Mbowe: Masha hakuwahi kuwa na msaada wowote CHADEMA

Ujio wa Lowasa, Nyalandu, Sumaye, Masha na wengine kutoka ccm bado nawaangalia kwa jicho la utafiti.... sidhani kama watatuvusha hawa... kesho utasikia Sumaye naye arudi ccm..
 
uchaguzi wa TLS?? masha did well

insipiration to new members..

mbowe akae kimya, kuna siku atahama.na yy wenzake watasema alikuwa mzigo
HAPANA MBOWE ALICHOSEMA NI KWELI MASHA ALIKUWA HANA MSAADA WOWOTE KWA CHADEMA YA SASA SIO CHADEMA YANGU YA ZAMANI YA DR SLAA MANA YA SASA LAZIMA UITUKANE SERIKALI,MTUKANE JPM,MASHA HAKUA ANATUKANA NDO MANA ANAMBIWA HAKUA NA MSAADA WOWOTE
 
Cha ajabu nini? This is politics. Ndio maana hata Nyalandu alipohama, ccm nao walianza kumnanga kwamba ni fisadi! This is politics kaka! Siasa sio dini, sio sawa na kuhubiri injili! Nadhani umenielewa, pambaf!

Ndo maana nikasema it's par for the course.

Au hujui maana yake hiyo?
 
Mkuu mimi najiuliza mtu ambaye hakuwa na msaada ndini ya chama,ilikuwaje,mara mbili jina lake likapelekwa kwenye bunge la jamuhuri,ili akapigiwe kura ,awe mbunge wa Afrika Mashariki?
Hata pale nafasi hizo ZILIPOJAZWA NA AKINA MAMA Mh Mbowe alilalamika bungeni,kuhusu kuchaguwa watu kishabiki bila kuangalia uwezo wa tatu waliopelekwa mbele ya bunge kupigiwa kura.
Hivi tafsiri sahihi ya mchango wa mtu ni nini,mali? Hekima?Ushauri?maono?
Kwa nijuavyo kila mtu amepata karama yake,kwa ujumla kwa karama zote,ndipo mambo yanaenda.Wamasiasa tujifunze kukaa kimya,pale unapoona huna haja,ya kukubali wala kukataa. SI MNASEMAGA NO COMMENT kisha huyo unasepa zako?
Hilo swali Ufipa hawawezi kukujibu!
 
Maneno haya hayana diplomasia,staha wala weledi.

Mbowe alitakiwa kumshukuru Masha kwa muda wote waliofanya kazi pamoja na kwa heshima aliyokipa CHADEMA kwa kuona ni chama kinachofaa kujiunga nacho. Pia, alitakiwa kusema kwamba,kama mwenyekiti wa chama ambacho kinasimamia demokrasia kiasi cha kuweka neno hilo katika jina lake, anatambua uhuru wa kikatiba alio nao Masha wa kuamua kujiunga na kujitoa chama chochote anachoona kinafaa. Mwisho, alitakiwa kusisitiza kwamba, ingawa Masha anajiondoa uanachama CHADEMA, hilo halina maana kwamba huo ndio mwisho wa kufanya kazi pamoja katika kutafuta maendeleo ya nchi, kwani CHADEMA kinafanya kazi na walio wanachama na wasio wanachama.

Hiyo ingekuwa kauli ya kidiplomasia na weledi.

Masha kwa kuwa waziri aliyehama CCM tu na kuingia CHADEMA alishaonesha CHADEMA kama chama kinachokubalika kwa watu waliofikia kada kubwa za CCM na kukaa kwenye vikao vya baraza la mawaziri. Hilo tu si dogo hata kama angeishia hapo.

CHADEMA ilimpa Masha nafasi ya kuwania ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki. Ina maana CHADEMA ilimpa mtu asiye na msaada wowote nafasi hii muhimu? Kama ni kweli, je CHADEMA ni chama makini kinachoweza kuongoza nchi? Kama si kweli, Masha si mtu ambaye hakuwa na msaada wowote, je, Mbowe ni muongo?

Kwa kauli ya masimamgo aliyoitoa Mbowe, ameonesha kwamba mtu yeyote anayefikiria kuhama CCM na kwenda CHADEMA sasa, ajifikirie mara mbili, maana akiona CHADEMA hapafai akaamua kuhama, CHADEMA hakina staha za kuagana kwa maneno mazuri.
 
Team Lowasa Chadema bora waondoke kuliko kumjenga MTU ambaye hana mchango kama Mbowe. Chadema kufika ilipofika kazi kubwa ilifanywa na Dr slaa Chadema kulikuwa chama kidogo mno kilichokuwa kinazidiwa na NCCR kwa idadi ya wabunge na madiwani.Slaa aka ki turn around kikawa so popular kikawa na wabunge wengi na madiwani wengi kuliko NCCR .Dr Slaa alipoondoka team lowasa akiwemo Masha wakaichukua Chadema wakaipaisha mno kuifanya iwe na Wabunge na madiwani wengi mno.Cha ajabu Mbowe anajitia kuchukua credit team Lowasa ikiondoka Chadema kwishilia mbali.Mbowe tapeli anabeba credit zisizo zake
 
ndio nimejua leo!! kumbe tuko wengi afadhali bana

hata MTAZAMO sio muumini wa vyama
Mimi sijawahi kuwa Chadema na haitotokea iwe hivyo.

Ila nachukizwa tu na madhira tuliyosababishiwa kama Taifa tena kwa makusudi na hawa ccm.

Watu wenye akili hatuhitajiki kwenye vyama, Idiots is those people who call themselves politician.
 
Tutafika Tu,mtu akihama CCM kwenda upinzani alikuwa fisadi,akihama upinzani anakuwa ni mtu ambaye hakuwa na msaada,aliyesema siasa ni mchezo mchafu hakukosea.
 
Tutafika Tu,mtu akihama CCM kwenda upinzani alikuwa fisadi,akihama upinzani anakuwa ni mtu ambaye hakuwa na msaada,aliyesema siasa ni mchezo mchafu hakukosea.
Ni shida mkuu. Wenyewe wanasema: CCM ni mtambo wa kuzalisha mafisadi na CHADEMA ni friza la kuhifadhia mafisadi. Yaani mafisadi yanapikiwa huku halafu yanakwenda kuhifadhiwa huko... Mianasiasa !!!
 
Mimi sijawahi kuwa Chadema na haitotokea iwe hivyo.

Ila nachukizwa tu na madhira tuliyosababishiwa kama Taifa tena kwa makusudi na hawa ccm.

Watu wenye akili hatuhitajiki kwenye vyama, Idiots is those people who call themselves politician.

asanteee

historia iko hivi ya kumtawala mtanzania iko hivi!

1.biashara ya utumwa
2.colonisation
3.CCM
 
Back
Top Bottom