MESAYA
Member
- Jan 4, 2012
- 55
- 52
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Nianze waraka wangu huu kwa kutanguliza salamu zangu za dhati kwako. Kwa taratibu za mila na desturi za kimasai, napaswa nikusalimie kama baba yangu kwa kusema "Airoroki papa". Tukirudi kwa lugha yetu mama ya taifa napaswa nikusalimu kwa kusema "Shikamoo baba". Vile vile kwa kuwa una wawakilisha watanzania wanaoamini kwa Imani za dini mbalimbali, nisiwanyime nao ladha ya salamu zangu kwako. Nianze kwa salamu za kikristu ambapo napaswa niseme "Bwana Yesu asifiwe Mheshimiwa Rais". Nikisema pia "Asalam Aleikum Warahman tulahi Allah wabarakatu" nafikiri utanielewa nawakilisha kundi lipi.
Mheshimiwa Rais, ama baada ya aya nzima ya salamu zangu kwako, nikupe pole sana kwa maradhi yaliyokupata hivi majuzi na kupelekea mwili wako kufanyiwa upasuaji. Pole sana kwa hilo na Mwenyezi Mungu mwingi warehema muumba wa mbingu na dunia akujalie kheri upone haraka na urudi katika hali yako ya kawaida kiafya ili uendelee kuwatumikia watanzania.
Mheshimiwa Rais, mimi ni kijana wa kimasai niliyebahatika kupata elimu hadi ya chuo kikuu kwa kutegemea ufugaji wetu ule ule wa kuhama hama kutafuta malisho ya mifugo na maji. Aina ya uchumi wetu huu umetusaidia tulio wengi kupata fursa za kusoma ijapokuwa kwasasa tumedhamiria kuwarudisha watu wa jamii hii katika lindi la umasikini tororo kwa kuona umuhimu wa mwekezaji kwenye ardhi yao na kuyapa kisogo matunda wanayoyapata kwa aina hii ya uchumi wanaoendesha kwenye ardhi yao.
Mheshimiwa Rais, nadhani umezunguka na kupita kila kona ya nchi hii. Nadiriki kusema kila hatua uliyopiga ndani ya viunga vya nchi hii, hujawahi kumkuta ama kumwona mtanzania mwenye asili ya umasai ambaye amekaa barabarani akisubiri wapiti njia wamtupie japo chochote kitu ili afanikishe kusonga mbele kwa maisha yake. Bali umekutana na wamasai ambao wamekuwa mstari wa mbele wakichakarika huku na kule ama kwa kuwalinda watanzania wengine ili apate ndarama za kuendeshea maisha yake, ama kwa kusokota na kusuka nywele za dada zetu ili tu mdomo uende kinywani, ama wakizunguku kila kona kutoa huduma za kuponya afya za watanzania kwa kuuza dawa za asili ili mradi tu kuitwe jioni na hatimaye kesho, ama wakisafiri huku na kule na mikokoteni yenye madumu ya maji wakihakikisha kwamba watanzania wote wanapata huduma ya maji kwa malipo yatakayowawezesha kupata mkate wa kila siku. Hiyo ndiyo asili ya mmasai, kamwe haishi kutafuta ili mkono uende kinywani na kamwe hawezi kuwa ombaomba.
Mheshimiwa Rais, Lengo langu kubwa leo si kukupa sifa za kabila hili la wa masai bali nimejaribu tu kukuonyesha ni athari gani tutapata jamii ya wamasai kama sera hii ya taifa itaendelea ya kutunyang'anya ardhi yetu tuliyopewa na Maulana na kumpa mwarabu ama mzungu kwa kisingizio cha uwekezaji.
Mheshimiwa Rais, Nisikuchoshe sana kwa utangulizi mrefu ambao sio lengo kuntu la barua yangu hii kwako. Lengo hasa la Makala hii kwako, ni kufikisha mawazo yangu kama mtanzania wa daraja la mwisho kabisa kwako ambaye sidhani kama ipo hata siku moja nikapata nafasi japo hata ya kukusalimu shikamoo na ukaitikia marahaba.
Mheshimiwa Rais, Mawazo yangu haya ya leo yanaweza yakawa yamezungumzwa na watanzania walio wengi wenye nafasi mbalimbali ndani ya nchi hii ila sidhani kama walizungumza kwa namna hii ambayo mimi leo nimeamua kuwasilisha kwako. Nimekuwa na desturi ya kuandika Makala za kila namna kwa umma kama njia niliyojiwekea kuwalipa fadhila watanzania wenzangu wa Vijiji vya Nadosoito na Mkonoo ambao naamini nimepata elimu na makuzi yaliyo bora kwa busara, hekima na malezi yao.
Mheshimiwa Rais, Kama mtiririko na muendelezo wa karia yangu ya uandishi wa Makala, leo nimeona niwasilishe Makala yangu kwako kwa namna ya barua kama alivyokuwa anafanya mwanamapinduzi wa India Nerhu kwa kijana wake Indra Ghandhi (Glimpses of the World history)
Mheshimiwa Rais, Makala yangu hii ya leo inahusu mustakabali wa muungano wetu kwa vizazi vijavyo. Naamini utavutiwa sana kuona uwepo wa vijana wachache ndani ya taifa hili ambao wanawaza juu ya mustakabali wa nchi hii na vizazi vijavyo.
Mheshimiwa Rais, Nianze kwa kukumbusha japo kidogo juu ya sababu za Tume ya Jaji Nyalali kupendekeza uwepo wa serikali ya Tanganyika. Sina maana kwamba hujui, wala sina maana kwamba umesahau, bali nataka nitengeneze msingi wa hoja yangu ya mustakabali ya muungano wetu kwa vizazi vijavyo.
Mheshimiwa Rais, Kung'ang'ania kusema kwamba Tanzania lazima itakufa kama serikali ya Tanganyika ikundwa ni jambo ambalo haliishi kushangaza walio wengi. Kwanza tunasahau kwamba ili kuunda Tanzania ilibidi kwanza iwepo Tanganyika. Kama kuwepo kwa Tanganyika 1964 hakukuzuia Tanzania kuzaliwa, kwanini leo kuwapo kwa Tanganyika LAZIMA kupelekea kufa kwa Tanzania? Hii ni mantiki ya wapi?
Mheshimiwa Rais, Kwa kuwa hoja ya msingi inayosimamiwa na wabunge wa CCM katika kupinga serikali tatu ni idadi ya watu ya watu waliotoa mapendekezo hayo kuwa walikuwa wachache, kwanini usifunguliwe mjadala utakaoongozwa na hasasi mbalimbali za kiraia juu ya hili ili ukweli upatikane?
Mheshimiwa Rais, Kama tunavyosema mwamba ngozi haishi kuvutia upande wake, chukulia mfano kukatokea ubishi kati ya serikali ya Zanzibar na ile ya Tanzania na ikabidi timu mbili zikutane kupata suluhisho, na upande mmoja ukiwakilishwa na wazanzibari watupu na upande mwingine ukawakilishwa na nusu wazanzibari na nusu watanganyika, huo utakuwa mjadala wa aina gani?
Mheshimiwa Rais, Kwa hakika, huu ni muundo ambao kudumu kwake kunategemea kutokuwepo na migongano ambayo inahitaji mjadala wa pande mbili, kila upande ukisisitize maslahi yake, jambo ambalo ni upuuzi kuliamini katika dunia hii ya nipe nikupe.
Mheshimiwa Rais, Aina hii ya Muungano wa serikali mbili uliyopendekezwa na "Bunge maalumu la Katiba la CCM" kwenye katiba pendekezwa ni bomu na manowari za kuuwa Muungano huku tukiimba wimbo wa "Tudumishe Muungano"
Mheshimiwa Rais, Rai yangu katika hili ni kwamba iwapo tunataka kudumisha Muungano, hatuna budi tuchague moja, ama tunaunda Muungano wa serikali moja ama tunaunda Muungano wa serikali tatu.
Mheshimiwa Rais, Ili kuendelea kuwa na Muungano ulio imara na unaokubalika na wananchi wa pande zote:
a) Hatuna budi kutambua kwamba wananchi hawawezi wakaupenda Muungano kwasababu tu viongozi wa pande mbili wanaalikana, hawa kwenda kule na wale kuja huku, wakastarehe na kufurahi basi. Ni lazima kuhakikisha kwamba wananchi wa kawaida wananufaika kutokana na manufaa yanayotokana na Muungano.
b) Hatuna budi kuachana na dhana potofu za kudhani kwamba Muungano uliopo ndio huo huo na wala hauruhusiwi kufanyiwa marekebisho
c) Viongozi na wananchi wanaowaongoza hawana budi kujenga utamaduni wa kujadili waziwazi matatizo yao badala ya kujiingiza katika manung'uniko ya chini chini, ambayo ni dalili ya unafiki na chanzo cha vurugu katika nchi. Kama uwazi na ukweli havitathaminiwa, kuvumiliwa na kuheshimiwa, matokeo yake yatakuwa ni chuki dhidi ya Muungano na dhidi ya viongozi na pia Tanganyika dhidi ya Zanzibar na Zanzibar dhidi ya Tanganyika.
d) Hatuna budi kuamini pia kwamba, jambo lingine linaloweza kuamsha hisia za chuki lile la upande mmoja kuona kwamba upande mwingine unaingilia mambo yake ya ndani huku hauna uwezo wala haki ya kuingilia mambo ya ndani ya upande ule mwingine.
e) Hatuna budi kuelewa kwamba hali ilivyo sasa wabunge wa Zanzibar wa kuchaguliwa wapo watano (5) Kwenye bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Maana yake kila mbunge anawakilisha wananchi wapatao laki mbili na sitini (260,000) wakati baadhi ya wabunge wa bara wanawakilisha wananchi zaidi ya laki tatu na thelathini (330,000). Pamoja na kuwepo kwa idadi hii ya wabunge watano kutoka Zanzibar kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado Zanzibar ina Baraza la wawakilishi ambalo lipo kwa ajili ya kutunga sheria zinazohusu Zanzibar pekee. Ilihali hawa wa Tanganyika wapo kutunga sheria za Tanganyika na Zanzibar kwa wakati mmoja kwani Bunge la Tanzania ndio hili hilo Bunge la Jamhuri. Ili kulinda muungano hatuna budi kutafuta na kuweka utaratibu ili wabunge wa Zanzibar wawe na idadi inayowiana na wingi wa wananchi wanaowawakilisha.
f) Ni lazima tutambue kwamba kuendelea na mtindo uliopo sasa, ni kuwanyima baadhi ya wananchi haki ya kuwa na uwakilishi unaofanana na mazingira yao. Kama haifai kuwa na serikali ya Tanganyika ambayo maana yake inakuwa na Bunge au Baraza la Tanganyika, itabidi tutafute njia nyingine ya kuhakikisha kwamba uwakilishi wa walio wengi haufutwi kwa nguvu ya wachache. Ninachosema ni kwamba, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania mabadiliko ya kikatiba hayawezi kupitishwa bungeni ila tu kwa kupata theluthi mbili ya wabunge wa Zanzibar. Hii ina maana iwapo wabunge wa Zanzibar hawataki jambo lipite, wanaweza kuliua kwa kukubaliana miongoni mwao, hata kama jambo lenyewe ni kipengele kinachohusu bara katika katiba.
g) Ni lazima yawepo mabaraza matatu, moja la Zanzibar, moja la Tanganyika na moja la Muungano. Katika Baraza la Muungano ambalo litakuwa kama Seneti, uwakilishi uwe sawa sawa kwa bara na visiwani, kwa kutambua usawa wa dola mbili zilizoungana. Yale mabaraza mengine mawili yafanye kazi kwa uhuru unaotambuliwa na katiba na yakubali kuelekezwa na Baraza la Muungano. La sivyo, kama serikali ya Tanganyika ni haramu kwa hiyo baraza lake pia ni haramu, tukubali kutekeleza mantiki ya uwiano wa wingi wa watu. Tanganyika ambayo ina watu wapatao milioni 43 iwe na wabunge 300 na Zanzibar yenye watu milioni 1.3 iwe na wabunge 5
Mheshimiwa Rais, nisikuchoshe sana kwa siku ya leo ila uapatapo barua yangu hii aitha moja kwa moja ama kupitia kwa vyombo vyako vya usalama, tafadhali legeza moyo wako na tafakari juu ya mustakabali wa Muungano wetu kwa vizazi vijavyo ili lisijebaki kama historia kama ilivyokuwa kwa Muungano wa Nchi za Kisoviet.
Mheshimiwa Rais, Nashukuru sana kwa kunipa muda wako kwa kupitia maandiko haya ya kijana wa kitanzania mwenye ndoto za kuvunjika kwa Muungano kama tutaendelea na mfumo huu wa serikali mbili. Mwisho kabisa nimalizie na usemi wetu wa Kimasai unaosema "Tanzania tamelono nimunyanu kanaa naishi oo kule"
Asante
Ni mimi wako katika harakati za ukombozi wa fikra,
Ole Mesaya
+255 712 814 285

- Kutambua usawa wa nchi mbili ambazo zimejiunga katika Muungano uliozaa Tanzania. Tume ilizingatia hali ya sasa ambapo nchi moja kati ya zile zilizoungana, inatambuliwa wakati nchi nyingine imefutika katika utambulisho wa serikali ya Muungano.
- Kwa kuipa Tanganyika serikali yake, unaondoa ile hofu ambayo imeelezwa mara kwa mara kwamba Zanzibar itamezwa na Tanganyika, hasa kwa kutambua ukweli kwamba masuala ya Tanganyika na yale ya Muungano yanashughulikiwa pamoja, jambo ambalo linawapa watendaji wa serikali ya muungano fursa ya kuingilia mambo ya Zanzibar bila sababu.
- Kuondoa hisia za watu wa Tanganyika kwamba wananyonywa na wazanzibari katika kuchangia gharama za uendeshaji na katika kugawana madaraka, hasa kwa kuzingatia hali ya sasa ambapo nafasi za Tanganyika ziko wazi kwa Wazanzibari wakati za Wazanzibari haziguswi na Mtanganyika.
- Kuondoa hali isiyoeleweka na isiyoingia akilini, ya kuwa na Muungano ambao unabaki ni kitendawili daima. Nchi mbili zinajiunga halafu moja inakuwa na serikali yake lakini ya pili serikali yake inaipata mumo humo ndani ya Muungano