Elections 2010 Mbowe awatawanya wafuasi wa CCM kwa bastola yake

sijui nini

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
2,553
1,285
MWENYEKITI wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe amewasihi wafuasi wa CCM kuacha vurugu kwenye mikutano ya Chadema ili kufanikisha uchaguzi wa amani na undugu.

Aidha amewashauri viongozi wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro kuwakemea wafuasi na wanachama wa chama hicho kutokana na acha kuvamia mikutano ya vyama vingine ili kuepusha vurugu zisizo za maana yoyote.Aalitoa wito huo alipozungumzia tukio la vurugu alilosema lilisababishwa na wana CCM ambapo yeye alilazim ika kufyatua risasi kadhaa hewani kwa kutumia bastola yake ili kuokoa maisha yake na ya wafuasi wake.

Mbowe alisema alilazimika kutumia mbinu hiyo ya kijeshi baada ya kuona maisha yake na ya wafuasi wake yapo hatarini baada ya kuzingirwa na vijana ambao ni wafuasi wa CCM ambao walikuwa wakiwashambulia kwa mawe.

Hata hivyo Mbowe ambaye pia ni mgombea Ubunge Jimbo la Hai, alisema chama hicho pamoja na wafuasi wake katika majimbo ya Moshi mjini na Hai wameanza kupoteza imani na utendaji wa Jeshi la Polisi mkoani humo.

“Sisi ndio tumefanyiwa fujo na wafuasi wa CCM, lakini ukisoma taarifa iliyotolewa na RPC inaibeba CCM na imeficha mambo mengi kwa maslahi ya CCM ,wala hakuna mahali inaposema Mbowe alifyatua risasi hewani,”alidai Mbowe.

Vurugu hizo zilizosababisha wafuasi kadhaa wa Chadema kujeruhiwa vibaya kwa mawe na magari kuvunjwa vioo na pikipiki kuharibiwa zilitokea juzi katika Kata ya Masama anakotoka mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Fuya Kimbita.

Mbowe alisema polisi walikuwa na taarifa ya Chadema kuwa na mkutano wa kampeni katika kata anayotoka mgombea Ubunge wa CCM ,hivyo haikuhitaji elimu ya chuo kikuu kwa polisi kujua kwamba walihitaji kuimarisha ulinzi.

“Matokeo yake hawakuleta ulinzi wa polisi na hata baada ya kupigiwa simu saa 10:00 jioni kwamba kuna dalili za vijana wa CCM kujiandaa kuleta vurugu, lakini bado walifika saa 12:15 mahali pa umbali wa dakika 10”alisema.

Mwenyekiti huyo alisema chama hicho hivi sasa kinajiuliza kama kweli Polisi Kilimanjaro wapo kwa ajili ya kulinda amani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi au lipo hapo kwa ajili ya kulinda maslahi ya CCM na wagombea wake.

“Sisi kama chama tunazo taarifa za kiintelijensia za vijana waliopewa fedha na pombe ili kufanya vurugu hizo, lakini polisi hawataki hata kutusikiliza ,vijana wetu wanapigwa Moshi na Hai, lakini hakuna mtu anayekamatwa”alilalamika.

CHANZO>>



SWALI: Nani alaumiwe??
 
Back
Top Bottom