Mbunge akifa kabla ya kuapa sheria inasemaje

bulunga

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
303
49
Ningependa kujua sheria inaseamaje kwa mbunge mteule akifa kabla ya kuapa inanakuaje, je 1) uchaguzi mpya utafanyika??? 2) Mshindi wa pili aliye fuatia kwa wingi wa kura ana weza kuchukua nafasi iliyo achwa wazi???:A S 465:
 
Utakuta katiba inakuwa bubu juu ya hilo...!
Lakini tayari rais ashamtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge , kuonyesha kwamba ndiye mfiwa mkuu kimhimili, na automatically hii inaleta majibu kwamba taratibu za kawaida za kutangaza nafasi yake upya zitafuata!
Thats my view!
 
Ningependa kujua sheria inaseamaje kwa mbunge mteule akifa kabla ya kuapa inanakuaje, je 1) uchaguzi mpya utafanyika??? 2) Mshindi wa pili aliye fuatia kwa wingi wa kura ana weza kuchukua nafasi iliyo achwa wazi???:A S 465:

Mbona j. Makamba anasema marehemu alikuwa nae bungeni his seat is a row behind january"s seat??

Aliingiaje bungeni bila kuapa?
 
Mbona j. Makamba anasema marehemu alikuwa nae bungeni his seat is a row behind january"s seat??

Aliingiaje bungeni bila kuapa?

Sikutaja jina la mtu wala jimbo, nilitaka kujua sheria inasemaje juu ya hilo
 
Ningependa kujua sheria inaseamaje kwa mbunge mteule akifa kabla ya kuapa inanakuaje, je 1) uchaguzi mpya utafanyika??? 2) Mshindi wa pili aliye fuatia kwa wingi wa kura ana weza kuchukua nafasi iliyo achwa wazi???:A S 465:

Nadhani hii post inafaa zaidi kwenye jukwaa la sheria,huko itapata michango ya maana kuliko hapa.Hapa siasa ndio zitatawala.
 
Katiba iko bubu juu ya swala hili. Sheria za uchaguzi zinasemaje ....................................?
 
Ningependa kujua sheria inaseamaje kwa mbunge mteule akifa kabla ya kuapa inanakuaje, je 1) uchaguzi mpya utafanyika??? 2) Mshindi wa pili aliye fuatia kwa wingi wa kura ana weza kuchukua nafasi iliyo achwa wazi???:A S 465:
kama unamzungumzia Sumari, alishaapishwa, kwa mujibu wa Katibu wa Bunge.
Lakini kisheria, mtu akishatangazwa na Tume ya Uchaguzi kuwa ni msindi katika kinyang'anyiro cha ubuinge, usiwani, urais, basi mtu huyo anahesabiwa kuwa ni diwani, mbunge, rais. Kile kiapo ni kwa ajili ya kuhalailisha mtu afanye kazi za kidiwani, kibunge na kirais
 
Huwezi kuitwa mbunge kama hujaapishwa,hivyo akifa kabla ya kuapishwa kiti cha jimbo hilo huwa wazi.Madaktari wakidhibitisha kifo cha mteule utafanyika uchaguzi mdogo.
Mtu wa pili kwa wingi wa kura hawezi kuwa mbunge kwa vile msimamizi wa uchaguzi akishamtangaza mshindi na kumpa cheti cha ushindi ambacho mteule hupeleka bungeni ili akapokelewe na taratibu zingine zifanyike. Kwa vile sheria ya uchaguzi hairuhusu msimamizi wa uchaguzi kutoa hati mbili za ushindi kwa jimbo moja.
 
Ndio maana tunahitaji kufanya mabadiliko makubwa sana katika katiba yetu, ili izungumzie kila kitu bila kuacha vitu vinaelewa, halafu vikitokea watu tunakuja na maana zetu kutoka mifukoni na kuzifanyia kazi.

Katiba ipo kimya juu ya mbunge aliyekufa kabla hajaapishwa.

Halafu hata hiii ya vyama kuwafukuza wabunge wao na hivyo kusema wamepoteza ubunge wao, katiba inasema hivi inapoongelea mbunge atakoma kuwa mbunge iwapo:-

Ibara ya 71 (1); (e) Iwapo Mbunge ATAACHA kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge.

Sasa swali langu mimi juha wa sheria na katiba ni hili, Hamad na Kafulila WAMEACHA UANACHAMA au wamefukuzwa? Je? Kufukuzwa uanachama na kuacha uanachama kuna maana moja?

As long as nasoma hii katiba, sioni sehemu ikisema mbunge akifukuzwa kwenye chama chake inakuwaje zaidi ya kusema akiacha.

Hebu tusaidieni wanacheria, kufukuzwa uanachama na kuacha uanachama kuna maana moja?
 
Ndugu,

Kama walivyosema wengine, Katiba yetu haisemi lolote kuhusiana na mada. Mbunge kabla ya kuapa hasitahili lolote (maana si mbunge kamili - ni mbunge mteule) mpaka aape ndipo atambulike kama mbunge. Sasa ikitokea akafa kabla ya kuapa si tu hastahili kuchukuliwa kama mbunge bali pia ni kupotesa raslimali za nchi akichukuliwa hivyo.

Vyama vya siasa kuwafukuza wabunge wao; Ibara ya 71 (1); (e) Uliyo nukuu ni tofauti na wazo lako maana ni jambo tofauti kidogo. Ila ukiangalia Ibara ya 67(sifa za mtu kuwa mbunge) na hasa 67(1) (b) inasema ni lazima mtu awe mwanachama na awe amependekezwa na chama cha siasa. Mbunge akiacha uanachama au akafukuzwa (sio mwanachama) huyo hapaswi kuwa mbunge.

Majibu ya swali lako yapo hapo juu. Haijalishi umeacha au umefukuzwa ilimradi tu si mwanachama wa chama cha siasa hupaswi kuwa mbunge kwa lugha nyingine awe diwani au rais bila kuwa na chama hakuna cheo hicho. Katika sura hii kufukuzwa uanachama na kuacha uanachama kuna maana moja. Pamoja na hayo soma 71(1)(f), unajua ndugu wakati mwingine katiba inasomwa kama biblia kwa maana ya kwamba usiegemee mstali mmoja tu!

Kwangu mimi Kafulila na hamad sio wabunge maana sio wanachama wa vyama vyao, ila TU kama vyama vyao wakati wa kuwasimamisha uanachama vilikiuka kanuni/taratibu na sheria. Hivyo tunaiachia mahakama iamue tu kama kanuni zilikiukwa au la vinginevyo mahakama haiwezi kuwarudishia uanachama hivyo kuwawezesha kuwa wabunge.
 
Back
Top Bottom