Mbunge kutoshiriki tukio muhimu jimboni kwake inamaanisha nini?

Anselm

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
1,710
291
Siku zote huwa naamini regardless utofauti wa itikadi za vyama lkn lengo kubwa la tuliowapigia kura na kuingia Mjengoni ni kuhanikiza maendeleo yetu na ya majimbo yetu sisi wapiga kura,lkn jambo lililonishangaza wakati mradi mkubwa kabisa wa maji ukizinduliwa Mjini Mbeya sikumbuki kuona uhusika wa Mheshimiwa Mbunge wa jimbo husika katika event ile,ninajiuliza maswali mengi sana kwa kitendo chake cha kutoshiriki, je hakuona umuhimu wa mradi ule ikiwa wapiga kura wake wameteseka kwa muda mrefu wakipata shida ya maji?,au ksbb jambo jema lile limefanikishwa na Serikali iliyo chini ya Chama tawala aliona aibu ku'show-up?
Embu nyie wapiga debe wao mnifafanulie hili,inakuwaje...
 
Namaanisha Mheshimiwa SUGU,si ndiyo Mbunge wa Mjini?
 
mbunge aliyepo mradi haumpi ujiko - unawapa CCM ambao ndo watautumia katika kuomba kura Mbeya mjini 2015!!!
 
Hebu rejea mizania yako ya uchambuzi wa mambo?! Kama hata huko mjengoni walikotumwa mahudhurio ni 30% unategemea nini kuhusu tukio ambalo kimsingi ni sherehe tu na uwepo wake is only symbolic na mbunge wala hakuwa mgeni rasmi?!. Now lipi muhimu zaidi kwako; kuhudhuria vikao vya Bunge ili kutimiza uwakilishi wa wananchi kwa kuchangia katika mijadala mbali mbali yenye tija kwa wananchi au kukimbilia jimboni kuhudhuria uzinduzi wa miradi wakati kikao cha bunge kikiendelea!? tafakari
 
Swali: Mbunge kutoshiriki tukio muhimu jimboni kwake inamaanisha nini?
Jibu: Haimaanishi chochote.

Kwanza mtoa hoja mwenyewe anaonyesha mashaka kama Mheshimiwa alikuwepo au hakuwepo kwenye tukio, yaana hana uhakika sana. Lakini pia angeweza kujenga hoja hiyo akiwa amejihakikishia mambo kadhaa: 1. kuwa Mheshimiwa huyo aliaalikwa na hakwenda kwa kutopenda tu, 2. Mheshimiwa huyo alialikwa na hakwenda kwa sababu maalum, labda kuwepo Bungeni au la 3. Mheshimiwa huyo hakualikwa, 4. Nk. utaona there are a lot of other issues to be analysed before accusing some one ! Maoni yangu tu.
 
mbunge aliyepo mradi haumpi ujiko - unawapa CCM ambao ndo watautumia katika kuomba kura Mbeya mjini 2015!!!

Mimi nafikiri point pale kuhusiana na ule mradi siyo ujiko,point ni jinsi wapiga kura wale watakavyonufaika nao,as long as Mradi ule unagusa maisha ya wapiga kura wake mimi nafikiri kwa Mheshimiwa Sugu alipaswa awakilishe whether alialikwa au hakualikwa kwanza kwa jinsi protocal ilivyo,tukio lile lisingeweza kufanywa without the concern ya Mbunge husika,hili nakataa
 
Ule mradi si wa CCM sasa mbunge wa CHADEMA ataalikwa vipi?

Dhana potofu sana,aliyekwambia mradi ni wa CCM ni nani?

Mradi ule umewezeshwa na serikali ya Jamhuri ya Tanzania kwa kushirikiana na Jumuiya ya Ulaya na Serikali ya Ujerumani,haya mambo ya kubaguabagua ndo yanayotuleteaga tabu siku zote na kauli kama hizi zinafaa zipigwe vita sana kwani hazikawii kuleta rabsha miongoni mwa Wanufaika..eeh leo hii watu wana CCM wa mbeya wakiwakataza wa CDM wasitumie maji kwasababu ni ya CCM utawalaumu ilhali wewe umetoa kauli kama hii?
 
Sasa kama maneno yako ni ya kweli kwa nini JK aliwakebehi wapinzani kwenye uzinduzi huo?
 
Hebu rejea mizania yako ya uchambuzi wa mambo?! Kama hata huko mjengoni walikotumwa mahudhurio ni 30% unategemea nini kuhusu tukio ambalo kimsingi ni sherehe tu na uwepo wake is only symbolic na mbunge wala hakuwa mgeni rasmi?!. Now lipi muhimu zaidi kwako; kuhudhuria vikao vya Bunge ili kutimiza uwakilishi wa wananchi kwa kuchangia katika mijadala mbali mbali yenye tija kwa wananchi au kukimbilia jimboni kuhudhuria uzinduzi wa miradi wakati kikao cha bunge kikiendelea!? tafakari

Samahani naomba nikujibu kwa swali, rejea ushiriki wa Mheshimiwa Sugu kwenye mazishi ya Marehemu Kanumba (RIP) pale leaders na hatimaye Kinondoni huku Bunge likiendelea na vikao vyake kule Dodoma,lipi lilikuwa ni muhimu kwako wewe Mpiga debe wake na Mheshimiwa husika, kushiriki Bunge au kuhudhuria msiba wa Msanii?
 
labda mtufafanulie taratibu zikoje. Raisi anapokua jimboni kuzindua miradi ya maendeleo mbunge husika huwa anashiriki kwa taratibu zipi.?
 
hitimisho,tunatakiwa tuweke pembeni itikadi ze2 za kisiasa kwenye baadhi ya mambo kama ilo la uzinduzi wa huo mradi ok!
 
Watanzania tunapenda sana sherehe kuliko kazi, hata tukijenga vyoo tunaandaa sherehe ya uzinduzi, halafu tunaenda kuuza sura kwa ajili ya malengo ya kisiasa.

Miaka 50 bado tunasherehekea uzinduzi wa vyoo, visima, barabara n.k.

Wenzetu wanapeleka bendera mwezini na kwenye mars sisi bado tunaangalia nani kahudhuria sherehe nani hajahudhuria, awepo asiwepo maji kama yapo yatatoka tu hata bila sherehe
 
Wewe uliyeleta hii mada tuambie ziara ya JK ilikuwa ya kichama au ya kiserikali? na kama ilikuwa ni ya kiserikali kwa nini alizungumzia mambo ya kichama na kukashifu upinzani?

SUGU ni Great thiker alijua kabisa JK lazima katika maelezo yake na kulingana na hali ilivyo sasa kisiasa kwa upande wa CCM lazima angetoa maneno ya kejeli kuhusu upinzani jambo ambalo lingemkwaza Mh. Sugu na ninavyo mjua angeweza kumvunjia heshima mkuu wa nchi.
 
My thought as well! Kama hakualikwa wala kushirikishwa, hawezi kujitokeza tu kama Lowassa alivyojipeleka kwenye hafla ya kanisa ifakara! He is better than that!
Mimi sio mpiga debe. Jibu la swali lako ni Hakualikwa/hakushirikishwa.
 
Watanzania tunapenda sana sherehe kuliko kazi, hata tukijenga vyoo tunaandaa sherehe ya uzinduzi, halafu tunaenda kuuza sura kwa ajili ya malengo ya kisiasa.

Miaka 50 bado tunasherehekea uzinduzi wa vyoo, visima, barabara n.k.

Wenzetu wanapeleka bendera mwezini na kwenye mars sisi bado tunaangalia nani kahudhuria sherehe nani hajahudhuria, awepo asiwepo maji kama yapo yatatoka tu hata bila sherehe

Ama kweli akili ni nywele kila mtu ana zake,Rafiki, mradi wa bilioni 80 (pesa iliyochangiwa na nchi za Jumuiya ya Ulaya na fedha za walipa kodi wa Ujerumani bila kusahau walipa kodi sisi unaufananisha na uzinduzi wa vyoo!!!!!!
Unakosoa hadi uwepo wa mwakilishi wa Jumuiya ile ya Ulaya na Balozi yule wa Ujerumani walioacha shughuli zao kuja kuhakikisha kazi waliyotumwa na wananchi wao ina'take-off vizuri na kutetea ziara zisizo rasmi za Sugu pale CBE Dodoma
Campus...ama kweli peruz JF ujionee
 
Back
Top Bottom