Mbunge Esther Malleko alishauri Bunge kutunga Sheria za Kuwadhibiti wabadhirifu wa Fedha za walipa kodi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MHE. ESTHER MALLEKO ALISHAURI BUNGE KUTUNGA SHERIA ZA KUWADHIBITI WABADHIRIFU WA FEDHA ZA WALIPA KODI

"Nampongeza Rais Samia Suluhu Hassan, nayasema kwa moyo wa dhati kwa namna ambavyo ameweza kufanya kazi kubwa. Tumeona miradi mikubwa inayofanyika katika Majimbo na mikoa yetu. Nitakuwa mnafiki kama nisipomsifia Rais wangu Mama Samia Suluhu Hassan" - Mhe. Esther Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Miradi mikubwa inatekelezeka, Barabara zinajengwa, Hospitali zinajengwa, Vituo vya Afya vinajengwa, Shule za mifano zinajengwa. Ni lazima Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayoifanya" - Mhe. Esther Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Watendaji wa Serikali wasimamie vyema rasilimali za nchi kwa kutumia mifumo na kuweka nidhamu. Kinyume na kufanya hivyo tutaenda kuua nchi yetu, tena tutakwenda kuiua sisi wenyewe" - Mhe. Samia Suluhu Hassan, Wakati akipokea Ripoti ya CAG

"Taarifa ya CAG na Kamati ya LAAC waliona changamoto na mapungufu yaliyojitokeza yaliyosababisha Halmashauri kupata hasara. Ukiukwaji wa ununuzi wa Umma, Serikali ilipata hasara ya Bilioni 106" - Mhe. Esther Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Watu wanaomsaidia Mama Samia Suluhu Hassan wapo walioajiriwa, walioteuliwa na waliochaguliwa, hawa wote ni jicho la Mheshimiwa Rais kumsaidia ili aweze kutimiza malengo kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" - Mhe. Esther Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Tukianza kufanya kazi kuanzia chini kwenye Kata, wao wanakuwa na taarifa ya kushughulika mradi kwenye Vijiji, kwenye Kamati anaingia Diwani, Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa. Wanapoenda kusimamia miradi wanapswa wawe na BOQ, kama hawana BOQ wanaenda lakini hawajui wanaenda kukagua nini" - Mhe. Esther Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Wakaguzi wa ndani (Internal Auditor) hawa watu wanafanya kazi gani? Au taarifa wanazozitoa wao huwa hazitumiki? Hawa wote wameaminiwa, wameajiriwa, wanalipwa mishahara lakini bado wanaendelea kumekwamisha Mheshimiwa Rais. Lazima hawa watu wachukuliwe hatua" - Mhe. Esther Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Kuna Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, TAKUKURU na Jeshi la Polisi. Sisi wabunge tunataka kuona hawa wabunge wanaokiuka Mikataba na ununuzi wa Umma wanachukuliwa hatua. Magereza pamejaa watu walioiba Kuku na kugombana na wake zao, hao ndiyo waliojaa" - Mhe. Esther Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Kuna watu walioliibia Taifa hili wanatembea barabarani, wakihamishwa kutoka Halmashauri hii kwenda Halmashauri nyingine. Kuna nchi ambazo zinafikia hatua ya kuwakata masikio au vidole waliobainika kufanya ubadhirifu kwenye fedha za Umma" - Mhe. Esther Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Nashauri Bunge tuweze kutunga sheria ambazo zinaweza kuwadhibiti wanakiuka sheria za Manunuzi lakini tusiache kuipongeza Serikali kwa namna ilivyoanza kuwashughulikia watu ambao wanakiuka na kufanya ubadhirifu" - Mhe. Esther Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro
 

Attachments

  • y2mate.com - MBUNGE ESTHER MALLEKO AONGEA KWA HISIA KALI TUTAKUWA NI WANAFIKI HAWA WANAFANYAKA...mp4
    55 MB
  • WhatsApp Image 2023-11-04 at 12.27.29.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-04 at 12.27.29.jpeg
    59.3 KB · Views: 2
Mpaka kutakapokuwa na Majority ya Wabunge wawe ni kutoka CHADEMA hakuna kitakachobadilika.
 
Back
Top Bottom