Mbowe atoa tamko: CHADEMA kuisimamisha nchi Machi 25, 2013

Go boys go!!!!


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza rasmi maandamano ya kuishinikiza serikali kuwajibika kwa Waziri Shukuru Kawambwa na wasidizi wake kujiuzulu kutokana na matokeo mabovu ya kidato cha nne mwaka 2012. Mbali na matokeo hayo, CHADEMA inaitaka serikali kueleza haraka hatma ya vijana 344,230 iliyowafeleisha kwa kukumbatia mfumo, mazingira na kuitelekeza sekta nzima ya elimu na hatimaye wanafunzi hao kumbulia madaraja ya IV na O kwa ujumla wao. Kwa taarifa za uhakika kutoka CHADEMA, Maandamano hayo yatfanyika katika majiji manne ya Tanzania, yaani Dar es salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya. Habari zinasema kuwa maandamano ya Dar es salaam yatakayoongozwa na baadhi ya viongozi wa kitaifa yataelekea ofisi za Waziri Mkuu wakati ya majiji mengine yataelekezwa kwa wakuu wa mikoa. Taarifa zinaendelea kueleza kuwa CHADEMA .... Taarifa nilizozipata kutoka jijini Mbeya zinasema Jeshi la polisi limegundua kuwa limebugi stepu kwa kuyapiga marufuku maandamano hayo huku CHADEMA Mbeya wakisisitiza liwalo na liwe siku ya Jumatatu watakuwa barabarani. Jeshi hilo teyari limesalimu amri kwa kuwaita viongozi hao kwenye meza ya mazungumzo siku ya Jumamosi. Kwa hapa mkoani Mwanza tayari matangazo yameshaanza kumiminika mitaani juu ya maandamano hayo wakati ripoti kutoka Arusha zinasema machalii wa mkoa huo wanasubiri kwa hamu siku ya tarehe 25.03.2013 kudai haki yao ya elimu iwe jua ama mvua kwa ruhusa bila ruhusa na kama ni mabomu basi wameshayazoea na kama jeshi la polisi litaamua kutumia maguvu yake basi na lifanye hivyo na dunia nzima ijue hivyo. Tafadahli kwa wale mlioko Mbeya, Dar es salaam na Arusha muendelee kutupa hali ya mambo kwenye maeneo hayo na sisi kutokea hapa Mwanza tutawajuza juu ya sakata hili.
 
Back
Top Bottom