Mbunge Elibariki Kingu atoa waraka wa kuaga Jimboni Singida Magharibi

Kanyunyu

JF-Expert Member
May 2, 2012
335
495
Taarifa kwa Jimbo la Singida Magharibi Pamoja na Ikungi

Napenda kwa masikitiko makubwa kuwataarifu wananchi wangu wa jimbo la Singida Magharibi na hasa wananchi na wapiga kura wa Minyughe kuwa hatutaweza kutekeleza ndoto ya kujenga chuo cha VETA kama nilivyoahidi wakati wa kampeni zangu za kusaka nafasi ya kuwa mwakilishi wenu kama Mbunge mwaka 2015.

Wapenzi wananchi wangu wa Singida Magharibi na hasa kata ya Minyughe ambapo chuo hiki tulishafnya kila maandalizi kukijenga naomba kuwaeleza ndoto hii haitafanikiwa;amnajua namna nimehangaika toka mwaka 2015 wakati Ikungi ikiwa na Siasa kubwa za ushindani ,Na mnajua namna Mbunge wenu nilijitoa kwa nafsi,Mali na Hali kuona Ikungi yote inakua na uwakilishi wa Chama changu CCM kwa ngazi zote,

Mnajua namna raslimali ambazo zilipaswa kuwanufaisha ninyi wapiga kura wangu nilizitumia kupeleka matumaini kwa jimbo jirani la Singida Mashariki ili kuwaamsha wakisaidie chama chetu kushika hatamu,

Mlinielewa watu wangu pale nilipowanyima ukarimu wangu binafsi kwa maslahi ya chama kuwasaidia wenzetu nyakati za giza,Misaada binafsi kama ya vikundi vya akina Mama tulipeleka Mungaa na kuwaomba akina Mama wa Minyughe mvumilie ili na wenzetu ambao hawakua na Mbunge wa CCM wapate matumaini,mnakumbuka tulisadia vitanda vya kujifungua kwa wenzetu wa Mashariki vyenye thamani ya zaidi ya miln 10 ili kuwapa wenzetu matumaini ya kuwa na wabunge wa CCM ambao Pamoja na kuwa wawakilishi imara lakini bado wana moyo wakutumia kipato chao binafsi kuwagusa maskini na kuleta usawa katika huduma za msingi,Mbakumbuka namna tulivyo jinyima kusaidia hata usafiri wa pikipiki za chama kwa kata ya Siuyu ili mradi tuu uongozi mpya wa udiwani uweke alama za unyenyekevu kwa kukiinarisha Chama cha Mapinduzi,mnakumbuka tulivyojinyima kusaidia matawi yote ya CCM jimbo la mashariki mamilioni ya pesa ili kukiimarisha chama chetu katika harakati za kujijenga na kurudisha heshima ya utumishi wa utu na umoja wa nchi ambao ulivurugwa na wawakilishi wa chama ambacho hakikua na uzalendo wa dhati kwa taifa na watu wake.

Mnakumbuka watu wangu namna tulivyo jinyima kuacha kutimiza ahadi zetu kwa watu wetu kusadia kuleta kila tumaini kwa wenzetu kusaidia cements katika mashuke mbali mbali huko jimbo la mashariki kwa kutoa mamilion ya Tshs.

Hatukua wabinafsi watu wangu tuliwagusa hata wenzetu wa jimbo la Singida kaskazini na Mkalama kwa kuwasaidia Mama Zetu vitanda vya kisasa vya kujifungua akina Mama vya thamani ya Mamilioni ya Shs,hatukufanya hayo sababu ya kutaka madaraka kwani mnajua Mbunge wenu nisingeweza kuomba kuwa Mbunge wa CCM kwa maeneo ambayo wijawahi kuishi ila upendo wa Yesu wa kinyenyekevu ulitusukuma kuwagusa ndugu zetu.

Watu wangu sio lazima tuthaminiwe kwa karama hii ya kinyenyekevu kwa watu wa a Mungu ,tunajua gharama ya kitume kwa kutenda mema mara nyingi duniani ni kejeli na matusi lakini Neema ya Mungu wetu ni kutufanya kubaki waaminifu kwake pekee hata kama tutakosa yote tunayotamani katika dunia hii.

Watu wangu mnakumbuka Mbunge wenu nimetumia kipato changu binafsi kwa zaidi ya Tshs miln 234,000,000 kusaidia watu wangu katika mashule,zahanati Mitaji kwa akina Mama nankusaidia pikipiki zaidi ya 26 kwa vijana lakini msihuzunike Haya si kitu katika ukimwengu wa siasa za chuki na fitina ,wao wanaandika taarifa kuwa hatujatekeleza ahadi vumilieni mimi nimetiwa moyo na huruma za Mungu kuwa dunia sio rafiki kwa wacha Mungu .

Mnakumbuka namna nimekua mwadulifu kwa pesa za jimbo ,hatujawahi kujinufaisha zaidi za kuzileta zote kiwango ambacho tumejenga zahanati mpya na mashule kila kona ya jimbo letu,kiasi cha kuleta matumaini kila mahali nikipita mnajaaa kwenye mikutano yangu kunitia moyo mimi na Chama
Changu.,,Wanasema hatujatekeleza tulieni watu wangu ila Jueni jambo moja Mungu huwa hadhihakiwi.

Watu wangu manakumbuka kata ya Minyughe ilikua na zahanati moja tuu hapo minyughe lakini nilipochagukiwa vijiji vyote tumeshajenga Maboma mapya ya zahanati ,tumejenga madara na nyumba za uwezo wetu kwa walipa kodi wa Mulagwe,bunku,Kinyarimi,Kikhomango na mwanduwataturu huku madaraja makubwa yanayozunguka mto Wa Minyughe yakiwa yamekamilika na nyumba za kisasa za waaalimu na madarasa yakiwa yamekamilika,mnakumbuka maji pia tumeshayachimba.

Watu wangu nayasema Haya mkijua kuwa yametendeka jimbo zima.

Watu wangu msinione Mbunge wenu nimeyafanya Haya na serikali kuyaleta kuna nyakati navuja damu ndani ya moyo wangu kwa fitina ngumu lakini sisemi maana ntawavunja moyo nanyi mtakata tamaaa.lakini mjue siku hizi fitina na majungu vina nguvu kubwa kuliko kujitoa na unyenyekevu;hasa kwa wale wasio na matawi ya uvuli nadhani mmenielewa.

Wapenzi wangu mnajua mnajua wanavyohangaika na roho ya Mbunge wenu tena watu ambao ndio wametumwa na Chama kusimamia misingi ya haki na umoja kisa tumekataa na kuchoshwa na ubinafsi wao wakodhani bila wao eti hatukakuwa na maisha ,ni wajinga kweli wamesahau kuwa sisi tunalo tumaini la Mungu na maisha mengine hata wakotuchubua na kutuangamiza

Watu wangu nawakumbusha,Toka nimekua Mbunge wa chama
Chenu nimekua mwaminifu kwacho Japo mapito yake ni magumu sana ila nyie siwaambii kuwavunja moyo

Watu wangu nawaomba shikamaneni nyakati hizi mkipe heshima chama
Hiki kwa kumuenzi mwalimu Nyerere na Baba wa Taifa hili achaneni wa wanaowakwaza,kapigeni kura za vitongoji na vijiji kuipa CCM ushindi na mimi niko Pamoja nanyi.

Watu wangu mnakumbuka alikuja Mama Samia Suluhu na kutupongeza kama alivyofanya Majaliwa Kassimu Majaliwa,Wamefanya Haya sababu wameshuhudiwa na Mungu juu yanuadilifu wetu kwenu watu wangu,

Watu wangu mnisamehe kwa kuwachosha ,nimesema hayo kuwaanda kuwa Hatutaweza kujenga chuo cha Ufundi Minyughe VETA.nina jua mtego huu sio wenu ni wangu Mbunge wenu lakini nawaambie ni vema uninase mimi ili nikiwa nje ya siasa nikiache chama kikiwa salama na kimoja,

Watu wangu mnajua mimi ni Mkristo katika imani;najua mnajua lini tuliahidi kujenga chuo cha VETA minyughe,mnajua ilikua mwaka 2015 wakati jimbo la mashariki likiwa upinzani,lakini Pamoja na juhudi kubwa tumefanya,dalili zinaonesha kumeibuka dalili ya vita kuhusu chuo kujengwa wapi

Wapenzi wangu CCM ni kubwa kuliko Minyughe,CCM ni kubwa kuliko mimi kupata sifa kwenu na kwa manajimbo,mnajua tumeshapima eneo na kufanya kila maandalizi ila wenye nguvu wapishe;nawaomba niadhibuni mimi kwa kushindwa kutimiza ahadi yangu kwenu kuliko mimi kushupaza shingo na kukiletea
Chama mpasuko.Najua tuna haki zote na tuliahidi ahadi hii kabla nuru haijawaka mashariki lakini warudia niadhibuni mimi kama Kingu Elibariki kukinusuru Chama
Changu Kugawanyika.

Mnajua nimewahibiria sana kujenga chuo mnajua nimetukanwa sana na wapinzani wangu hasa wa hapo Minyughe kuwa sitafanikiwa ndoto hii;najua chumba kimefunguliwa dhidi ya kutukanwa kwangu na kusemwa kwangu kwa utabiri huo,Na najua ni jaribu kubwa kwangu watu wangu nawaahidi nalibeba kwa Maslahi ya hiki chama.

Watu wangu zimeshaanza propaganda kubwa sana hasa nyakati hizi za chaguzi za serikali za mitaaa huko sepuka na Italala ila jueni mna Mbunge mwenye akili kubwa na asiyetishwa;Wanatumia mbinu za kipumbavu ambazo wanajua mimi ni smart sana mashinikizo Nya barua za kijinga kumkatisha tamaa mtu aliyejitoa na kushuhidiwa na Mungu wao kuwagurahisha waliowatuma ni jambo kubwa kukiko hata kumheshimu Mungu,mbunge wenu nina hekima na akili ninajua wafanyalo ila CCM ni kubwa kuliko chuo cha Minyughe cha VETA.

Watu wangu wa Minyughe nitakuja hapo kwenu kufanya mkutano;kuwaeleza kuwa hatutajenga chuo tena hapo,Najua madhara ya mtego huu kwangu kisiasa lakini nimepima uzito mimi na Chama nani wakumpa maslahi nimeona nikipe chama kukiacha kimoja.

Rais ametujali sana watu wangu
Chama hiki kimenipa heshima

Acha na mimi nikiheshimu kwa kukifanya kimoja kuliko kukiletea migawanyiko mimi kwa asili ni mtu wa kusamehe.


Jueni jambo moja mimi ninawapenda sana

Najua mapenzi yenu kwangu;
Najua upendo wenu kwangu,

Tuwe tayari sisi kuumia ila tukiache chama hiki kimoja na salama

Rasmi Mbunge wenu nimeahidi kutoa ushirikiano kuhakikisha chuo cha VETA kinajengwa jimbo la Singida Mashariki

Kidumu Chama Cha Mapinduzi

Wenu

Elibariki Immanuel Kingu
Mbunge Singida Magharibi
 
Na watu awa ndo tuna imani kua watalivusha Taifa ili. Lakini ngoja niheshimu tu haki ya kutoa hoja na maoni yako( Mabeberu wanasema Freedom of Speech)
Singida Mashariki ni jimbo la Kimkakati ..
 
Singida Mashariki alikuwepo Lissu,Rais anampa nguvu kwanza Mtaturu,wewe Kingu unataka kuchomoa betri,utakosa ubunge 2020,acha kabisa,tulia hivyohivyo,wa Mashariki waaminishwe kua Lissu alikua hafanyi lolote.
 
Sasa kama ndani ya ccm unalia mapito yake ni magumu huko kwa wengine itakuwa ni jehanamu bila shaka.

Sawa,tunakushukuru utuachie jimbo tumuweke mchapakazi. Maana wewe ulilete unafiki dhidi ya wananchi wako.
 
Pale mshirikina anapomtaja Mungu kila mara ili kutakatisha uchafu wake. Huyo Kingu ni mtu wa siasa za fitina na kupenda sifa za kipuuzi, alikuwa anamfitini Lissu bila kujua ukiua kwa upanga utauwawa kwa upanga. Sasa ngoja Magufuli aue vyama vya upinzani kisha wabaki ccm wenyewe wakishirindana kwa majungu, Udini na fitina, kwani sera na hoja zitakuwa hazina nafasi.
 
Mnamtaja Mungu utafikri ni watumishi wa Mungu kweli, mwenzenu amepigwa risasi Kama mvua,lakini hakuna hata sehemu moja uliompa Pole ila unahuruma na jimbo lake, hata pole kwa wananchi waliomchagua hakuna ila unajifanya kuwa na uchungu nao, ni heri ungemtaja shetani ikajulikana,kuliko kumsingizia Mungu ambaye hata matendo yake hayapo mioyoni mwenu, mwenzenu amepuruchuka kwenye kaburi kama ndenge aliyepuruchuka kwenye mtego,hata pole ya kiswahili kwake na kwa waliomchagua inawashinda kweli!, lakini jimbo lao mnalitaka.
 
Aisee kumbe hata wachawi huwa wanamjua Mungu kwenye harakati za kuwahadaa watanzania utawala wa giza kweli yupo hata pole hamna kwa lissu sita wahi kuwaamini ccm mpaka kaburini!!!!
 
Ulie andika Huu waraka Elibariki Kingu ni mbunge wa jimbo la Iramba mashariki na sio magharibi Magharibi ni Mwigulu Nchemba
 
Back
Top Bottom