Mbeya: Mbaroni wakitorosha Madini yenye Thamani ya Shilingi 1.5 Bln. Waziri Mavunde aagiza kufutwa kwa leseni zao ndani ya nchi

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,051
49,735
Mavunde.jpg

Watu 10 wamekamatwa Jijini Mbeya Wakitorosha Madini ya Dhahabu kilo 9.5 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.5 na kuisababishia Serikali hasara.

Waziri wa Madini Antony Mavunde ameagiza Kamishna wa Madini kufuta leseni za watu hao popote pale ndani ya Nchi.Tukio hili la utoroshaji limekuwa ni la pili Mkoani Mbeya.

---

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu kumi kwa tuhuma za kutorosha kilo 9.5 za madini ya dhahabu.

Waziri wa madini Anthony Mavunde amesema thamani ya dhahabu iliyokamatwa ina thamani ya shilingi bilioni 1.5 ambapo watuhumiwa hao walikamatwa katika eneo la Ilomba Jijini Mbeya.

Mavunde amesema tukio hili ni la pili kutokea mkoani Mbeya na kuagiza Kamishna wa madini kuzifuta leseni zote zinazomilikwa na watu hao pamoja na leseni zote zinazomilikiwa na watu hao nje ya Mkoa wa Mbeya

Watu hao wamekamatwa wakiwa na vifaa vya kuchomea dhahabu na mizani ya kupimia pamoja na dawa za kusafishia ambapo uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani

--
My Take
Wizara ya Madini kaeni na wadau wote wa Madini muangalie Kwa nini wanatorosha Madini Ili kujiridhisha na sababu Ili kama Zina mashiko mtafute suluhisho Ili tusipoteze pesa Kwa utoroshaji.
----
DHAHABU KILO 9 ILYOKUWA INATOROSHWA YAKAMATWA JIJINI MBEYA **

Waziri Mavunde aingia mtaani na kikosi kazi kwenye eneo la maficho

Aupongeza Uongozi wa Mkoa na Vyombo vya Usalama Mbeya

Aagiza kusimamisha Leseni za biashara ya Madini za watuhumiwa

Dhahabu iliyokamatwa ina thamani ya Tsh 1,555,476,586

Serikali ingepata mapato ya Tsh 144,659,322


Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia wafanyabiashara wa madini 10 kwa tuhuma za utoroshaji wa madini Kilogramu 9.8 yenye thamani ya Tsh 1,555,476,586.

Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari,Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amesema wafanyabiashara hao walikamatwa siku ya Jumamosi saa 10:27 Alfajiri Katika mtaa wa Ilomba Jijini Mbeya kwenye nyumba waliyokuwa wamepanga wakiwa na vipande 344 ya dhahabu iliyochomwa yenye uzito wa Kilogramu 9.8 pamoja na vifaa mbalimbali kama vile Precious Metal analayzer (XRF) aina ya Niton DXL thermoscientific, mitungi ya gesi, jiko na vyungu kwa ajili ya kuchomea dhahabu, Kipimo cha maji cha kupimia dhahabu, mizani kadhaa pamoja na kemikali aina ya borax.

Mhe. Mavunde ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Mbeya chini ya Mh. Juma Homera na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na Kikosi Kazi cha Wizara ya Madini kufanikisha ukamataji wa watuhumiwa hao.

Pia, Waziri Mavunde ametoa rai kwa wafanyabiashara wote wa madini kuhakikisha wanazingatia sheria na kanuni za kufanya biashara ya madini nchini na wote watakaobainika kutorosha madini watachukuliwa hatua za kisheria pamoja na kufutiwa Leseni zao.

Aidha, Waziri Mavunde ameagiza kusimamishwa kwa Leseni za biashara ya Madini za watuhumiwa nchi nzima wakati taratibu za upepelezi zikiendelea kabla ya kufikishwa Mahakamani.

Akizungumza katika zoezi hilo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya wa Chunya Mhe. Mbaraka Batenga amewataka viongozi wote wa mitaa na vijiji kuwatambua watu katika maeneo yao kwa kuwasajili katika daftari la wakazi na kuwataka wamiliki wa nyumba za kupanga kuhakikisha wanawafahamu vyema wapangishaji wao na shughuli zao.
 
Mzigo mdogo sana huo msitafutie kiki mkatuambia miaka mitatu ya samia hayo ndio madini yaliyotoroshwa kilo tisa tu!
 
Jamaa wamekamatwa Mbeya 10 na madini ya bilion 1 plus

Mh waziri ikabidi akayasimamie akaenda Mbeya

Swali waliokamatwa mh waziri mbona awakuonyeshwa?

Wezi wa mifugo Mbeya tunaonyeshwa kila siku hawa ni nani

Na wanafikishwa mahakaman lini
 
Back
Top Bottom