Mbunge Esther Malleko agawa tani moja ya Mbegu bora za Alizeti - Kilimanjaro

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
944
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Esther Edwin Malleko amegawa TANI MOJA ya Mbegu Bora za Mazao ya Alizeti kwa Wanawake wa Mkoa wa Kilimanjaro ili kuwainua Wanawake Kiuchumi katika shughuli zao za kila siku ikiwemo kilimo cha Alizeti, Kahawa, Ndizi pamoja na Shughuli za Utalii kwa lengo la kukuza tija na mnyororo wa thamani katika Mazao na Biashara kumkomboa Mwanamke.

Katika hotuba yake, Mhe. Esther Malleko amesema kuwa nchini Tanzania Uhitaji wa Mafuta ya kula ni TANI 570,000 kwa mwaka na tunazalisha TANI 250,000 kwa mwaka na Tunaagiza nje ya nchi TANI 360,000 ili kutimiza mahitaji ya ndani. Mhe. Rais wetu Dr. Samia Suluhu Hassan anapambana sana kutuinua Wanawake na Taiafa kwa ujumla, UWT nayo inapambana sana kumpigania Mwanamke ikiongozwa na *Mhe. Mkt wetu Marry Chatanda na uongozi wote mpaka kata na mimi Malleko ni Askari wao lazima nikomae kuwasaidia Mama zangu kazii hii ya utu na kibinadamu kutekeleza ILANI kimkakati kwa ari na mali ili tumuokoe Mama katika kila familia kwa mapenzi ya dhati.

Mhe. Esther Malleko amesema kuwa ukiangalia mahitaji ya ndani bado uhitaji wa Mafuta ya kula nchini ni mkubwa sana kwa mahitaji ya ndani ukilinganisha na kiwango cha mafuta ya kula tunayoagiza kutoka nje ya nchi, kiwango cha mafuta ya kula tunachozalisha ndani ni kidogo kuliko kiwango tunachoagiza.

Mhe. Esther Malleko amesisitiza Wanawake na wadau wengine wa Kilimo cha mafuta ya kula ikiwemo wawekezaji kuwekeza kwa wingi kwenye kilimo cha biashara, kilimo chenye tija kwa kinachotumia Mbegu bora, mbolea, na kuzingatia ushauri wa Wataalam wa Kilimo ili kuwa na kilimo cha uhakika na yeye ataendelea kuwa nao Bega kwa Bega.

Vilevile, Mhe. Esther Malleko amesema kutokana na uhitaji mkubwa wa mafuta ya kula nchini, ameamua kuwawezesha wanawake wenye nia ya kuwekeza kwenye kilimo ili kuinua uchumi wa wanawake na kuisaidia Serikali kupunguza mzigo wa kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi na kuhakikisha mafuta yanayozalishwa ndani yanakuwa mengi kuliko yanayoingizwa nchini.

Aidha, Mhe. Malleko amesema kuwa kwa sasa Serikali imeelekeza nguvu zaidi kwenye kilimo cha kuzalisha Mbegu bora za Alizeti na kufanya utafiti wa Mbegu bora ili kukidhi mahitaji ya malighafi katika viwanda vya ndani na kuongeza uzalishaji wa Mbegu bora za Alizeti na Michikichi.

Kwa upande wao, Wanawake wa Mkoa wa Kilimanjaro baada ya kupokea Mbegu bora za Alizeti, Wamemshukuru sana Mbunge wao, Esther Malleko kwa kuwajali katika msimu huu wa kilimo kwani wataweza kujipatia kipato cha kusaidia familia zao.

WhatsApp Image 2024-03-03 at 20.05.03.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-03 at 20.05.04.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-03 at 20.05.30.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-03 at 20.06.28.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-03 at 20.08.57.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-03 at 20.09.32.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-03 at 20.09.32(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-03-03 at 20.09.33.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-03 at 20.14.19.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-03 at 20.14.19.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-03 at 20.14.20.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-03 at 20.14.21.jpeg
WhatsApp Image 2024-03-03 at 20.14.21(1).jpeg
WhatsApp Image 2024-03-03 at 20.14.22.jpeg
 
Back
Top Bottom