Esther Edwin Malleko amechangia Hotuba ya Bajeti Wizara ya Elimu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

ESTHER MALLEKO AMECHANGIA HOTUBA YA BAJETI WIZARA YA ELIMU 2023-2024

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Esther Edwin Malleko leo tarehe 16 Mei, 2023 Bungeni jijini Dodoma amechangia hotuba ya Bajeti Wizara ya Elimu ya Shilingi Trilioni 1.675 iliyosomwa na Waziri mwenye dhamana Mhe. Prof. Adolf Mkenda

"Nampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya. Tumeona bajeti ya Sekta ya Elimu imeongezwa kwa wastani wa asilimia 18. Imetoka Bilioni 4.7 kwa mwaka wa fedha 2021-2022 hadi kufikia Bilioni 5.7 kwa mwaka wa fedha 2022-2023" - Mhe. Esther Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Nampongeza Waziri wa Elimu, Mhe. Prof Adolf Mkenda, Naibu Waziri Elimu, Mhe. Kipanga na watendaji wote wa Sekta ya Elimu kwa kazi nzuri wanayoifanya maana tunaona kazi nzuri inayofanyika ya kuendeleza Elimu katika nchi yetu ya Tanzania 🇹🇿 " - Mhe. Esther Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Wigo wa Elimu bila ada Umeongezeka kwa kidato cha Nne, Tano & Sita. Na Serikali inatenga takribani Shilingi Bilioni 10.3 kila mwaka kwa ajili ya fidia za kulipia wanafunzi hawa, tunaipongeza sana Serikali" - Mhe. Esther Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro

"Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu imeongezwa sana na sasa imefikia asilimia 14.7, ilitoka Shilingi Bilioni 570 na sasa imefika Shilingi Bilioni 654. Pesa ya kujikimu wanafunzi imetoka Shilingi 8,500 mpaka Shilingi 10,000 kwa siku moja. Hilo ni jambo kubwa sana la kuipongeza Serikali" - Mhe. Esther Malleko, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro
WhatsApp Image 2023-05-16 at 13.42.03(5).jpeg
 
Ni kupoteza muda tu. Huu wigo wa elimu ni upi? Shule hazina walimu, madawati, nk, halafu mnasema wigo. Nchi hii ni shida tupu. Hili ni bunge la vilaza tu, la ndiyooo ipiteee.
 
Back
Top Bottom