Haya ndiyo mazao ya falsafa ya 4R

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
19,675
59,778
Kitendo cha Jeshi la Polisi kuruhusu maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo, Jumatano Januari 24.2024 ni ishara ya utekelezaji wa falsafa ya 'R4' iliyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo inatajwa kuimarisha Demokrasia na umoja Nchini

CHADEMA imepanga kufanya maandamano hayo jijini Dar es Salaam ikidai marekebisho ya Sheria za Uchaguzi na Katiba Mpya

Kabla ya Rais Samia kuingia madarakani mwezi Machi 2021, maandamano ya upinzani na mikutano ya hadhara ilipigwa marufuku na Polisi Nchini lakini katika hali ambayo haikutarajiwa Polisi wametoa ruhusa kwa CHADEMA kufanya maandamano yao ya leo kwa amani na kuwaahidi ushirikiano

Hata hivyo, Polisi wamewapa Viongozi wa CHADEMA masharti manne ili kuhakikisha kuwa maandamano hayo yanafanyika salama

Masharti hayo ni pamoja na kuhakikisha kuwa waandamanaji hawaleti uvunjifu wa amani au kusababisha mali za watu kuibiwa na kuharibiwa, Viongozi na mashabiki wa Chama hicho cha upinzani pia wameonywa na Polisi kuwa wasitumie lugha za uchochezi na kejeli ambazo zinaweza kuleta uvunjifu wa amani au makosa ya jinai

Pia waandamanaji wameambiwa wafuate njia zilizokubaliwa na muda uliopangwa ili kuepusha kusababisha foleni na tafrani Barabarani

Kufuatia hatua hiyo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) amempongeza Rais Samia kwa uongozi wake wa maridhiano wa kuruhusu maandamano hayo

"Big up kwa ⁦Polisi, tunawaahidi amani mwanzo mwisho, Big up sana pia kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa hili" -Sugu

Sugu ameongeza kuwa Rais Samia ameonesha kuwa hana hulka ya kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kuminya demokrasia Nchini

Naye, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amewapongeza Polisi chini ya Rais Samia kwa ushirikiano wao kwa chama chake

"Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa busara hii, karibuni Watanzania wote, tuandamane kwa amani" -Mbowe

Falsafa ya R4 (Reconciliation, Resilience, Reforms na Rebuilding of the Nation) ya Rais Samia imebadili upepo wa siasa nchini

Hii siyo mara ya kwanza kwa Serikali ya Rais Samia kuruhusu maandamano ya upinzani kwani mwezi Mei mwaka jana, Polisi jijini Dar es Salaam waliruhusu maandamano ya Umoja wa Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) kwenda Ofisi za Bunge na kuwapatia ulinzi

Rais Samia ameimarisha Demokrasia kwa kuruhusu maandamano, kuruhusu vyama vya upinzani vifanye mikutano ya hadhara nchi nzima na ameimarisha usalama na kufanya wanasiasa wa upinzani waliokimbia nchi kurejea nchini

Rais Samia pia ameongeza uhuru wa wananchi wa kuongea, uhuru wa vyombo vya habari na asasi za kiraia

Aidha, Wananchi kadhaa wakitoa maoni yao kupitia kwenye mitandao ya kijamii wamemtaja Rais Samia kama 'Mama wa Demokrasia' wa Tanzania kwa uongozi wake wa maridhiano

Chadema wananufaika sana na falsafa hii ya 4R. Maana kwa sasa wanaandamana na kupewa ulizi. Hii inaitwa ukomavu wa kisiasa wa Rais wa Tanzania.
Haya ndiyo matokeo ya 4R.
4R ni nini?
1706089508961.png
 
Barabara nzuri zinajengwa na serikali. Chadema wanapita tu kwa uhuru. Haya ndiyo matokeo chanya ya 4R

1706089621576.png
 
Je 4R inatekelezwa na akina nani?
CHADEMA ni sehemu ya utekelezaji wake.

1706089784837.png
 
Hongela sana vyama vya siasa kwa kutekeleza falsafa ya 4R kwa vitendo

1706089913082.png
 
Kitendo cha Jeshi la Polisi kuruhusu maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo, Jumatano Januari 24.2024 ni ishara ya utekelezaji wa falsafa ya 'R4' iliyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo inatajwa kuimarisha Demokrasia na umoja Nchini

CHADEMA imepanga kufanya maandamano hayo jijini Dar es Salaam ikidai marekebisho ya Sheria za Uchaguzi na Katiba Mpya

Kabla ya Rais Samia kuingia madarakani mwezi Machi 2021, maandamano ya upinzani na mikutano ya hadhara ilipigwa marufuku na Polisi Nchini lakini katika hali ambayo haikutarajiwa Polisi wametoa ruhusa kwa CHADEMA kufanya maandamano yao ya leo kwa amani na kuwaahidi ushirikiano

Hata hivyo, Polisi wamewapa Viongozi wa CHADEMA masharti manne ili kuhakikisha kuwa maandamano hayo yanafanyika salama

Masharti hayo ni pamoja na kuhakikisha kuwa waandamanaji hawaleti uvunjifu wa amani au kusababisha mali za watu kuibiwa na kuharibiwa, Viongozi na mashabiki wa Chama hicho cha upinzani pia wameonywa na Polisi kuwa wasitumie lugha za uchochezi na kejeli ambazo zinaweza kuleta uvunjifu wa amani au makosa ya jinai

Pia waandamanaji wameambiwa wafuate njia zilizokubaliwa na muda uliopangwa ili kuepusha kusababisha foleni na tafrani Barabarani

Kufuatia hatua hiyo Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) amempongeza Rais Samia kwa uongozi wake wa maridhiano wa kuruhusu maandamano hayo

"Big up kwa ⁦Polisi, tunawaahidi amani mwanzo mwisho, Big up sana pia kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa hili" -Sugu

Sugu ameongeza kuwa Rais Samia ameonesha kuwa hana hulka ya kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kuminya demokrasia Nchini

Naye, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amewapongeza Polisi chini ya Rais Samia kwa ushirikiano wao kwa chama chake

"Nalipongeza Jeshi la Polisi kwa busara hii, karibuni Watanzania wote, tuandamane kwa amani" -Mbowe

Falsafa ya R4 (Reconciliation, Resilience, Reforms na Rebuilding of the Nation) ya Rais Samia imebadili upepo wa siasa nchini

Hii siyo mara ya kwanza kwa Serikali ya Rais Samia kuruhusu maandamano ya upinzani kwani mwezi Mei mwaka jana, Polisi jijini Dar es Salaam waliruhusu maandamano ya Umoja wa Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) kwenda Ofisi za Bunge na kuwapatia ulinzi

Rais Samia ameimarisha Demokrasia kwa kuruhusu maandamano, kuruhusu vyama vya upinzani vifanye mikutano ya hadhara nchi nzima na ameimarisha usalama na kufanya wanasiasa wa upinzani waliokimbia nchi kurejea nchini

Rais Samia pia ameongeza uhuru wa wananchi wa kuongea, uhuru wa vyombo vya habari na asasi za kiraia

Aidha, Wananchi kadhaa wakitoa maoni yao kupitia kwenye mitandao ya kijamii wamemtaja Rais Samia kama 'Mama wa Demokrasia' wa Tanzania kwa uongozi wake wa maridhiano
 
Falsafa ya 4R (Reconciliation, Resilience, Reform, na Rebuild) inaweza kuchangia ujenzi wa haki nchini Tanzania kwa njia kadhaa. Hapa ni jinsi kila nguzo inavyoweza kusaidia kujenga haki:

1. Reconciliation (Maridhiano):
- Kupitia maridhiano, jamii inaweza kusonga mbele kutoka kwenye migogoro ya zamani na kujenga mazingira ya amani. Kukuza maridhiano kunaweza kuleta upatanishi kati ya makundi yanayokumbana na migogoro ya kisiasa, kijamii, au kitamaduni.

2. Resilience (Ustahimilivu):
- Ustahimilivu wa kijamii unaweza kujenga mazingira ambayo jamii inaweza kukabiliana na changamoto bila kuvunja misingi ya haki. Kusaidia jamii kuwa na uwezo wa kurejea na kujikwamua kutokana na mizozo na matatizo inaweza kusaidia kudumisha haki.

3. Reform (Marekebisho):
- Marekebisho ya miundo ya kisheria na kisiasa yanaweza kuleta haki na usawa. Kupitia marekebisho, serikali inaweza kuboresha utawala wa sheria, kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wananchi wote, na kusimamia haki za binadamu.

4. Rebuild (Ujenzi Upya):
- Ujenzi upya wa jamii unaweza kutoa fursa ya kuhakikisha kuwa haki inazingatiwa katika kila hatua. Kupitia ujenzi upya, jamii inaweza kuimarisha mifumo ya elimu, huduma za afya, na miundombinu, na hivyo kuhakikisha upatikanaji sawa wa rasilimali na fursa.

Kwa kuzingatia hayo, hapa ni jinsi falsafa ya 4R inaweza kuchochea mchakato wa kujenga haki nchini Tanzania:

1. Kusaidia Kupatikana kwa Haki:
- Mchakato wa maridhiano unaweza kusaidia katika kutatua migogoro na kutafuta suluhisho linalozingatia haki na usawa kwa pande zote.

2. Kuimarisha Mifumo ya Haki:
- Marekebisho ya miundo ya kisheria yanaweza kusaidia kuimarisha mifumo ya haki na kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa kila mwananchi.

3. Kutetea Haki za Wanyonge:
- Marekebisho na ujenzi upya wa jamii unaweza kutoa fursa za kuboresha haki za wanyonge, kama vile wanawake na vijana, na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika maendeleo.

4. Kupinga Ubaguzi na Unyanyasaji:
- Marekebisho na ujenzi upya wa jamii vinaweza kuwa na lengo la kupinga ubaguzi na unyanyasaji, kuhakikisha kuwa haki inapatikana kwa kila mwananchi bila kujali hali yao.

5. Kukuza Usawa wa Kijinsia:
- Kupitia marekebisho ya kijamii na kiuchumi, falsafa ya 4R inaweza kusaidia kujenga mazingira yanayoshughulikia tofauti za kijinsia na kusaidia kufikia usawa wa kijinsia.

Kwa ujumla, falsafa ya 4R inaweza kuchangia katika kujenga mazingira ambayo haki inatambuliwa, inalindwa, na inatekelezwa kwa wananchi wote nchini Tanzania. Hata hivyo, ni muhimu kuhakikisha kuwa utekelezaji wake unazingatia mahitaji na matakwa ya jamii yote na unaleta mabadiliko chanya kwa wengi.
 
Bendera fuata upepo. Majuzi habari ilikuwa wajeda kusafisha town mkasema oyeeeee!! Leo kibao kimegeuga sasa ruhsa. Nanyi tena mwashangilia oyeeee
 
Back
Top Bottom