Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 6,977
- 12,440
Achana na huyo katibu mwenezi uchwara wa Chadema. Sugu na Profesa J ni watoto kindaki ndaki wa mama. Hivyo usishangae mwaka 2025 akawapiga chenga ya mwili Chadema katika dakika za mwisho, kwa kujitoa Chadema na kuhamia CCM kwa lengo la kumuacha Dr Tulia aendelee kugombea bila upinzani.Sugu hawezi kushindana na msomi na mwanasheria nguli. Mbeya mjini siyo jimbo la wahuni .sugu apeleke uhuni wake huko na ubabaishaji wake huko.amekaa miaka kumi bungeni lakini ukimuuliza ni kipi anajivunia na alama aliyoiacha pale Mbeya huwezi ukaonyweshwa hata kwa tochi.
Sugu hana chake tena Mbeya mjini.hakuna mwenye akili Timamu anayeweza kumpigia kura. labda vichaa na wendawazimu ndio wanaweza kumpigia kura lakini kwa bahati mbaya ni kuwa hakuna anayeweza ruhusu vichaa wapige kura. kwa hiyo sugu akae kwa kutulia tu maana hatapata tena ubunge mbele ya Dr Tulia Rais wa IPU anayeangaliwa na kutizamwa na Dunia nzima
Alaf baadae mama akampa sugu ubunge wa kuteuliwa, na hatimae kumteuwa tena kuwa waziri wa michezo na utamaduni akisaidiana na msanii mwenzake Mwana FA.
Sugu ni miongoni mwa wapinzani wachache ambao muda wowote wanaweza kwenda ikulu kuonana na raisi na wakaruhusiwa bila shida.