mimi si msemaji wa yeyote yule lakini mengine si ni kutumia common sense tu. Labda ulipekleka gari kwa makanika hakifunga tairi/stud akisahau.

Mbona hata Madaktari husahau vitu kama Gauze, Forceps, na viti vingine TUMBONI mwa mgonjwa baada ya upasuaji.
Baaada ya masaa kadhaa MAUMIVUya mgonjwa huongezeka sana tumbo kuuma ama kuvimba.
Ndo wanasema hebu tumrudishe katika CHUMBA cha UPASUAJI

Wanapompasua wanagudua walifanya MAKOSA. WANAVITOA VITI HIVYO.
Je nayo huwa ni njama ya Doctor ama ni BINADAMU walisahau?
 
Tulishawashauri kuwa fungeni sensor ikiambatana na kamera ya siri ktk magari yenu,lakini hamtaki kusikia.
 
Huu ni upumbavu Wa hali yajuu yaan mtu hata akigongwa na nzi tayar anaanza kusakamwa na utawala Wa raisi magufuli.

Mtu kapaki gali sehem za hovyo wahuni walitaka kuchomoka na tairi anakimbilia kuulaumu utawala Wa magufuli..

Kweli mtu ukikosa hoja unakuwa unatapatapa sana. Naona upinzani ni mwendo Wa kutafuta huruma tu
ndio mjue watu kutokea nchi ya jirani nakubandikwa wasiojulikana walivyocost yale ya dodoma
 
Back
Top Bottom