MBARALI RAHA: Polisi wameua na Wananchi wateketeza KITUO CHA MAFUTA!

Kuna haja ya kupitia mfumo mzima wa mafunzo ya jeshi la polisi, Hawajui majukumu yao? Au ouga unawasumbua? Mbona wanakimbilia kufyatua risasi bila hata kujaribu kutuliza ghasia! Hawa jamaa wanatia aibu, Said Mwema naona anataka kumzidi hata Mahita kutotumia akili, alikaa Interpol ndio alifundishwa haya, Shame on you Mwema.... Sioni tofauti ya askari polisi na wanamgambo wa kijiji stupid!
 
Watu sasa wameamua kuchua hatua mkononi kwa sababu wanaona serikali hawasikilizi sauti zao.

Inasikitisha, na huyu JK asipokuwa makini, nchi haitakalika.

Mkubwa nchi haikaliki kwa walala hoi. Bora sasa isikalike kwa wote!!! Hao wakubwa na walalahoi vilevile!!!
 
Police force has totally lost confidence among citizens, kila mara huwa nawashauri wabadili uniform zao wavae kijani, njano na nyeusi na pia waweke jembe na nyundo, hii itadhihirisha kuwa wao ni CCM then no one will ever blame them, Hatulihitaji jeshi hili kabisa nchi hii
 
Katika taarifa ya habari ya BBC ya jioni, hii RPC Mbeya katika mahojiano yake na mtangazaji wa shirika hilo alithibitisha kuwa mtu mmoja aliuwawa kwa risasi na polisi huko Mbalali. Alisema hii ilifuatia umati mkubwa wa wakazi wa eneo hilo kuvamia gari la mafuta na kulichoma moto, ikiwa ni pamoja na kituo cha petroli. Alisema polisi walijaribu kutawanya kundi hilo kwa kutumia mabomu ya machozi ikashindikana, ndipo walipo amua kutumia risasi za moto. Alipo ulizwa kisa cha uvamizi huo alisema wananchi wana bifu na mmiliki wa roli hilo kwasababu amefunga maji ya mto na kusababisha mashamba ya mpunga ya wenyeji kukauka. Kauli hiyo ya RPC imenishutusha; hivi huko mbeya hamna serikali! kama ipo, mtu anawezaje akafunga maji ya mto unao tumiwa na watu wote.
 
Alipo ulizwa kisa cha uvamizi huo alisema wananchi wana bifu na mmiliki wa roli hilo kwasababu amefunga maji ya mto na kusababisha mashamba ya mpunga ya wenyeji kukauka.

Kwa hiyo wananchi ndio wenye shida na mwenye gari!! Serikali haikuona hilo tatizo mpaka ugomvi umefikia hapo ulipofikia. Mtanzania mwingine amepoteza maisha, Arusha ni mgogoro wa kisiasa, Mbeya ni mgogoro wa Ardhi. Dodoma ni mgogoro wa Elimu na kuendelea.

Tatizo la serikali kudharau wananchi wake. Tatizo la serikali kuwapuuza raia. Tatizo la serikali kujiona wao ndio bora na wenye kujua kila kitu. Tatizo la serikali kutokuwajali wananchi. Uchaguzi si umepita? Ukiongea unaambiwa subiri uchaguzi 2015!! Maamuzi ya kawaida kabisa yanashindwa kutolewa maelezo badala yake yanaachwa mpaka madhara yatokee. Baada ya kuzuia malori yenye uzito wa zaidi ya tani 10 yasipite Serikali ilitoa alternative gani?? Au walizuia halafu basi? Wananchi wanatakiwa waheshimu dola! Huu ni upumbavu. Dola isiyojiheshimu haiwezi kuheshimiwa hata siku moja. Mamlaka ni wananchi, viongozi ni wawakilishi siku zote. hiyo ndiyo demokrasia.

Taratibu kuuwawa kwa raia inakuwa jambo la kawaida na la kuzoeleka. Muda si mrefu raia kuua polisi litakuwa jambo la kawaida na kuzoeleka. Tabia ya kulipiza kisasi itajengeka madhara yatakuwa makubwa zaidi. Serikali itabaki kusema kuna mkono wa mtu na ni siasa!! Hali hii isiruhusiwe kuendelea. Lazima tuipigie kelele. Wanaoishi Mbarali kuweni mfano na kutetea haki, sis wengine pia tutaungana nanyi kuteteta haki.

Maggid, kuandika haitoshi na sasa umethibitisha hilo. Ni makosa kufikiri kwamba serikali yetu inasikiliza. Kama ingekuwa inasoma na kusikiliza matatizo mengi ya hii nchi yanegkuwa yametatuliwa. Ni vyema ukasimama na kuwa mstari wa mbele kuwatetea ndugu zako wanyonge!! Kuwaambia kwamba uliandika halafu basi ni kuwatukana!! Hawakukupeleka shule uandike halafu maisha yaendelee!! Wao hawaandiki wanaumia!!
 
Back
Top Bottom