Mbunge kutoshiriki tukio muhimu jimboni kwake inamaanisha nini?

Ama kweli akili ni nywele kila mtu ana zake,Rafiki, mradi wa bilioni 80 (pesa iliyochangiwa na nchi za Jumuiya ya Ulaya na fedha za walipa kodi wa Ujerumani bila kusahau walipa kodi sisi unaufananisha na uzinduzi wa vyoo!!!!!!
Unakosoa hadi uwepo wa mwakilishi wa Jumuiya ile ya Ulaya na Balozi yule wa Ujerumani walioacha shughuli zao kuja kuhakikisha kazi waliyotumwa na wananchi wao ina'take-off vizuri na kutetea ziara zisizo rasmi za Sugu pale CBE Dodoma
Campus...ama kweli peruz JF ujionee

Pole sana Anselm! Wewe ni mmoja wa watanzania wengi ambao bado wanatukuza WAZUNGU kutokana na misaada. Badala ya kusikitika ni kwanini baada ya miaka 50 serikali bado inahitaji misaada ya kijinga kama hii kujenga miundombinu ya maji, wewe unaona fahari kuendelea kutegemea misaada ya wakoloni wa zamani. ungenambia kuwa uwepo wa kiongozi fulani katika sherehe hiyo una umuhimu gani badala ya kusema kuwa eti hadi wazungu wamefika ndo kila mtu ababaike au? Unajua msafara wa kikwete umegharimu kiasi gani cha pesa kwa ajili ya kwenda kwenye hiyo sherehe ungemshauri amuachie hiyo kazi mkuu wa mkoa wa mbeya. Acha kuendekeza fikra za kizamani amkaaaaaaa......
 
Back
Top Bottom