Mbona malalamiko ya waislamu hawaitaji CCM kama chanzo

Ukisoma katika Biblia takatifu agano la kale kuhusu uzao wa baba Ibrahamu utagundua kwa nini wakristo na waislamu wana chuki isiyoisha.
Ibrahamu alizaa na kijakazi aliyeitwa Hajira raia wa Misri. Mtoto aliyezaliwa aliitwa Ishmaeli.
Baadaye Ibrahamu alizaa na mke wake wa ndoa aliyeitwa Sarai. Mtoto aliyezaliwa aliitwa Isaka.
Ukoo wa Waarabu umetokana na Ishmaeli na ukoo wa Waisrael umetokana na Isaka.
Yesu Kristo ni MwiIsrael na ndiye aliyeleta ukristo baada ya kutumwa na Mungu. Mtume Mohamadi ni Mwarabu ambaye Uislamu umetokana naye baada ya kutumwa na Mungu.
Waarabu wametokana na uzao wa mama mdogo na Waisrael wanatokana na uzao wa mama mkubwa. Siku zote mtoto wa mama mkubwa na mtoto wa mama mdogo huwa hawapatani. Mataifa mengine na hasa Waafrika tulipoamini dini hizi za Kikristo na Kiislamu tulirithi na mbegu mbaya ya chuki ya Mwarabu na Mwiisrael. Kama vile ambavyo mpenzi wa timu ya Yanga ambaye hatathubutu kuisifia timu ya Simba ikifanya vizuri na kinyume chake, vilevile sheikh wa kiarabu hawezi kumsifu Askofu wa kiisraeli akitenda jambo jema ingawaje naweza kusema kwa kujiami kuwa Askofu wa kiafrika au taifa lingine ukiacha waisraeli anaweza kumsifu Sheikh akitenda jambo jema na kumkemea akifanya jambo baya.
Tunaona shule za kwaida, viuo vikuu, mahospitali na taasisi zingine za kikristo za kutoa misaada wakati wa maafa hazibagui wanafunzi wa kikristo na wa kiislamu wala wagonjwa wa kiislamu.
Ndugu zangu waislamu tuwaachie waarabu na waisrael chuki yao na tufuate habari njema iliyoko kwenye dini zetu. Hutaenda peponi kwa sababu ya uislamu wako ila kwa sababu ya matendo yako.
Baba wa Taifa hayati mwalimu Nyerere alitaifasha shule zote zilizokuwa zinamilikiwa na Wakristo kwa manufaa ya waislamu lakini hakuna Askofu aliyemlalamikia Nyerere.
Tukiendelea na chokochoko hizi tujue kabisa inchi yetu tutaigeuza mashariki ya kati.
 
Back
Top Bottom