Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama

Kuna jambo nakubaliana nawe!!

Falsafa huzaa itikadi ambayo ndiyo hubeba mrengo wa chama unaotumika kutengeneza Sera ambazo mwisho wa siku ndizo huzaa Ilani inayonadiwa kwa kaulimbiu.

Wanasiasa Wa Tanzania wengi wao kama Siasa isingekuwa "ajira" Leo hii wasingekuwepo kwenye Siasa.

Wanasiasa wengi Tanzania ni wasaka tonge na watumia tumbo.

1. Umenituhumu kutomtaja Mbowe. Hili nalo nilikuwa nimekuandikia wewe mapema:

IMG_20231218_142659.jpg


Nalo tuseme hukuliona?

2. Niseme wazi, si kila mtu anafanya petty politics za kimaslahi labda kama nyie au wengine wowote.

3. Ifahamike kuwa ninakataa kumhukumu yeyote "kifo" kwa tuhuma za kibinadamu hapa duniani.

4. Kwangu mimi sina rafiki wala adui wa kudumu.

5. Kwangu miye ukimya wenye harufu ya opportunism ni usaliti mbaya zaidi:

F3k78Z8a0AAldWM.jpeg


6. Wewe huoni hivyo ndugu?
 
Hakuna mahali nimekushambulia .

Kuandika unavyotaka wewe niandikie ni kama vile unafanya kile ulichokataa denoo JG asikufanyie.

1. Wapi nimesema umenishambulia?

2. Nimesema umenituhumu. Mawili hayo ni tofauti.

3. Tuseme au tukubaliane tuhuma hii si kweli?

"Lakini CHADEMA kwa Sasa inaongozwa na Mbowe, mbali ya kulitaja Jina lake kwenye kichwa cha bandiko lako, hakuna mahali umetaja umahiri wake wa kiuongozi kuliko unavyomtaja Lissu."

4. Tafadhali thibitisha Ili tuufunge ukurasa huo pamoja ikikupendeza.
 
Hakuna mahali nimekushambulia .

Wapi nimesema umenishambulia?

Kuandika unavyotaka wewe niandikie ni kama vile unafanya kile ulichokataa denoo JG asikufanyie.

1.(a) Tangu lini hii ya kukutaka wewe kujikita kwenye hoja:

IMG_20231219_091311.jpg


(b) Ikafanana na hii ya denoo JG kunitaka mimi kuandika atakavyo yeye?

IMG_20231217_140458.jpg


2. Huoni kuwa kauli yako ni jitihada iliyoshindwa ya kujificha kama za huyu ndugu?

IMG_20231219_090845.jpg


3. Ninakazia:

Hoja haikimbiwi wala kupingwa kwa rungu!
 
III. MBOWE LISSU NYINYI WENYEWE KWANZA SHIKENI NIDHAMU, MAHAKAMA IMESEMA MNAONEA WATU UHURU WA KUJITETEA..Ĺ
Mada kama hizi huelekezwa kwenye vile vyama vyenye ule wito mtakatifu wa ukombozi.

"Ikiwapendeza waheshimiwa, waungwana kabisa:"

Falsafa ya chama ni jambo la msingi zaidi katika chama chochote. Falsafa hutoa utambulisho halisi wa chama. Ikaweza kutofautisha baina ya vyama. Ikazaa imani za chama.

"Ya kuwa chama kinasimamia nini? Kwanini hii ni CHADEMA siyo CCM. Kwanini hii ni CUF siyo ACT? Tofauti haiwezi kuwa majina. Inapaswa kuwa wazi ili wafuasi wakajua kamili kama walipo ni sahihi."

Watazipigania vipi kwa moyo wao wote, sera au agenda za chama kama falsafa ya chama haijulikani?

Falsafa za vyama zitaweka wazi misimamo ya vyama kuhusu mambo yote yakiwamo yaliyo tata na ikaondoa mikanganyiko isiyokuwa na tija.

"Kwa mfano, nini misimamo ya chama kuhusu Katiba Mpya, vita vya Ukraine, HAMAS, Gaza, Palestina, nk?"

Misimamo rasmi ya chama ni "binding." Mfuasi hawezi kuwa na msimamo tofauti na wa chama huku akijinasibu hadharani kuongea kwa niaba ya chama.

Tunapiga hatua, mdogo mdogo tutafika tu:

I. Mbowe, Lissu chukueni hatua kurejesha nidhamu kwenye chama

II. Mbowe, Lissu nidhamu inaporejea wafundeni wafuasi heshima
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom