Mbunge wa viti maalumu wa mkoa wa Singida (CHADEMA) Jesca Kishoa Kafulila apata ajali Dodoma, hali yake ni mbaya

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mbunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Singida (CHADEMA) Mhe Jesca Kishoa, amepata ajali Dodoma muda wa saa nne, hali yake ni mbaya.

Tutawajuza kinachoendelea
FB_IMG_1526030773070.jpg

kishoa.jpg


==========

Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Jesca Kishoa amelazwa hospitali ya Bunge jijini Dodoma baada ya kupata ajali ya gari leo asubuhi Mei 11, 2018 wakati akienda bungeni.

Akizungumza na Mwananchi amesema; “Hapa nimelazwa hospitali ya Bunge, nasikia maumivu katika mguu wa kulia lakini naendelea vizuri.”

“Nimechomwa sindano ya kutuliza maumivu na ninaendelea vyema,” amesema Kishoa mke wa mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, David kafulila

Kuhusu mazingira ya ajali, Kishoa amesema; “katika mataa ya pale Area D, taa zilivyoruhusu, yule wa mbele yangu hakuwa ameonyesha kama atakata kona, sasa alivyokata kwa ghafla, mimi kufunga breki kwa nguvu ikafeli, nikaigonga kwa nyuma.

Chanzo: Mwananchi
 
Mungu aiponye roho na mwili wa huyo mpambanaji, natoa wito kwa madereva wa viongozi muwe makini maana siku hizi mnaendesha rafu saana.
 
Pole sana Jesca,Naona hayo ni maeneo ya mjini kabisa Sijui nini kilitokea. Oooh Mwenyezi Mungu aendelee kukulinda.
 
Pole sana Mama ,tunakubea kwa Mungu akupe Nafuu urudi ktk hali yako ya kawaida.
 
Back
Top Bottom