Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 864
Wakuu kwanza niombe radhi kwa kutokuwa hewani kwa muda kidogo.Nisingependa nitoe sababu za kutokuwa kwangu hewani. Kwa sasa niko likizo mkoani Tanga.Nikiwa huku Tanga nimepata bahati ya kuhudhuria Operesheni Sangara ya CHADEMA,kwakweli CHADEMA wanajitahidi kuchanja mbuga.Katika speeches nilizovutiwa nazo katika operesheni hii ni hii ya Mbunge Grace Kiwelu,yeye alisema kwamba Mbunge mmoja wa CHADEMA ni sawa na wabunge 20 wa CCM kwa utendaji,akadai kwamba wabunge wengi wa ccm sio watendaji kazi yao ni kupiga makofi tu wanapokuwa bungeni.Nakubalina na kauli ya Mbunge huyu kwamba CHADEMA imejaliwa kuwa na wabun ge vichwa na CCM imejaza makapi.Ila mimi naongeza kwamba mbunge mmoja wa CHADEMA ni sawa na wabunge 50 wa CCM