Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,403
- 219,814
Taarifa ya Mkuu wa Mkoa huo Juma Homera , inaeleza kwamba , watu 40 (idadi yao yaweza kuongezeka) wamekamatwa kwa tuhuma za kutengeneza mtandao wa kujipatia mapato ya Halmashauri kinyume cha sheria za Nchi .
Mnyororo wa Watu hawa umeanzia Mbarali , ukaja Busokelo hadi Mbeya Mjini , Taarifa zaidi zinaeleza kwamba Mtaalam Msomi aliyetengeneza mchepuko huo amekamatiwa Jijini Dar es salaam , bado mpaka muda huu hatujapata majina ya watuhumiwa hao (Juhudi zinaendelea)
Bali Mshangao wa wengi ni kuhusu Watuhumiwa hao kukamatwa Mara tu baada ya Kauli ya Rais , ina maana huko Mbeya hakuna viongozi wala vyombo vya dola vyenye uwezo wa kubaini mambo haya ?
Ushauri : Viongozi wote wa Polisi , Tiss , RC na Ma DC wa maeneo yaliyotajwa Watimuliwe mara moja .