M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,020
Mkuu, tuache hayo niliyowekea wino mwekundu ambayo naona yana tone ya maslahi binafsi zaidi.....Chadema yenyewe itanufaika na nini kama chama???Kiongozi wa upinzani bungeni ni Waziri Mkuu Kivuli ingawa analipwa mshahara na marupurupu kama waziri wa kawaida. Anayo ofisi ya hadhi bungeni inayohudumiwa na serikali, Shangingi kama la Mawaziri na anakuwa na uwezo wa kuunda serikali kivuli. Hii ni nafasi ya juu kabisa katika duru za kibunge inashika nafasi ya tatu au ya nne kwa heshima ukianzia ya spika, waziri mkuu,kiongozi wa upinzani/naibu spika.
kwa hiyo anachokipigania Zitto ni ukubwa na marupurupu .
Kinachopiganiwa hapa na heshima, mishahara na marupurupu yanayo izunguka ofisi hii. Lakini sijui kwa nini hili lijadiliwe sasa maana nafasi hiyo inatakiwa kuchukuliwa na most senior official and a member of parliament aliyeko kwenye hicho chama.
Vyovyote itakavyo kuwa, hiyo ni nafasi ya mwenyekiti wa Chadema. Ndiye aliyekifikisha chama hiki mahali kilipo! He is the most senior Party official in the Parliament, hivyo hakuna ubishi wowote. Yeye ndiye mgombea urais wa chama hiki aliyeko bungeni sasa, hivyo yeye ni mtu wa kupimana ubavu na Kikwete na Waziri Mkuu atakayeteuliwa kwa vile mgombea wao Dr. Slaa atakuwa nje ya bunge for the time being.
Hoja zilizoletwa na Zitto kwenye BBC jana eti Balozi Ndhobo wa NCCR Mageuzi alikuwa Kiongozi wa upinzani bungeni wakati Mwenyekiti wake Lyatonga Mrema akiwa bungeni hazina maana wala kishikio chochote. Amesahau kuwa Mrema aliingia bungeni baada ya uchaguzi mdogo wa Temeke (muda ulikuwa umepita). Pia wakati ule hakukuwepo na chama rasmi cha upinzani bungeni. Ndhobo alikuwa Kiongozi wa wabunge wa NCCR Mageuzi bungeni, wala hakuwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni.
Halafu umem-single out Zitto kuwa anakimbilia hayo marupurupu....which only goes to prove a point that this role should be assigned to a non-Chadema MP kwa sababu kama eventually Zitto akashindwa halafu akadai amefanyiwa mizengwe (hata kama si kweli), Chadema (and by extension the whole opposition camp) inaweza ikakosa cohesion ndani ya bunge, cohesion ambayo sisi sote tunaomba iwepo kulifanya bunge liweze kulinda maslahi ya taifa more effectively.
Haya mimi nayaongea kwa nia njema kabisa kukisaidia Chadema.