The Analyst
JF-Expert Member
- Feb 26, 2011
- 464
- 246
Baadhi ya Wazenji wapinga-muungano wanadhani wabara wanaulilia saaana Muungano eti tu kwa sababu JK na wenzake hawajawawekea mazingira ya kuuvunja kwa haraka. Ngoja niwaambie ninachokiona Bara:-Majority ya wabara ni wakarimu na wasiopenda mizozo. Kwao hawa Zanzibar inawekera inapolalamika saana kuonewa na Bara wakati inajulikana wazi kuna mambo mengi sana Wazanzibar wanapendelewa katika Muungano huu (pengine hii inafanywa maksudi ili wasilalamike zaidi). Wazanzibar ni watanzania wanapokuwa huku Bara wakati ambapo sisi ni Wabara tunapoenda Zanzibar.Aina nyingine ya Wabara ni ile ya wanaotaka Zanzibar iache kudekezwa ili wanaopenda purukushani za mara kwa mara kama UAMSHO (Wapenzi wa CUF) wajue maisha ya sasa ni kufanya kazi kwa juhudi na si kulalamikia kukosa misaada ya OIC na FIFA kila unaposikia njaa. Mfano wa hawa ni Mimi, Mh. Tundu Lissu nk.Nisiwafiche ndugu zangu wa "nchi ya visiwa jirani". Katika hali practical huwezi kuwa na Muungano wenye usawa kati ya Tanganyika na Zanzibar hata siku moja. Sababu ni hizi zifuatazo:-1. Kuna tofauti kubwa sana zitakuja katika kuchangia gharama za Muungano huo. Can these Brothers contribute equally?2. Imagine nani atakubali kuwa soko la mitumba inayotoka Jpn, Dubai, England na kupitia kwa mwingine kama inavyotokea kwa sasa wakati wote tuna bandari zetu?3. Kama nafasi za kazi katika vyombo vya Muungano kama jeshi la ulinzi, polisi nk zitatolewa kwa idadi sawa kila upande, Zanzibar itaweza kulipia gharama za watumishi hao? Ununuzi wa vifaa vya kijeshi, kulipia mkonga wa taifa, nk je?Nikipata nafasi nitaandika thread kuelezea umaana wa serikali mbili (japo hata mimi sizitaki) pamoja na kwamba watu wanamponda mwalimu kwa muundo wa Muungano.